Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,792
- 4,444
Ofisa Elimu Sekretarieti ya Mkoa wa Singida (REO), Nelasi Mulungu alieleza kuwa kati ya idadi hiyo, wasichana wa shule za sekondari ni 15, watatu waliobaki ni kutoka shule za msingi.
Akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Singida (RCC) mjini hapa juzi, Mulungu alisema wanafunzi waliopata mimba wamepungua kufuatia ushirikiano mzuri baina ya wazazi, jamii, walimu na wanafunzi.
“Natoa mwito kwa jamii kuendelea kushirikiana na serikali ili kutokomeza tatizo hilo. Naomba wasichana wanaosoma kujitambua na kujiona wana thamani kubwa kuchangia maarifa kwa maendeleo ya familia zao na taifa,” alisema.
Alitaka kila halmashauri ya wilaya kujenga hosteli za wasichana za kutosha ili kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kasi ya ujenzi wa madarasa, maabara na nyumba za walimu ili kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu bora.
Kuhusu upungufu wa walimu, Mulungu alisema mahitaji bado makubwa na serikali itakabili changamoto kadri fedha zinavyopatikana ili kuhakikisha elimu nchini inakuwa bora zaidi.
Chanzo: Habari Leo