kiraremapojoni
JF-Expert Member
- Nov 30, 2018
- 391
- 512
Nilistushwa sana na uamuzi wa Ndugu yete E N Lowassa juu ya mauzi yake ya kikatiba ya kurejea kwenye chama chake pendwa cha CCM. Inawezekana ikawa ni maamuzi yake binafsi kama ambavyo anazungumza au pengine kuna ambayo yako nyuma ya pazia yaliyojificha ambayo ndiyo hasa yamempa msukumo mpaka kuchukua hatua hii ya kufunuka kombe ili mwanaharamu apite.
Inafahamika fika kuwa mkwe wake Bwana Lowasa ambaye ni Ndugu Sioi yuko jela kwa muda mrefu sasa na hatima ya kesi yao haijulikani kwani inazungumzika kama utashi wa mkwe wake inawezekana ikawa ni fimbo ya kuadhibiwa ili aongee na mkewe amshauri baba yake arudi kundini ili akazikane na wafu wenziwe wa CCM.
dhamana ya kina Mbowe na Esther MAtiko ilikuwa mikononi mwa Lowasa na mara baada ya kuamua kurudi kundini imetokea sintofahamu ya Jaji Rumanyika kushangaa maamuzi ya hakimu wa Kisutu juu ya kufuta dhamana na kuwaweka jela kwa kipindi chote hiki.
Sasa Lowasa amesharudi kundini na wale ambao walibambikiwa makosa ya kuhujumu uchumi nna hakika nao watapewa dhamana kama ambavyo alipewa ndugu yake rostam Azizi mara baada ya kwenda ikulu na kuongea na mkuu pamoja na kumpokea Bwana lowasa ndani ya chama siku aliyoamua kurudi kundini
Tanzania ya viwanda kwa stahili hii bado sana kwani hakuna fedha ya dhuluma iliyo na baraka kwa ajili ya kuendeleza vitu vya maendeleo