Sintafanya biashara na mtanganyika

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,071
27,008
Mimi ni Mtanganyika but kamwe sitathubutu kufanya "Biashara" na Mtanganyika!. Kwanini? Kwa sababu WATANGANYIKA HAWAJUI HESABU! Kwao namba hazina maana yoyote! Mtu a siyejua umuhimu wa namba ni hatari sana katika ulimwengu wa biashara na faida.

KWANINI NINASEMA WATANGANYIKA HAWAJUI HESABU?

Here i come

1. Kwa mujibu wa sayansi na historia, mtu wa kwanza duniani aliishi katika nchi ya Tanganyika zaidi ya miaka BILIONI MBILI iliyopita. Hii ina maana kuwa ustaarabu wa mwanadamu ulianzia Tanganyika au kwa lugha nyingine, Ustaarabu wa MTANGANYIKA una MIAKA BILIONI MBILI.

Karne kadhaa zilizopita nchi yetu ilivamiwa na WAARABU na WAZUNGU ambao walikuja na ustaarabu wao na kuwalazimisha/kuwashawishi watanganyika kuufuata.

USTAARABU WA WAARABU ( UISLAMU ) UNA MIAKA 1500 tu tangu uanze kuwepo.

But Mtanganyika amekubali ku exchange ustaarabu wake wenye umri wa miaka BILIONI MBILI kwa ustaarabu wa kiarabu wenye umri wa miaka 1500!!!!

ITS ONLY A FOOL WHO WILL EXCHANGE HIS/HER 2 BILLION SHILLINGS with 1500 SHILLINGS.


USTAARABU WA WAZUNGU ( UKRISTO ) UNA MIAKA 2000 tu tangu uanze kuwepo.

But Mtanganyika amekubali ku exchange ustaarabu wake wenye umri wa miaka BILIONI MBILI kwa ustaarabu wa wazungu wenye umri wa miaka 2000!!!!

ITS ONLY A FOOL WHO WILL EXCHANGE HIS/HER 2 BILLION SHILLINGS with 2000 SHILLINGS.



2. KUHUSU KILE KINACHOITWA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.


Watanganyika tupo MILIONI 43 na ushee , WAZANZIBARI wapo MILIONI 1 na ushee.

Halafu Watanganyika tunakubali kuunganisha taifa letu lenye watu MILIONI 43 na ushee na kisiwa chenye watu MILIONI MOJA ambao idadi yao ni ndogo kuliko idadi ya wakaazi wa mkoa mmoja uliopo katika taifa la Tanganyika!!!!

NI MFANYABIASHARA MPUMBAVU TU NDIO ANAYEWEZA KUUNGANISHA MTAJI WAKE WA SHILINGI MILIONI 43 NA MTAJI WA SHILINGI MILIIONI MOJA KUTOKA KWA MTU MWINGINE KISHA WAKAANZISHA BIASHARA MOJA WAKITEGEMEA KUPATA FAIDA SAWA SAWA.



3. Serikali ya CCM (TANU ) ipo madarakani tangu mwaka 1961. Imetusababishia matatizo mengi sana sisi watanganyika ( Do i need to talk about it ? Please excuse me! )

Lakini still bado kuna watu leo hii wanaishabikia CCM.

Ni mpumbavu tu anayeweza kukiunga mkono chama ambacho kimemfanya aendelee kuwa masikini kwa zaidi ya miaka hamsini ili kiendelee kumfanya awe masikini kwa miaka mingine zaidi.

RAI YANGU KWA WATANGANYIKA WENZANGU:

Tukatae Muungano wa serikali tatu, tuukatae Muungano. Tuidai nchi yetu ya Tanganyika, tuikatae CCM.

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA.
 
Bangi za kuvutia chooni hizi zina madhara sana, kasome vitabu kwanza ujuwe cold war ni nini ndio utajuwa maana ya Tanganyika kuungana na Zanzibar kulikuwa na malengo gani.

Siku nyingine jiepusha kuchanganya bangi na kubeli halafu unashushia na kiroba haya ndio madhara yake.
 
Bangi za kuvutia chooni hizi zina madhara sana, kasome vitabu kwanza ujuwe cold war ni nini ndio utajuwa maana ya Tanganyika kuungana na Zanzibar kulikuwa na malengo gani.

