Singida: Rais Magufuli awasihi Watanzania kuchapa kazi. Corona haikuanzia Afrika na imewakoromea wote hata wale wenye uwezo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,873
Amewaponngeza Watu wa Singida na kufurahi mnama mkoa huo unavyopendeza. Amesema amefurahi kuona Watanzania wakiwa wandelea kuomba kuhusu #COVID19

Rais #Magufuli:

Janga la #COVID19 limepungua sana pamoja na kuwa bado hailijaisha.

Ndugu zangu tuendelee kuchukua hatua. Katika mkoa wa Singida kwenye vituo vyetu wamebaki wagonjwa 3 na wanaendela vizuri. Ni taarifa nzuri tuendelee kuomba na kuchukua tahadhari

Tusiongope tusitishane, na uzuri Singida hamjaogopa na hata waliovaa barakoa ni wachache, hata mimi sikuvaa hata RC kwa kuwa Mungu yupo pamoja nasi. Endeleeni kuchukua tahadhari. Ugonjwa huu ukijifungia uwezo wa mwili kupambana na magonjwa unapotea.

Sikutaka kuwafungia watu nyumbani kwa maana wanaolima mpunga wangelima nini? Wanaouza mtumba wangeuza nini? Sikufunga mtu ndani kwa Kisukuma wanasema 'lockdown' endeleeni kuchapa kazi.

Taa hizi (za barabarani) zimefungwa wakati wa COVID19. Tuchape kazi. Uchumi wetu ni muhimu kuliko kitu chochote

Kenyatta alinipigia simu nikiwa Chato. Leo pia kanipigia tumezungumza pia. Tumezungumza kama migogoro kule mipakani. Kenya ni marafiki zetu. Tumekubaliana mawaziri wetu wa uchukuzi na wakuu wa Mikoa watakutana mpakani na Kenya wazungumze hili walimalize.

Hii korona isiwe chanzo cha migogoro. Haiwezekani kila dereva anayekwenda huko awe na korona. Nawaomba viongozi wa mikoa inayopakana na Kenya wasitatue matatizo yao kwa jazba. Wazingatie uchumi wa nchi zetu.

Ninafahamu mtu ukichokozwa kidogo ukanyamaza, na wewe unachokoza kidogo. Nataka Wakenya na Watanzania wafanye biashara vizuri”

Naomba, na kwakuwa tumezungumza vizuri na Mheshimiwa Kenyatta, sisi tumeyamaliza.

Haiwezekani mtu anasafiri anaenda nchi jirani anaambiwa akae mpaka sijui siku ngapi wakati amepakia bidhaa

Korona haikuwanzia Afrika. Na imewakoromea wote hata wale wenye uwezo.

Huu ni wakati wa kujenga uchumi. Tunataka Kenya waje wachukuwe maziwa hapa. Tunataka vitunguu vya Singida viuzwe mpaka Kenya.

Tunataka Kenya mafuta ya alizeti yafike mpaka Kenya. Huo ndiyo uchumi wakweli

Ndugu zangu Madereva endeleeni kutulia kwani hili litatatuliwa na serikali zote mbili

Maendeleo ya Singida ni tofauti sana na nyuma.

Endeleeni kushikamana, Musibaguane kwa sababu ya vyama, musibaguane kwa sababu ya dini, musibaguane kwa sababu ya rangi. Sisi wote ni Watanzania na lengo letu kubwa ni kujenga uchumi wa nchi yetu.

 
Ni taarifa niliyoipata muda mfupi uliopita ila tusubiri muda utathibitisha.

Mliokula night za kutosha hongera zenu!!!
1589978799550.png
 
Back
Top Bottom