Singida: TAKUKURU yawapandisha kizimbani Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) na wengine wawili kwa tuhuma za rushwa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
593
1,000
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, imewapandisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Iramba watu wawili akiwamo Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Msingi kwa tuhuma za kuomba rushwa ya shilingi milioni tano.

Kesi hiyo ambayo ipo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iramba, Sydney Nindi inawahusisha Mkuu wa FDC Msingi, Elia Wony Jackson Urio na Mhandisi Mshauri, Ahmed Mohamed Ahmed.

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru Mkoa wa Singida, Edsoni Mapalala, alidai kwamba Septemba13, mwaka huu walitenda makosa hayo kwenye maeneo ya Manispaa ya Singida, mkoani Singida.

Kwa mujibu wa Mapalala, FDC Msingi ilitangaza zabuni ya kusambaza mbao za kujengea majengo ya chuo hicho, na kwamba mfanyabiashara aliyemtaja kwa jina la Aikande Amani Swai ndiye aliyeshinda zabuni hiyo.

Mapalala hata hivyo alidai kwamba baada ya mfanyabiashara huyo kushinda tenda hiyo ndipo mkuu wa FDC Msingi alipokwenda kwa mfanyabiashara huyo na kumwomba rushwa ya shilingi milioni tano ili aweze kumkabidhi kazi hiyo, vinginevyo kazi hiyo hataweza kuipata.

Mwendesha mashtaka huyo alidai zaidi kuwa baada ya Aikande kugoma kutoa kiasi hicho cha fedha ndipo mkuu wa chuo hicho alitoa kazi ya kusambaza mbao kwa mtu mwingine.

Hata hivyo washtakiwa hao baada ya kusomewa shtaka lao wamekana na wapo nje kwa dhamana ya shilingi milioni tatu kila mmoja hadi Desemba 11, mwaka huu kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa kwa uchambuzi wa awali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom