Sina imani na Magufuli ila bado naamini CCM ni chama bora kabisa

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,444
25,358
Ingawa kuna mambo mengi yanayotokea ndani ya chama cha mapinduzi ambayo kwa kiasi fulani yanachangia maisha kuwa magumu kwa watanzania wengi ila bado naamini na naendelea kuamini kwamba CCM bado ni Chaka bora kabisa ila kinachoifanya CCM ionekane mbaya ni mwenyekiti wake ndugu John Pombe Magufuli

Magufuli kwa kiasi kikubwa anachangia kukiongezea maadui chama cha mapinduzi kwa uongozi wake wa kidhalimu unaokiuka haki na sheria.

CCM walifanya kosa kubwa sana ambalo litawaghalimu kwa kipindi kirefu kwa kumsimamisha huyu kiumbe awe mgombea wao wa kiti cha urais

Ndani ya CCM bado kuna viongozi wengi wazuri ambao wana sifa ya kupewa dhamana ya kuongoza taifa ,mfano wa viongozi hao ni kama vile Kasimu Majaliwa ,Hussein Bashe nk

Sidhani vyama vya upinzani mpaka sasa kama wanapaswa kupewa dhamana ya kukabidhiwa kiti cha urais ,bado sijaona mtu mwenye sifa zitakazonishawishi nimpe kura kwa kweli .

Mtu kama mbowe naona hana tofauti na huyu Magufuli ,wote wana asili ya udikteta ingawaje udikteta wa magufuli umezidi na unaonekana wazi wazi .

Mwisho kabisa napenda kuwashauri CCM wasikubali kumsimamisha Magufuli 2020 awe mgombea wao wa kiti cha urais wataanguka vibaya sana tena sana na kuna uwezekano wasipewe dhamana tena ya kuongoza nchi kwa kuwa chama pinzani kitakachopata ushindi kuna uwezekano mkubwa wqkishaingia madarakani wakabadili katiba na kutengeneza mazingira ya kuwawezesha kudumu katika uongozi

Bado wananchi wengi tuna imani na CCM kuwa ni chama kizuri ila kuna kasoro zinabidi zirekebishwe ili kurudisha imani kwa wananchi kama vile kutompa dhamana ya kugombania kiti cha urais na kama kuna uwezekano hata nafasi yake ya uenyekiti wamtoe kwa kutozingatia maadili ya uongozi.
 
mbowe ushawahi kumpima wapi, mutaisoma namba labda cha kushauri wagombea wote wapimwe magonjwa ya akili kwanza
 
mbowe ushawahi kumpima wapi, mutaisoma namba labda cha kushauri wagombea wote wapimwe magonjwa ya akili kwanza
Mbowe naye mbabe mbabe tu ,tukimkabidhi nchi tumekwisha kwa maana atatumia rasilimali za nchi kujinufaisha
 
lakn hebu nambie kuna cr gan kati ya czonje na bashite, mbon wengne kawatumbua ye ana nn
 
Nimependa na kukubali sentesi yako moja kuwa "CCM ni chaka bora kabisa ") hata mi nakubali hili chaka la wezi,majambazi, mafisadi
 
Very interesting, yaani una imani na chama ambacho kinasurvive kwa kuiba kura, naona uko kazini wewe.
 
Ushauri
Ingawa kuna mambo mengi yanayotokea ndani ya chama cha mapinduzi ambayo kwa kiasi fulani yanachangia maisha kuwa magumu kwa watanzania wengi ila bado naamini na naendelea kuamini ..........................................Mwisho kabisa napenda kuwashauri CCM wasikubali kumsimamisha Magufuli 2020 awe mgombea wao wa kiti cha urais wataanguka vibaya sana tena sana na kuna uwezekano wasipewe dhamana tena ya kuongoza nchi kwa kuwa chama pinzani kitakachopata ushindi kuna uwezekano mkubwa wqkishaingia madarakani wakabadili katiba na kutengeneza mazingira ya kuwawezesha kudumu katika uongozi.................

Ushauri wako ni mzuri ila vema kama ungepeleka sehemu husika ya CHADEMA
 
Ati ni sawa na kusema sina imani na bakhresa ila Bidhaa zake ni boora kabisa, CCM ni genge la wahuni
 
Unalinganisha kwa kuangalia utawala upi uliopita? Chama gani zaidi ya TANU, AFRO SHIRAZI na CCM ambacho kilishashika dola? Ungekuwa umeona huyo Mbowe unayemwita dictator amekuwa mwenyekiti wa chama na akawa na Rais ambaye amefanya madudu kama tunayoona ungesema heri kurudi CCM.

Yawezekana ni kati ya watu mnaowekewa video za Rwanda na Somalia kila uchaguzi unapokaribia. Alifanya hivyo Mzee Mengi 1995, 2000 kwenye ITV na watu waliogopa wakaambiwa upinzani utamwaga damu. Tangu chaguzi zote nani wanamwaga damu kama siyo viongozi au mashabiki wa wapinzani? Mwenyekiti wa Geita Chadema alifanywaje, Mwangosi, Dr. Mvungi je wakasingizia wezi ambao waliondoka na laptop tu je, woga upo kwenye upinzani? Mzee Mengi ulifanyia kitu kibaya upinzani na ukweli uwe unakumbuka uliyofanya kila uchaguzi ulipokuwa unakaribia sababu wewe ndo ulikuwa na coverage kubwa kuliko tv yoyote wakati huo.
Kuna kimama kimoja wakati wa kampain kagera kilisimama kikaanza kuwaambia watu eti msidhubutu kupa upinzani kura tukumbuke ya Rwanda. Je tangu Lwakatare awe mbunge Bk Mjini kuna damu gani imemwagika? Sasa hivi usafi na mipango ya huko nasikia ni mizuri. Arusha, Moshi angalia wanavyopeta kimaendeleo na kila kitu. Mbeya mjini je, Iringa kwa Msigwa? Kawe je? Damu gani imemwagika kwenye upinzani zaidi ya wapinzani wenyewe kuwa wahanga?
 
We mzima kweli? mbona hatra unachoandika ni ufyongo? Kweli fisiem inaweza kuonmgoza tena ktk zama hizi? umetoka shimoni leo au? Tambua kuwa Fisiem wako kwa ajili wizi wa kura, vitisho, gilba, uongo, unafiki na undumi la kuwili.
 
WanaCCM bana watu wa ajabu sana, juzi mlisema mna imani na Magufuli na sio CCM leo tena hamna imani na Magufuli lakini bado mna imani na CCM chama ambacho mwenyekiti wake ni Magufuli.
 
Ni sawa na kuuamini mti unatoa matunda alafu unayakataa matunda yake na kusema ni sumu

Ukipenda boga penda na ua lake
 
Back
Top Bottom