SINGIDA: Mwanafunzi wa kidato cha nne afa maji akiogelea

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Mwanafunwa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Lulumba, Lameck Jeremieh (18),amefariki dunia baada ya kuzama na kunywa maji mengi, wakati akiongelea kwenye bwawa la magereza lililopo New Kiomboi, wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi,mkuu wa wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula, alisema tukio hilo limetokea juzi saa kumi jioni huko New Kiomboi mjini.

Alisema siku ya tukio Lameck (marehemu) na wenzake 15 waliungana na wenzao 10 wa sekondari ya New Kiomboi,kwa ajili ya mazoezi ya uskauti.

Luhahula alisema kuwa baada ya kumaliza kufanya mazoezi ya uskauti, wanafunzi hao walikubaliana kwenda kuogelea kwenye bwawa linalomilikiwa na Jeshi la Magereza.

“Kiongozi wa kikundi hicho cha skauti, James Israel, aliomba kibali cha kuogelea na askari wa kusaidia kupima kina cha maji kwa uongozi wa magereza. Mrakibu wa Jeshi la Polisi, Frank Mwakijungu, alitoa kibali hicho”, alisema na kuongeza.

“Hata hivyo, kiongozi huyo wa wanafunzi aliwataka wenzake wamsubiri mwalimu Magdalena Mwagala, aje awaongoze namna ya kuogelea kwa usalama wao.”

Akifafanua, alisema baada ya mwalimu Magdalena kushindwa kufika, Lameck alivua nguo na kisha kutumbukia kwenye bwawa na hakuchukua muda, alizama chini ya bwawa na hakutoka tena.

Mkuu huyo wa wilaya, alisema wanafunzi hao waliweza kutoa taarifa kwa wananchi ambao walifika mara moja na kuanza kuutafuta mwili wa Lameck.

“Giza lilipoingia bila kupatikana kwa mwili huo, niliahirisha zoezi hilo hadi kesho yake. Hiyo kesho zoezi halikuchukua muda mrefu, mwili wa mwanafunzi huyo uliweza kuopolewa kutoka kwenye tope,” alisema.

DC Luhahula, ametumia fursa hiyo kuwataka walezi kuwakataza watoto wao kuogelea kwenye bwawa hilo mali ya magereza.

Na Nathaniel Limu, Iramba
 
Back
Top Bottom