Sina kazi wala kipato chochote; nadharaulika na ndugu zangu

Mimi ni graduate ninaye hold Masters Degree ya Public Administration.

Kinachosababisha nitamani dunia ifike mwisho ni namna ambavyo nadhaurika na kunyanyaswa na ndugu zangu na jamaa zangu, sina kazi, sina kipato.

Naombeni wana JF wenzangu mnisaidie mwenzenu. Nilipokuwa nafanya kazi project imemaliza muda wake Tanzania.

Ahsante sana
Yaan una madegree yote hayo bado unalalamika maisha magumu?!,je alieishia la 7 ambae hana upeo wa maisha yalivyo atasemaje
 
Pakti moja ya sigara Embassy inauzwa kwa bei ya jumla Tsh.3250/= bei ya rejareja ni tsh.250@zinakaa sigara 20. Ukinunua pakti 2 na kuziuza zote,utapata tsh.10000/= ukitoa mtaji ambao ni tsh.6500/= utabaki na faida ya tsh.3500/= hiyo ni item moja tu ndogo. Maji ya kunywa ya uhai kwa mfano,bei ya jumla kwa katoni ni tsh.2400/= bei ya rejareja ni tsh.600@ yanakaa 6. Kila katoni utapata tsh.1200/=na maji ya speed sana,unaweza kuuza kwa siku mpaka katoni 15. Na si lazima uwe na mtaji wa katoni 15,kwa sababu maji ya jumla yapo kila mahali. Ukiweka pipi,biscuit,soda za take away nk. Kwa siku utatengeneza faida isiyopungua tsh.35000/= ambayo kwa mwezi ni zaidi ya 1ml. Mtaji wa hi biashara haufiki laki 5. Na hakuna gharama za lesseni wala Kodi ya frem. Tafuta mwamvuli wa tigo ambao ni bure,tafuta eneo stand za daladala uweke. Hii kazi itakufanya milionair baada ya miaka 3 tu...!
Achual swal kauliza yy lkn lime2wakilisha wa2 weng.
Broo".. umeongea in fact->thnk
 
Ulipokuwa nazo ni je uliwatenga? Ukajihisi wewe ndo wewe? Yamekufika pia vumilia kama kweli uliwafanyia sivyo.
 
Tafuta pesa mkuu, siku moja watakusalimia kwa heshima...
Huna kipato, wala kazi lakini una Akili na Elimu; tumia akili na elimu yako kutatua changamoto zinazokukabili...
Kazi ya Dunia ni kumeza, ukizubaa itakumeza kweli....
 
Mimi ni graduate ninaye hold Masters Degree ya Public Administration.

Kinachosababisha nitamani dunia ifike mwisho ni namna ambavyo nadhaurika na kunyanyaswa na ndugu zangu na jamaa zangu, sina kazi, sina kipato.

Naombeni wana JF wenzangu mnisaidie mwenzenu. Nilipokuwa nafanya kazi project imemaliza muda wake Tanzania.

Ahsante sana
Stupid guy. Una masters halafu huwezi kujiongeza mpaka uajiriwe ? Alokwambia kuna ajira awamu ya tano ni nani ? Awamu hii ni kupunguza wafanyakazi. Kutumbua majipu na bomoa bomoa. Ni pm nikusomeshe jinsi ya kujikwamua kimaisha. Ajira itakufanya utimize malengo ya aliyekuajiri na sio malengo yako. Kama huna malengo ktk maisha wala usini pm
 
Waliofanikiwa si kwamba wote walisaidiwa na ndugu na jamaa zao ...Wengine walifanikiwa kwa sababu walitengwa!!
Pambana!
 
Nilikua nauza sabuni za kuogea za lungu family na mo soap natembeza mtaani mitaa ya kawe kinondoni msasani .wengi wananifahamu sana nauza Sabuni tatu 1000 . waliniona mjinga sana mi nilikua napiga had 50000 KWA siku na sasa nimeacha ile biashara nina duka GESI na bodaboda yg na nimejenga salasala .vijana tusidharau kazi
 
Nilikua nauza sabuni za kuogea za lungu family na mo soap natembeza mtaani mitaa ya kawe kinondoni msasani .wengi wananifahamu sana nauza Sabuni tatu 1000 . waliniona mjinga sana mi nilikua napiga had 50000 KWA siku na sasa nimeacha ile biashara nina duka GESI na bodaboda yg na nimejenga salasala .vijana tusidharau kazi
hongera
 
Ulimwengu una maajabu Mi nadalasa langu LA saba sijawahi kuwa Na mawazo hayo. Tuliza akili kijana wengi wasomi wa Leo wanataka mambo makubwa sana Tena gafla. Kuna jaamaa zangu nilimaliza nao la 7 wakasikia niko dar hapa wakanitafuta nikakutana nao mlimani city kilicho nishangaza walevi siku Hiyo walinitia shot ilanikajikaza kisabuni kumbe hata hella hawana nikalipa bill. Sasa walipo pajaua nyumani ikawa baalaa. Kifupi hawaishi maisha halisi wanataka mambo kwa haraka mno. Tena wakitutana na wenzao ooh Mi Niko TPA gari nzuri. Tulia mambo mazuri yanakuja kikubwa uwe mzima na usiwe teja maaana huko mipango yote inakufa kifo cha asili.
 
Pole io ni kawaida. Ukikosa hela hata mbwa wako atakung'ata.
Biblia pia inasema " maskini huchukiwa na ndugu zake".
 
Pole sana ila ni mapito tu hayo omba sana Mungu au kama kuroga roga sana
 
Wimbo wa zamani sana wa Wu Tang Clan tukiwa tunasoma Msalato
Hapana Kiongozi.

Hao ni DEAD PREZ, na wala si WU-TANG.

Watu wengi hawawafahamu Wasanii wa Sampuli hii, sababu hawavumi ila wanakuwa wakali sana.

DEAD PREZ ukiacha SCORE.

Walivuma na Kibao chao cha kuitwa MIND SEX.

Vibao vyao vingine vikali ni HIP HOP.

Na bila kukisahau Kibao chao matata sana ambacho mie HARUFU nakikubali kupita maelezo.

Kibao chenyewe ni cha kuitwa THEY SCHOOLS
 
Back
Top Bottom