Simulizi ya Mapenzi Hisia

Mzurulaji

Member
Sep 25, 2021
15
45
Simulizi;Hisia
Mtunzi;Raja Mastory
Whatsapp;0762827579
SEHEMU YA KWANZA ( 01 )

Anza nayo....

Kiza kinene kilitawala lakini bado vijana wa mtaani hapo hawakuacha kuendelea kupiga story kama ilivyokuwa kawaida yao.

Hatimaye yalifika majira ya Saa tano kamili usiku. Lakini bado mazungumzo hayakufua dafu. Ndipo bado kundi la vijana hao waliendelea kuongeza mada juu ya mada.

Ilidhaniwa kuwa baada ya wapita njia kuacha kuonekana kabisa. Huenda mtoa stori pamoja na wachangiaji wangechoka, lakini sivyo tofauti kabisa ukilinganisha na idadi yao maana walikuwa wachache. Walikuwa ni wanaume watatu tu.

Wakiwa bado ni watu waliochangamka hasa. Utulivu ulitawala kwa muda. Hapo ni baada ya mada zilizokuwa zikizungumziwa kufika tamati.

Walisikia sauti ya kike ikisikika kwa mbali. Huku muhusika wasauti hiyo akiendelea kuomba msaada.

Haikushia hapo sauti iliendelea kusikika vyema na kwa ukaribu zaidi tofauti na mwanzo. Na hii iliashiria muhusika wa sauti hiyo. Analikaribia eneo hilo kwa kasi.

Vijana hao waliokuwa wakakamavu kweli kweli. Walijiami kwa kujificha sehemu zilizotawaliwa na kiza kinene ili wapate kushuhudia nini kinaendelea...

Mdada aliokuwa na maumbile makubwa kwa nyuma huku akiwa uchi wa mnyama alikuwa akikimbizwa na vijana wawili walioshikiria silaha za kumdhuru mdada huyo.
Mmoja kati ya vijana hao wawili, alikuwa na kisu mkononi huku akikimbia kwa kunyoosha mkono uliokuwa umeshikiria kisu, na pia kijana mwingine alikuwa ameshiriia panga naye alikimbia huku akiwa amenyoosha mkono mbele.

Kwa bahati mbaya zaidi George hakupendezwa na tukio lile alijitokeza mbele ya wale vijana huku akiwa hana silaha yoyote ile.

Kwakuwa vijana hao wenye silaha nzito walikuwa wamefunika nyuso zao. Hawakuwa na shaka kabisa.
Walisimama huku wakiwa wanahewa kwa zamu. Mmoja wa vijana hao ambaye alionekana kuwa na umbile kubwa kwa haraka haraka ni wale vijana wanaofanya sana mazoezi ya kimwili.
Aliosegea pole pole na kumkaribia George aliokuwa hana silaha yoyote. Huku yeye akiwa ameshirikilia panga lake lile lile tena kwa ukakamavu.

George alikunja ngumi ili liwalo na liwe lakini kwa bahati mbaya alikanywagwa na teke zito kifuani na kumfanya adondoke chini huku akiendelea kutokwa na damu mdomoni.

"Nina uwezo wa kukuua lakini sidhani kama huu ni wakati wako wa kufa." Jitu hilo lilizungumza huku akimshtua mwezake kwa ishara wapate kuondoka.

Baada ya kupotea kabisa ndipo marafiki wawili wa George waliokuwa wamejificha walijitokeza huku Ngoda akiwa amemshirikia mdada huyo aliokuwa akikimbizwa.

Kumbe wakati George alipokuwa akijibizana
****
nao. Mdada aliokuwa akikimbizwa alipata kujificha sehemu ambayo alikuwa amejificha Ngoda rafiki yake George naye alipata kushudia kila kila kitu.

Ila mwanzo alivyouona uwepo wa Ngoda alitaka kupiga kelele kwa kuhisi ni moja kati ya majambazi lakini Ngoda alimsihi kwa sauti ya chini yakuwa yupo mahali salama.

Ndipo alivua shart lake na kumsitiri nusu ya mwili wake maana alikuwa uchi wa mnyama. Japo alikuwa na hofu sana.

****
Walitoka baada ya vijana wale makatili kupotea kabisa.

Hussen na Ngoda pamoja na Mdada huyo walikuwa kwenye majonzi maana waliona namna ambayo George amejitoa, hawakuwa na budi kumuwahi kisha wakambeba maana alionekana yuko hatarini kupoteza maisha.
Wakiwa wamembeba kwa kumlaza chali huku Ngoda akiwa ameshikiria mikono na Hussen akiwa ameshikiria miguu.
Ghafla......

Je, nini kitaendelea..........
IMG_20211121_194604_218.jpg
 

Mzurulaji

Member
Sep 25, 2021
15
45
Simulizi;Hisia
Mtunzi;Raja Mastory
Whatsapp;0762827579
SEHEMU YA KWANZA ( 02 )

ILIPOISHIA....

Hussen na Ngoda pamoja na Mdada huyo walikuwa kwenye majonzi maana waliona namna ambayo George amejitoa, hawakuwa na budi kumuwahi kisha wakambeba maana alionekana yuko hatarini kupoteza maisha.
Wakiwa wamembeba kwa kumlaza chali huku Ngoda akiwa ameshikiria mikono na Hussen akiwa ameshikiria miguu.
Ghafla......

ENDELEA NAYO....

George alipoteza fahamu papo hapo.
Kwa mbali mwanga hafifu ulionekana.
Ndipo Ngoda alipopiga kelele za kumshihi dereva aweze kukata kona na kuja mahali walipo.

"Heii heiii Usafiri usafiri."

Alikuwa ni boda boda aligeuza piki piki na kwenda hadi mahali walipo kisha kwa haraka sana.

Wakampakiza George ila wakati wa kupanda ilikuwa vigumu wote kuenea mahali hapo.
Ilimbidi Hussein aende na George hospitalini, aliokuwa amepoteza fahamu. Ngoda alibaki na mdada huyo ambaye mpaka kufika muda huo hakuwa amezungumza chochote.

"Endesha kwa kasi tuelekee Bugando."

Ngoda akiwa amebaki na mdada huyo alimsihi waondoke kisha wakapiga hatua kadhaa za kuelekea mahali anapoishi.
Na mdada huyo hakuweza kukataa kabisa kwani alijua tayari yupo mikono salama.

***

Dereva aliendesha kwa kasi sana na ndani ya dakika 15 tayari walikuwa wamefika Bugando na mapokezi ya haraka yakafanyika.

Tayari kwa kuanza kupewa huduma.

Si kwamba George alikuwa na hali ambayo ingempelekea kulazwa. Lakini alikuwa kwenye hali ambayo ilihitaji msaada wa haraka zaidi.

Baada ya kupokelewa na kupewa chumba alianza kupewa huduma za haraka pamoja na kuchomwa sindano za maumivu ili aweze kurudi kwenye hali yake.

Huduma zilifanyika kwa ustadi wa hali ya juu.
Kisha Nesi akatoka ndani ya Ward na kwenda kumpa taarifa Hussein aliokuwa upande wa nje.

Baada ya Hussein kumuona Nesi aliopewa dhamana ya kumuhudumia George, alisimama kwa heshima huku akionekana dhahiri mapigo yake ya moyo yanadunda kwa taarifa itakayotoa kwa wakati huo.

"Kaka habari, mgonjwa wako yuko salama hana shida na kwakuwa ulisema mwanzo alishambuliwa na majambazi hivyo tulikuwa tunahakikisha tunatoa huduma kwa ufanisi ili kunusuru uhai wake. Pia huwa si utaratibu kumuhudia mgonjwa alioweza kushambuliwa na majambazi au aliokuwa na jambo lolote kinyume na sheria pasipokuwa na dhamana yoyote kutoka kituo cha polisi. Hivyo tunakuomba uweze kufatilia PF3 katika kituo chochote cha polisi kisha urejee mahali hapa. Pia kwa hali alionayo mgonjwa wako kuna huakika hatutomlaza unaweza kuondoka naye pindi utakaporejea."

Kwa haraka zaidi Hussein aliondoka na kwenda kufuatilia PF3 kwenye kituo chochote kile. Maana hiyo, ni kama dhamani ya matibabu maana kwa hayo maswala ya uvamizi yapoga chini ya Serikali. Hii inamaanisha huenda ukawa unamtibu jambazi anayetakiwa awe chini ya mikono ya sheria.

***

Baridi ilikuwa kali sana japo Ngoda na mdada walikuwa tayari wameshaingia ndani ya nyumba iliokuwa na vyumba vinne pamoja na Jiko na bafu bila kusahau na Sebule.
Ni nyumba ambayo ilikuwa imekamilika kila idara.

Ngoda alimsihi mdada huyo aweze kumfuata kwa nyuma, hapo ni baada ya kuwa wameingia ndani ya nyumba hiyo. Nyumba waliokuwa wakiishi watu watatu Ngoda, Hussein na George. Baada ya kumpeleka kwenye chumba cha wageni na kumkaribisha.

Alirudi chumbani mwake kisha akachomoa tracker iliokuwa na Sweta lake kisha akampelekea chumbani.
Na kumsihi aoge kwanza ndipo avae nguo hizo.
Hakuishia hapo alimletea na taulo kisha akamuelekeza na bafu ilipo. Huku mdada huyo akimfuata kwa nyuma.

Baada ya huakikisha tayari mdada huyo alikuwa yupo ndani ya bafu akikoga maana bafu ilikuwa moja tu kwenye nyumba hiyo.

Alienda jikoni kisha akawasha gesi haraka sana na kupasha wali pamoja na maharagwe baada ya dakika 10 akapakua na kwenda hadi chumbani mwa mdada huyo.

Alivyofika aligonga mlango kwani tayari alikuwa ameshamaliza kukoga. Akamkabidhi chakula na kumsihi aweze kula kisha mdada huyo akaitika kwa kichwa ndipo Ngoda alipoondoka zake.

****

Hussein alirejea hospitalini, hapo ni baada ya kutoka kwenye kituo cha polisi mabatini kwa kutoa maelezo kamili na kupewa PF3 kama ruhusa.

Kwa bahati nzuri alimkuta tayari George ameshamka japo alikuwa akihisi maumivu kifuani kwa mbali sana.

Alikabidhiwa dawa za kumeza hapa ni baada ya kuwapatia PF3 kisha Hussein akalipa fedha waliokuwa wanadaiwa wakaita boda wakaondoka kurudi nyumbani.

***

Ngoda alishindwa kula kabisa, tayari alikuwa akiuwaza muonekano wa yule dada. Alijua tu lazima Hussein atarudi asubuhi kwani tayari alifanya makadirio. Kwa hali aliokuwa nayo George ni mbaya itamlazimu Hussein kulala.

Baada ya kupiga hesabu za haraka haraka huku akiwa chumbani kwake.

Akatoa uamuzi moja anaenda kumuomba mchezo maana hisia tayari zilikuwa zishampanda. Ikishindikana ambake na kumfukuza.
Na ikitokea wakina Hussein na George wamekuja kesho yake awadanganye alivyoamka hakumkuta.
Alivuta droo yake kisha akachomoa Condom za kuweka paketi zima mfukoni na kuanza kupiga hatua za kuelekea mahali kilipo chumba alichokuwepo mdada huyo.

Je, nini kitaendelea.....
Kama unahiitaji Yote nicheki Whatsapp namba 0762827579
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom