Single mama alivyotaka kukatisha uhai wake kwasababu yangu

mweee, kilichokusibu umtafute tena ni nini na ikiwa ulishamuacha bila huruma? Unataka kumharibia huko woooooi
Hahaa mtumwa hummis mtesi wake na ilivo kwa mtesi, wala siwez mualibia maana alimweka wazi
 
Habari wakuu

Wakati tunaendelea kusubiri mwezi wacha tupige story kidogo,

Huyu bi dada nilimpata sehemu nilihudhuria harusi ya rafiki yangu, katika meza nikabahatika kukaa nae karibu hapo simjui, nilimsalimia tu ila nilimscan kabla sijanywa ni binti mzuri umri wake haujaenda sana, kwa kumkadiria hakuzidi 30 yani 27-29.

Kula gambe mdogo mdogo mazoea na pombe ni kitu ch fasta tu,yule dada nikaanza kumchombeza, kiserious namuongelesha

Unajuwa nimekuwa ispired sana kwa kuhudhuria hii harusi nimejikuta ninatamani kuoa leo kesho, kumbe nae ndo kitu alikuwa anahitaji

Sikuwa namanisha wala usiriasi kiasi icho ila kwa namna moja ama ingine kweli kuna mzuka wa kuoa unaniingia alafu unatoka,

Yule dada akanza kuwa mchangamfu pale story zikanoga huku gambe zinaendelea, harusi ikaisha pale kiukweli sikuwa serious wakati wa kuondoka nikaona nashikwa bega

Nikamkumbuka tukabadilishana namba pale safi, hee safari ya mahusiano ikaanza kesho yake baada ya kuongea sana ktk simu.

Yule mwanamke kama nilivyowaza kweli akilikuwa mbele goli moja toto la kiume, ila mumewe alifariki alinitumia picha la kaburi,

Mahusiano yakanoga nogile haswa aisee nikatubu nilikuwa muigizaji ila ikafika kipindi nikawa serious kidogo alafu ndo ivo,

Tulidate kipind Sana ye akiwa mkoa mi mkoa mwingine, haijawah pita siku hatujazungumza alikuwa na mapenzi ya kweli mno alinipenda nilimpenda kwa asilimia kadhaa grade B,

Alikuwa mtafutaji mchangamfu kama unavyowajuwa waha wa kigoma walivyo,

Mahusiano yakaendela mwaka ushakatika ila ikumbukwe sijaonja papuchi,

Tukawa tunashare mambo kadhaa kadha kupeana suport n.k, inshot aliamini mi ni mtu sahihi 101%,

Alinisihi sana nisimuache,alipa kisa cha rafiki yake wa kike alifariki kwa presha iliyotokana na sonona baada ya kuachwa na boy ake kisirisiri akaenda kuoa mwanamke mwingine,

Rafiki yake uyo alivyokuja sanuka too late akafunga safari kweli akathibitisha ndipo presha na sonona ilipomuanzia, hakukukaa mwezi akafariki,

Basi kisa icho kikawa kinamuogopesha mno wakati anadate na mimi, ukweli nilimtoa hofu na kumuhakikishia sitomuacha(Mungu nisamehe sijui nilikuwa nasema ukweli au la!)

Alishawahi nitamkia siku nikimuacha anaweza jiuwa,kiukweli alikuwa serious nilishtuka kidogo


Siku zikasonga penzi linazid kunawiri, akaanza kunisihi nikamtolee mahari ili tuwe huru zaidi hata kama mipago ya ndoa tuipage vyema,

Hapo ndo alipoanza kunivuruga,kiukweli sikuwa na mpango wa kuoa mwaka huu wala kesho,naye yupo moto anakimbizana na age pia kuondoa ile hofu


Hakika baada ya kuzungumza hayo nikawa kama gia zimepunguwa,nikarudisha penzi hadi grade C ,nikaanza movie zisizoisha mpka akashtuka ile change


Kiukweli ningemuoa ila sio kwa haraka kiasi kile, pia nikaona wacha nichukue uamuzi wa kiume ili nisije nikafanya uamuzi too late ,kwa kumpotezea muda zAidi alafu nisimuoe,

Picha likaendelea nikamlia buyu kama wiki simtafuti,simpigii sipokei nikipokea namwambia ntakupigia alafu imeisha simpigii,

Wiki nzima siku akanitumia gazeti, akanipigia nikapokea

Alikuwa analia sana kwikwi nyingi, akaniomba nimwmbie ukweli kama no more

Hadi leo sikumbuki vizuri kama nililelewa,au shetani gani aliniingia maana sikuwa yule ambaye nipo normal, roho yangu ilikuwa haina huruma hata wala ile haya

Nikamwambia naomba tuishie hapa naona nikukwaze mapema kuliko too late fulani, sina jinsi ila nimekaa nikawaza nikaona sitoweza kamilisha dhamira yako mapema,

Ila usijali nimekuacha kwa wema japo nakupenda na unastahili mume bora mwenye kujali hisia zako, ila niseme nimeishia hapa. Thank you for your love ..flan.atakuja wa zaidi yangu

Alilia sana ktk simu nilijawa na hisia flani ila sikujali,

Tangia hapo sikumtafuta hakunitafuta nikawa kama yalitokea ndotoni, sijujuwa alipitia hali gani,sikujali aliendeleaje

Siku zikaenda zikarudi miezi ikapita, juzi kati nikaja kumtext maana namba yake nilikuwa nayo

Akaniuliza we nani nikamjibu, akanirukia hewani tukazungumza salamu tu na mambo ya kawaida kirafiki,

The next day tukachati akanambia amepoka cent kadhaa kama kiinua mgongo kwa mwanae baada ya kifo cha baba yake alikuwa muajiriwa halmashauri, so apewa ml kadhaa

Nikampongeza kwa kumpambania mwanae nikampa na ushauri basi akanishukuru

Siku iliyofuata nikamchombeza nimemisi, siunajuwa watesi huwamis watumwa wao na watumwa pia huwamis watesi wao,

Ndo akaanza kufunguka kwamba kapata mwngine na analipiwa mahari soon, atanipq update ,

Akanikumbushia jinsi nilivyomuacha nikasingizia bangi ,maisha na pombe(sio mtumiaji vyote)

Akalalamika sana nilimuacha, alipitia kipindi kigumu nilimuacha gafla sana, alikonda gafla, alifikiria zaid ya mara moja kujiua, ila maombi yalimuokoa

Ila kwa bahati nzuri akampata mwingine siku tatu nne baada ya breakout yetu, akamtuliza na akarecover now ndo wapo ktk mipango ya kuoana


Kiukweli nimefurahi sana kusikia ivyo maana hakuwa na baya yule mwanamke, niimpenda yeye na mwanae, ila hii Karma itanirudia na nipo tayari kuipokea ,

Naambatanisha text

View attachment 2207554

View attachment 2207555
Una ukatili mwingi sana aisee

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Sasa unamtumia meseji za nini?

Nyie vijana bhana ndiyo mnawaharibia hawa wanawake maisha kisha mnakuja kuwatukana humu.

Mwache aendelee na maisha yake.
 
Hahahah ulifanywa Zoba na Kukazobeka kweli. Yaani ndani ya Muda Mfupi keshapata wa Kumtuliza? Hahahah Hawa Viumbe Wanawaharibu sana Wanaume msiotumia akili nzuri

Anasingizia Alitaka Kujiua Ili uingie Ujinga Kichwani kwamba alikuwa anakupenda kumbe Target yake ilikuwa haijatimia(NDOA)

Na hapo Bado haijatimia maana Wanaume wengine hukimbia kabla ya Ndoa kufungwa

HUYO HAJA YAKE NI NDOA ILI AJIFUNUE MAKUCHA AKIWA NDOANI. Na ndio utajua ukweli wa Kwanini Baba Mtoto alifariki
 
Sasa unamtumia meseji za nini?

Nyie vijana bhana ndiyo mnawaharibia hawa wanawake maisha kisha mnakuja kuwatukana humu.

Mwache aendelee na maisha yake.
Sio kimahusiano wala nimemkumbuka
 
Back
Top Bottom