Sina chuki nao, ila mishahara ya wabunge ni 'too much'

Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja.

Ajira ya ubunge sasa imekuwa ni ya kufa na kupona. Hivi kazi hii kweli mmeifuatilia na kipimo cha mtu anachokwapua, wengi huwa wanachomekea tu lakini ukweli hii kazi ni ya kupata hela kiulaini kabisa, wewe upige meza tu na kuunga mkono kila jambo, inatosha kabisa kuwepo salama kwa muda wote.

Kuna haja sasa mishahara yao iangaliwe upya inawadhalilisha wengine kuna watu wapo tayari kupoteza roho zao kwa kulinda nchi hii, kuna wanaofanya kazi hatarishi za kupambana na majangili na majambazi ambao roho zao zipo nje ndani wakati wa utekelezaji, inakuwaje hawa wapiga meza na blah blah wanalipwa hela iliyovuka mipaka?
Ukitaka kuijua CCM-A na CCM-B,paguse hapo kwenye mshahara.
Hawakuachi salama.

Hebu ona mdee na kundi lake pamoja na kuitwa Kamanda miaka nenda Rudi,wametia mpira kwapani na pamba masikioni.

Mcheki Mbowe uchaguzi serikali za mitaa alivyoupotezea ila uchaguzi mkuu wa ubunge kajisahulisha.No kususa
 
Issue hapo siyo hela wanayopewa . The issue ni kwa nini?? wapewe hizo hela ili hali nchi yetu bado nifukara hata malipo ya mishahara za watumishi wa umma. tunakopeshwa,na hela za miradi za mikakati tunapewa na waisani.

So ni kwa nini baadhi ya watumishi wakwapue pesa nyingi kiasi hiki.

Katiba yetu inatakiwa mabadiliko makubwa
 
View attachment 1820017View attachment 1820018

Picha hizi mbili zitoshe kutupa majibu.

Ni nchi moja ambayo kiongozi anapiga full tank magari ya kifahari kwenye mikutano ya kampeni.

Watoto wa wanaopiga kura wanakaa chini! Zaidi ya hapo wanaambiwa ufaulu umeongezeka ila ikifika January wanaambiwa wasubiri madarasa yajengwe na huku kuna watu wanavuta 15M mfukoni kwa mwezi na gari la 200M+ kiyoyozi muda wote huku watu wakiambiwa ni wanyonge na wamepata mtetezi!

"HUO NDIO UKWERI , NASEMA UONGO NDUGU ZANGU? HII NCHI IMECHEZEWA SANA.
Fact.
 
Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja.

Ajira ya ubunge sasa imekuwa ni ya kufa na kupona. Hivi kazi hii kweli mmeifuatilia na kipimo cha mtu anachokwapua, wengi huwa wanachomekea tu lakini ukweli hii kazi ni ya kupata hela kiulaini kabisa, wewe upige meza tu na kuunga mkono kila jambo, inatosha kabisa kuwepo salama kwa muda wote.

Kuna haja sasa mishahara yao iangaliwe upya inawadhalilisha wengine kuna watu wapo tayari kupoteza roho zao kwa kulinda nchi hii, kuna wanaofanya kazi hatarishi za kupambana na majangili na majambazi ambao roho zao zipo nje ndani wakati wa utekelezaji, inakuwaje hawa wapiga meza na blah blah wanalipwa hela iliyovuka mipaka?
Ni kweli. Ila wewe unatetea upande wa askari tu au?Hujui kuna watumishi hata posho hawazijui?
 
Hii inauma sana.Ila Yesu wetu atawalipa sawasawa.
View attachment 1820017View attachment 1820018

Picha hizi mbili zitoshe kutupa majibu.

Ni nchi moja ambayo kiongozi anapiga full tank magari ya kifahari kwenye mikutano ya kampeni.

Watoto wa wanaopiga kura wanakaa chini! Zaidi ya hapo wanaambiwa ufaulu umeongezeka ila ikifika January wanaambiwa wasubiri madarasa yajengwe na huku kuna watu wanavuta 15M mfukoni kwa mwezi na gari la 200M+ kiyoyozi muda wote huku watu wakiambiwa ni wanyonge na wamepata mtetezi!

"HUO NDIO UKWERI , NASEMA UONGO NDUGU ZANGU? HII NCHI IMECHEZEWA SANA.
 
Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja.

Ajira ya ubunge sasa imekuwa ni ya kufa na kupona. Hivi kazi hii kweli mmeifuatilia na kipimo cha mtu anachokwapua, wengi huwa wanachomekea tu lakini ukweli hii kazi ni ya kupata hela kiulaini kabisa, wewe upige meza tu na kuunga mkono kila jambo, inatosha kabisa kuwepo salama kwa muda wote.

Kuna haja sasa mishahara yao iangaliwe upya inawadhalilisha wengine kuna watu wapo tayari kupoteza roho zao kwa kulinda nchi hii, kuna wanaofanya kazi hatarishi za kupambana na majangili na majambazi ambao roho zao zipo nje ndani wakati wa utekelezaji, inakuwaje hawa wapiga meza na blah blah wanalipwa hela iliyovuka mipaka?
Uko sawa, ni kweli jamaa wamnalipwa mshahara mkubwa wa bure kabisa, hakuna wanachofanya zaidi ya kupiga piga meza, lakini mimi napingana na wewe kuhusu kuwaonea hururma polisi, polisi hao ndio huwa wanawachunga wabunge wanapoiba kura kwenye chaguzi, acha wakomeshwe na mishahara hiyo midogo ndio inawafaa mpaka siku akili zitakapowakaa sawa, wale wenzao wa usalama barabarani wao hawahitaji mshahara kwani wanazokusanya barabarani zinawatosha, hao mapolisi waliompiga risasi Lissu waache wakomeshwe
 
Wabunge wanachostahili kulipwa ni posho ya kuhudhuria vikao, na hizo posho wanatakiwa wachangiwe na wananchi wanaowawakilisha kule jimboni. Sasa serikali kulipa posho na mishahara ya wabunge ni rushwa iliyojificha ndo maana kila jambo linaloletwa na serikali utasikia meza zikigongwa pwa pwa pwa, naunga hoja mia kwa mia ndugu bwana chupika......
 
Hiyo ni roho mbaya, kutaka wenye kingi kipunguzwe si sawa, wewe komaa upate kama wao
Mwendazake mbona alipunguzaga mishahara ya Wakurugenzi wa mashirika ya umma? Umesahau??? Alisema mwisho ni Tsh 15M au hili kwako ni sawa but sio kwa wana siasa?
Mi najiuliza tu, hivi kwamfano tusipokua na bunge nchi itapata hasara gani? Lakini nchi haiwezi kwenda tusipokua na MD wa Tanesco, TANAPA, NSSF, PPF etc. So naunga mkono hoja ya mleta HOJA, wabunge wapunguziwe either posho, mishahara. Fikiria eti mtu anapewa lita 1000 za mafuta kwa mwezi, huyu anaendaga wapi wakati baada ya bunge wote wanahamia Dar???
 
Kinachoumiza binge ndio linachelewesha sana maendeleo. Mbunge anayeongea matani mengi ndiyo maarufu na anafatiliwa zaid!! Basis tujaze mule kina joti,mkudesimba nk.
 
Inasikitisha hata kama ni roho ya chuki
 
Back
Top Bottom