SINGIDA: Watu wawili wafariki dunia katika matukio mawili tofauti

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,505
Watu wawili wamefariki dunia mkoani Singida, katika matukio tofauti likiwemo la mwanamke kuuawa na mume wake kwa kile kilichodaiwa ni hisia tu kuwa ana mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa.

Mwanamke huyo Sele Shija (34) amefariki dunia baada ya kupigwa kwa fimbo kubwa kichwani na sehemu mbalimbali za mwili na mume wake Gyuda Jackson (35).Wote ni wakazi wa kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba mkoa wa Singida.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba, alisema tukio hilo limetokea agosti 14 mwaka huu saa 7.40 mchana, huko katika kijiji cha Ntikwe.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo,ni wivu wa kimapenzi baada ya Gyuda kuhisi mke wake Sele, ana mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa.

“Hisia hizo zilisababisha ugomvi baina ya wana ndoa hao na kupelekea Gyuda kufunga mlango ili majirani wakose nafasi ya kuamua ugomvi huo.Wakati wakiendelea kugombana, Sele (marehemu) alimzidi nguvu mume wake. Kitendo hicho kilisababisha Gyuda achukue fimbo kubwa na kumpiga kichwani na kusababisha jeraha kubwa. Jeraha hilo lililosababisha atokwe na damu nyingi na kufariki papo hapo,” alifafanua.

Kamanda Magiligimba alisema kwa sasa wanamshikilia Gyuda kwa ajili ya upelelezi zaiidi na mara utakapokamilika,mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya kumuawa mke wake kipenzi.

Katika tukio la pili,kamanda huyo,alisema mchimbaji dhahabu katika mgondi wa Sekenke One kitongoji cha Nkonkilangi tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Msafiri Matiko (21) amefariki dunia agosti 13 mwaka huu saa moja usiku.

Amefafanua kuwa Msafiri wakati akitoka kwenye shimo duara namba 38B yeye na wachimbaji wengine sita, aliteleza kwenye ngazi na kutumbukia ndani ya shimo, na kupata majeraha makubwa.

Magiligimba alisema wachimbaji wenzake waliweza kumwokoa/kumtoa nje ya shimo hilo,lakini alifariki dunia akiwa njiani akikimbizwa hospitali ya wilaya ya Iramba,kwa matibabu.

“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wamiliki wa migodi kuboresha mazingira na kuyaweka kiusalama kwa wafanyakazi wao.Pia wahakikishe kunakuwepo na vifaa stahiki vya kujikinga na madahara wakiwa ndani ya migondi,” alisema kamanda Magiligimba.

Chanzo: Mo Dewji
 
Back
Top Bottom