Simulizi ya Kweli: Nimeanguka kimapenzi na mtu nisiyemjua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simulizi ya Kweli: Nimeanguka kimapenzi na mtu nisiyemjua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by fiksiman, Apr 14, 2009.

 1. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu mnaweza kushangaa ama kuhisi nimepungukiwa na akili kama nikiwasimulia kisa hiki kilichomkuta rafiki yangu wa karibu. Yeye ametokea kupendana na msichana baada ya kuchat nae kwenye simu na hadi dakika hii anafanya mpango wa kumuoa. Shida ni moja tu kuwa mawasiliano ni kwenye simu tu na hawana njia nyingine ya kuonana. Hii inamaana kuwa kama mmoja hana simu hata kwa mwezi basi hakuna njia ya kuwasiliana si kwa marafiki wala ndugu. kisa kilianza hivi:

  Miezi sita iliyopita karimu alipokea ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwa mtu asiyemjua ukisema "Hi dear, I miss you". Haikuwa ni mara yake ya kwanza kupokea ujumbe wa namna hii na mara nyingi huwa hajishughulishi kujibu wala kushtushwa na sms za namna hiyo. Hata hivyo alijikuta akiuhifadhi ujumbe huo bila sababu. Simu ya karimu mara huwa bize na hupokea sms nyingi kwa siku. Hivyo wakati mwingine hulazimika kuzifuta ili kutoa nafasi kwa sms zingine kuingia. Pamoja na utaratibu huo hakuwahi hata siku moja kufikiria kuifuta ile sms.

  Ilimchukua mwezi mmoja na nusu bila kufanya jambo lolote na ile sms, hakuijibu wala kuifuta sms ile ya ajabu.

  Fuatilia kisa hiki na upate kujua..karimu atachukua hatua gani baada ya kukaa na sms ile kwa takribani miezi miwili bila kumtafuta mhusika.....wiki ijayo hapa hapa JF

  ............................Mpya...........................Mpya................Mpya....................

  Kijana Karimu anakutana na sms yenye utata na anaumua kufuatilia undani wa sms hiyo na mwisho wa siku anajikuta kwenye dimbwi zito la mahaba na mtu asiyemjua huku akipitia vikwazo vingi kutoka kwenye familia ya mpenzi wake. Je nini hatma yao wawili hao ambao wampendana bila kujuana sura wala umbo.

  katika simulizi iliyopita tulipata kuona namna Karimu alivyoamua kumsaka mhusika aliyemtumia ujumbe ule wa mapenzi kwa kumpigia simu...tuendelee.

  Sauti ya upande ilimshtua kidogo karimu kwa kuwa alihisi kama si ngeni masikioni pake. Akatulia akijaribu kuvuta kumbukumbu wapi aliwahi kusikia sauti hiyo bila mafanikio. Ndipo aliamua kuendelea na mazungumzo. Wakati huo wote alikuwa na uhakika na salio kwani alijiunga na mtandao maarufu kwa huduma ya extreme hivyo hakuwa na haraka ya kuishiwa salio.

  Sauti: (kwa ukali) wewe nani na upataje namba yangu?

  Karimu alijitutumua na kuendelea kumbana na maswali. "Utaniulizaje mi nani wakati wewe ndo ulienitumia sms, kwanza unaitwa nani na uko wapi?" sauti ile ilipoona karimu anakuja juu ilitulia na kurejea katika hali yake ya kawaida na kujitambulisha

  Sauti: Mi naitwa nasma. niko unguja, mbona mi sijawahi kukutumia sms! alijibu kwa mshangao.

  Karimu: "Sasa kama hukuwahi kunitumia sms hii ni ya nani au nikuforwardie uone ulituma lini na saa ngapi? Kuwa makini unapotumia simu sio mnasumbua watu nyie ndo mnaovunja ndoa za watu kwa papara zenu." alimaliza na kukata simu.

  Pamoja na ukweli kuwa karimu alikata ile simu bado rohoni aliamini kuna jambo kwenye sauti ya nasma. Hiyo ilikuwa asubuhi jumatano ya tarehe 7 wiki moja tu baada ya kuona mwaka mpya.

  Baada ya nusu saa ya mazungumzo yale alipokea sms kwenye simu yake na alipofungua alishtuka kuona imetoka kwa nasma. Iliandikwa hivi, "Nimeenda kwenye kabati langu na kuangalia notebuk ya mdogo nimekuta amesave namba hii kama mbongo, hivyo inawezekana ni yeye alikutumia sms hiyo" nilijikuta natabasamu bila sababu.

  akamjibu kwa jeuri, "Basi mi nataka kuongea na huyo aliyenitumia sms, akifika mwambie anitext au aniflash". Nae akajibu "poa" akionyesha kutoridhika na jibu alilopata toka kwa karimu. Hadi dakika hiyo bado alikuwa na hisia za kuitambua sauti ile.

  Kwa faida ya wafuatiliaji wa kisa hiki, Karimu ni kijana mwenye umri kati ya 25 na 30, anajishugulisha na uandaaji wa vipindi vya Redio na Tv na mara nyingi husafiri sehemu mbalimbali za Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa shughuli hiyo, hivyo aliamini inawezekana aliwahi kukutana na sauti ile wakati alipokuwa zanzibar ingawa hakuwa na uhakika.

  Basi, karimu baada ya kumalizana na nasma aliendelee na shughuli zake huku kichwani sauti ya nasma ikijirudiarudia. Ilikuwa majira ya saa kumi na moja jioni ilipoingia sms kutoka kwa nasma, "Haya aliyekutumia sms huyo hapa chat nae, bye" ilimaliza sms hiyo.

  Alipatwa na wasiwasi kidogo kwani alihisi nasma anataka kumghiribu hivyo akaamua kupiga badala ya kuchat nae. Basi mtoto wa kiume akaenda hewani, brrr brrr brrr brrr, simu ikaita na upande wa pili ikapokea, "Hello, Assalaam aleykum" akajibu Aleykum assalaam, naongea na nani? Ikajibu upande wa pili, mi naitwa raisa. Akaendelea kuuliza, wewe ndo uliyenitumia sms? Ikajibu ndio. Karimu akaishiwa na maneno.

  Baada ya kimya kifupi karimu akachokoza, "Sasa raisa wewe umesema unanimiss kivipi wakati hata hunijui kwanza umepata namba yangu?" Raisa akajibu kwa utulivu, nimeitoa kwenye kipindi chako. Hapo mchezo ukaisha akabaki mdomo wazi kwa mshangao. Raisa akaendelea, "unajua karimu mi nakupenda na nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu vipindi vyako". Hapo uzalendo ukamshinda Karimu akahoji, "Utanipendaje wakati hunijui wala sikujui huoni unataka kunizingua?" Raisa akaendelea kung'ang'ania na msimamo wake. Karimu alishindwa cha kusema zaidi ya kucheka.

  Baada ya mazungumzo ya dakika kama 15 hivi, Raisa akaomba waongee usiku kwa kuwa dada yake (nasma) amekasirika sana ametumia simu yake kuwasiliana na wanaume na matokeo yake yeye anatukanwa bila sababu hivyo amelala kichwa kinamuuma sana. Akaendelea, "dada ni mkali sana na hapendi wanaume kwani anamashetani kichwani na wanaume wengi wamemtaka amewakatimua". Karimu hakushtuka sana kwani alijua kwa maneno yale lazima angekasirika tu. Pia aliona ahueni kwani muda wa extreme ulikuwa unaelekea kuisha.

  Basi wadau tuishie hapo kwa leo...inshallah tukijaliwa tutaendelea kesho. Pia niwashukuru kwa maoni yenu hasa wale ambao hawakioni kisa hiki kama ni muhimu au msaada. Sina majibu ya kuwapa ila naamini wapo wanajamii wenzangu wanahamu ya kutaka kujua mwisho wake au walishakutana na kisa kinachofanana na hiki.

  Ahsanteni.
   
  Last edited: Apr 18, 2009
 2. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Hadithi za shigongo nini?!...Endeleeea na toleo lijalo
   
 3. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hiyo ni ya kiukweli kabisa...subiri upate habari zake.
   
 4. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapa sio kindagateni uwapa watoto wa chekechea hadithi za bunuwasi...eti watu wasubiri mpaka juma lijalo...usingeileta kama haijakamilika basi.
   
 5. K

  Kijunjwe Senior Member

  #5
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ilikuwa busara ungekamilisha hiyo hadithi(Simulizi) kabla ya kuja na kutuandikia kuwa tusubiri mpk next week.
   
 6. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  wadau mwataka kumtoa roho...subirini niwaongezee kidogo.

  Basi ilikuwa tarehe 7 mwezi wa kwanza...mwaka 2009 baada ya pilikapilika nyingi za kuukaribisha mwaka mpya ndipo karimu alipoamua kufanya uamuzi wa kujua nani aliyemtumia sms ile. kumbuka sms hiyo aliipata mwezi wa novemba kwenye tarehe 10 hivi. Asubuhi na mapema baada ya kufungua kinywa akajishauri ni njia gani atumie kuwasiliana na mtu huyo alimweka akilini bila kujua sababu. Moyoni aliamini atakuwa anamjua kwa jinsi sms ilivyotumwa. Baada ya saa kama mbili aliamua kumpigia simu moja kwa moja. Shida ikawa moja anzie wapi hasa ukitegemea kuwa ni muda mrefu toka apokee ujumbe huo.

  Akachukua simu yake ya kiganjani na kwenda hewani huku moyo ukimndunda mithili ya simba aliyekuwa akifukuzwa na kundi la mbwa mwitu wenye njaa kali ya wiki nzima.

  Simu ikaanza kuita...brrr brrr brrr...sauti ya tamu ya kike ikapokea na kuita. halloo. Moyo ukalipuka kwa hofu huku ukidunda kwa kasi ya ajabu. karimu akajikaza kisabuni na kujibu, hallo habari za asubuhi....nzuri tu we nani(ikauliza ile sauti). kimya kikatwala kwa sekunde kadhaa......karimu akawa hajielewi uwezo wa kuongea ukaanza kuelekea kumuisha. Akajitumumua na kusema kwa kujiamini. Nikuulize wewe si ndo umenitumia sms!!

  Naam wadau mambo ndo yameshaanza kukolea...karimu kaamua kwenda hewani baada ya muda mrefu. je nini kitatokea. Endelea nami kesho naona wadau wameanza kunitia kinywani. Hadithi hii si ya kubuni bali ni kisa cha kweli kilichomtokea mtu fulani hivyo sijaitunga tafadhali wadau.
   
  Last edited: Apr 14, 2009
 7. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Jina lenyewe linajitosheleza, fix tupu hakuna la zaidi teh teh sina mbavu. Please mcheki Shigongo kama vipi.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Uwizi mtupu..
   
 9. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Sasa naona ushakuwa uwanja wa hadithi huu!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,588
  Trophy Points: 280
  Hiyo hadithi yako inabore itafutie mahali pengine, hapa JF haifai kabisa maana haina mwelekeo.
   
 11. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #11
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mh! kaaaazi kweli kweli!
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  JF jukwaa huru maana hata mafiksmen wapo humu.
  Itabidi tuwalengeshe kwa lyatonga wakaMFIKSI
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Jina lako tu ni mtu wa fiksi sasa sijui tuamini huu ukweli>?
  Na fiksi ni uongo....ngoja twendelee kuburudika.
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ukiona hivyo hiyo stori hana hakimiliki nayo hivyo anaitoa kwa kuiba iba.
  Kelly upo wapi laziz?
   
 15. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  naona sasa jamvi hili taratiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiibu linaanza kupoteza ule umaana wake
   
 16. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Aliyeileta hii fiksi anajiita fiksiman, the nick name itself is enough. Alipochagua nickname hiyo perhaps inakwenda sambamba na jinsi alivyo!!! Anyway, let us not become fiksiman like him by discussing this, it is a wastage of our precious time, energy and resources!
   
 17. M

  Msindima JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Naona riwaya hiyo inaanza ngoja tuisubirie.
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  fiksi tupu humu
   
 19. locust60

  locust60 Senior Member

  #19
  Apr 15, 2009
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mkuu hiyo hadithi ungepeleka kwenye magazeti ingesaidi kuuza magazeti lakini humu ndani hata si mahara pake.fikiria vizuri.
   
 20. kisale

  kisale Senior Member

  #20
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani kama alikuwa anahitaji ushauri wetu angejaribu kutueleza mambo ya muhimu then tuangalie tutamsaidiaje.Au tuambie kabisa Hadithi yako inatufundisha nini,kwa sababu muda wa kusoma tamthilia hatuna.Au una nia gani kuandika hiyo story.
   
Loading...