Sinema ya Bongoland II


PastorPetro

PastorPetro

Senior Member
Joined
Feb 25, 2008
Messages
187
Likes
1
Points
35
PastorPetro

PastorPetro

Senior Member
Joined Feb 25, 2008
187 1 35
Nimepokea hii kwa e-mail, najua hapa ni pa siasa lakini someni:

BONGOLAND II - NI JUMAMOSI HII - APRIL 5th

Hii ni kukumbusha kuwa Jumamosi ijayo (kesho), ndio uzinduzi rasmi wa sinema ya Bongoland II. Hii ni sinema iliyoshutiwa mjini Dar-es-salaam mwaka jana. Ni sinema ambayo iliwahusha wasanii mbali mbali wa kutoka Tanzania. Kama Mzee Kipara, Huyu ni mzee wa zamani sana ambaye alicheza katika michezo ya redio na umaarufu wake katika sana Tanzania bado ni wa hali ya juu.

Pia yumo Bi Chuma Selemani Mzee ambaye huko Afrika Mashariki ameshiriki katika sinema nyingi tu zilizotengenezewa pale Dar-es-Salaam. Kwa upande wa kizazi kipya kuna wasanii chipukizi wengi hasa hasa watu kama Peter Omari ambaye alikuwa mkazi wa Minneapolis na ambaye ndiye msanii mkuu katika sinema hii. Peter alikuwa katika sinema ya Tusamehe kama mchungaji. Unaweza kusoma habari za wasanii wote waliosiriki katika sinema hii hapa

Vile vile kuna wasanii chipukizi kama Shafii Abdul ambaye kusema kweli anaonyesha uzoefu mkubwa katika fani hii ya usanii.

Mwanamziki maafuku wa bongo BUSHOKE naye yuko katika sinema hii.

Katika utengezaji wa sinema hii, Kibira Films ilishirikiana na chuo kikuu cha UCLA kwa vitivyo vya filamu na Kiswahili. Wanafunzi wanane walisaidia kitaalamu katika harakati za Bongoland II pale mjini Dar.

Kwa ujumla, hii ni hatua kubwa sana kwa sababu lengo letu ni kuupamba utamaduni wa watu wa Afrika Mashariki na hasa Tanzania. Pia ni kuvionyesha vipaji vya wasanii katika sehemu za kimataifa.

Kwa hiyo sinema hii itaonyeshwa kwa mara ya kwanza hapa Minneapolis saa nane na saa kumi na moja hapa OAK STREET CINEMA

Unaweza kuona Trela ya kwanza hapa au ya Trela ya pili hapa.

Tunategemea kuwa utaweza kufika. Kwa maelezo zaidi ya uzinduzi unaweza ukayapata hapa.
 
KadaMpinzani

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2007
Messages
3,750
Likes
27
Points
0
KadaMpinzani

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2007
3,750 27 0
naweza kuwa featured kwenye hiyo movie ??
 

Forum statistics

Threads 1,236,462
Members 475,125
Posts 29,258,766