Singida, the sleeping Giant?

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Wana jamvi asubuhi hii naelekea mkoani Singida hii ikiwa ni mara yangu ya pili baada ya miaka miwili; naambiwa mkoa umepiga hatua kimaendeleo; nakwenda kujionea! Lakini naleta kwenu kuwa huu ni mkoa wenye potential kubwa kiuchumi na kama maeneo mengine unaonaekana kusahauliwa katika kuexhaust hizo potentials?

Nini tatizo? na nini kipewe kipaumbele kuwainua wakazi wa mkoa huu?
 
Sio Singida tu. Kila sehemu ya Tz imependelewa rasilimali za kutisha ajabu.
 
Kama tungeliweza kujua economic activities za kila eneo lingetoa mwanga ni namna gani in future maeneo hayo yanaweza kusaidiwa. Kwa mfano, inawezekana kuna ufugaji mkubwa na kilimo cha mazao ya chakula na biashara maeneo ya Singida. Masoko ya bidhaa zao pengine ni tatizo. Haya makampuni ya wadosi huwa yanawalalia sana wakulima wakienda kununua product zao vijijini. Kwa kuwa kile wanachokifanya kinaweza kuwalipa ila hawajui wapi kuna masoko ya uhakika, ingekuwa muhimu kuunganisha information hizo zote za potentials za maeneo yetu tofauti na kama itawezekana watashauriwa namna ya kupata masoko ya uhakika. Kwa njia hii ya wadosi kwenda fron kununua mazao, tusitegemee lolote katika kupunguza umaskini. Ni walaliaji kweli
 
Back
Top Bottom