Sintofahamu inayoendelea mpakani Namanga mwandishi huyu achukuliwe hatua

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,121
Kumekuwa na taarifa kwamba kuna vurugu mpakani mwa Kenya na Tanzania nimejaribu kusoma makala iliyoandikwa na gazeti la the star kenya Namanga cuts water to TZ in protest against listing Kenyans nimegundua kuna upotoshaji uliofanywa na huyu mwandishi anayejiita Bob Lyimo,

Suala la kuandikisha wakazi legal residents ni agizo la serikali kupitia NIDA, pale mpakani watu hupita bila pasi (ujirani mwema) kwenda kununua bidhaa ama matembezi ila wapo wanaolowea na kuzamia. Sasa hawa ndugu zetu wakenya waliolowea wamekamatwa wameanza vurugu ikiwa ni pamoja na kufunga mpaka kuchoma matairi nk.

Huyu mwandishi kama jina analotumia kweli ni lake kama ilivyo kwenye makala hiyo ni bora achukuliwe hatua kwa sababu wakati anahojiwa na gazeti hilo la nchi jirani badala ya kusema sheria inasema au tangazo la serikali limesema yeye ametamka Magufuli kasema ambapo ametengeneza chuki.
 
Daa nimesoma hiyo kitu jamaa anapotosha kweli kweli na kitu ya ajabu anayehusishwa na hii scandal eti ni rais magufuli. Pia huyo jamaa sijui ndiyo Bob Lyimo ameharibu kabisa kabisa kwa kumpa uongo.
 
pale mpakani watu hupita bila pasi (ujirani mwema) kwenda kununua bidhaa ama matembezi ila wapo wanaolowea na kuzamia.
  • Nimechukia:mad: baada ya kusikia kuna utaratibu wa kupita bila pasi (a.k.a ujirani mwema)
  • Kwa kweli waufute hatutaki Wezi na Majambazi wa kigeni; Magaidi wa Kisomali; Spys; Majangili; Wauza madawa; Wauza magendo na nk
 
  • Nimechukia:mad: baada ya kusikia kuna utaratibu wa kupita bila pasi (a.k.a ujirani mwema)
  • Kwa kweli waufute hatutaki Wezi na Majambazi wa kigeni; Magaidi wa Kisomali; Spys; Majangili; Wauza madawa; Wauza magendo na nk
Usichukie hii ni kawaida kwenye mipaka kati ya nchi na nchi. Kuna distance toka mpakani ambayo mtu wa nchi jirani anaweza kuingia bila kusimamishwa na kuulizwa vibali. Unakuta kuna huduma mbali mbali kama maduka, baa, biashara nyingine mfano kubadilisha fedha, hata huduma za maji mtu anapata upande wa pili wa mpaka.
 
Back
Top Bottom