Simulizi Ya Kweli:Nilimuoa Jini Nikamsaliti

SEHEMU YA 16

Magari yalibeba mizigo kama kawaida na kuisambaza kwenye maduka yote ikiwemo kutenga makontena mawili kwa ajili ya duka la Posta lililounguzwa vitu vyake na moto wa ajabu. Baada ya kufikishwa zoezi la kufungua makontena lilianza mara moja. Msimamizi alishtuka kuona majivu ndani ya kontena bila bidhaa zilizoagizwa.
Hakuamini macho yake, alifungua lingine hali ilikuwa ileile, ilibidi apigiwe simu Thabit kuelezwa kilichoonekana kwenye kontena badala ya bidhaa walikutana na majivu kama yale yaliyokutwa dukani kwake.
Taarifa ile ilimfanya Thabit kwenda haraka kujionea, alipofika alioneshwa mali iliyoteketea kwa moto wa ajabu. Lilikuwa pigo jingine, hakuamini alikwenda kwenye makontena yote hali ilikuwa ileile. Ilikuwa mali ya fedha nyingi sana aliamini kabisa wamemmaliza.
Kutokana na mshtuko alianguka chini na kupoteza fahamu, ilibidi akimbizwe hospitali. Alipimwa vipimo vyote lakini ugonjwa haukuonekana. Upande mmoja wa mwili wake ulipooza ghafla. Lilikuwa pigo mujarabu lililomchanganya sana, Subira naye alichanganyikiwa na kumpigia simu mzee Mukti na kumueleza kilichotokea.
“Mzee wangu mbona kila siku matatizo yanazidi?”
“Kilichotokea kilikuwa nje ya uwezo wangu, ndoto ya kuungua vitu ndani ya maji niliiona lakini sikujua ilikuwa ina maana gani.”
“Kwa nini hukuzuia?”
“Ilikuwa vigumu kama ningeingia kwenye ufalme wao wa maji kwa ajili ya vita nisingerudi salama, wangenipoteza kwa njia yoyote.”
“Sasa tutafanyeje maana hali na mpenzi wangu ni mbaya sana?”
“Atapona ni mshtuko tu.”
“Nini hatima yetu?”
“Ulichelewa kunijulisha tungeweza kuanza mchakato mapema ili kuokoa mali zenu.”
“Mmh! Nitaolewa kweli?”
“Utaolewa, kuna dawa utaletewa na kuitumia kumpa itamsaidia.”
“Sawa, na mali iliyobakia itasalimika kweli?”
“Ile ipo salama wala usihofu.”
“Sawa basi nasubiri.”
Mzee Mukti ilibidi aangalie ugonjwa wa Thabit tatizo nini, jibu lilimtisha kuonesha bila kazi ya ziada Thabit atakuwa mlemavu milele. Aliamini dawa zake zote zisingeweza kumtibu ilikuwa lazima asafiri kwa siku mbili ili afuate dawa ambayo nayo ilikuwa bahati nasibu japo ilionesha kila dalili za kulemaa kwa Thabit.
Ugonjwa wa Thabit ulifanya iwe furaha kwa Hailat na mama yake.
“Mama Thabit kwisha.”
“Kwa nini?”
“Kazi uliyonituma imeleta matokeo mazuri.”
“Imekuwaje?”
“Amepooza upande mmoja si wa kupona leo kesho.”
“Sasa tuone kama yule mwanamke ataendelea kuwa naye.”
“Halafu yule mganga anajitia kiherehere kumtibu, tumshughulikie nini?”
“Mwache amtibu, lakini atachukua muda kupona na muda wote huo lazima yule mwanamke atamkimbia.”
“Kama hivyo sawa.”
Nargis akashangaa kuona mama na dada yake wakinyamaza ghafla baada ya kumuona. Ilimshtua sana na kuamini kuna kitu juu yake walikuwa wakimteta. Aliwapita bila kuwasemesha lakini moyoni alijawa na wasiwasi juu ya kikao kile cha faragha cha mama yake na dada yake. Alizunguka na kujificha nyuma ya mlango.
Alichokisikia roho ilimuuma sana na kuona jinsi gani familia yake imeamua kwenda kinyume na makubaliano juu ya mumewe Thabit kumuacha kama alivyo. Hakutaka kusema chochote alijipanga kurudisha kila kitu kilichopotea kwa mpenzi wake bila kujua kama akirudi duniani atakubaliwa na mumewe au atatoswa.
Alijipanga kuondoka usiku kwenda kurudisha kila kitu cha mumewe kilichopotea kuanzia dukani mpaka kwenye makontena. Naye aliamua kufanya kwa siri ili familia yake wasijue kinachoendelea. Usiku baada ya kuwaweka vizuri wanawe alitoka chini ya bahari na kwenda moja kwa moja nyumbani kwake.
Alipokaribia kwenye nyumba ya Thabit aliona bahari, japo moyo ulimuuma nyumbani kwake kuwa kwenye hali ile.
Alijaribu kuingia katika umbile la kijini joto la maji ya moto lilimzuia, akalazimika kurudi katika umbile la kibinadamu na kuteremka kwa mbali kidogo. Aliweza kuiona nyumba yake.
Alitembea taratibu kuelekea kwenye nyumba ile, alipokaribia moto mkubwa ulionekana ukiizunguka nyumba yake. Alijua nyumba imezindikwa ili yeye na majini wote wasiingie katika nyumba ile. Kwa vile shida yake ilikuwa kurudisha mali iliyopotea aliondoka hadi dukani.
Kama kawaida alijirudisha katika umbile la kijini na kuruka kwenda sehemu ya maduka. Alipokaribia alijirudisha katika umbile la kibinadamu na kuweza kusogea kwenye duka. Aliusogelea ukuta wa duka na kuushika, akafumba macho na kuvivuta vitu vilivyopotea.
