'Singida: RPC Sweetbert Njewika, amekanusha kauli yake iliyodai kuwa dereva bodaboda aliyeuwawa mkoani humo, hakuwa kiongozi wa CHADEMA'

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,349
2,000
RPC Singida akanusha kauli yake

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Sweetbert Njewika, amekanusha kauli yake iliyodai kuwa dereva bodaboda aliyeuwawa mkoani humo, hakuwa kiongozi wa CHADEMA na kusema kuwa alinukuliwa vibaya.

1582877549282.png

KAMANDA WA POLISI SINGIDA SWEETBERT NJEWIKE.

Akizungumza leo Februari 28, 2020 na EATV&EA Radio Digital, kamanda Njewike amesema kuwa walioitoa taarifa hiyo hawakumnukuu vizuri kwani yeye hakutoa taarifa ya moja kwa moja kuwa Jonas hakuwa kiongozi wa CHADEMA.

"Nilichosema kwamba yule ni bodaboda inawezekana anafanya kazi nyingine, sikukanusha kwamba yule siyo kiongozi wa CHADEMA, naomba mninukuu vizuri na ndicho nilichokisema" amesema Kamanda Njewike.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa Alex Joas alikuwa ni Katibu wa CHADEMA Manyoni Mashariki.

Naye Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Chadema ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter "Nikiwa Mwenyekiti wa @ChademaTz Kanda ya Kati, nathibitisha kwamba Alex Joas alikuwa Kiongozi mwandamizi wa Chadema Jimbo la Manyoni Mashariki akiwa Katibu wa Jimbo. Taarifa ya @tanpol Singida kwamba Alex hakuwa kiongozi wa Chadema sio sahihi. Waliomuua wakamatwe"

Baadae aliandika tena "AlexJoas ametwaliwa kwa makali ya upanga. Alitoka nyumbani hakurudi. Familia wamelia machozi usiku na mchana tangu waliposikia mateso yaliyosababisha kifo cha mpendwa wao. Alikuwa raia, baba, mume, kaka, na mtoto kwa wazazi wake. Aliendesha bodaboda na aliongoza Chadema"

Alex Joas inadaiwa kuwa mwili wake uliokotwa mbugani mbali na barabarani, ukiwa na majeraha ya kuchomwachomwa na kitu chenye ncha kali na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini nani aliyehusika na mauaji hayo.

Zaidi, soma: https://www.jamiiforums.com/threads...-bodaboda-na-sio-kiongozi-wa-chadema.1695825/
 

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
12,649
2,000
RIP Alex!Kwa atmosphere hii watu wakikufuata uunge mkono juhudi utakataa kweli?
 
Top Bottom