Sina imani na baadhi ya waaandishi wa habari.

njija

Senior Member
Jun 30, 2011
110
62
Naomba nilete kwenu taarifa ambaye ilitolewa na baadhi ya magazeti ya leo kuhusu ajali waliyo pata wanajeshi wetu katika mazoezi yao jana. Nikweli kabisa kuwa kuna mmoja alifariki lakini yule mwingine baadhi ya magazeti yameripoti kuwa yuko MAHUTUTI, kamanda huyo ni ndugu yangu kilichoandikwa na ukimuona yeye ni vitu viwili tofauti, kwanza hata yeye alisoma gazeti na kushangaa. Nawashauri waandishi wetu KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KUANDIKA KWANI KUNA NDUGU BAADA YA KUONA MAGAZETI WALICHANGANYIKIWA.

Naambatanisha na Picha ya kamanda aliyepata ajali jana na kunusurika, naye ana soma gazeti moja la leo.
 

Attachments

  • 100_0877.jpg
    100_0877.jpg
    842.4 KB · Views: 99
Hapo ndio ushangae kuna waandishi vihiyo kweli tanzania, Angalia magazeti Kama tazama, habari Leo, uhuru, jambo Leo ni ubabaishaji mtupu, kila habari utasikia na mwandishi wetu, shame on media.
 
Kwa kuwa hivyo vyombo vya habari vinawapotosha ni vema mkaacha kuvitumia kupata habari... tafuteni vyanzo vingine
 
Mimi siku hizi nasoma JAMHURI, Raia Mwema na daily news. Haya mengine ni balaa tupu!
 
Waandishi gani hawa wanaotaka kuongeza mauzo?
Hawana habari za kweli niuongo mtupu na yule waziri wao aliyekuwepo kama chupa na kizibo!
 
Mimi toka lilipofungwa gazeti la watanzania la Mwanahalisi niponipo sijui gazeti la kusoma tena.
Hasa pale waandishi wengine niliowaamini walipoonyesha udhaifu wao kwa kumwalika Nchimbi
kwenye maandamano yao kwa mlango wa nyuma sina imani na wengi tena.
 
Back
Top Bottom