Sina upendo kabisa kwa mama yangu mzazi

Duh! inasikitisha sana unaweza kuangusha mchozi...Pole sana Mkuu hayo ni mambo yaliyo nje ya uwezo wako. Mpe heshima yake kama mama yako. Jitahidi kujiendeleza zaidi na kuitunza vizuri familia yako na nduguzo pia.
 
Hii story imenifanya nishindwe cha kuandika...............ngoja nifute machozi nirudi kuandika tena maana hapa hata screen siioni

mie ndo nimeliaaa mpaka haja kubwa na ndogo zinapiga hodi... jamaanii
 
what goes around must come around believe me .
mimi huwa naamini kuwa mtu aliyeau anayenikwaza ni bora nikae nae mbali kuliko niendelee kumwona nitamsamehe ila nakaa mbali naye kabisaaaaaaaaa;
pia katika maisha nasikiaga wakubwa wakisema sio manawake wote ni mothery material hii alisema Tuko one day
 
Last edited by a moderator:
Ila kuna umuhimu wa kupunguza mazoea hata kama utamsamehe
Kuna watu wengine chuki zao haziishi haraka
Asike akakudhuru wewe au wanao.

Hajaniambia chochote taarifa ya ujio wake ni wa nini ameniambia wife kuwa anataka kwenda nyumbani kwao na mke wangu maana mwaka jana mwezi wa kumi mke wangu alifiwa na mama yake mzazi.
 
pole sana.
unajua najiuliza maswali mengi sana kichwani.
huyo mama sijui anajua kuwa aliwakosea na anahitaji kuomba msamaha kabla hajajiingiza kwenye kitu chochote kinachohusu maisha yenu?
sijui anajisikia tu kuwa yeye kwa vile ni mama basi ana mamlaka tu na maisha ya wanawe kwa vyovyote vile?
 
WanaJF wenzangu natumai hamjambo kabisa.Ni story ndefu sana ila nitajitahidi kuifupisha.Ni mkasa (ugomvi) ulioikumba familia yetu kuanzia mwaka 2000 kati ya mama yangu na baba yangu.Kwa asilimia mia moja ugomvi huo ulisababishwa na mama nasema hivyo kwa sababu vituko alivyoanza kumfanyia baba tulikuwa tunaviona ilipelekea aliwahi kutoka nyumbani na kwenda kuishi Mwanza pasipo baba kujua alipeleleza hadi hapo alipogundua kuwa yuko mwanza ndipo alipochukua jukumu la kumfuata alimsihi sana arudi nyumbani aje kuwalea wadogo zangu akakubali kumbe ilikuwa danganya toto aliporudi hakukaa zaidi ya miezi sita akaondoka tena ila kwa kipindi hiki sasa baba aliamua kutomfuata tena akasema kwa kuwa sii mtoto mdogo siwezi kumlazimisha.Katika ugomvi huo sikuwahi siku hata moja kumuona baba ameinua mkono wake kumpiga mama yangu.Yote hayo yalisababishwa na mama kuwa na hawara mimi na dada yangu ninayemfuata kwa mara ya pili tulikuwa tunachukizwa sana na vitendo vile ambavyo mama alikuwa anamfanyia baba na hiyo ilisababisha mama kunichukia mimi na dada yangu akidai sisi ndio tunampatia baba taarifa ya yale anayoyafanya.Ninachomshukuru sana baba yangu alitumia sana busara kukabiliana na hali ile kwa sababu ilifikia wakati baba aliingiwa na mawazo ya kutaka kuua kutokana na dharau zile alizokuwa anafanyiwa.Ilipofika mwaka 2004 mama aliondoka moja kwa moja akimwacha mdogo wetu wa mwisho akiwa darasa la kwanza.Kitendo hicho kilimuumiza baba na hata sisi,pia upande wa kielimu ilituatiri sana kwa kipindi hicho nilikuwa kidato cha tatu. Ilikuwa tukitoka shule ndio tunajiandalia chakula au wadogo zangu waliokuwa wanasoma shule ya msingi tulikuwa tunakuta wamepika halafu wametubakizia chakula wao wamerudi shuleni.Mwaka 2005 Nilihitimu kidato cha nne ila kwa bahati mbaya sikuweza kuchaguliwa kuendelea na masomo sikukata tamaa niliamua kuingia mtaani kujifunza mambo ya ufundi wa umeme na masuala ya IT ambayo kwa kiasi ninayamudu pia mimi ni installer wa hizi dishi za satellite za tv.Nikiwa na ndoto mbili 1.kuwa na uelewa mkubwa zaidi juu ya masuala ya IT au 2.Kuwa oparetor wa ile mitambo ya kulima barabara.Mwaka 2008 niliamua kuoa nimejaliwa kupata mtoto mmoja.Mwaka 2009 mdogo wangu anayenifuata kwa mara ya pili alihitimu kidato cha nne alikuwa na uwezo mzuri sana shuleni alipatwa na ugonjwa tulimpeleka hospitali tulimuuguza kwa kipindi hicho chote tukiwa na baba ila kabla matokeo hayajatoka ambapo hapo baadae matokeo yalitoka akawa amefaulu kuendelea na kidato cha tano ila kwa mapenzi yake mola alimchukua mdogo wangu alinifia tukiwa naye wodi nakumbuka aliniambia KAKA YANGU SIJUI KAMA NITARUDI NYUMBANI NAOMBA UWASALIMIE WADOGO ZANGU NA MAMA KAMA ATAKUJA KWENYE MAZISHI YANGU kauli hiyo huwa inaniumiza sana kila ninapoikumbuka.Ilipofika saa kumi jioni mdogo wangu alifariki.Tulishughulikia taratibu za mazishi tulimzika mdogo wetu bila ya mama kuhudhuria mazishi ya mwanae.Baada ya miezi miwili sijui ni nani alimpa taarifa ndio akaja kuliona kaburi la mdogo wetu.Na juzi amekuja amefikia kwangu yaani nampa heshima tu ya mama ila kiukweli simpendi kabisa.

