SINGIDA: Dereva atiwa mbaroni kwa kuachia usukani na kuanza kucheza wimbo wa msanii Darasa

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Mar 25, 2016
10,522
13,110
Dereva huyo ambaye ameonekana kwenye video akiwa anaendesha gari aina ya Coaster ambayo inafanya safari zake Dodoma kwenda itigi akiwa anafanya kitendo cha hatari cha kuacha gari likiwa kwenye mwendo na kisha yeye kusimama na kuanza kucheza muziki huo akamatwa.

Kesho atapandishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili yeye pamoja na wenzake ambao alikuwa nao kwenye Gari hilo.



Picha chini ni taarifa iliyotolewa na ROAD SAFETY AMBASSADORS(RSA)baada ya dereva huyo kukamatwa!
bf2357032cf306a7479bf40ef5700d3b.jpg


15355687_10210270825220395_181687064743187818_n.jpg

Hawa ndio wahusika walio kuwepo kwenye tukio hilo..

=======

POLISI mkoani Singida inamshikilia dereva wa gari dogo la abiria la Super Mamuu, kwa tuhuma za kuendesha kwa mwendo wa hatari.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Mayala Towo, alimtaja dereva anayeshikiliwa kuwa ni Saidi Juma (26) mkazi wa Dodoma ambaye inadaiwa siku ya tukio alikuwa anaendesha basi aina ya Nissan Civilian lenye namba za usajili T.360 DAY huku akicheza muziki.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4, mwaka huu, saa 11: 00 jioni katika Mji Mdogo wa Itigi wilayani Manyoni wakati mtuhumiwa akiwa na wenzake watatu, alipoendesha gari hilo kwa mwendo wa hatari kwa kucheza muziki huku akiachiana usukani na wenzake hao wakati gari hilo likiwa kwenye mwendo.

Kamanda Towo aliwataja watuhumiwa wengine ambapo pia wanashikiliwa na Polisi kuwa ni Joseph Ramadhan (27), Ezekiel Joseph (24) na Sebastian Godfrey (23) wote wakazi wa Majengo, Itigi.
 
elezea kidogo RSA
Kazi nzuri RSA.. Kumbuken RSA ni kama JF kila mwananchi anaweza kuwa trafiki au polisi..
Kula group za watsapp telegram na fb.
Ukishareport kama hivyo sekunde hio hio harua zinachukuliwa
 
Back
Top Bottom