Siku nyingine jiepusha kuchanganya bangi na kubeli halafu unashushia na kiroba haya ndio madhara yake.

Utabakia kulaumu wachawi bure, aliyekuroga wewe, ni aliye kataa kukupeleka shule.
 
Mh.LIKUD, mchana mwema ulivyo panga inaonesha wazi NATURE ya kiTanganyika siye niyo tulivo toka enzi hizo labda ulisahau kuandika Tulikuwa tunashabikia nyimbo za kiCongo na kutelekeza nyimbo zetu; Tulishangilia tmu za wageni na kuponda timu zetu; Tulikuwa na Siasa za maBabu zetu Tukashikilia Siasa za kichina na Ukomisti; Tulikuwa tunaAbudu miungu ya watu na kuisahau miungu yetu!! vipi hapo? hayo ni majunguu tu nchi hii haina mwenyewe hata ikilazimisha utaachwa ku-mataa tu. Ustaarabu wa kigeni utaendelea Muungano utaendelea kazi yetu itakuwa kufuata tutafuata What ever comes!!
Siye tupo tupo!!
 
Mwaya mi sijaelewa kitu, napiga kimya Mpwa wangu LIKUD sitaki maneno mie ngoja ningoje saizi yangu. Hii yan'pwaya mie
 
Last edited by a moderator:
Afadhali yangu mimi ambaye sikwenda shule kuliko wewe uliyekwenda shule kusomea ujinga.

Ujinga wangu una akili kuliko werevu wako. Anywaysa i respond 2u one time and one time only
 
Na mimi ningekuunga mkono lakini haona ulipopuliza umeacha moshi mkubwa
Kuhusu Muungano kote unachemsha mm nataka Serikali 3, kila moja ijitawale na ikishindwa ilale mbele
Kuitoa CCM na nkuingiza chama kingine ni ngoma ya mashetani ya kinyamwezi kwani kwa mimi mwenye kuomba serikali 3
Lazima visiwani itabaki ya Kiislamu na Chama cha Kiislam
kwa bara itakuwepo ya Dini ingine ili kupingana na ile ya Visiwani
sasa Serikali kuu si ndio balaa maana umeshawasifia Waarabu kwa hiyo wachukue Serikali ipi?
Hutaki hata CCM
HAPA NA MIMI BANGI UMESHANINUSISHA NAONA KM SERIKALI MBILI NA TUUVUNJE MUUNGANO?
kweli Bangi kali
 
Sijui kwa nini wa bara (tanganyika) tunang'ang'ania huu muungano!sioni faida hata moja ya muungano huu.Bidha zote za zanzibar soko ni bara,sisi tunauza nyama tuu za ng'ombe huko na umeme wa bure tunawapa
 
Afadhali yangu mimi ambaye sikwenda shule kuliko wewe uliyekwenda shule kusomea ujinga.

Matola usihangaike na watoto wa siku hizi, ujanja mwingi lakini uwezo wa kufikiri na kuona mbali hawana. Kwa hiyo wala tusingaike nae, watoto wa siku hizi michezo yao ipo kwenye computer na huyu LIKUD yupo hapa JF ni moja ya michezo yake
 
Matola usihangaike na watoto wa siku hizi, ujanja mwingi lakini uwezo wa kufikiri na kuona mbali hawana. Kwa hiyo wala tusingaike nae, watoto wa siku hizi michezo yao ipo kwenye computer na huyu LIKUD yupo hapa JF ni moja ya michezo yake

Nia yako ni kujaribu kubadili trend ya huu uzi, nilicho kiongea sio kipya hapo, nimerudia kile ambacho wa\\kimekuwa kikizungumzwa kwa muda mrefu sasa. Watanganyika hatuitaki CCM na hatuuhitaji muungano pia kama amavyo wazanzibari wasivyo itaka ccm na muungano. Mbona nashindwa kuona mashiko ya hoja yako?
 
Sijui kwa nini wa bara (tanganyika) tunang'ang'ania huu muungano!sioni faida hata moja ya muungano huu.Bidha zote za zanzibar soko ni bara,sisi tunauza nyama tuu za ng'ombe huko na umeme wa bure tunawapa

Tell them brother
 
Back
Top Bottom