Sindano zaambukiza watu milioni 20 VVU

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92

Monday, 08 November 2010 21:28

aids.jpg.gif
Silvan Kiwale

IMEBAINIKA kuwa zaidi ya sindano milioni 20 walizotumika kuwachomwa wagonjwa katika nchi za Afrika, zilikuwa na virusi vya Ukimwi.
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti ya Reid na zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka 2009.

Tatizo hilo kwa sasa limeelezwa kuwa ni kubwa zaidi na Shirika la Afya Ulimwenguni, (WHO), limesema asilimia 50 ya sindano zote zilizotumika kuwachoma wagonjwa duniani, hazikuwa salama.

Tayari Shirika lisilo la Kiserikali la SafePoint Trust, chini ya Mark Koska likishirikiana na baadhi ya Watanzania, limeanza kushughulikia tatizo hilo kwa kusambaza ujumbe wa 'mara moja ni maisha mara mbili ni kifo.

Katika kuhakikisha kuwa ujumbe huo unafika kwa hara kwa wananchi, shirika hilo, limemteua msanii wa kundi la vichekesho la Orijino Komedy, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ kuwa balozi wake hapa nchini.

Akizungumza katika utambulisho wa shirika hilo, mmoja wa balozi wake,Catherine English wa Canada, alielezea kufarijika kwake kwa shirika kumpata balozi huyo hasa ikizingatiwa kuwa anafahamika na watu wa rika zote nchini.

Alielezea matumaini yake kuwa kitendo hicho, kitarahisisha kufikisha ujumbe kwa wananchi.

"Tumefurahi kumpata Masanja kama balozi na natamani ningejua Kiswahili, nijue alichokuwa akizungumza na kuwafanya watu wacheke,"alisema.

Kwa upande wake, Masanja aliyepachikwa jina la daktari Mgosi, alisema amefarijika kuwa balozi wa shirika hilo na kuahidi kufanyakazi bega kwa bega katika kuhamasisha wananchi na madaktari kote nchini kutotumia bomba moja la sindano katika kutibu wagonjwa.

Ujumbe wa mabalozi hao uliondoka jijini Dar es Salaam jana kwebnda kuleta mabomba ya sindano yatakayosambazwa hadi vijijini.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Ukisoma habari hii, inaonyesha dhahiri kwamba ipo kama tangazo la biashara, mana 50pecent ya bomba zina vvu, halafu ushauri Dr Mgosi (masanja) anaoenda kusambaza ni usitumie bomba moja la sindano kwa wagongwa tofauti.
Hasakama hilo bomba lina vvu hata likitumika moja kwa mgonjwa mmoja siatapata tu? Nadhani kama hilo shirika lina uhakika na utafiti wake basi shirika huska la viwango litakuwa na dosari, na vilevile njia hilo shrika gunduzi inayotumia sio sahihi.
 
Back
Top Bottom