Sina Amani: Mtoto wetu Njiti (Premature) halii

JourneyMan

Member
Apr 1, 2020
21
13
Kama heading inavyoeleza hapo juu,
Leo ikiwa ni siku ya 3,
Mwenetu amezaliwa na weeks 32/miezi 7 na kdg,

Physical yuko sawa, ana 3.2kg. Alipozaliwa tuu wakamuweka kwenye Mashine, baadae akaweza kupumua mwenyewe wakamtoa wakamhamisha kwenye chumba cha watoto njiti (premature) kwa ajili ya joto na care nyingine.

Changamoto tunayoipata hapa ambayo inatukosesha amani ni hili suala la kutotoa sauti kabisa, lakini pia Hawezi kuvuta maziwa inabidi tumpe lactogen 1.

Je, ndugu zangu hili suala ni la kawaida? Nini nashauriwa?, kama kuna ambaye ashapitia hali hii au hata kusikia/kuona naomba msaada wake.

Ni mwanangu wa kwanza hivyo sina raha ndugu zangu.
 
Watoto njiti wanasumbua Ila wanakua, mkitoka hospital chumba chenye joto, kisafi na watu wasiingie hovyo, na pia anaitaji Sana joto la mama, kangaroo style.
 
Kama heading inavyoeleza hapo juu,
Leo ikiwa ni siku ya 3,
Mwenetu amezaliwa na weeks 32/miezi 7 na kdg....
sasa ataliaje hali ya kuwa amewahi kuzaliwa ikifika tarehe ambayo ndo anatimiza miezi 9 ndo atalia so kuwa mpole ndugu ni kawaida hiyo kwa njiti
 
Kama heading inavyoeleza hapo juu,
Leo ikiwa ni siku ya 3,
Mwenetu amezaliwa na weeks 32/miezi 7 na kdg,

Physical yuko sawa, ana 3.2kg. Alipozaliwa tuu wakamuweka kwenye Mashine, baadae akaweza kupumua mwenyewe wakamtoa wakamhamisha kwenye chumba cha watoto njiti (premature) kwa ajili ya joto na care nyingine.

Changamoto tunayoipata hapa ambayo inatukosesha amani ni hili suala la kutotoa sauti kabisa, lakini pia Hawezi kuvuta maziwa inabidi tumpe lactogen 1.

Je, ndugu zangu hili suala ni la kawaida? Nini nashauriwa?, kama kuna ambaye ashapitia hali hii au hata kusikia/kuona naomba msaada wake.

Ni mwanangu wa kwanza hivyo sina raha ndugu zangu.
Uko hospitali gani?mimi nilijifungua njiti pia mtoto akiwa na 1.9kg na nilikaa kwenye chumba cha joto na ndani ua wiki alipungua hadi akafika 1.64.. ila Mungu alisaidia akakua na sasa ni mkubwa na hana tatizo.Shida ya kunyonya kwa kipindi hicho ilinitokea pia kwan alikuwa havuti maziwa hadi nimnyweshe ila alivyoendelea kukua alianza kuvuta maziwa ila anachoka haraka.Dr akasema anachoka hivyo ili ashibe lazima nimnyweshe.Kuhusu kulia embu ongea na dr atakusaidia maana nachojua watoto wadogo huwa wanalia sana tena wanavyokuwa wenyewe wanalia hadi unakuta amesogea alipolazwa. Pole sana atakaa sawa
 
Ni kawaida kwa njiti...wanakuwa dhaifu ...

Huyo atalia tu mwenyewe na mtakesha naye... .. niliona kwa sis .
..kalikuwa kimya na kadogo mpaka unakaogopa..ila baada ya mwezi ..weeh..

I likuwa kukesha kwa zamu..

Kwa wengine huwa kuna majani flani yanaitwa jimbo ...wiki tu anachangamka na anakuwa vzr kama wengine..
 
Pole kwa kuwa na mashaka..Ila kikubwa anapumua na hana dalili zingine za hatari kama kubadilika rangi ya mwili n.k so atakua sawa tuu
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom