Sintaacha kazi ya UGANGA kwa sababu ya UBUNGE, Prof. Maji marefu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sintaacha kazi ya UGANGA kwa sababu ya UBUNGE, Prof. Maji marefu.

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Leornado, Dec 25, 2010.

 1. L

  Leornado JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sioni ubaya wa wananchi wa Tanga kumpa ubunge mganga maarufu wa kienyeji maji marefu. Inaonekana wamechoshwa na mafisadi wasomi ndio maana wameamua kuchagua mganga wa kienyeji awawakilishe bungeni. Pamoja na ubunge, Maji marefu atendelea na kazi yake ya kuagua mapepo na kutibu magonjwa mbali mbali.


  Pamoja na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mganga maarufu wa Tiba Asilia, Mheshimiwa Steven Ngonyani ‘Profesa Maji Marefu’ amesema hawezi kuacha kazi hiyo ya uganga.

  Prof. Maji Marefu aliyechaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu, alikaririwa akiyasema hayo hivi karibuni na gazeti moja litokalo kila siku.

  “Ubunge ni dhamana iliyokuja nikiwa mganga wa tiba asilia, sasa nikisema niache nitakuwa siitendei haki dhamira yangu na wateja wangu,” alisema Mheshimiwa huyo.

  Alisema kuwa alianza kuguswa na masuala ya siasa mwaka 1995 baada ya kuteuliwa kuwa meneja wa kampeni wa aliyekuwa mgombea na baadaye Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM), Laus Mhina.

  Aliweka kweupe kwamba, tofauti na siasa, mambo ya tiba asilia alikuwa nayo hata kabla ya ‘kubatizwa’ uprofesa wa masuala hayo mwaka 1989 nchini Nigeria hivyo hawezi kuyaacha.

  Kwa mujibu wa watu wanajua tiba asilia, kazi hiyo ni kama uchawi hivyo kumtafsiri Prof Maji Marefu tofauti na wabunge wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Prof. Maji Marefu ni mbunge mwenye historia ndefu ikiwa ni pamoja na kuzunguka ndani na nje ya nchi kwa kazi hiyo ya uganga huku makao yake makuu yakiwa wilayani Lushoto, Tanga.
  Bingeni patakuwa hapatoshi, nani atadiriki kubishana hoja na maji marefu??

  Interview kwa hisani ya GPL.
   
 2. Mzee Dogo

  Mzee Dogo JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Haya watanzania, ndiyo maamuzi yenu...
   
Loading...