Sina amani naye japo nampenda huyu binti

Kweli kabisa ndege wafananao huruka pamoja umemshika mungu tafuta mshika mungu mwenzako lasivyo utakutana na kitu kitakacho kutoa kwenye njia.
Kweli mkuu,, kuna kipindi moyo unakuwa mgumu natamani naihirishe lakini nashindwa kuchukua maamuzi.
 
Bwana wetu Yesu asifiwe wapendwa, Asalaam naalykum kwa waisilam wote natumaini mu wazima wote.

Moja kwa moja nizame ndani ya maada wapendwa. Mimi nikijana ambaye natarajia kuingia kunako ndoa ikimupendeza Mungu wangu,
Umri wangu miaka 25

Kuna binti ambae tulikutana kwa mazingira fulani tukazoeana na tunaishinae mitaa ya karibu japo kuna umbali kidogo, baadae alichukua namba yangu bila mi kujua, baadae ndo kuanza kuchati pamoja na mazungumzo kwa njia ya simu na ana kwa ana hadi kufikia binti kunitamkia kuwa anahitaji me niwe mme wake wa ndoa na ananipenda ,, basi sikumpa jibu la kumaanisha nikamwambia poa ikimupendeza Mungu tutakuwa pamoja.

Nimekaa nae hivo huku nikiendelea kumchunguza basi nami moyo wangu ukazidi kumpenda kila kukicha na nipo radhi kumuoa japo hapa katikati ilitokea changamoto fulani ambayo nikawa najiuliza saana, kuna kuna jamaa ambae tunasali nae kanisa moja nae akawa anamtaka kwamba anahitaji kumuoa na binti akawa ananitumia zile chating za jamaa akimuomba anahitaji kuwa nae.

Binti akanithibitishia kuwa anipenada mie na akamtumia jamaa sms kuwa mi ndo ntakuwa mumewe au baba watoto wake,, lakini sijajua kama jamaa bado wanaendelea nae katika harakati hizo.

Changamoto ya huyu binti :
Au niseme asili yake ambayo nishaiona kwake ni mtu ambae anapenda kuongea na kila mtu halafu nimwongeaji sana halafu marafiki wengi wa kiume na kuchati anachat sana kila wakati yaani chaji yake huwa inaisha mara nyingi kwa kuchat hata nikiwa nae sms mara kwa mara zinaingia kwake, hiyo hali inanitia shaka je atakuwa mwaminifu kweli kama mimi nilivyo mwaminifu kwake?

Je, ntaiweza kweli hii hali maana mpaka tusha elewana me nikipata mahari nimchukue mtoto niweke ndani,,

Wadau kwa hili limekaaje?
ukiona kitu, unakipendaa ila huna amani nayo mara nyingi kuna vitu anavifanyaa ambavyo huvipendi na ukivijuaa utamchukiaa milele!!



Tumsifu Yesu Kristo!
 
ukiona kitu, unakipendaa ila huna amani nayo mara nyingi kuna vitu anavifanyaa ambavyo huvipendi na ukivijuaa utamchukiaa milele!!



Tumsifu Yesu Kristo!
Amina sana,, point ya maana sana mpendwa, nichuke uamzi wa kumchunguza??
 
Tafuta mwanamke mwingine 'mpendwa' uoe..huyo ktk ulimwengu wa kiroho nafsi yako imeshamkataa..lazma kutakua na kitu kibaya mbeleni.
Nikweli mpendwa kuna wakati roho inakuwa na mashaka sana juu yake na amani haijawa kubwa sana moyoni mwangu juu yake.

Sasa labda kuna vitu Mungu anihusisha nisije nikazama shimoni.
 
25 yrs zidisha maombi na jikite zaid kuimarisha uchumi wako utajanishukuru baadae. Kama huna mpango wa kuoa ndani ya miaka miwili ijayo fanya maamuzi sahih

Kwanini wanawake hua mnaencourage sexual violence?

As in hapa umetoa ushauri huyu jamaa akampige kofi huyo binti na maoni yako wanashare wanawake wengi nilioongea nao. Mmoja aliwahi sema kwamba siku nyingine mwanamke anaamka anakua anatamani kupigwa.
Acha kukuza mambo.

Sexual violence ndo ipi?
 
Back
Top Bottom