Watu wawili wamefariki dunia na wengine wapatao 20 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya National Express lolilokuwa likitoka Iramba mkoani Singida kwenda Dar es Saalam kuacha njia na kupinduka katika eneo liitwalo Tumuli.
Ni bus lililokua linatoka wilayani kiomboi mkoa wa Singida kwenda jijini Dar es Salaam. Limepata ajali eneo la Tumuli mkoani Singida.
Chanzo cha ajali: Mashuhuda wamesema ni mwendokasi na hivyo bus kumshinda dereva lilivyofika kwenye kona na ikizingatiwa palikua na hali na unyevu barabarani.
Vifo:
Mpaka sasa kumeripotiwa vifo viwili yani dereva wa bus na abiria mmoja.
Majeruhi ni wengi pia.
Note:
Madereva tuweni makini barabarani na trafiki fanyeni kazi sio mnakaa na tochi kama chanzo cha mapato tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.