Sindano za makalioni; wale tusiopenda /waoga wa hii kitu tukutane hapa.

Mwanzo nilikuwa sipendi japo pia nilikuwa siogopi sindano. Baada ya kupata ajali nilizizoea kabisa sindano. Tena kuna moja nilikuwa nikidungwa kwenye paja nasikia maumivu yote yameisha na ku-relax kabisa. Doctor wangu aliniambia haitakiwi kuizoea kwani inaleta u-teja na inatumika pale tu mgonjwa anapokuwa na maumivu makali sana. Mpaka sasa sindano kwangu we choma upendavyo siogopi kabisa.
 
Mimi mpaka leo nikienda hospital nikimuona doctor anaanza kuhangaika na masindano namwambia achana nayo
 
Jaah kama me yan bora unipe gunia limejaa vidonge kuliko sindano ya tak.. Alaf kuna ma nurse wapenda sifa utasiki wakijiulizisha ivi Mara ya mwisho kupaka mafuta kwenye aya makalio ni Lin ..? Maana yanafanana na vumbi LA chokaa
 
Mie sipendi sindano yoyote ile, wala dawa yoyote ile Mungu nisaidie nisiugue.

Nikiwa kidato cha kwanza mwaka 1980 niliandikiwa sindano za masaa, nakumbuka nilichoma moja tu. Zingine sikurudi tena na nyumbani walikuwa wanajua nilikuwa nakwenda kuchoma kumbe naishia njiani.
 
Aisee sindano siipendi yani niko lazi ninywe paramangret kuliko kuchomwa sindano

Kuna siku nilikua naenda kununua dawa kwenye zahanati moja hapa kitaa, docta akananishauri nipime ili nipate uhakika wa ninachoumwa kuliko kuchukua dawa bila kujua.

Nikamkubalia nikamwambia ila kwa sharti moja tu usinichome sindano. doctor akatahamaki akasema haiwezekani ukapimwa bila kuchukuliwa damu, nikamwambia kama shida yako damu basi usijari kuna kakidonda mguuni niliumia jana kama vipi tuchukue damu hapo hapo kuliko kutoboa sehemu nyingine kuniongezea kidonda cha makusudi.
 
Sasa yani uko form three afu bado bikira jamani? Unataka hiyo biology izibe?

Au kwani hapa inazungumziwa sindano ipi???
Babu unazeeka vibaya ujue, akili zimerudi utotoni kabisa , mleta uzi kasema zile sindano zinazowekwa dawa kulingana na umri Wa mgonjwa arrgh
 
Babu unazeeka vibaya ujue, akili zimerudi utotoni kabisa , mleta uzi kasema zile sindano zinazowekwa dawa kulingana na umri Wa mgonjwa arrgh
Hahahaha nisamehe mjukuu. Unajua sisi wazee wa zamani tushazoea kuongea kimafumbo. Kumbe hapa inazungumziwa sindano ya mahospitalini?

Basi hebu upelekeni huu uzi jukwaa la utabibu...
 
1- mgonjwa anatakiwa awekwe sawa kisaikolojia na arelax misuli kabla ya kuchomwa sindano
2- kabla ya kumchoma mgonjwa sindano nesi anatakiwa kumtaarifu mgonjwa eneo sindano inapoenda kutua ili asikaze misuli ya sehemu hiyo ili kutosababisha maumivu yasiyo ya lazima
3- sindano inapochomwa inatakiwa kuwa angle 90° na iingizwe kwa haraka kidogo kiasi cha nusu kichuma cha sindano kuzuia kugusa mfupa; dawa inaposukumwa kwa syringe inatakiwa iingizwe taratibu mwilini tofauti na jinsi sindano ilivyo ingizwa mwilini ili kupunguza maumivu.
4- utoaji wa sindano unatakiwa itolewe mwilini ktk angle 90°kama jinsi ilivyoingizwa.
5- mgonjwa kupewa pole na kupongezwa kwa uvumilivu
Asante sana nesi kwa kutujulisha hili
 
Hahahaha nisamehe mjukuu. Unajua sisi wazee wa zamani tushazoea kuongea kimafumbo. Kumbe hapa inazungumziwa sindano ya mahospitalini?

Basi hebu upelekeni huu uzi jukwaa la utabibu...
Hahaaaa, babu wewee enzi zenu kulikua na sindano gani zingine tofauti? ,babu nimekushindwaaa
 
Back
Top Bottom