Singida: Madaktari vijana watuhumiwa kuwatongoza wagonjwa wasichana na wanawake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
CHAMA Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida, kimeibua tuhuma nzito kwa madaktari wa Hospitali ya Rufaa mkoani hapa, ikiwamo madai ya madaktari vijana kuwatongoza wagonjwa wasichana na wanawake, wanaofika hospitalini hapo kupata huduma ya tiba.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Singida, Martin Lissu, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa pamoja kati ya kamati ya siasa mkoa na viongozi wa hospitali hiyo. Alisema amepokea malalamiko mara kwa mara hasa kutoka kwa wasichana kwamba wanapoingia kwenye chumba cha daktari kijana, baadhi yao hutumia fursa hiyo kutongoza.

“Mbaya zaidi, baadhi yao huwa wanawambakizia magonjwa ambayo hawana. Lengo aweze kufanikisha lengo lake ovu la matamanio ya ngono.

“Aidha wanapoteza muda mwingi na kusababisha wagonjwa wengine kuchelewa kupata huduma. Vitendo hivyo vinasababisha baadhi ya wasichana kuikimbia hospitali, jamani tunakwenda wapi,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu CCM Mkoa wa Singida, Alexandrina Katabi, alisema kuwa inafika wakati hata wagonjwa wanapofika hospitalini hapo huambiwa hakuna dawa hali ya kuwa zipo.

“Dosari zipo nyingi, tunazoziona na tunazozishuhudia. Mfano hai ni kwamba kuna kipindi tulikuwa na maiti mochwari ya hapa, ilitulazimu kuchukua saa zaidi ya 12, kuipata.

“Mhudumu wa mochwari alitafutwa kwa simu na akafuatwa nyumbani, hakupatikana, ila alikuwa Ilongero. Kwa ujumla uongozi wa hapa unapaswa kusimama imara kuhakikisha wafanyakazi wa ngazi zote, wanabadilika haraka, vinginevyo hatua stahiki zitachukuliwa,” alisema Katabi.

Mmoja wa wajumbe wa bodi ya hospitali hiyo, Diana Chilolo, alisema kero zinazolalamikiwa nyingi wamezisikia, ambapo aliahidi bodi yao itafanyia kazi dosari hizo kwa wakati.

Alisema wao wanataka kuona hospitali hiyo inafanya kazi iliyotarajiwa na Serikali ya kutoa huduma kwa ubora kwa watu wote kwa mujibu wa sheria na pindi linapojitokeza jambo ni wajibu wao kukaa na kufuatilia na kisha kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Naye Katibu Mwenezi wa Mkoa, Ahmed Athumani aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama ya kuangalia uwezekano wa daktari bingwa ambapo kwa sasa ni Sh 15,000 hadi 20,000.

Alidai kiwango hicho ni kikubwa na wananchi wengi hawana uwezo wa kumudu gharama hizo kutokana na tofauti ya kipato.

Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Juma Kilimba, alisema kuwa kwa mujibu wa ibara ya 189 ya Ilani ya uchaguzi, wanawajibika kukagua utekelezaji wa ilani hiyo ya uchaguzi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.

“Utekelezaji huu ni pamoja na kuona kama mnatoa huduma stahiki. Tuna uhakika serikali imetoa fedha kutosha kununulia vifaa tiba na madawa, kilichosalia ni ninyi kuwatendea wananchi haki wananchi,” alisema.
 
Watulie hao sasa mtu anaomba namba usiku anakupigia Au mnachati unaona kabsaa Huyu ananitaka
Kwa kwel watatusamehe tutaendelea kuwatafuna maaadam Sio wanafunzi hakuna shida

Kwa sababu hatutongozani kazin ni baada ya kazi Ndiyo tunafanya yetu

Hao wanasiasa wana wivu sanaa
Wakitaka nao wakasome fani ya udaktari waje watibu watu
Kila mahali siasa uchwara tuu hatuendishwi hivo wanavo fikiri
Tuna maadili yetu tunafuata Sio kauli zao
Sitongozi Mwanamke eneo la kazi
Tukimaliza kazi tunafanya yetu Basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Wasichana na Wanawake"
Mimi hapa ndipo nimepata kitu huko kwingine endeleeni tu.
 
Kweli taaluma imeingiliwa hii
Heshima ya doctors imeingia dosari kubwa sana



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Wanaume kuweni makini mkiwa mnawapeleka wake zenu wenye mimba hospital

Sent from my I phone
 
Back
Top Bottom