Baada ya muda aliviona vitu vyote vilivyokuwemo kabla, alivivuta taratibu mpaka kila kitu kilirudi kama zamani. Alitabasamu kuona mali ya mpenzi wake imerudi na duka lilijaa kama mwanzo.
Baada ya kumaliza zoezi lile alijirudisha katika umbile la kijini na kuruka hadi kwenye makontena yote na kuyashika kila moja na kurudisha kila kitu. Baada ya hapo alikwenda hospitali alipokuwa amelazwa mumewe.
Kwa vile hakukuwa na zindiko aliingia katika umbile la kijini na kuwapita watu bila kumuona.
Baada ya kuingia kwenye wodi aliyokuwa amelezwa mumewe, wakati huo hakukuwa na mtu mwingine chumbani.
Alimuangalia kwa huzuni na kuona ubaya wa viumbe kutaka kumuua mumewe bila sababu.
Akiwa amelala kitandani alipotaka kumshika alipigwa na shoti kama umeme na kumrusha upande wa pili. Alijua tayari na mumewe amezindikwa ili asiwe naye karibu. Hakuondoka alisimama pembeni ya Thabit aliyekuwa amelala hajitambui.
Kutokana na uchungu moyoni alijikuta akilia na machozi kumtoka, kwa vile alikuwa ameinama machozi yake yalitua kwenye paji la uso wa mumewe. Alishangaa kumwona akibadilika rangi mchanganyiko huku mwili ukitikisika kisha alirudi katika hali ya kawaida na mwili ulitulia.
Itaendelea wiki ijayo.
Alimuona Thabit akifumbua macho na kupepesa kasha alijinyoosha kuonesha yupo sawa. Nargis alitaka kumsemesha lakini hakutakiwa kufanya vile kwa vile sicho kilichompeleka na muda ule.
Aliamini kila alichokipanga kimekwenda kama alivyotaka aligeuka na kuondoka na kumuacha mumewe akiwa hajambo na kuamini taarifa atakayoisikia juu ya mali zake kurudi atamuongezea furaha.
Kwa vile alikuwa ametoka usiku sana aliwahi kurudi chini ya bahari kabla familia yake haijagundua kitu.
Inaendelea
 
SEHEMU YA 17

Kutokana na uchungu moyoni alijikuta akilia na machozi kumtoka, kwa vile alikuwa ameinama machozi yake yalitua kwenye paji la uso wa mumewe. Alishangaa kumwona akibadilika rangi mchanganyiko huku mwili ukitikisika kisha ilirudi yake ya kawaida na mwili ulitulia.
Alimuona Thabit akifumbua macho na kupepesa kisha alijinyoosha kuonesha yupo sawa. Nargis alitaka kumsemesha lakini hakutakiwa kufanya vile kwa vile sicho kilichompeleka muda ule.
Aliamini kila alichokipanga kilikwenda kama alivyotaka aligeuka na kuondoka na kumuacha mumewe akiwa hajambo na kuamini taarifa atakayoisikia juu ya mali zake kurudi atamuongezea furaha. Kwa vile alikuwa ametoka usiku sana aliwahi kurudi chini ya bahari kabla familia yake haijagundua kutoka kwake.
Thabit baada ya kujiona yupo vizuri alinyanyuka kitandani na kutoka nje ya wodi, muuguzi alishtuka sana kumuona mtu aliyekuwa yupo hoi hajiwezi ameweza kunyanyuka kitandani na kutembea kama kawaida.
“Kaka vipi?”
“Safi.”
‘Si...si ni wewe uliyekuwa u...u..kiumwa?” muuguzi alishtuka.
“Ndiyo.”
“Mmh! Haya ni maajabu, muda mfupi ulikuwa hoi na mimi nimetoka kukuhudumia. Nashangaa kukuona ukiwa mzima…halafu kuna dada alikuja kukuona yupo wapi?”
Wakati Nargis akija katika umbile la kibinadamu alikutananaye akitoka kumpa dawa mgonjwa akiwa hajiwezi. Lakini dakika chache alishtuka kumuona akitoka akiwa mzima wa afya njema kama hakuwahi kuugua ugonjwa wowote, lakini yule dada mrembo hakumuona.
“Dada gani?” Thabit alishtuka.
“Kuna dada mmoja mrembo sana, aliniomba akuone, nilipomkatalia alianza kulia kwa kusema wewe ni mtu wake muhimu sana na asipokuona leo itachukua muda wa miaka minne kuonana. Nilimruhusu lakini ajabu alivyotoka sikumuona na wewe kukuona hujambo.”
“Kwa kweli sijamuona mtu, ila namshukuru Mungu sasa sijambo.”
Thabit akiwa bado anazungumza na muuguzi aliyemshangaa simu yake iliita.
“Haloo.”
“Asalam aleykum mpenzi?”
“Waleykum salam, mpenzi wangu nani?”
“Huwezi kunitambua kwa kujieleza mpaka unione, nilitaka kukujulisha nimefurahi kukuona umepona pia mali zako zote zipo kama kawaida.”
“Mali zangu zipi?”
“Kwani kipi kilichokufanya uugue ghafla?”
“Mmh! Za dukani.”
“Basi kila kitu kipo vizuri, ila kumbuka ahadi.”
“Ahadi gani?”
“Utaijua baada ya miaka minne.”
“Sawa.”
“Kwaheri ya kuonana,” baada ya ujumbe wa utata Nargis alikata simu na kurudi zake chini ya bahari.
Baada simu ya Nargis kukatika bila kumshtua Thabit juu ya ahadi aliyowekeana na mkewe siku aliporudi chini ya bahari kujifungua baada ya kuvurugwa akili na Subira na kumfanya asimkumbuke tena mkewe Nargis.