pole xana hilo nitatizo langu pia kwa upande wa baba.nina story inayofanana na hyo.
 
Poleni sana, ila mama ni mama, huna mwingine, jikaze endelea kumheshimu
 
Mwombe MUNGU sana atayafanya yatakuwa mepesi kwako utakuwa na roho ya kusamehe,POLE SANA
 
Hii ndio theme ya huu uzi, na umeweka story ya mama yako ili watu wawe na sympathy juu yako, if kweli, msamehe mama yako, na kama ni uongo ila ni story tu ya kutafuta kipato basi wewe ni zaidi ya msanii.
 
Toka asubuhi nachungulia na kutoka humu. Yaani sina ushauri positive hata kidogo. Mie sinaga mswalie mtume na hizi issue za kutelekezana. Msamehe ili roho yako ipone, lakini keep distance naye! Wekeza kwa baba yako kama return ya kuwatunza na sacrifice zote. Duh! Pole bana!
 
Hii ndio theme ya huu uzi, na umeweka story ya mama yako ili watu wawe na sympathy juu yako, if kweli, msamehe mama yako, na kama ni uongo ila ni story tu ya kutafuta kipato basi wewe ni zaidi ya msanii.

Sina chochote cha kukujibu ndugu yangu pia sijaja hapa kusimulia ili nionewe huruma ili nisaidiwe na hapa nilipofika si kwa msaada wako zaidi ya kukwambia nilichokiandika ndicho kilichonikuta na nilichonacho ndani ya maisha yangu na kama ningelikuwa nahitaji kuigiza nisingesita kwenda huko kwa wauza sura.
 
She might have not been herself!
Msinitolee mimacho hasa Kongosho na King'asti; nasema hivyo kwanini; real shit do happen. Nimeona far worse things (shuhuda) kuliko hiyo kwenye TV (Emmanuel). Yaani mama anaattempt kuuwa watoto wake mwenyewe, as a result ya evil spirit iliyomuingia at one point of her life; during deriverance lipepo linasema kila kilichokuwa kinatendeka and how, baada ya kuombewa na lispirit kumtoka anakuwa mtu mwingine kabisa.

Sina explaination yoyote ya mama mwenye akili zake timamu kuikimbia familia kwa kiasi hicho, it has to be the work of the devil.

Kaka kama unaamini, jaribuni kusali kwa imani yenu na kumuombea huyo mama yenu hiyo roho imtoke; sio tu mtakuwa mmemsaidia yeye lakini na familia yenu pia.
 
