Sina Imani na Jeshi la Wananchi wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sina Imani na Jeshi la Wananchi wa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukolo, Feb 21, 2011.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu wana JF, naomba mwongozo. Hivi inapotokea wananchi wamekosa imani na jeshi lao wanapaswa kufanya nini?
  Mimi sina imani na jeshi la wananchi, kwa bahati mbaya mimi si mbunge, vinginevyo ningepeleka hoja binafsi bungeni. Na kwa sababu hiyo napenda niweke hapa sababu zangu za kutokuwa na imani na jeshi letu.

  1. Jeshi la wananchi ni jeshi la ulinzi wa nchi lenye jukumu la kulinda uhai wa watanzania na mali zao dhidi ya uvamizi wa wageni. Jeshi hili pia hubeba jukumu la kuokoa maisha ya watanzania pale wanapopatwa na maafa mbalimbali kwa kutumia mbinu na vifaa mbalimbali vya uokozi kama vile helikopta na vitu kama hivyo. Cha kushangaza jeshi hili limegeuka na kuwaua raia wake badala ya kuwalinda. Jeshi la wananchi wa tanzania limekuwa na kashfa za mara kwa mara za kuwapiga na kuwaua raia, na sasa kuruhusu mabomu yalipuke na kuwaangamiza watanzania wasio na hatia. Ninasema kuruhusu kwa kuwa naamini kwamba milipuko hii imetokana na uzembe wa jeshi katika kuzidhibiti silaha zao
  2. Jeshi la wananchi ndilo linalozijua silaha zake na madhara yatokanayo na silaha lilizonazo. Cha kushangaza tangu milipuko imeanza hadi imekwisha, jeshi halikuchukua hatua zozote za kuwatangazia wananchi wake juu ya nini cha kufanya katika harakati za kujiokoa dhidi ya mabomu yale yaliyokuwa na milipuko ya kuogofya. Jeshi pia lilishindwa kuwaelekeza watanzania wa gongolamboto na maeneo ya jirani watulia majumbani mwao siku ile ya pili baada ya mabomu kutulia. jambo lililowasababishia wananchi usumbufu mkubwa sana wa kuishi uhamishoni. Katika hili mimi naliona jeshi la wananchi kuwa ni katili na korofi dhidi ya watanzania ambao limepewa jukumu la kuwalinda.
  3. Jeshi la wananchi ndilo linalonunua na kuhifadhi silaha za kivita ambazo sisi wengine hatuzijui. Hakuna raia mwenye uelewa wala ufahamu juu ya silaha hizo za jeshi. Iweje leo jeshi liseme halijui kilichosababisha milipuko iliyotokea gongo la mboto. Na iwapo halijui, ina maana kwamba halina uwezo wa kuizuia hiyo milipuko mahali pengine nchini? Je Jeshi litatuhakikishiaje kwamba wale watanzania wanaoishi karibu na Lugalo, makuburi, kunduchi, mgulani, kisarawe, kigamboni na hata upanga, wapo salama? Kama hawajui kwanini silaha zinalipuka, je haimaanishi kwamba hata huko kwenye kambi nyingine (mikoani) mabomu yanaweza kulipuka na kuangamiza roho za watanzania, pasipo maelezo? Na je kusema kwamba hawajui kwanini zimelipuka hakumaanishi kwamba hawa wanajeshi wetu hawana utaalamu wa kutosha dhidi ya mabomu wanayomiliki? Na iwapo hawana utaalamu, ni kwa vipi wataweza kuyatumia pale itapotokea adui ametuvamia? Napata shaka kwamba hili jeshi letu halina uwezo.
  4. Kitendo cha milipuko ya mabomu kujirudia katika kipindi cha miaka miwilii tu ni dalili kwamba jeshi halijali maisha ya watanzania na wala halioni umhimu wa kulinda silaha zake ili kulinda maisha ya watanzania. Kama jeshi limeshindwa kuchukua hatua mhimu za kuzuia mauaji na uharibifu mwingine kama ule wa mbagala kujirudia tena, ni dhahiri kwamba jeshi letu hili si la wananchi tena bali ni la watu binafsi na linatekeleza maagizo ya watu fulani kwa maslahi yao binafsi.
  Nina sababu nyingine nyingi ambazo nitaendelea kuziweka hapa mezani kwa kadri ya nafasi itakavyoniruhusu. Lakini ukweli ni kwamba sina imani na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sasa.

  Lukolo
   
 2. n

  nyantella JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Unaishi wapi?
  ila kazi zinazozofanywa na JWTZ ni nyingi sana hata hao viongozi wako wanajua hilo hospital za jeshi hapa nchini zinahudumia wananchi wote bila kuabagua, juzi juzi railway iliboboka huko kilosa wanajeshi walikesha usiku na mchana kulijenga.

  amini usiamini hii ni ajali, watu wamekufa kweli lakini kumbuka ajali za mabasi zinauwa watu wengi zaidi ya hiyo milipuko, na maderevava sii wanajeshi.

  halafu unadai eti huna imani na jeshi, its fun kwa sababu haijatokea duniani, na jeshi siku zote ni neautral na likiasi ni balaa zaidi. in short usiwe na mawazo kwamba eti uongozi wa nchi ukibadilika jeshi litafutwa muanzishe lingine, si rahisi hata kuifuta polisi, kwani ujuzi walio nao utapeleka wapi?

  in short hukufikiri rationally wakati unapost thread hii, kwani kumbuka ajali huja kwa njia mbali mbali, sunami, tetemeko la ardhi, mafuriko, ajali za magari n.k. na yote hupoteza maisha na mali. so think as a great thinker na sii kama mtoto wa primary.

  wewe hata
   
Loading...