Single mothers huwajaza watoto wao chuki mbaya sana

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Baada ya wazazi wawili kutengana mara nyingi mtoto hubaki kwa mama na hapo ndipo mama hutumia nafasi hiyo kujenga chuki mbaya kwa mtoto kumhusu babake.

Mtoto akiwa mdogo ataanza kusimuliwa mabaya yote ya babake tena kwa kuongeza mengine ili mradi tu mtoto amchukie babake wakati mwingine wanawake hukataa msaada toka kwa baba ili kumfanya mtoto aamini kuwa babake ni mbaya na hampendi.

Mathalani inaweza ikawa mama aliachika kwa sababu ya uzinzi wake lakini atamwambia mtoto tofauti kwamba babake aliniacha sababu ya wanawake alikuwa hanipendi na hakupendi, wakati mwingine humzuia mzazi wa kiume kumsalimia mtoto wake ili asiwe karibu na mtoto wake aendelee kumwaga sumu vizuri zaidi.

Madhara ya tabia hii ni kwamba mtoto hujenga chuki mbaya sana kwa babake hali inayopelekea hata kushindwa kumthamini babake akiwa mkubwa kwa sababu tangu akiwa mdogo anaambiwa baba yako mbaya hakupendi.

Nitoe wito kwa masingle maza muache tabia ya kupandikiza chuki kwa watoto wenu wazazi wote wana thamani sawa hali hii humfanya mtoto kubeba mzigo mzito unaoathiri hata makuzi yake tofauti za baba na mama zisiwaathiri watoto kwa kumfanya apige vita isiyokuwa yake.
 
Ukweli mtupu, hawajui tu athari za chuki zinavyoweza kumtesa mtoto vizazi na vizazi mtoto anateseka na chuki yake kumbe mama alkuwa na nafasi ya kumuonesha mtoto anapendwa na wazazi wake wote
 
we umejuaje au umeamua kuandika kwa hisia zako

Hizi ni moja ya hasara za uhuru wa mawazo kila mtu anajiamulia kuharisha anachotaka na anapotaka

Sasa unafikiri watu wote ni wajinga kama hivyo ulivyoandika ?

Je kama anachomwambia mwanawe ni ukweli napo itakua kumjaza chuki ?

Ujinga ujinga tu
 
Baada ya wazazi wawili kutengana mara nyingi mtoto hubaki kwa mama na hapo ndipo mama hutumia nafasi hiyo kujenga chuki mbaya kwa mtoto kumhusu babake, mtoto akiwa mdogo ataanza kusimuliwa mabaya yote ya babake tena kwa kuongeza mengine ili mradi tu mtoto amchukie babake wakati mwingine wanawake hukataa msaada toka kwa baba ili kumfanya mtoto aamini kuwa babake ni mbaya na hampendi, mathalani inaweza ikawa mama aliachika kwa sababu ya uzinzi wake lakini atamwambia mtoto tofauti kwamba babake aliniacha sababu ya wanawake alikuwa hanipendi na hakupendi, wakati mwingine humzuia mzazi wa kiume kumsalimia mtoto wake ili asiwe karibu na mtoto wake aendelee kumwaga sumu vizuri zaidi.
Madhara ya tabia hii ni kwamba mtoto hujenga chuki mbaya sana kwa babake hali inayopelekea hata kushindwa kumthamini babake akiwa mkubwa kwa sababu tangu akiwa mdogo anaambiwa baba yako mbaya hakupendi.
Nitoe wito kwa masingle maza muache tabia ya kupandikiza chuki kwa watoto wenu wazazi wote wana thamani sawa hali hii humfanya mtoto kubeba mzigo mzito unaoathiri hata makuzi yake tofauti za baba na mama zisiwaathiri watoto kwa kumfanya apige vita isiyokuwa yake.
Mtoto ni mali halali ya mama ake, ambacho hamkielewi ni kwamba kwa huyo mama ukimkataa yeye na mtoto umemkataa automatically.
Wengine kwa ukweli hata huduma shida ila mtoto akifanikiwa mnajifanya ndo baba zao sana mkiona hampati response mnaanza kusema mnachukiwa, mara mama kapandikiza chuki lakini kiukweli huyo mtoto wako hana bond yoyote na wewe kama kumwona mara mbili tu kwa mwezi. ..yaani hakujui hivyo uchungu na wewe hana.
Mnapozaa bila mpango mfikirie
 
we umejuaje au umeamua kuandika kwa hisia zako

Hizi ni moja ya hasara za uhuru wa mawazo kila mtu anajiamulia kuharisha anachotaka na anapotaka

Sasa unafikiri watu wote ni wajinga kama hivyo ulivyoandika ?

Je kama anachomwambia mwanawe ni ukweli napo itakua kumjaza chuki ?

Ujinga ujinga tu
Usiwe mpumbavu kuna maneno hata kama ni ukweli hutakiwi kumwambia mtoto hasa akiwa mdogo sijui umekulia kwenye jamii gani wewe usiyeona haya yanayotendeka huko
 
siwezi kumwambia mwanangu upumbavu wa babayake heri nimwambie baba alikufa kama sitaki wawe na mawasiliano kuliko kumharibu mwanangu na ujinga wangu na mwenzangu!!
Mama wa hivi anadhani anamkomoa baba kumbe anaharibu mtoto wake mwenyewe!
 
Sikumbuki siku nikiambiwa mabaya yake,tena nilikuwa nasisitizwa nimtafute baba,baba ni baba,akivuta kamba huyo utatamani ungepatana nae...ila mzee alizingua mwenyewe kwahio chuki aliopata ilitokana na watoto kushuhudia matendo yake wenyewe
My point wababa pia angalieni matendo yenu,watoto wanaweza kuelewa mambo madogomadogo na wakashika wewe ukidhani wamesahau,wakikua utasema mama yao kawafundisha kumbe mchawi ni wewe mwenyewe
Lakini single mamas wanaopandikiza chuki kwa watoto wapo na single babas pia wanaopandikiza chuki watoto wawachukie mama zao wapo pia...tabia mbaya sana,Mungu hapendi
 
Mtoto ni mali halali ya mama ake, ambacho hamkielewi ni kwamba kwa huyo mama ukimkataa yeye na mtoto umemkataa automatically.
Wengine kwa ukweli hata huduma shida ila mtoto akifanikiwa mnajifanya ndo baba zao sana mkiona hampati response mnaanza kusema mnachukiwa, mara mama kapandikiza chuki lakini kiukweli huyo mtoto wako hana bond yoyote na wewe kama kumwona mara mbili tu kwa mwezi. ..yaani hakujui hivyo uchungu na wewe hana.
Mnapozaa bila mpango mfikirie
Navyoamnini kina mama wengi huwa hawapendi kueleza ubaya kabisa kuhusu mababa bali ni matendo ya hao mababa ndio yanawabdadili watoto. Mababa webgine hudhani kwa kuwa ni watoto hawatambui kuwa wazazi wao hao wa kiume wamewatenga. Hawajui adha za kina mama wanazopata. Wanadhani kwa kuwa ni watoto hawatambui labda hili ni soma kwa wanaume wote wwenye watoto wa nje ( kwa hao masingle mom) muelewe kuwa watoto huelewa tangu wadogo sana shida zinazowapata na kuwa nyingi zapo zinasababishwa na hao wa kina baba sasa hizo huwa ni reaction tu za watoto lakini hawakawii kuwasingizia mama zao eti wanapandikiza chuki naamino 90% it is not true ila huo ukweli uchukueni chamuhimu ni " If you don't want to be your wife don't make her a mother'
 
Yani hao watoto hata usipowajaza chuki wakikua watampendea nini baba yao kama alikua hajishughulishi kwenye maisha ya familia? My mom is a single parent. Yeye siku zote ni kuimba mpendeni baba yenu, mwombeeni, muwe mnamjulia hali etc lakini
mimi ndo sina interest yani nimempotezea maana mzee ni stress tu. Kwa hiyo kama wewe baba ulikua haupo kwenye maisha ya mwanao don't expect hugs and kisses when you get back!
 
This is very true!
 
Back
Top Bottom