Sindano ya kupanga uzaz zina haribu mimba?

Baba Matatizo

JF-Expert Member
May 5, 2011
334
64
Leo ni siku
za 4 mama watoto hajaona siku zake.Leo kachoma sindano ya kuzuia mimba.hawez kuiharibu mimc?NATAKA NIMPIGE TARAKA .HAKUNISHIRIKISHA.
 
Amechomaje kama hajaona siku zake?.. Usimpige talaka.. Kaeni muyamalize taratibu. Labda anasababu za kutokukushirikisha. Mna mtoto/ watoto?
 
Kwa kweli sijui, ngoja waje wataalam. Ila vyovyote vile hakuna haja ya kuachana...
 
Amechomaje kama hajaona siku zake?.. Usimpige talaka.. Kaeni muyamalize taratibu. Labda anasababu za kutokukushirikisha. Mna mtoto/ watoto?

nadhan anaogopa sana nisijue kama ana mimba.pia kuna tetesi nimezipata kwamba hizo sindano zinatoa mimba. Tuna mtoto mmoja tu.Msaada jamani
 
kamcheki DNA huyo mtoto ujue kama ni wako, ikibainika sio wako wapige wote wawili talaka-yeye na mwanae
 
kamcheki DNA huyo mtoto ujue kama ni wako, ikibainika sio wako wapige wote wawili talaka-yeye na mwanae
Tumia akili unapomshauri mwenzako. Unafikiri DNA ni rahic kama unavyojua? Au talaka ni kama barua ya kuombea mkopo benk? Acha hizo mwenzako ana matatizo makubwa yanayohitaji ufumbuzi wa kina.
 
Leo ni siku
za 4 mama watoto hajaona siku zake.Leo kachoma sindano ya kuzuia mimba.hawez kuiharibu mimc?NATAKA NIMPIGE TARAKA .HAKUNISHIRIKISHA.

Sindano ya kupanga uzazi (Depo-provera) 'haiharibu mimba'....bali 'inazuia mimba'! Unatakiwa uitumie kabla ya kupata mimba, na ukishapata mimba basi haiwezi kukusaidia kutoa hiyo mimba!

Ukichoma sindano ya kuzuia mimba yes hupati siku zako..na hudumu kwa miezi mi3 halafu unachoma nyingine. Utakapokuja taka kuzaa basi lazima ipite si chini ya miezi mitatu ndio muanze kujaribu.

Mwenza wako alikuwa anataumia njia ya uzazi wa mpango kabla ya hapo? njia gani? alipokosa siku zake alifanya kipimo kujua kama ni mja mzito (hospitali hawawezi kumchoma depo-provera wakati ana mimba)? Inawezekana alipokosa siku alijihisi ana mimba akatahayari na akapima labda, alipongundua hana ndio akaamua achome sindano ya uzazi wa mpango ili kuondoa wasiwasi in the future...je, utamlaumu kwa hilo?!

Tuliza moyo na fikra, muongee au muende huko alikopata huduma hiyo ya uzazi wa mpango ili nawe upate elimu..na msupport mkeo, kama anafikiri si muda wakupata mimba kwa sasa muelewe! Utakapomuelewa atakushirikisha tuu, lakini kama we 'cha ukali' na talaka nje nje lazima afanye mambo nyuma ya mgongo wako!
 
Leo ni siku
za 4 mama watoto hajaona siku zake.Leo kachoma sindano ya kuzuia mimba.hawez kuiharibu mimc?NATAKA NIMPIGE TARAKA .HAKUNISHIRIKISHA.

Baazi ya njia za uzazi wa mpango zina madhara kwa wanawake. Kwa mfano kwa mujibu wa taarifa ya habari ya bbc swahili, ya leo tarehe 4/10/2011, kuna njia moja inaweza kuambukiza virus vya ukimwi. Sikiliza bbc swahili kupitia tovuti hii
http://www.bbc.co.uk/swahili/
Au soma jarida la afya la lancet kupitia tovuti hii
http://www.thelancet.com/journals/lancet/article/PIIS1473-3099(11)70247-X/fulltext
 
Back
Top Bottom