Singida: Mke wa rais na Mke wa Waziri Mkuu, wawatembelea Wazee wasiojiweza wa Sukamahela

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.

Wake hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.

Wameyasema hayo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni Mkoani Singida.

Katika kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi.

Akizungumza na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka eneo hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na hakikisheni kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.

Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.

“Watanzania wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo na hiki tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada mbalimbali kkwa kadri tutakavyojaaliwa,” amesema.

Awali Mkuu wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida.

Bw. Ngoo alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja huku mahitaji yakiwa ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na zina nyufa.

Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza.
image.jpeg

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa furaha walipowasili katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017
image.jpeg

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa msaada wa vyakula tani 7.5 katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017
image.jpeg

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017
image.jpeg
image.jpeg

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na Bibi Agnes Kamota (75) walipomtembelea nyumbani kwake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida Februari 13, 2017
 
Ni mstaarab hadi anafariji lakini upande wa pili daaaa kweli nampa pole sana naamini hajja enjoy maisha yake kwa kiwango alichostahili! Mateso aliyopata MUNGU ndie anajua!! Huyu ni mwanamke kwa kweli! Heri ata alipokimbia maana alizidiwa!! Ubabe hadi kwa mkeo? Ambae ndio pambo? Sasa una entertain vimada ili iweje??? Mtoto wa mjini yule hata sio size yake!! Amemchuna vilivyo!! Zile gorofa si lingekuwa la Mama na watoto? Sasa sio lao naye sio lake! Chezea watoto watoto wa town wewe?? Ukija macho juu unapigwa cha juu
 
Kebizx
 
She is doing her duties...mnamsifia as if yeye ndiyo wa kwanza kuwatembelea hao wazee.

Nothing new,nothing special
 
Jambo jema kuwatunza wazee na wasio jiweza mungu azidi kuwapa ufahamu na kuzidi kuwasaidia wenye dhiki.
 
Ni mstaarab hadi anafariji lakini upande wa pili daaaa kweli nampa pole sana naamini hajja enjoy maisha yake kwa kiwango alichostahili! Mateso aliyopata MUNGU ndie anajua!! Huyu ni mwanamke kwa kweli! Heri ata alipokimbia maana alizidiwa!! Ubabe hadi kwa mkeo? Ambae ndio pambo? Sasa una entertain vimada ili iweje??? Mtoto wa mjini yule hata sio size yake!! Amemchuna vilivyo!! Zile gorofa si lingekuwa la Mama na watoto? Sasa sio lao naye sio lake! Chezea watoto watoto wa town wewe?? Ukija macho juu unapigwa cha juu
Nchi yetu ni ya ujamaa, uyo anacho na yeye anavyo! Starehe tupu! Hana shida yoyote huyu First Lady. Mwacheni astarehe. Ana Nyota ya Jaha
 
Sio hvo mkuu huyu mama kanyimwa haki yake kama first Lady... Naomba niishie hapa..
Kanyimwa u-first Lady kwa namna gani. Katika maisha kila mtu na hulka yake. Seh is humble. Yeye hajauvaa Urais kama mafirst Lady wengine . Yeye ndio ana jua maana ya ufirst lady maana wengine wanajifanya ndio marais wenyewe tulikwishachoka. Asante amam Janeth Magufuli!
 
Moyo wa kujitolea ulifubaa basda ya tetemeko bk
Hata hivyo tuwapongeze wake wa viongozi hao kwa kuvitaka vituo vya kulelea wazee kufikishiwa misaada walengwa kutoka kwa wadau
 
Mke wa Rais + ..... + Mke wa PM. Kuna mmoja ali-miss hapo ili timu ikae vizuri. By the way, binafsi simfahamu mwenza wa VP wetu kama ninavyowafahamu wenza wa President na PM. Mwenye japo kapicha na ka-CV kake atupie humu.
 
Mi sielewi Mara Kasimu Majaliwa Kasimu Mara mama Marry hebu nitoeni tongo tongo
 
Back
Top Bottom