Singida: Mkurugenzi(DED) wa Halmashauri ya Itigi adaiwa kumuua mwananchi kwa risasi

Shija amezoe kuchunga ng'ombe tu ukimpa asimamie watu anawalenga kwa risasi. Tumeona hata kwa Tundu Lisu alivyolengwa
 
Hapa ndipo watu halisi wasiojulikana (wananchi wenye hasira kali) watakapofanya yao..

Huyo mkurugenzi siku yake yaja.

Sent using Sukhoi Su-57
 
Mna
Kuna Habari ina sambaa na inasema hivi ;nna Nukuu.

Habari za jioni baada ya kufuatilia Jambo hili kwa kina nnaomba kutoa Taarifa ifuatayo kwanza Mkurugenzi mwenzetu yupo salama na ana endelea na Kazi na hakuhusika na kumfyatulia Mtu Risasi.Chanzo cha Tatizo ni kwamba kuna Wananchi na wawekezaji walipewa Mashamba ambayo ni ya Serikali kulima.Baadhi ya Wananchi wakawa wame anza kuhujumu Mashamba ya baadhi ya Wawekezaji na Wananchi kwa kuchoma Moto Vipando na Majengo ya wanao endeleza Mashamba hivyo Mkurugenzi pamoja na Mgambo walikwenda kuwa kamata Wananchi wanao haribu Mali za wenzao.

Wakiwa kwenye Eneo la Tukio Mkurugenzi aliwaacha Mgambo na kwenda kuwachukua Askari Polisi ili kuwaongezea Nguvu Mgambo.Huku nyuma baadhi ya Wananchi wakaanza kuwashambulia Mgambo ndio ktk kujitetea Mgambo mmoja alifyatua Risasi na kumuua huyo Mtu alie fariki wakati Mkurugenzi anafika na Polisi tayari tukio lilikuwa limesha tokea.

Mwisho wa kunukuu..
Mna hamisha magori tuu, na hiyo video ya R.P.C inatotambaa mitandaoni ni akina Joti wanaact au?
 
Watanzania wanataka maendeleo, maendeleo shirikishi na si maendeleo lazimishi. Huko Itigi tumesikia DED kafanya uvamizi kanisani na kufanya Mauaji ya kiumbe kilichoshindwa kulipa ushuru, yamkini alishindwa kulipa kwa sababu Ana watoto wanasoma,au kilimo hakijalimlipa msimu huu au vinginevyo.

Naamini hakustahili kufuatiliwa kanisani, hakustahili kutuatwa na timu ya watu wakiongozwa na mkurugenzi, hakustahili kukimbizwa wala kuadhibiwa kwa kushindwa kulipa ushuru bali alipaswa kuelekezwa au kuchukuliwa hatua za kisheria endapo zipo.

Kwa sababu viongozi wetu wamelelewa kwenye KUTUMIA nguvu na mabavu basi waliona ni vyema kuingia hadi kanisani kukusanya ushuru....wakati mwingine wanaingia maeneo mbalimbali Kama walivyofanya kanisani na tunawapigia makofi na kuwafanya wajione wanafanya kazi.

Leo ndugu yetu ambaye pia ni jasusi flani ametekeleza Mauaji kwa kiumbe asiye na hatia, ameua kanisani, mbele ya watoto na vijana, mbele ya waumini na mbele ya wakinamana huku akijiona anatekeleza majukumu yake.

Naamini huyu hakutumwa na mtu kuua bali roho ya Mauaji alizaliwa nayo na yamkini amewaua wengi toka utotoni mwake.

Mtu huyu alianza kisirani siku tu alipoteuliwa, ilifika hatua Mhe Rais akapiga naye picha kumsafisha KUTOKANA NA tuhuma za elimu yake, lakini pia aliwahi kumpinga bosi wake adharani Waziri Jafo kwamba amewadanganya wananchi na katika mabya yake hakuna aliyewahi kumkemea na leo ametekeleza unyama au ugaidi Kama alivyouita RPC.

Lakini pia nidhamu ya woga kwa Watanzania imekuwa kubwa ndiyo maana vyombo vya habari havijaripoti habari hii. Nadhani angekuwa DED ndiye kapigwa na wananchi front page zingeng'aa kwa habari hiyo.

Poleni wafiwa, shime kwa viongozi wetu acheni kujitwalia madaraka ya mwenyenzi Mungu. Hamkupewa madaraka muue bali mlipewa madaraka mwongoze watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nchi inapita katika bonde la uvuli wa kifo. Watendaji wanaonekana wanachapa kazi kutokana na kiasi gani wanaweza kuwa wakatili dhidhi ya wananchi.
 
Kama vyombo vya habari vimezuiwa kutangaza basi....changanya na za mbayuwayu!!! Kesi imeyeyuka kama barafu kwenye moto
 
Back
Top Bottom