Singida: Ajali inayohusisha Lori imetokea na kusababisha moto mkubwa maeneo ya Misigiri, 2 wapoteza maisha

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Habari wakuu,

Kuna ajali imetokea Misigiri njia ya Singida. Lori imekosa breki na kutumbukia mtoni. Umetokea moto mkubwa sana. Hijajulikana kama kuna vifo.

Habari zaidi stay tuned...
moto misi.JPG

Hii picha imepigwa kwa mbali kidogo, ila ntawaletea picha za karibu muda si mrefu. Samahani kwa picha ilopigwa usawa wa angle of declination.

UPDATES:

Muda huu mkoani Singida lori la mafuta limeanguka na kuwaka moto katika eneo la Mlima Sekenke na watu wawili wanaripotiwa kufariki.

-RPC Singida Deborah Magiligimba amethibitisha kutokea kwa ajali.

RPC Singida Deborah Magiligimba amesema kwamba, ajali hiyoimetokea saa nne na nusu asubuhi milima ya Senkenke Wilaya ya Iramba barabara ya Singida - Nzega.

Gari iliyohusika kwenye ajali hiyo ni namba T167 DTC aina ya Flight liner ambayo ilikuwa na Trailer namba T 960 ALS. Hili gari ni mali ya Petromac Africa Dar es salaam.

Gali iliacha njia na kupinduka ambapo ililipuka na kusababisha moto mkubwa uliopelekea vifo vya watu wawili ambao ni wanaume.

Uchunguzi wa jeshi la Polisi wa awali baada ya kufatilia kwenye mzani wa Singida, gari ilipimwa mzani wa Singida saa moja na dk 27 asubuhi dereva alikua anaitwa Erasto Abedi Rusazi na alikuwa na tingo msaidizi wake anayeitwa Ramadhani Hashim Ramadhini wote ni Wakazi wa Tabata Dar Es Salaam.

RPC Deborah Magiligimba, ametoa wito kwa madereva watii sharia za barabarani ili kuepusha ajali.
gari.jpg

lori2-jpg.723270

gari2.jpg
gari3.jpg
gari4.jpg

Mbali hivyo umejuaje kama ni gari limedumbukia.mtoni?

Misigiri ni kule kama waelekea sekenke ni pabaya mno, lakin hebu weka ushawishi zaidi juu ya habari hako

Yawezekana wanachoma nyika au mkaa unasema ajali ya gari,

Au ingekuwa ndege tungesema umeona ilivyoshuka kwa gafla toka juu, lakin wapi

Hapo sawa kama umeupdate ukaweka video
 
Gari wewe inachukulia toyota hiace yaweza kuwa gari kubwa la mafuta,

Swissme
 
Mbali hivyo umejuaje kama ni gari limedumbukia.mtoni?

Misigiri ni kule kama waelekea sekenke ni pabaya mno, lakin hebu weka ushawishi zaidi juu ya habari hako

Yawezekana wanachoma nyika au mkaa unasema ajali ya gari,

Au ingekuwa ndege tungesema umeona ilivyoshuka kwa gafla toka juu, lakin wapi
Subiri ntahakikisha nakupatia habari kamili. Yaani hapo unapaona mbali kwa kizazi hiki cha Smartphone? Nmeshangaa sana swali lako.
 
Kama hakuna vifo ni jambo jema, na vipi hapo picha ilipopigwa kuna mradi gani unaendelea
 
Picha itakuwa imechukuliwa mbali sana ,yaani huko kwenye machimbo ya dhahabu karibu na Ntwike.
Moshi unaonekana kwa mbali kati ya shelui na Misigiri
Haya ni machimbo madogo pale misigiri
Njia ya kuelekea Kiomboi,
Kuna mto pale kwenye kale ka mlima
Mwaka jana kuna familia ilipatia ajali pale.
 
Kuna jamaa kanitumia msg kama dk zimepita ila sikuwa na uhakika,

poleni sana wafiwa
 
Mbali hivyo umejuaje kama ni gari limedumbukia.mtoni?

Misigiri ni kule kama waelekea sekenke ni pabaya mno, lakin hebu weka ushawishi zaidi juu ya habari hako

Yawezekana wanachoma nyika au mkaa unasema ajali ya gari,

Au ingekuwa ndege tungesema umeona ilivyoshuka kwa gafla toka juu, lakin wapi

Hapo sawa kama umeupdate ukaweka video
We ni ndugu yake Tomaso yule student wa jesus
 
Mbali hivyo umejuaje kama ni gari limedumbukia.mtoni?

Misigiri ni kule kama waelekea sekenke ni pabaya mno, lakin hebu weka ushawishi zaidi juu ya habari hako

Yawezekana wanachoma nyika au mkaa unasema ajali ya gari,

Au ingekuwa ndege tungesema umeona ilivyoshuka kwa gafla toka juu, lakin wapi

Hapo sawa kama umeupdate ukaweka video
Huyo ni raia mwema
 
Back
Top Bottom