Singida: Kiwanda cha Alizeti Mount Meru Millers Ltd kimefungiwa

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
3,792
2,362
Kiwanda cha Alizeti Mount Meru Millers Ltd kimefungiwa
kiwanda+pic.jpg


Kwa ufupi
Lugola amesema kwamba kiwanda hicho kimetekeleza agizo la kununua mashine ya kutibu maji taka, lakini maji taka hayo, hayajaelekezwa kwenye mashine hiyo.

Singida. Serikali imekifungia Kiwanda cha kukamua mafuta cha Alizeti Mount Meru Millers Ltd muda usiojulikana kwa madai ya kukaidi agizo la kulipa faini ya Sh20milioni.

Uamuzi wa kukifunga kiwanda hicho umetolewa jana Jumatano na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira ,Kangi Lugola alipokuwa kwenye kwanda hicho kilichopo kijiji cha Manguanjuki Manispaa ya Singida.

Kabla ya kutoa uamuzi huo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Singida, Lugola alisema Novemba 29 mwaka jana, mtangulizi wake Luhaga Mpina, aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho ulipe faini ya Sh20milioni kwa kosa la kutiririsha maji taka yenye kemikali kwenye makazi ya watu .

“Maji taka yameelekezwa kwenye makazi ya wananchi wanaokizunguka kiwanda .Pia maji hayo yenye kemikali, yameelekezwa kwenye ziwa la Singidani lenye viumbe hai wakiwemo samaki. lakini hadi leo, agizo la Waziri Mpina, halijatekelezwa’’ amesema Lugola na kuongeza kwamba

‘’Kutokana na ukiukwaji wa sheria za mazingira, Mpina alikipa adhabu ya kulipa faini Sh20milioni ambayo haijalipwa hadi leo”, amesema Waziri Lugola kwa masikitiko.

Lugola amesema kwamba kiwanda hicho kimetekeleza agizo la kununua mashine ya kutibu maji taka, lakini maji taka hayo, hayajaelekezwa kwenye mashine hiyo.

“Maji hayo yenye kemikali bado yameendelea kuwa kero kwa wananchi hadi leo, na yanaathiri viumbe hai vilivyopo kwenye ziwa Singidani. Hii dharau kwa serikali haikubaliki”, amesema
Naibu waziri huyo, amesema wananchi wanaozunguka kiwanda hicho wamekuwa wakitoa kilio chao serikalini kwa miaka minne, kwamba wanaathiriwa na maji yenye kemikali na moshi mnene wa kiwanda cha Maount Meru.

“Binafsi leo nimefika kwenye kiwanda hiki na baada ya kufanya ukaguzi wa kina, nakiri kwamba kilio cha wananchi wa Manguanjuki ni cha kweli na kinahitaji tiba ya kudumu. Mkuu wa wilaya ya Singida, naagiza kuanzia sasa, usimamie kufungwa kwa kiwanda hiki”,amesema na kuongeza;

“OCD pia nakuagiza uwatafute Wakurugenzi wa kiwanda hiki Atul Nittal, Arvind Mittal na Tarsem Aggarwal, popote walipo na kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria kwa kukaidi agizo la Serikali”.

Kwa upande wake meneja Uhusiano, Nelson Mwakambuta, amesema kiwanda hicho kimekuwa kikifanyiwa ukaguzi mara kwa mara na mamlaka mbalimbali. Lakini wamekuwa wakiwaambiwa na viongozi hao kuwa kiwanda hicho, hakina tatizo lolote linalohusiana na kwenda kinyume na sheria za mazingira.

“Kufungwa kwa muda usiojulikana kwa kiwanda hiki, kutaathiri ustawi wa watumishi wengi wa kiwanda na familia zao. Pia wakulima wa zao la alizeti ndani na nje ya mkoa wa Singida, nao watakuwa wamepata pigo. Hatupingani na serikali tutatekeleza yale yote tuliyoagizwa”,amesema meneja huyo.

Chanzo: Mwananchi
 
HATA KAMA TUNAHITAJI VIWANDA ILA KAMA VINAKWENDA KINYUME NA SHERIA YA MAZINGIRA HATUVITAKI...
TUNAHITAJI UCHUMI IMARA UNAOENDANA NA HALI NZURI YA KIMAZINGIRA
 
Kufungwa kutaathir mamia ya watu kiuchumi ila kutaokoa maelfu ya watu kiafya
 
Sina maana sijali afya za wananchi bali naona njia za mazungumzo na mashikiano zingefaa zaidi. Njia ya kila anayeonekana hajatimiza kitu flani fungia sidhani kama ndio optimal solution.
Simply Optimize what you already have.
 
Back
Top Bottom