Sina imani na Division 1.7 wanazopata wanafunzi siku hizi kidato cha nne

Tupac alikuwa ni mkali sana wa kutunga mashairi yake na kuflow hadi free style.

Hakupiga pesa nyingi ssna

Drake sidhani kama anamfikika hata robo Tupac ila anagonga ngawira kikuda sana!

Unadhani tatizo liko wapi?
 
Ungepita shule kadhaa za A level kuona maendeleo yao kabla ya kufanya conclusion. Hao div1.7 ni very smart mkuu, usiwachukulie poa.
 
Matokeo ya kidato cha sita ya mwaka jana ilikuwa kituko...walipika hadi serikali ikajistukia sema hakukuwa na namna Mfalme ilikuwa lazima afurahishwe tu
 
Kama sikosei, enzi zetu A ilikuwa inaanzia 81%, B 61%, na C 41%. Kwa sasa kuna uwezekano A inaanzia 70%.
Kwa sasa A inaanzia 75 C 45 B 65 D 30 pia kuna vitu vingi wamebadilisha kuanzia muundo wa mtihani ,mfano kidato cha pili ili ufaulu kwenda kidato cha tatu ukiwa na D mbili unafaulu lakini zamani walikuwa wanatumia wastani pia kidato cha nne mitihani ni rahisi kiukweli tofauti na zamani
 
Zile one simple sana kizipiga mkuu. Ungesoma english medium ungepiga tu. Alafu inaonekana hata watoto wako home work ufuatilii home work. Mtoto wa darasa la nne anasoma science ya form three kwann usipige one?
Simple minded folk
 
Wakuu leo nipo kisomi zaidi kuongelea hili suala la kitaifa.

Wote ni mashahidi wa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 yalivyosheheni division 1.7 karibu kila shule. St Francis Mbeya ilikuwa nazo nyingi sana. Kama ni za kweli na za haki nawapongeza NECTA, Waalimu, Wanafunzi, Wazazi na wote waliohusika kupatikana. Hakika ni matokeo ya kimbunga.

Ila mimi nina mashaka makubwa na matokeo hayo. Kwa tuliosoma miaka ya nyuma hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 mtakuwa mashahidi ilivyokuwa ngumu kupata Division One za 7,8 na 9. Sisi tuliziita one za digit. Ni wakali wachache walikuwa wakizipata. Matokeo yakitoka one zinakuwa nyingi ila za 7 ni chache mno. Kwa mfano Ilboru, Mzumbe na Kibaha zilikuwa zinatoa one nyingi mno ila hizo za 7 ilikuwa ngumu kuwepo nyingi.

Na waliokuwa wakizipata walikuwa ni wale magenius wa ukweli au wale ambao walikuwa na bidii ya kusoma karibu muda wote. Kuna majamaa walikimbiza kuanzia o-level hadi UDSM. Sisi wengine tulipiga tu One za kawaida. Wengi kuanzia one ya 12 hadi 17. Je, miaka ile wanafunzi hawakuwa na akili kama wa sasa? Hawakuwa na jitihada kuliko wa sasa?

Kwangu mimi inawezekana kweli zimepatikana kihalali. Pia nahisi zile tetesi za baraza "kupanua goli" ni za kweli. Kama kweli walipanua goli itakuwa jambo la kusikitisha mno. Ni kujidanganya. Mimi kwa leo nimepost tu wasiwasi wangu ila muda utatupa majibu sahihi kuhusu hawa watoto wetu.
Roho mbaya tu
 
Back
Top Bottom