Simulizi za Kusisimua: Nyerere alipoingiwa huruma Mwana-TANU Mwenzake kukosa Nauli...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Leo Ni Tisa Disemba. Ni Siku yetu kuu kusheherekea Uhuru wetu. Tumetimiza miaka 55 ya uhuru. Tuna kila sababu za kusheherekea.

Nitapenda niweke hapa simulizi ya kihistoria yenye kusisimua, na kuelimisha pia.

Kwenye andiko lake lililojenga nadharia ya kisiasa. ' The Prince' kwa maana ya Mwana Mfalme, Mwanafalsafa Machiavelli anazungumzia juu ya kiongozi aweje. Machiavelli anamtaka kiongozi kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia madarakani na hata wenye kumzunguka. Kwa mujibu wa Machiavelli, hutokea kwa Mwana Mfalme "kuwajeruhi" waliomsaidia kuupata utawala.
Hii ni kwa kutowatimizia yote yale waliodhani kuwa ni haki yaokutimiziwa.

Badala yake, Mwana Mfalme huwaingiza kundini wawe kama wengine.
Katika manung'uniko yao, Mwana Mfalme hawezi kutumia dawa chungu dhidi
yao kwa vile hujihisi ana deni kwao. Lakini, cha msingi kwa MwanaMfamle ni kuzingatia ukweli, kuwa, hata kama atakuwa na maaduiwachache, katika kuchukua nchi, muhimu ni kuwaridhisha walio wengi, nahapa ni wananchi.

Huwezi kutawala kwa amani bila upendo na utashi wa walio wengi. Ni kwa sababu hizi, Mfalme Louis XII wa Ufaransa aliweza kwa kasi ya ajabu kuitwaa Milan na kwa kasi ya ajabu kuipoteza Milan.

Hakukidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi waliomfungulia
milango.Mtawala aliye mbali na asiyejali maslahi ya watu wake walio
wengi ni mtawala mwenye hofu. Na mtawala mwenye hofu zaidi na watu
wake kuliko adui wa nje, basi, hujijengea kasri ama ngome imara ya
kujihifadhi ingawa hilo halitamsaidia kuzuia nguvu za umma za
kumwondoa madarakani. Kwa mtawala, kasri ama ngome iliyo imara ni
kuepuka kuchukiwa na wananchi, kuacha ubinafsi na kujali maslahi ya
wengi.

Ni katika hili, kuna ambao walimtarajia Julius Nyerere kuwapendelea wale waliomsaidia kuingia kwenye mamlaka. Lakini, Nyerere aliwaacha waingie kwenye kundi kuu, kwa maana wawe miongoni mwa wananchi. Wafanye kazi ya siasa lakini si kwa kupewa vyeo vya juu, kwa vile tu, walikuwa ni miongoni mwa wale 17 waliounda TANU.
Hapa nawazungumzuia watu kama akina Chifu Kunambi na Dossa Aziz. Chifu Kunambi alitoa hata eneo lake kwa maekari ili kijengwe Chuo Kikuu. Chifu Kunambi amekufa miaka kadhaa iliyopita akiwa anaishi maisha ya kawaida pale Ubungo Msewe.

Na kuna , Julius Nyerere alimuonea huruma sana Dossa Aziz alipokutana nae kule Kizota , Dodoma. Dossa Aziz alikuwa ni MwanaTanu mwenye kadi nambari 4. Ni Dossa Aziz aliyetoa Landrover yake itumike na TANU, ndio gari aliyotumia Nyerere kuzunguka vijijini kwa wananchi kuitangaza TANU. Ni Dossa Aziz na wenzake waliomchangia Julius nauli ya kwenda UNO kudai uhuru wa Tanganyika.

Lakini, pale Kizota, Dodoma, miaka ile ya 80 mwishoni, Julius Nyerere alimwona Dossa Aziz aliyechoka sana. Julius akaambiwa, kuwa hata nauli ya kwenda Dodoma, Dossa Aziz alisaidiwa na rafiki yake na classmate wake wa tangu Kitchwele School, Ally Sykes.

Julius Nyerere aliingiwa na huruma. Inasemwa, kuwa Julius, kwa fedha zake mwenyewe, alimnunulia Dossa Aziz gari la kutembelea.

Naam, simulizi ni nyingi...

Maggid Mjengwa.
0688 37 36 52 ( Whatsapp)
0754 678 252

1.jpg
 
Mkuu mleta mada,mwaka 2004,nilimfuata mzee kunambi kumdadisi mambo mbalimbali ikiwemo historia ya chuo kikuu.Kati ya aliyoniambia ni kwamba alikuwa registrer wa kwanza wa Udsm,na alihusika sana na kupanua eneo la chuo ambayo maeneo mengi yalikuwa mashamba ya korosho lakini hakuniambia kwamba alitoa eneo lake.Yeye na ndugu yake Kobelo,walichukua maeneo yao ya makazi pale Msewe na jina Msewe walilitoa wao kwa kuenzi kijiji alichozaliwa mama yao.
 
Kweli kabisa. Na kwa kuongezea, wakati Chief Kunambi anakuwa REGISTRAR wa kwanza UDSM, alikuwa ni mmoja wa watanganyika wachache kusoma ughaibuni, kama Kumbukumbu ziko sawa, alisoma US.
 
Balibabambonahi,
Shukran, nami pia nimeambiwa na ndugu wa Chifu Kunambi na ni mwanazuoni. Yumkini ni mapokeo, lakini, ibabaki, kuwa Chifu Kunambi amechangia sana TANU na kupanuliwa na Chuo chetu kikuu.
Maggid
 
Uko sawa kabisa mkuu,hilo nalo aliniambia,akaendelea kusema,kilichokiua chuo hicho kikuu ni kiingiza siasa pale alipoondolewa dk. ..fulan akapelekwa Pius Msekwa.kwamba Pius Msekwa aliisomea digree ya kwanza akiwa tayari ni VC.Ukumbi wa Nkrumah,pesa zake zilikuwa zimeshatengwa na wajeruman ilitakiwa vc aende kusaini,lakin Msekwa hakuweza kufatilia.
 
Ni kweli Maggid lakin mzee alikuwa analalamikia kiasi cha malipo ya uzeeni aliyokuwa anapokea,kwamba ilikuwa kidogo sana.Nilipomuuliza kuhusu kifo cha Sokoine,mzee alisema ,,,,aaa wapi,kawawa wanamsingizia tuuu,aliyemuua bado yuko serikalini na ni mtu mkubwa tuuu.Nilijitahid kumdadisi lakin wap mzee hakuniambia aliyekuwa anamaanisha.
 
Uko sawa kabisa mkuu,hilo nalo aliniambia,akaendelea kusema,kilichokiua chuo hicho kikuu ni kiingiza siasa pale alipoondolewa dk. ..fulan akapelekwa Pius Msekwa.kwamba Pius Msekwa aliisomea digree ya kwanza akiwa tayari ni VC.Ukumbi wa Nkrumah,pesa zake zilikuwa zimeshatengwa na wajeruman ilitakiwa vc aende kusaini,lakin Msekwa hakuweza kufatilia.
Mkuu sisi kama watanzania tuna shida sana. Matumbo, Ubinafsi na Kujuana kuna tuponza sana.
 
Maggid umeguswa na suala la nauli badala ya kuhoji kwa nini Dossa Aziz na wengine hawasomeki katika historia ya nchi?

Hawakuwa na vigezo vya kuwa viongozi hasa wakilinganishwa na nani?

Kwa nini kabla ya uhuru walikuwa matajiri na wanaonekana kufilisika baada ya uhuru na hata vizazi vyao havisikiki?

Mabinti,vijana,na wajukuu wao wako wapi? kwa nini familia ya Bibi Titi haisikiki?

Nini kiliikumba familia ya kambona? ina maana hakuna mwana familia ya kambona aliye excel hata kielimu?

watu tunahoji mambo trivial badala ya kujiuliza maswali magumu
 
Naona kabisa walimu wako hawajapata hasara kuandaa kichwa chako!

Namfahamu kitukuu wa Akina Dossa, nadhan yuko bandarini lakini haijui hata historia ya babu zake,juzi nilimuona Dully Sykes akihoji juu ya kusahauliwa babu zake.Yuko wapi Deisy Sykes?
 
Mkuu mleta mada,mwaka 2004,nilimfuata mzee kunambi kumdadisi mambo mbalimbali ikiwemo historia ya chuo kikuu.Kati ya aliyoniambia ni kwamba alikuwa registrer wa kwanza wa Udsm,na alihusika sana na kupanua eneo la chuo ambayo maeneo mengi yalikuwa mashamba ya korosho lakini hakuniambia kwamba alitoa eneo lake.Yeye na ndugu yake Kobelo,walichukua maeneo yao ya makazi pale Msewe na jina Msewe walilitoa wao kwa kuenzi kijiji alichozaliwa mama yao.

Naelekea kukuamini wewe kwa hili kuliko maelezo ya comrade Mjengwa hili....eneo la chuo kikuu ni kubwa sana...sipati picha kama kweli mzee kunambi alimiliki lote hilo...
 
mzee huyu itabidi anaenda beyond,

hawa tunaowaita eti waandishi wakongwe wanaona mambo ya nauli halafu wanasema eti mtu kumpa mtu nauli ni jambo la kusisimua
Hapana,usimlaumu Majjid,huenda alitaka kuonesha jinsi mzee Dossa alivyotumia nguvu na mali zake na uhuru ulipopatikana hakuna aliyemjali akaishia kuwa fukara na akakutana na mnufaika wa juhud na mali zake,akaishia kumpa tuu nauli na kumnunulia gari ya kutembelea.Unajua kila jambo lina angle zake kadhaa ambazo mtu mmoja hawezi kuziona zote.
 
Naelekea kukuamini wewe kwa hili kuliko maelezo ya comrade Mjengwa hili....eneo la chuo kikuu ni kubwa sana...sipati picha kama kweli mzee kunambi alimiliki lote hilo...
Yeye alihusika kuyakamata na kukimilikisha chuo,raia wengi waliyaachia bure tuu,na wengine walipewa fidia kidogo.Mzee Kunambi alidai ni chuo cha pili duniani kuwa na eneo kubwa kikizifiwa na chuo kikuu kimoja kipo Canada. Nilikuwa na rafiki yangu Chambanenge sjui yuko wapi siku hizi.
 
Maggid umeguswa na suala la nauli badala ya kuhoji kwa nini Dossa Aziz na wengine hawasomeki katika historia ya nchi?

Hawakuwa na vigezo vya kuwa viongozi hasa wakilinganishwa na nani?

Kwa nini kabla ya uhuru walikuwa matajiri na wanaonekana kufilisika baada ya uhuru na hata vizazi vyao havisikiki?

Mabinti,vijana,na wajukuu wao wako wapi? kwa nini familia ya Bibi Titi haisikiki?

Nini kiliikumba familia ya kambona? ina maana hakuna mwana familia ya kambona aliye excel hata kielimu?

watu tunahoji mambo trivial badala ya kujiuliza maswali magumu
Chief umenena sana hapo. Nina uhakika hatuwezi jua na wala sidhani kama kuna mtu anaweza kua na details za maswali hayo
 
Hapana,usimlaumu Majjid,huenda alitaka kuonesha jinsi mzee Dossa alivyotumia nguvu na mali zake na uhuru ulipopatikana hakuna aliyemjali akaishia kuwa fukara na akakutana na mnufaika wa juhud na mali zake,akaishia kumpa tuu nauli na kumnunulia gari ya kutembelea.Unajua kila jambo lina angle zake kadhaa ambazo mtu mmoja hawezi kuziona zote.
Sasa leo hamuwataki waislam kweli ??
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom