NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,024
- 2,486
Jambo! Hakuna matata! Nimezaliwa nikayakuta maandishi haya kwenye t-shirts na kazi zingine za sanaa hasa katika maduka ya watalii kule Moshkwetu. Yamekuwa pia kibwagizo katika matangazo ya utalii kwa miaka mingi. Sina shaka kuwa ni mali ya Tanzania. Nilijisikia fahari kusikia Hakuna Matata katika sinema mpya ya The Lion King ambapo Simba mtoto wa Mufasa alitamkiwa maneno haya na rafiki zake wawili waliompokea ukimbizini ili kumtuliza. Swali langu ni je, huko Dysney Hakuna Matata imefikafikaje? Anayewahi studio ndo mmiliki wa wimbo au bado tuna nafasi ya kudai haki yetu? Hii si mara ya kwanza kuibiwa haki zetu (japo hatuzijui sometimes) na watengeneza sinema wa mbele. Muziki wa Saida Karoli uliwahi kutumika kwenye sinema huko majuu na sidhani kama kuna mtu alimsaidia kupata haki yake. Naiomba serikali iamke. Isione ni jambo dogo. Hawa mabepari siyo wa kuwachekea. Angalia walichowafanyia Wasotho. LV kajimiliksha blanketi lao la asili katengeneza vijishati anauza dola 1000 na ushee eti kawahi studio. Tusishangae mashuka ya wamasai nayo akatokea 'designer' huko akajitwalia umiliki. Wale wanaharakati wetu, hili ni pia ni swala la haki za bindamu; siyo kukomalia siasa tu.