Last edited by a moderator:
Ila kuna umuhimu wa kupunguza mazoea hata kama utamsamehe
Kuna watu wengine chuki zao haziishi haraka
Asike akakudhuru wewe au wanao.
unajua sisi wazazi tuna-take advantage ya nafasi zetu kwa watoto. kuna wakati tunawaumiza sana watoto wetu, tena sometimes kwa makusudi kabisa halafu tunategemea baadae watoto waku-treat vizuri sababu tu wewe ni mzazi
 
She might have not been herself!
Msinitolee mimacho hasa Kongosho na King'asti; nasema hivyo kwanini; real shit do happen. Nimeona far worse things (shuhuda) kuliko hiyo kwenye TV (Emmanuel). Yaani mama anaattempt kuuwa watoto wake mwenyewe, as a result ya evil spirit iliyomuingia at one point of her life; during deriverance lipepo linasema kila kilichokuwa kinatendeka and how, baada ya kuombewa na lispirit kumtoka anakuwa mtu mwingine kabisa.

Sina explaination yoyote ya mama mwenye akili zake timamu kuikimbia familia kwa kiasi hicho, it has to be the work of the devil.

Kaka kama unaamini, jaribuni kusali kwa imani yenu na kumuombea huyo mama yenu hiyo roho imtoke; sio tu mtakuwa mmemsaidia yeye lakini na familia yenu pia.
Ni kweli kabisa Kaunga, lakini huyu kasema kabisa kuwa mama alipata penzi jipya, akaamua kulimwaga la babake. na kwa vile hakuja na mtoto pale basi akamwachia na wanae, isiwe tabu
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma hii post na utu uzima wangu huu nimelia. Nasema mama siku zote ndiyo kitovu cha watoto na mama kweli kama una uchungu na watoto wako huwezi kuwaacha come shine come rain. Kitendo cha mama yule kuacha watoto aende kwa bwana bila hata kuwachukua basi ni kwamba hana upendo na wanawe. Aliweza kupata usinginzi kweli? Mzazi yeyote awe baba au mama unapokuwa na watoto kuna bloody attachment ambayo hata ukiwa mbali na familia ni lazima uikumbuke? Yeye mama huyu hakuwa na muda wa kukumbuka watoto wake? Toba rabi, msamehe bure Mungu angu ila mimi kama Zogwale sitakaa nimsamehe mama kama huyu. Acha nife na dhambi hii. How can you leave behind your own children, tena wadogo huyo wa darasa la kwanza si alikiwa 6-7 years?? How dare, how dare. Liwalo na liwe simpendi mama huyu.
 
Pole sana ndugu KIBURUDISHO kwa yaliyowakuta,

Sie tulifundishwa kutoingilia ugomvi wa wazazi....kwa sababu wanayogombania chumbani kwao kamwe huwezi kuyajua!

Kwa sasa umekuwa mkubwa, nakushauri usijitafutie laana ya mama...Kwa hiyo, unatakiwa kumsamehe ili upate nafasi adhimu ya kujua walau mambo kidogo yaliyomfanya akakengeuka kiasi hicho...Naamini unaweza kujikuta mdomo wazi akiamua kukusimulia ugomvi wao na baba yako in her own perspective!!

Mama ni mama na hakuna mwingine.....Uwe mwangalifu sana!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Hii ndio theme ya huu uzi, na umeweka story ya mama yako ili watu wawe na sympathy juu yako, if kweli, msamehe mama yako, na kama ni uongo ila ni story tu ya kutafuta kipato basi wewe ni zaidi ya msanii.

Kwa uandishi wa hii post, kisa ni cha kweli na mwenye kuleta post ameumizwa moyoni hivyo anahitaji majibu ya faraja kwa kiasi fulani.. Binafsi nimemwambia siwezi kumsamehe mama kama huyu maana akina mama wanatakiwa wawe na huruma hasa kwa watoto wao.
 
Ni kweli kabisa Kaunga, lakini huyu kasema kabisa kuwa mama alipata penzi jipya, akaamua kulimwaga la babake. na kwa vile hakuja na mtoto pale basi akamwachia na wanae, isiwe tabu

Mdogo wangu Fixed Point,

Watu si wanasema hapa kila siku kuwa mwanamke hawezi kuanza kucheat bila sababu?? Kwa nini huyu tusimpe benefit of doubt kwamba inawezekana kuna kitu kilimtokea na kumharibia her mental soundness??

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom