Sina imani na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sina imani na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rimbocho, Jun 19, 2011.

 1. r

  rimbocho Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nimekuwa nikifuatilia sana hoja na mijadala mbalimbali pale mjengoni, nilichoweza kukiona mpaka leo ni kuwa hakuna hoja ya kumtetea mwananchi wa tanzania hata moja ambayo inapewa kipaumbele. hili bunge letu chini ya Mama Makinda limekuwa likijaa mabishano na miongozo ya spika mpaka muda mwingi na pesa nyingi za walala njaa na wakosa matibabu zinapotea bure, kumbuka siku moja ni mamilioni ya pesa wanalipwa hawa jamaa hata wakibishana siku nzima.
  Hili ni bunge la ndio na hapana. hakuna hoja itakayo badilisha kile kilichoamuliwa na waziri wa ccm. hata kama hoja ninzuri itawekwa pembeni. mfano mzuri ni huu upuuzi wa waziri mkuu aliyesema posho zilipwe kwa kuwa ombaomba bado wanazihitaji. hivi katika mabunge yenye misukumo ya wananchi kuna waziri mkuu atakaye thubutu kuwaita wapiga kura wake ombaomba???

  pendekezo.
  tusiwe na vikao vya kujadili bajeti au mswada wa serikali ili kupunguza matumizi ya posho zisizo za lazima, kwani tuliona mswada wa katiba umeingia bungeni ukatoka kama ulivyo na kuletwa kwa wananchi ukakataliwa.
  tuwe na mijadala ya umma zaidi kuliko wawakilishi kwani wanawakilisha maslahi yao binafsi. mfano bajeti hii tukipiga kura wananchi wengi wataikataa lakini kura hiyo ikipigwa bungeni itakubaliwa.
   
Loading...