Single Mothers: Nani wa Kulaumiwa? Wanaume au Wanawake Wenyewe?

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,309
Maoni yenu wanajamvi, jinsia gani hasa ndio inachangia kwa kiasi kikubwa hili tatizo?

Kwa sasa sio ajabu tena kusikia binti fulani kazaa mtoto/watoto akiwa bado hajaolewa na unaweza kukuta watoto wote wana baba tofauti tofauti.

Tunakoelekea watoto wengi sana watakosa malezi ya wazazi wote wawili kutokana na hili janga.

Kitu kinachonipa shida sana kichwani mwangu ni kwamba siku hizi elimu ya uzazi imewafikia watu wengi sana tulitegemea hili tatizo lipungue lakini ndio kwaaanza linazidi kuongezeka kwa spidi kali.

Kingine hili janga lipo sana mijini ambako kidogo tunaamini watu wameelimika lakini ni kinyume chake.

Nini hasa tatizo? Jinsia ipi inapaswa iwe accountable?

download-10.jpeg
18.jpeg
 
Back
Top Bottom