Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,775
Habari za Ijumaa wapendwa,
Imetokea umepata mwenza anaekupa masharti kuwa mtoto wako asifike nyumbani kwenu utachukua uamuzi gani?
Yalimtokea shosti, alipata mimba akiwa form six, kichwani alikua njema na alipata nafasi USDM baada ya kujifungua. Ilibidi aahirishe mwaka na wazazi waliachiwa kichanga nyumbani.
Akiwa chuo alikutana na kijana mmoja ambae alifunga nae ndoa. Ingawa kijana alifahamishwa hali halisi na alishamuona mtoto lakini hali ilikuwa tofauti pale wote walipopata ajira na mdada kutaka kumchukua mwanae amlee.
Mume alipinga vibaya sana. Shosti alikuwa imara, alimwambia angalia hapa huyu mtoto bila mimi asingekuja duniani, wewe una wazazi waliokulea mpaka hapo ulipofika, kama hutaki kuishi na mwanangu na mimi ninaondoka. Jamaa alijifikiria sana, katika vikao vya kusuluhisha ndoa jamaa alijiona amechemka.
Mwisho wa yote alimlea yule mtoto kwa mapenzi yote.