Simwogopi Rais, acheni uwoga! -DC Yamungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simwogopi Rais, acheni uwoga! -DC Yamungu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Mar 1, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  MKUU wa Wilaya ya Maswa, James Yamungu, amesema kama Rais Jakaya Kikwete atamfukuza kazi kwa kumuunga mkono aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini, Albert Mnali, kwa kuwacharaza viboko walimu, yeye hatishiki, badala yake atarejea kijiji kwake lakini atasimamia alichokisema na wananchi ndiyo watakaoamua.

  Yamungu alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu tamko la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Shinyanga, kumtaka Rais Kikwete kumfukuza kazi Yamungu kwa kuunga mkono kitendo cha Mnali cha kuwachapa viboko walimu wa wilaya yake, kwa madai ya kushusha kiwango cha elimu.

  Akizungumzia na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kutoka Maswa, Yamungu alisema yeye alitoa kauli hiyo kwa moyo mweupe kama raia wa Tanzania bila kuathiri jambo lolote kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 18, inayoeleza uhuru wa kujieleza.

  Alisema hata kama Rais Kikwete ataamua kumfukuza kazi kama alivyofanya kwa Mnali, kuhusu suala la kuwachapa viboko walimu, hatishiki kwani atakwenda kijiji kwao Songea lakini ameeleza ukweli na wananchi ndiyo watakaopembua mchele na pumba.

  ‘Hata kama Rais atanifukuza kazi kwa kumuunga mkono Mnali, nitakwenda kijijini kwetu huko Songea, lakini ukweli lazima uelezwe na wananchi ndiyo watakaotoa maamuzi ya kupembua pumba na mchele ni upi,” alisema Yamungu.

  Awali akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, kulaani kauli ya Yamungu, Katibu wa CWT mkoani hapa, Emmanuel Samala, alisema ameshangazwa na kauli ya DC huyo ya kumpongeza Mnali kuwa ni shujaa kwa kuwachapa walimu.

  Alisema Yamungu amelewa madaraka kiasi cha kumkosoa mkubwa wake wa kazi - Rais Kikwete - ambaye hakupendezwa na kitendo alichokifanya Mnali.

  ‘Ni wazi sasa kuwa Yamungu amelewa madaraka kiasi cha kumkosoa mkubwa wake (Rais Kikwete), kwa maamuzi aliyoyatoa dhidi ya kitendo alichofanya Mnali...nafikiri naye anapaswa kuchukuliwa hatua,” alisema.

  Kauli ya DC huyo ni ishara kuwa Rais Kikwete amekuwa akiwapa watu madaraka makubwa huku baadhi yao wakiwa hawana uwezo wa kuongoza, hali inayofanya kuwa na viongozi mizigo ndani ya serikali yake na kushindwa kuwahudumia wananchi na kusababisha migomo ya mara kwa mara.

  Ifike mahali Rais Kikwete asitumie kigezo cha kumteua mtu kuwa kiongozi kwa sababu ya kuwa mwanajeshi, kwani walio wengi wamekuwa wakitumia vibaya madaraka yao na mfano ni katika Mkoa wa Shinyanga.

  ‘Hili liwe fundisho kwa Rais ili anapoteua watu wa kumsaidia asitumie kigezo cha mtu kuwa mwanajeshi, kwani kwa sasa wengi ni wakuu wa wilaya na baadhi wamekuwa wakitumia vibaya madaraka yao na mfano hai ni katika Mkoa wa Shinyanga,” alisema.

  Aliendelea kueleza kuwa hapendi kubishana na Yamungu, aliyezoea amri za kijeshi na kumtaka aende akajifunze taratibu na sheria zinazoongoza ajira ya walimu ili asiongelee mambo asiyoyajua na matokeo.

  Katibu huyo wa CWT alisema chama hicho mkoani Shinyanga kimelaani kauli ya Yamungu na kumwomba Rais Kikwete kuchukua hatua kama alizochukua kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Vijijini, Mnali.

  Kauli ya Yamungu ikiachwa inaweza kusababisha walimu waendelee kudhalilishwa na baadhi ya viongozi aina ya Mnali na Yamungu. Yamungu juzi wakati akifungua mkutano wa tatu wa Nyalikungu SACCOS mjini Maswa, alimpongeza Mnali aliyefukuzwa kazi na Rais Kikwete, baada ya kuwachapa walimu viboko na kumwita kuwa ni shujaa.

  Alisema licha ya Mnali kufukuzwa kazi na Rais Kikwete, anabaki kuwa shujaa aliyekuwa akiwatetea Watanzania kuhusu suala la elimu.

  “Ndugu zangu pamoja na Rais kumfukuza kazi Mnali, wazazi katika wilaya ya Bukoba Vijijini pamoja na umma wa Watanzania wanamuunga mkono na kumwona kama shujaa ambaye ana uchungu na taifa letu hasa katika sekta ya elimu,” alisema DC huyo.

  Yamungu ambaye pia ni Katibu wa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara, alisema kitendo alichokifanya Mnali ni sawa na kauli aliyotoa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa katika ziara mikoa ya Kanda ya Ziwa, baada ya kukerwa na vitendo vya baadhi ya watu wanaowaua walemavu wa ngozi (albino) na kutaka nao wauawe bila kujali sheria.

  Klabu ya Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara inasikitika kumpoteza mtu muhimu, kwani alikuwa mchapakazi mzuri na mambo aliyofanya wilayani Geita akiwa mkuu wa wilaya, ni mfano wa kuigwa kwani alihamasisha wananchi kujenga shule nyingi za sekondari na alifanikiwa.

  Ni vizuri kwa wanachama wa chama hicho kuiga mfano huo wa kutetea mambo yaliyo na manufaa kwao, kwa ajili ya kuendeleza SACCOS hiyo na hatimaye kuwa benki kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

  Mnali aliamrisha kuchapwa viboko kwa walimu wa shule za msingi za wilaya yake ya Bukoba Vijijini, kwa kile alichodai kukithiri kwa utoro, uvivu na kusababisha wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba.

  Kutokana na kosa hilo, Rais Kikwete aliamua kumvua madaraka kwa madai kuwa alikiuka kanuni za utumishi wa umma na kulidhalilisha taifa, huku mwenyewe akijigamba kuwa
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nimetembelea badhi ya shule za msingi za Wilaya ya Rorya ,Tarime , Musoma Mjini , Arusha , Arumeru, Mtwara, Njombe, Dodoma kule Mpwapwa nk hali inatisha kuanzia shule za Kata na msingi .Kuna shule nimeingia nikakuta kuna walimu 3 pekee na hii secondary na nyingine ya msingi ina walimu 11 lakini wote wame enda mnadani kabakia Mkuu na mwalimu mmoja .Nimefika kwa Afisa Elimu wa Wilaya ku hoji michango ya 20,000/= kwa kila Kaya ili kuwapa nafasi watoto kuingia kidato cha kwanza ambapo mwishoni wengi wamerudi kwa kuwa hawakuwa na sifa za kuingia secondary ila pesa yao wakaonyeshwa mithani .Naunga mkono viboko kuchapwa walimu wote kabisa .
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...bado sijaona wapi huyu mheshimiwa aliposema "simwogopi Rais!", sana sana huyo katibu wa CWT mkoa ndiye anayemkosoa rais na mh Yamungu, na amri za kijeshi.

  ...licha ya hilo rais na kiongozi yeyote anatakiwa kuheshimiwa, sio kuogopwa!
  CWT mnaanza kudeka sasa wakati kiwango cha elimu kinashuka, grow up!!!
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hicho kichwa cha habari cha mleta mada. Ukisoma hii habari kwa Tanzania Daima kichwa kilichotumika ni "DC amchokonoa JK-Asema hatishiki akifukuzwa kwa kumtetea Mnali".

  Naungana nawe Mbu, hutakiwi kumuogopa Rais bali kumuheshimu. Ni sawa na mzazi tu, unamuheshimu na si kumuogopa. Ukifikia kumuogopa kiongozi wako huwezi tenda kazi itakiwavyo, manake kuna masuala unatakiwa kumshauri, sasa kama unamuogopa huwezi kumshauri.
   
 5. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Sweetbaby salam,
  Katika taarifa hii inayyomuhusu DC Yamungu nimeshindwa kuona pale anapotamka "HAMWOGOPI RAISI ACHENI UWOGA" kama kichwa cha habari cha taarifa yako kinavyosomeka: SIMWOGOPI RAISI ACHENI UWOGA- DC Yamungu.Kukosekana kwa sentensi hiyo ndani ya taarifa yako itatafsirika kuwa DC YAMUNGU hakutamka bali wewe UNAMLISHA maneno yako (you feed DC YAMUNGU with your wards) na hali hiyo inazaa UPOTOSHAJI WA HABARI na kuleta mashaka kwa mtoa taarifa muhusika.Tafadhali ipitie tena taarifa yako pengine mimi ndie niliepitiwa na niwie radhi kama hilo limetokea.
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mh Yamungu anastahili kupongezwa kwa kuwa mkweli na muwazi. Hana na wala hataki unafiki. Kushuka kwa elimu Tanzania pamoja na mishahara kiduchu wanayolipwa waalimu lakini pia tabia na mienendo ya waalimu imechangia kwa kiasi kikubwa. Waalimu wanaondoka shuleni na kwenda mitaani kama si kulewa basi kufanya biashara. Kama wao waalimu wafanyavyo kuwachapa watoto wetu viboko kwa makosa kama kuchelewa shule, kupiga kelele darasani nk nao pia inabidi wachapwe bakora kwa makosa wanayoyafanya.
  Na hakuna haja ya kumuogopa Raisi lakini kuna haja ya kumuheshimu na kumwambia ukweli ni kumpa heshima yake anayostahili.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Naamini Yamungu anajua anacholisema... si ajabu alikuwa pampja jeshini na Kikwete
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Mar 1, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,427
  Trophy Points: 280
  .....kikwete anakumbatia wazembe always ...haiwezekani anashindwa kuwafukuza kazi mafisadi...na anajitetea kuwa watamdai fidia ..yet anamfukuza kazi outright mkuu wa wilaya mnali ambaye naye kama mizengo pinda waliteleza tu kwenye maamuzi yao....tena afadhali mnali amekubali kuwajibika kuliko pinda ambaye alilia....

  mbona hakumfukuza kazi yule kanali mkuu wa wilaya wa nyamagana aliyejibizana na lowasaa..au kwa sababu alishaaza kuwa na vita baridi na lowassa enzi hizo....
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mfumwa na Mbu tuambieni tofauti ni ipi kumuogopa Raisi na kumuheshimu Raisi?
  Ni ipi tofauti hasa? Naomba kujua kwa kina!
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hichi ni chama cha wababe kila mmoja anaonyesha ukakamavu wake na hakuna anaeweza kumfanya kitu.
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ama kweli usipoona ya Musa utaona ya Farao.
  Hivi kweli bado watanzania tuna pioneer kuwapa watumishi wa serikali adhabu ya viboko kwa kutowajibika ipasavyo?
  Mbona mimi naona watumishi wa serikali na mashirika ya umma kama asilimia 95 mnastahili kupata viboko kila siku?
  Tena tunaanzia watumishi wa ikulu na kisha tunashuka kuja chini. Tena hawa wakuu wa wilaya hao ndio usiseme maana hata Prime Minister aliyepita alishawambia kukitokea njaa watawajibishwa na sasa njaa ipo kila sehemu wala sioni lolote. Sijui tungeanzia kwao?
  By the way hawa wakuu wa wilaya kazi zao ni zipi hasa? ni viranja? mi nadhani hata bila hawa kama watu wana nidhamu ya kazi kazi zitakwenda. Hawana kazi hawa mbali na kuwa tax users tu. Lakini nimefuatilia nyendo za watanzania woooote including walio katika ajira za serikali na wanaojiajiri kwa kweli watu hawafanyi kazi ipasavyo.
  Watanzania wengi upenda anasa sana kuliko kazi. Nashangaa utaona saa 4asubuhi baa zimejaa watu wanakunywa pombe. Na hapo hujaenda baa za pombe zinaitwa za kienyeji. Huko wamejaa puuuuuuu.
  Sasa tuanzie kuchapa nani? Ukienda Polisi utachapa wote kuanzia IGP. Maana kama sivyo angeshamchapa na kumfukuza kazi Abdalah Msika. Ukienda jeshini uko ndiko usiseme ufisadi wa pesa za umma kibao. Nenda benki kuu ambako wezi hawakuchapwa viboko. Nenda hospitalini, huko ndiko usiseme watu wengi wanakufa kwa ujinga wetu tu. Sasa nani atapona fimbo hizi.?
  Kwa nini watu wamepoint waalimu peke yao? system nzima ya serikali iko hoi. Hakuna malengo ya kazi. Watu hawajitumi.
  Nilikuwa siku za karibuni nikiuguza ndugu yangu katika hospitali ya mkoa fulani hapa Tanzania. Kila mahali pachafu. Ward aliyolazwa haikuwahi kufagiliwa siku zote 14 alizokuwapo huyo mgonjwa wangu kiasi kwamba wagonjwa wenye nafuu na wasaidizi wao walifanya zamu kupiga deki sakafu na kusafisha choo.
  Shuka hazikuwa zikibadiliswa wala kufuliwa na bado wagonjwa hawakuruhusiwa kuweka shuka zao binafsi eti si sheria. Vyandarua vilikuwa vimejaa matobo.
  Dawa hazikuwapo hadi ukanunue na adha nyingi nyingi tu je hawa nao wapate viboko?
  Mbona walimu wanaonewa kila kitu??????
  Mi napendekeza wote waliopelekwa mahakamani kwa ufisadi nao wachapwe kwanza ndio wapelekwe mahakamani.
  Huu mtindo wa kishenzi ulioanzishwa na hawa wapiga soga wa kitanzania toka SISI M. mnawaita ma DC wa kupiga watu si wa kiungwana. Huyu Yamungu anamkejeli Rais wake wazi wazi na baadhi hapa tunaona anafanya sawa. Mimi sijui kiongozi wake huyo analionaje. Lakini hizi hukumu tunazozitoa nje ya sheria ni ushenzi sawa na jinsi tunavyoua albino au wezi mitaani hata kama tunaona hii ndio sawa. Hakuna tena sheria kila mtu anafanya analoona.
  Tukomeshe hivi vitendo vya kijinga na tufuate sheria.
  Mtumishi wa umma akikosea zipo sheria za ajira anazotakiwa kukabiliana nazo sawa na Mr mheshimiwa sana Mnali alivyokutana nazo. Au na yeye alitakiwa apate kiboko? Mambo ya kuchapana fimbo ni ya kijinga maana hata walimu sasa hawatumii fimbo kama adhabu kwa wanafunzi wao. Iweje wao wapate adhabu hii? Mnali na Yamungu wote si waungwana ila natumia neno moja tu kama sifa yao. Ni washenzi. Mark you hili si tusi ila ni sifa yao. Maana washenzi ni watu wasiokuwa na ustaaraabu.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni ubabe tu hakuna kitu jamaa wameshampima Kikwete na CCM yake na kuona si uongozi kitu zaidi ya ubabaishaji.
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180

  Afu mnataka rais awe effective wakati uzembe huko kwenye DNA ya watanzania.
   
 14. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #14
  Mar 1, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Yamungu tulikuwa wote katika Military Training Monduli. Katika intake yetu,kila tukiambiwa kukimbia,Yamumgu alikuwa wa kwanza.
  Kwa hiyo Yamungu labda ni mtu wa nidhamu sana,na hapendi kona utovu wa nidhamu.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Lakini kama hapendi kuona utovu wa nidhamu inakuwaje yeye nimtovu wa nidhamu?
  Mimi sijawahi kwenda Monduli lakini nilikwenda JKT wakati ule tuliotakiwa kwenda kwa mujibu wa sheria. Moja ya kosa kubwa la askari ilikuwa ni ku question amri ya mkubwa siyo?
  Sasa hapa Yamungu unaweza kusema ana nidhamu kweli? na kama akionekana kwa kufanya hivyo ni nidhamu themn nita question nidhamu ya majeshi yetu hapa.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Ni bora tu Kikwete atangaze kutogombea tena 2010 ili kuinusuru nchi. Si siri kwamba uongozi wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu umemshinda, Tunataka Rais mwenye ujasiri, asiye muoga na asiye na makundi, ambaye hajazungukwa na mafisadi na mabye siku zote ataweka mbele maslahi ya nchi mbele badala ya marafiki zake ambao ni mafisadi. Kikwete tutangazie Watanzania kwamba 2010 hutagombea tena kipindi cha miaka mitano kinachokwisha kinakutosha kabisa.
   
 17. e

  eddy JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,370
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Jamani tusilete uchonganishi usiokuwa na msingi, yamungu anahaki ya kutoa maoni yake! Ila tunapata picha kuwa wananchi wameshachoka, serikali isipolifanyia kazi watakuja chomwa moto siku moja. bukoba wamechapwa, singida walichomwa visu.

  Walimu wanahitaji sasa "performance contract", kila mwisho wa mwaka wafanyiwe evaluation wanao underperform wakatafute kazi zingine. Anaeona mazingira ya kazi magumu akafundishe kwa giriki FEZA. Kule wanapewa chai na mkate asubuhi.
   
 18. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #18
  Mar 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  feza ni ya waturuki sio uguriki
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Yamungu amekosa nidhamu...PERIOD.....na mtu ambaye amekosa nidhamu kuna taratibu zake.........
   
 20. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #20
  Mar 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kamanda wa iddi amin dada alikuwa anaitwa mali ya mungu
   
Loading...