“Kaka naomba niwasiliane na mganga mkuu ili nimueleze maajabu haya ili nijue atafanya nini,” muuguzi alishindwa kumruhusu.
“Hakuna tatizo niache niondoke .”
“Subiri.”
Muuguzi alimjulisha mganga mkuu aliyefika pale na kumshangaa Thabit ambaye walikuwa wakipanga kumpeleka nje ya nchi kimatibabu.
“Haya ni maajabu, mtu uliyekuwa hujiwezi lakini ghafla umepona!”
“Kwani nilikuwa naumwa sana?”
“Kila aliyekuona alikuwa akilia, mpaka sasa hivi naona kama ndoto.”
“Yote ni maajabu ya Mungu.”
“Basi tunaomba tukufanyie vipimo kabla ya kukuruhusu kwa vile bado akili yangu haiamini.”
“Hakuna tatizo.”
Walikwenda chumba cha uchunguzi ili kumfanyia uchunguzi wa kina Thabit, muda wote muuguzi na mganga mkuu walikuwa wakijiona kama wapo ndotoni. Wakiwa chumba cha uchunguzi simu ya Thabit iliita, alipoangalia ilikuwa ikitoka kwa msaidizi wake.
“Haloo.”
“Bosi?”
“Ndiyo.”
“Haya ni maajabu ya karne.”
“Kwa nini?”
“Kuna simu nimepigiwa na mwanamke mmoja yenye lafudhi ya mwambao na kunieleza kuwa vitu vyote vya bosi wako vimerudi kama zamani, vyote tulivyoviona ilikuwa kiini macho. Niliondoka hadi kwenye makontena na kukuta kweli vitu vyote tulivyoagiza vipo.
“Kingine alichoniambie eti hata ugonjwa wako ni kiini macho na kama siamini baaada ya kuona vitu vyote nikupigie simu. Baada ya kukuta vitu vyote vipo nimekupigia simu na wewe kupokea na kukuta hujambo haya ni maajabu ya karne.”
“Hata mimi mtu huyo kanipigia simu na kunieleza kuwa vitu vyangu vimerudi.”
“Ni nani?”
“Hata simjui amesema nitamjua baada ya miaka minne.”
“Sasa atakuwa nani?”
“Akija tutamuona.”
“Basi bosi lazima tufanye sherehe kubwa.”
“Lazima tufanye.”
Baada ya kuzungumza na msaidizi wake, alifanyiwa vipimo vilivyoonesha hakuwa na tatizo lolote mwilini. Kabla ya kuondoka alimpigia simu Subira aliyekuwa amefuata dawa Kigamboni kwa mzee Mukti. Baada ya kupokea alishtuka na kusikia anayezungumza ni mpenzi wake Thabit alikataa.
“Wewe unayezungumza ni nani?” Subira hakuamini kusikia sauti ya mpenzi wake.
“Nini mpenzi wako.”
“Hebu acha utani, niambie wewe ni nani?”
“Subira mpenzi wangu ni mimi Thabit mpenzi wako.”
“Siwezi kuamini wewe si Thabit,” Subira alikataa katakata.
“Nifanye nini ili ujue mimi ni mpenzi wako?”
“Hata ufanyeje siwezi kukukubalia,” Subira alibisha kutokana na hali aliyomuachanayo jioni ile.
Itaendelea
 
SEHEMU YA 18

“Subira mpenzi wangu ni mimi Thabit mpenzi wako.”
“Siwezi kuamini wewe si Thabit,” Subira alikataa katakata.
“Nifanye nini ili ujue mimi ni mpenzi wako?”
“Hata ufanyeje siwezi kukukubalia,” Subira alibisha kutokana na hali aliyomuachanayo jioni ile.
SASA ENDELEA...
Mpaka kukimbilia kwa mzee Mukti ambaye aliangalia na kumweleza mpenzi wake atapona lakini ugonjwa lazima ungemsumbua na kuchukua muda mrefu.
“Fanya hivi nifuate hospitali, kwani upo wapi?”
“Nipo Kigamboni.”
“Basi fanya haraka nimeruhusiwa muda si mrefu.”
“Nakuja, lakini wewe si Thabit,” bado alikataa.
Subira pamoja na kuelekea hospitali alipokuwa amelazwa Thabit akiwa na dawa za kumchua na kunywa alizopewa na mzee Mukti.
Aliendesha gari hadi hospitali na kulipaki pembeni na kukimbilia ndani ya wodi. Kutokana na papala alimpita mpenzi wake aliyekuwa amekaa mapokezi.
Aliingia mpaka wodini na kushtuka kukuta kitanda kitupu mawazo yake yalimpelekea labda Thabit amefariki. Alijikuta akiangua kilio cha sauti na kufanya muuguzi kumfuata na kumuuliza analia nini.
“Yupo wapi mpenzi wangu?”
“Umemuacha mapokezi.”
Bila kusema neno aligeuka hadi mapokezi na kumkuta Thabit amejaa tele akiwa mzima wa afya kwa mshtuko alianguka chini na kupoteza fahamu asiamini alichokiona na kuona kama yupo ndotoni.
Alipewa huduma ya haraka iliyomrudisha katika hali yake ya kawaida.
Baada ya kupata nafuu alimuangalia mpenzi wake asiamini kilichotokea bado alijiona kama yupo ndotoni.
“Ni wewe mpenzi wangu?”
“Ni mimi.”
“Hapana,” Subira alisema huku akimpapasa mpenzi wake ili kuhakikisha kama ni yeye kweli au anaota mtu aliyemuacha muda mfupi akiwa hajitambui viungo vyote havifanyi.
“Ni mimi.”
Subira alimkumbatia Thabit kwa furaha baada ya kuamini kweli aliyembele yake ni mpenzi wake akiwa mzima wa afya njema.
“Yaani siamini.”
“Basi amini, hata vile mali zilizopotea zimerudi.”
“Unasema!”
“Mali zilizoungua dukani na kwenye makontena zimerudi kama kawaida.”
“Jamani huu si utani au unanitania mpenzi wangu?”
“Sikutanii kama umenikuta mzima kabisa basi na kila kitu changu kipo salama.”
“Haya ni maajabu ya dunia.”
“Walaa si maajabu lile ni jasho langu la halali haliwezi kutoweka kiajabu.”
Kabla ya kuondoka Subira alimpigia simu mzee Mukti kumjulisha juu ya tukio lile la ajabu ya karne. Taarifa ile ilimshtua sana na kuuliza:
“Ha! Unasema kweli?”
“Kweli kabisa ninavyokuambia nipo naye sasa hivi mzima wa afya kabisa.”
“Subira unanigeuza mtani wako wa kunitania?”
“Walaa kweli kabisa.”
“Mmh! Unajua siamini.”
“Kama huamini ngoja nikupe uzungumze naye.”
“Hebu nipe.”
Subira alimpa simu Thabit aliyezungumza:
“Haloo mzee.”
“Wewe ni Thabit?”
“Ndiyo.”
“Mpenzi wa Subira?”
“Ndiyo.”
“Mmh! Kimetokea nini?”
“Kwa kweli mpaka sasa sijui, namshukuru Mungu kama nilikuwa mgonjwa lakini sasa mzima wa afya.”
“Sawa, umeishafika nyumbani?”
“Ndiyo nataka kutoka hospitali.”
“Basi kapumzike.”
“Sawa mzee naomba basi utengeneze mambo naona wabaya wangu bado wananiandama.”
“Hakuna tatizo.”
Kabla ya kukata simu Subira alichukua simu na kumwambia kitu mzee Mukti kilichozidi kumshangaza.
“Babu yaani haya ni maajabu ya mwaka hata vitu vyote vilivyoungua dukani na kwenye makontena vimerudi.”
“Wewee!” mzee Mukti aliona sasa ule ni utani.
“Hata mimi nilikuwa kama wewe, kwangu bado naona kama ndoto lakini huo ndiyo ukweli wenyewe.”
“Hebu subiri niangalie kipi kimetokea.”
“Sawa, sisi tunakwenda nyumbani, vipi zile dawa nimpe?”
“Usimpe mpaka nitakapokupa maelekezo.”
“Sawa.”
Baada ya Subira kukata simu na kumshika mkono mpenzi wake ili waondoke, mzee Mukti alichanganyikiwa na kuingia kwenye rada zake kuangalia nini kimetokea tofauti na kitu alichokiona juu ya matukio yale. Kwanza kwenye rada yake kuonesha moto mkubwa.
Hakukubali alitumia uwezo wake wote kutaka kujua nini kimetokea tofauti na kitu alichokiona. Baada ya moto kutulia aliona jinsi jini Nargis alivyo mponya Thabit na kurudisha mali zote zilizoteketezwa kijini. Matukio yale yalimshangaza na kujiuliza kufanya vile alikuwa na maana gani.
Lakini aliamini mali yote iliyorudi haitateketea tena kwa vile sehemu ile alikuwa imeizindika. Ila kwenye makontena kulionesha pepesi hivyo palitakiwa kudhibitiwa usiku ule kabla upande wa pili haujarudi tena.
Aliwapigia simu na kuwajulisha baada ya mali kurudi walitakiwa kuzizindika ili zisiharibike tena. Walikubaliana na mzee Mukti alikwenda kuzizindika na kazi ilifanyika usiku wa manane.
Siku ya pili ilikuwa sherehe kwa wafanyakazi wote waliokata tamaa baada ya kuchanganyikiwa kutokana na mali kuteketea kila kukicha. Hali ilirudi kama kawaida na biashara iliendelea kwa Thabit kufungua maduka mengine makubwa kila kona ya jiji na kuanza kujipanga kufungua matawi mikoani.
Subira naye alitumia nafasi hiyo kuomba ndoa, Thabit hakuwa na pingamizi aliwatuma washenga walikwenda nyumbani kwao na Subira ndoa ilipangwa mara moja na siku ilipofika Subira aliolewa na Thabit kuwa mke wake halali wa ndoa.
Ilikuwa furaha isiyo na kifani baada ya Subira kutimiza ndoto yake ya kuwa mke wa Thabit.
Inaendelea
 
SEHEMU YA 19
Kutokana na kutoa ahadi kwa mzee Mukti Buguju kama akiolewa atampa zawadi kubwa, alimnunulia gari la kifahari la kutembelea na kumjengea nyumba kubwa pamoja na fedha taslimu milioni kumi. Alimuahidi kuendelea kumpa vitu vingi kwa vile alimfikisha alipopaota na kuona muujiza kufika pale.
Siku nazo zilikatika huku muda wa Nargis kurudi kwa mumewe ukikaribia, ilikuwa miaka ikawa mwaka ukawa mwezi na hatimaye siku. Nargis akiwa na wanawe wenye umri wa miaka kumi kila mmoja. Alikwenda kwa wazazi wake na kuwaeleza wiki ile alikuwa anarudi kwa mume wake Thabit baba wawili Zumza (Kurwa) na Zamzu (Doto).
“We Nargis una kichaa, utawezaje kurudi kwa mumeo ikiwa umeambiwa wanadamu wamekuwahi?”
“Mama mwanadamu na jini nani zaidi?”
“Jini, lakini mwanadamu yupo kama kinyonga hivyo anaweza kukuharibia maisha yako.”
“Mama kwa vile sasa nina uhuru wa kwenda popote, niacheni mwenyewe nakuhakikishia kama haitarudi maiti yangu hapa basi nitarudi na mume wangu.”
“Mmh! Mtoto wewe mbishi sana, we nenda yatakayokukuta usitushirikishe.”
“Hilo nalijua ila nilitaka kuwajulisha kuwa natoka kama nikifa nitunzieni wanangu.”
“Sawa.”
Nargis alirudi chumbani kwake kuwaaga wanawe, aliwakusanya kisha aliwaeleza:
“Wanangu, leo ninawaacha nakwenda kumtafuta baba yenu.”
“Mama unakwenda kumtafuta wapi wakati ulitueleza tutaondoka wote kwenda kwa baba?”
“Walimwengu wamenizidi akili lazima nitatumia uwezo wangu wote kumrudisha baba yenu mikononi mwangu la sivyo mtakuwa watoto wasio na baba.”
“Kwa nini tusiende wote?” Zamzu alimwambia mama yake.
“Hapana wanangu ninyi pumzikeni kazi hii nitaifanya bila tatizo.
“Mama mimi nina hamu ya baba naomba nikamuone tu kisha nirudi,” Zumza (Kurwa) naye alimwambia mama yake.
“Hapana wanangu nitamleta huku.”
“Mama mbona hatukuelewi mara unaenda kumtafuta umlete huku wakati ulituambia muda umebakia mdogo twende kwetu huku siyo kwetu sasa unakwenda kumleta baba aje afanye nini?”
“Zumza na Zamzu wanangu majibu yenu yote nitawajibu nikirudi.”
“Haya mama safari njema msalimie baba.”
Nargis baada ya kuagana na watoto wake alitoka rasmi kwenda duniani kumfuatilia mumewe.
Akiwa katika umbile la kibinadamu, jini Nargis alitokea duniani baada ya muda wake wa kukaa chini ya bahari kwisha.
Kabla ya kuondoka eneo la Salenda alitembeza macho kuiangalia dunia aliyoikosa kwa muda mrefu. Moyoni alijiapia hatarudi chini ya bahari mpaka amempata mumewe au arudi yeye akiwa maiti.
Baada ya kiapo chake aliachana na bahari na kutembea taratibu hadi karibu ya barabara na kujishika katika paji la uso baada ya muda mfupi alikuwa mbele ya ofisi ya Thabit ambayo ilikuwa imepanuka na kuwa ya kisasa zaidi.
Akiwa katika umbile la kibinadamu alitembea hadi akaingia ndani. Alifika mapokezi ambako ndipo alipokuwa mbaya wake Subira aliyemchukulia mumewe. Japokuwa moyo ulimuuma lakini alijikaza na kuficha hasira zake kwa vile hakurudi duniani kwa shari bali kuitafuta suluhu ya kumpata mumewe bila kumwaga damu.
“Asalaam aleykumu?” Nargis alimsalimia Subira aliyekuwa bize na kazi.
“Waleykum salaam,” Subira aliitikia huku akinyanyua uso kumwangalia aliyemsalimia mwenye sauti nzuri huku pua zake zikilakiwa na harufu nzuri ya manukato. Alishtuka kumuona mwanamke mzuri amesimama mbele yake.
“Karibu dada,” alimkaribisha bila kumjua ni nani.
“Asante.”
“Nikusaidie nini dada yangu?”
“Bwana Thabit yupo?”
“Mmh! Yupo, unaweza kukaa hapo ana wageni.”
“Inshaallah.”
Nargis alikaa kwenye kochi na kutulia kusubiri kuingia ofisi ya mumewe ambaye wakati huo alikuwa amemuoa Subira. Subira pamoja na kuendelea na kazi alimtazama kwa wizi mwanamke huyo mrembo aliyekuwa amekaa kwenye sofa akitembeza macho kuiangalia jinsi ofisi ilivyopendeza.
Baada ya nusu saa alitoka mtu aliyekuwa akizungumza na Thabit, kabla Subira hajanyanyua simu amweleze kuna mgeni, Thabit alitoka.
“Vipi kuna mgeni?”
Aliuliza baada ya kumuona Nargis aliyekuwa ametulia kwenye kochi.
“Ndiyo sweet.”
“Karibu,” Thabit alimgeukia Nargis na kumkaribisha.
“Asante,” Nargis alijibu huku akinyanyuka.
Thabit alitangulia mbele kuingia ofisini huku akifuatwa nyuma na Nargis, Subira alijikuta akivutiwa na mshono wa gauni alilovaa mgeni huyo. Thabit baada ya kukaa kwenye kiti alimkaribisha tena mgeni wake.
“Karibu bibie ukae.”
“Asante,” Nargis alijibu huku akikaa.
Thabit alijikuta akivutiwa na mgeni kwa uzuri wake na jinsi alivyovaa kiheshima na manukato, aliamini kabisa ni mmoja wa wateja wake lakini mwenye uwezo wa juu.
Inaendelea
 
SEHEMU YA 20

Thabit baada ya kukaa kwenye kiti alimkaribisha tena mgeni wake.
“Karibu bibie ukae.”
“Asante,” Nargis alijibu huku akikaa.
Thabit alijikuta akivutiwa na mgeni kwa uzuri wake na jinsi alivyovaa kiheshima na manukato, aliamini kabisa ni mmoja wa wateja wake lakini mwenye uwezo wa juu.
ENDELEA..
“Karibu bibie.”
Kwa vile Nargis alikuwa amejitanda ushungi aliutoa na kumtazama Thabit ili amtambue aliyekaa mbele yake ni nani. Ilikuwa tofauti na mawazo yake macho ya Thabit yalishawekwa upofu na kumfanya amuone mwanamke mrembo lakini asiyemfahamu.
Pia hakupenda hali ile kwa vile mkewe angeingia angeweza kumfikiria vibaya kuwa ana uhusiano na yule mwanamke wakati hamjui na siku ile ndiyo ya kwanza kumuona.
“Samahani bibie hapa ni ofisini halafu aliye mapokezi ni mke wangu, akiingia ndani na kukuta kwenye hali hii unafikiri atanifikiriaje?”
“Thabit,” Nargis alimwita kwa sauti ya upole bila ya kuurudisha mtandio.
“Naam.”
“Mimi ni nani?”
“Kwa kweli nimekusahau, unajua kampuni yangu inatembelewa na wateja wengi.”
“Najua, lakini mimi si mteja kama unavyonifikiria.”
“Kama si mteja wewe nani?”
“Hebu niangalie vizuri.”
Thabit alimuangalia Nargis kama atamkumbuka lakini kumbukumbu hazikumpa kabisa kama yule ni nani. Baada ya kushindwa kumkumbuka alimjibu:
“Mmh! Kwa kweli sikukumbuki kabisa.”
“Hebu rudisha kumbukumbu ya miaka kumi nyuma na siku moja.”
“Huo muda sina hebu nieleze wewe ni nani?”
“Naitwa Nargis.”
“Jina zuri lakini bado sikukumbuki.”
“Thabit unasema kweli au unatania?”
“Mimi na wewe tumeanza kutaniana lini?”
“Thabit mimi ndiye mkeo niliyeondoka miaka kumi iliyopita kwenda kujifungua na kufanikiwa kupata watoto mapacha. Nimerudi leo kwa mume wangu.”
“Mume wako nani?”
“Wewe Thabit.”
“Utakuwa umekosea huenda Thabit mwingine siyo mimi,” Thabit alimruka mkewe kwa vile dawa za mzee Mukti zilikuwa zikifanya kazi.
“Thabit ni wewe mume wangu najua walimwengu tayari wamesha kuroga, ahadi yetu ipo wapi, kwa nini umenisaliti mume wangu?” Nargis alisema huku akilia.
“Dada eeh, naomba uondoke usije nivunjia ndoa yangu bure.”
“Thabit…Thabit…nimechoka kuua kwa ajili yako, hebu nihurumie nimejitoa kwa ajili yako kumbuka matatizo yaliyokutokea lakini nilisimama kuokoa maisha yako na mali zetu.”
“Samahani dada naona umechanganyikiwa, naomba utoke ofisini kwangu,” Thabit hakumuelewa aliona akimchanganya.
“Sitoki mpaka nipate haki yangu nataka kurudi kwa mume wangu na nyumbani kwangu ili tulee wanetu niliokwenda kujifungua nyumbani.”
Thabit aliona kama anapotezewa muda alinyanyua simu ili kumwita mlinzi amtoe nje.
“Wala usisumbuke sipo kwa shari, nitatoka kwa hiyari yangu, ila kesho nitarudi tena, ukitoka hapa kajifikirie.”
“Wala usisumbuke kurudi, mtafute mtu wako siyo mimi.”
Nargis alinyanyuka na kuzunguka meza kisha alimpiga busu Thabit shavuni na kutoka nje bila kuongeza neno. Alitoka hadi mapokezi na kumuaga Subira huku roho ikimuuma na kutamani kummaliza lakini bado alizuia moyo wake kuendelea kuua kwa ajili ya mume wake.
“Mpenzi nakwenda.”
“Ooh! Mara, karibu jamani.”
“Asante, kesho nitakuja.”
“Karibu dada yangu.”
Subira alimsindikiza kwa macho na kutamani kumuuliza gauni lile zuri alilovaa kalishona au kalinunua wapi ili na yeye akanunue, aliamini kwa utajiri wa mume wake angeweza kununua kitu chochote. Lakini kwa vile alisema atarudi kesho yake alipanga kumuuliza au hata kumtuma.
Baada ya Nargis kutoka Thabit alinyanyuka na kutoka mpaka kwa mkewe Subira aliyemkuta bado yupo kwenye mawazo ya kumuwaza mgeni.
“Mpenzi,” alimwita kwa sauti ya chini.
“Abee mume wangu.”
“Kuanzia leo sitaki mgeni mwanamke,” alisema kwa hasira.
“Kwa nini mume wangu?”
“Sipo hapa kutafuta wanawake bali kufanya kazi?”
“Mbona sijakuelewa una maanisha nini?” Subira alishindwa kumuelewa mumewe aliyeonekana uso umejaa hasira.
“Yule mwanamke aliyekuja amekuja kutangaza mapenzi eti ananipenda wakati anajua kabisa mimi ni mume wa mtu.”
“Mmh! Kwa hiyo umemuambia nini?”
“Ameondoka baada ya kumtisha kumuitia polisi.”
“Mmh! Sawa nimekuelewa mume wangu, nashukuru kwa uaminifu wako angekuwa mwanaume mwingine kwa uzuri wa yule mwanamke angemkubali tu na kunisaliti.”
“Mpaka nakuoa niliamua kuachana na mambo yote mabaya.”
“Asante mume wangu.”
Lakini wakati Thabit anageuka ili aingie ofisini Subira alishtuka kuona love bite (alama ya midomo iliyobaki baada ya mtu kumbusu mtu akiwa na rangi ya mdomo) zilikuwa nyingi kwenye shati jeupe la mpenzi wake. Alijikuta akishtuka na mapigo ya moyo kwenda mbio na kuamini mumewe alikwenda kujihami lakini yule ni mpenzi wake.
“Thabit,” alimwita kwa sauti kama ya mtu mwenye pumu.
“Naam mke wangu,” Thabit aliyekuwa ameshika mlango wa ofisi ili afungue aligeuka kumsikiliza mke wake.
Itaendelea wiki ijayo.
Alipogeuka hali ilikuwa ile ile ‘love bite’ zilikuwa kifuani na kwenye mashavu na mdomoni. Subira alizidi kuchanganyikiwa na hali ile na kuona jinsi Thabit asivyo muaminifu na alitoka ili kumhadaa lakini ndani kulikuwa na matendo ya mapenzi.
“Mume wangu!”
“Naam.”
“Unanifanyia nini?”
“Kivipi?”
“Yaani unanigeuza mtoto mdogo kwa nini?” Subira aliuliza huku akilia kitu kilichomshangaza Thabit na kutaka kujua kulikoni.
“Mke wangu umekuwaje leo?”
“Siyo nimekuwaje, ila unaonesha jinsi gani ulivyo muongo tena si muaminifu.”
“Mbona sikuelewi una nini mke wangu?” Thabit alizidi kumshangaa mkewe na lawama zake.
“Unanidanganya eti umemfukuza kama mbwa kumbe ndani mlikuwa na matendo ya kimahaba.”
“Mimi Thabit?”
“Ndiyo, hata kama kusoma sijui basi picha nimeiona.”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Hebu angalia kifuani mwako.”
Thabit alijitazama na kukuta kuna love bite na kushtuka.
‘Ha!”
“Unashtuka nini? Eti nilimfukuza kumbe mpenzi wako Mungu kakueleleza,” Subira alisema kwa hasira huku amemshikia pua.
“Hii ni ajabu vitu hivi vimetoka wapi, nakuapia mke wangu hakunibusu kwenye nguo alinibusu shavu kwa nguvu na kutoka baada ya kumkatalia mambo aliyokuja nayo ya kimahaba,” Thabit alijitetea.
“Siwezi kukuamini naona unipendi na kumwita yule mwanamke mzuri ili kunionesha.”
“Sijamwita hata hizi love bite nashangaa kuziona.”
“Si mbele tu angaliana na nyuma.”
Kauli ile limfanya Thabiti kuvua shati ili aangalia, hali ilikuwa vilevile alama ya midomo ilikuwa kingi kwenye shati jeupe na kumfanya Thabit abakiwa akiduwaa na kujishangaa alama zile zimetoka wapi.
 
SEHEMU YA 21

Alijikuta akishtuka na mapigo ya moyo kwenda mbio na kuamini mumewe alikwenda kujihami lakini yule ni mpenzi wake.
“Thabit,” alimwita kwa sauti kama ya mtu mwenye pumu.
“Naam mke wangu,” Thabit aliyekuwa ameshika mlango wa ofisi ili afungue aligeuka kumsikiliza mke wake.
SASA ENDELEA...
Alipogeuka hali ilikuwa ileile ‘love bite’ zilikuwa kifuani na kwenye mashavu na mdomoni. Subira alizidi kuchanganyikiwa na hali ile na kuona jinsi Thabit asivyo muaminifu na alitoka ili kumhadaa lakini ndani kulikuwa na matendo ya mapenzi.
“Mume wangu!”
“Naam.”
“Unanifanyia nini?” Subira alimuuliza huku akiangua kilio.
“Kivipi?” Thabit alishtuka.
“Yaani unanigeuza mtoto mdogo kwa nini?” Subira aliuliza huku akilia kitu kilichozidi kumshangaza Thabit na kutaka kujua kulikoni.
“Mke wangu umekuwaje leo?”
“Siyo nimekuwaje, ila unaonesha jinsi gani ulivyo muongo tena si muaminifu.”
“Mbona sikuelewi una nini mke wangu?” Thabit alizidi kumshangaa mkewe na lawama zake.
“Unanidanganya eti umemfukuza yule mwanamke kama mbwa kumbe ndani mlikuwa na matendo ya kimahaba.”
“Mimi Thabit?” Thabit aliuliza huku akijishika kifuani kwake.
“Ndiyo, hata kama kusoma sijui basi picha nimeiona.”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Hebu angalia kifuani mwako.”
Thabit alijitazama na kukuta kuna love bite na kushtuka.
‘Ha!”
“Unashtuka nini? Eti nilimfukuza kumbe mpenzi wako Mungu kakuumbua,” Subira alisema kwa hasira huku amemshikia pua.
“Hii ni ajabu vitu hivi vimetoka wapi, nakuapia mke wangu hakunibusu kwenye nguo alinibusu shavuni kwa nguvu na kutoka baada ya kumkatalia mambo aliyokuja nayo ya kimahaba,” Thabit alijitetea.
“Siwezi kukuamini naona hunipendi na kumwita yule mwanamke mzuri ili kunionesha.”
“Sijamwita hata hizi love bite nashangaa kuziona.”
“Si mbele tu angalia na nyuma.”
Kauli ile limfanya Thabiti kuvua shati ili aangalia, hali ilikuwa vilevile alama ya midomo ilikuwa kwenye shati jeupe na kumfanya Thabit abaki akiwa ameduwaa na kujishangaa alama zile zilitoka wapi.
Wakati huo Subira alikuwa akiendelea kulia kwa kuamini kwa uzuri wa yule mwanamke hana chake. Moyoni aliapa kama aliweza kumdhibiti jini basi hatashindwa kumdhibiti mwanadamu mwenzake hata angekuwa mzuri kama malaika.
“Mke wangu nakuapia yule mwanamke hakunibusu kote huku bali shavuni kwa nguvu na kutoka nje.”
“Si kweli Thabit una uhusiano naye hawezi kukubusu tu bila kuwa na uhusiano naye, kama umenichoka nipe talaka yangu,” Subira alitikisa kiberiti.
“Hapana mke wangu siwezi kufanya hivyo nakuhakikishia nakupenda wewe peke yako,” Thabit alisema huku akipiga magoti mbele ya mkewe kuomba afute kauli ya kuomba talaka.
“Mume wangu hunipendi,” Subira alijilaza kiuongo kuonesha ameumizwa.
“Haki ya Mungu sina uhusiano wowote na huyo mwanamke ndiyo maana nimekuambia asimruhusu kesho akija.”
“Nimekuelewa mume wangu,” Subira alisema huku akimnyanyua mumewe alipopiga magoti.
Thabit alirudi ofisini na kumuacha Subira akiwa na mawazo juu ya kauli ya mumewe kuhusu alama za midomo ya busu kwenye shati na usoni. Alijiuliza kama mumewe hakubusiwa sehemu zote zile basi aliamini yule mwanamke huenda si kiumbe wa kawaida.
Japokuwa alikuwa hajawahi kumuona jini lakini alisikia sifa zao kuwa majini wa kike huwa wazuri sana. Alijikuta akiingiwa na wasiwasi labda yule mwanamke ni jini, lakini alipingana na mawazo yake kutokana na kuelezwa na mzee Mukti Buguju kuwa jini hata wasogelea.
Lakini alitaka kujiridhisha alimpigia simu mzee Mukti ili kuupata ukweli wa tukio la yule mwanamke mrembo aliyemtia wasiwasi hasa kutokana na kauli za mpenzi wake. Baada ya simu kuita kwa muda bila kupokelewa alirudia tena mara mbili lakini haikupokelewa pia.
Alishtuka simu ya mzee Mukti kushindwa kupokelewa, alijiuliza kuna nini. Wakati akiwa katika lindi la mawazo simu yake iliita. Alipoangalia ilikuwa inatoka kwa mzee Mukti, aliipokea haraka.
“Haloo babu,” alipokea huku akihema.
“Eeh! Vipi mjukuu mbona presha juu kuna nini tena?” mzee Mukti alishtuka.
“Kuna kitu kimenichanganya mzee wangu!”
“Kitu gani?”
Subira alimueleza kilichotokea muda mfupi ofisini kwake, habari ile ilimshtua sana mzee Mukti akamuuliza:
“Unasema huyo mwanamke aliingia ofisini?”
“Ndiyo.”
“Yukoje?”
“Mmh! Mzee wangu uzuri wa yule mwanamke ndiyo kwanza leo nimeuona, tena hata manukato yake ni mageni puani kwangu, sijawahi kuyasikia.”
“Mmh! Subiri.”
Mzee Mukti alikata simu na kuangalia kwenye rada zake alijikuta mwili ukimtetemeka baada ya kuona ni jini Nargis mke wa Thabit waliyemdhibiti asiingie popote alipo Thabit na mkewe. Alijiuliza amekosea wapi mpaka kuingia alipopafunga, baada ya kuangalia zaidi aligundua ujaji wake ndiyo uliomaliza nguvu za kumzuia pale alipokwenda kibinadamu tofauti na mwanzo alipokwenda kijini.
Inaendelea
 
SEHEMU YA 22
Mzee Mukti alikata simu na kuangalia kwenye rada zake alijikuta mwili ukimtetemeka baada ya kuona ni jini Nargis mke wa Thabit waliyemdhibiti asiingie popote alipo Thabit na mkewe. Alijiuliza alikosea wapi mpaka kuingia alipopafunga, baada ya kuangalia zaidi aligundua ujaji wake ndiyo ulioua nguvu za kumzuia pale alipokwenda kibinadamu tofauti na mwanzo alipokwenda kijini.
SASA ENDELEA...
Lakini alifarijika kwa vile hakuwa na madhara yoyote na kilichotokea kilikuwa kiini macho kisicho na madhara yoyote. Kwa vile aliweza kuingia popote katika umbile la kibinadamu alitafuta dawa ya kumdhibiti asiingie popote kwa umbile lolote. Baada ya kujua kilichotokea ofisini alimpigia simu Subira kumjulisha. Baada ya kuita ilipokelewa upande wa pili.
“Haloo mzee wangu.”
“Nimeliona tatizo.”
“Umeona tatizo gani?”
“Aliyekuja hapo ni mke wa mumeo jini Nargis.”
“Mungu wangu nimekwisha,” Subira alishtuka kusikia vile.
“Usiogope hawezi kukufanya chochote,” mzee Mukti alimtoa hofu.
“Si ulisema umemdhibiti imekuwaje ameweza kuingia ofisini?”
“Yule mwanamke ana akili sana najua atanisumbua lakini mimi ndiye mwisho wa viumbe wale. Baada ya kuja katika umbile la kijini kushindikana aliamua kuja katika umbile la kibinadamu lakini lisilo na madhara.
Kwa nilivyotengeneza hawezi kufanya chochote hata ningemuacha aje asingewazuru.”
“Babu sitaki kumuona kwa uzuri wake akikutana na Thabit lazima watarudiana.”
“Hawawezi, ila kuna dawa itakayomdhibiti kila kona atakayowafuata hawezi kuwafikia.”
“Tena ifanye leo hii.”
“Baada ya kuona hivyo silazi damu ila kilichotokea usimwambie mumeo, mwache kama zuzu ili tufanikishe mambo yetu.”
“Sawa babu, tena nitakupa zawadi kubwa kwa vile unanipigania.”
“Viumbe hawa mimi ndiyo kiboko yao,” alijigamba mzee Mukti.
“Nakuaminia mzee wangu.”
Mzee Mukti alitengeneza dawa nyingine ya kumdhibiti Nargis na kwenda kuiweka nyumbani na kwenye maduka yote na kumweleza Subira aliyoiweka ni kiboko, Nargis akiigusa lazima apotee kabisa.
“Mmh! Nashukuru mzee wangu, natamani kusikia amekufa kwani sina raha.”
“Dawa niliyoiweka akigusa anapotea.”
“Utazidi kunifurahisha mzee wangu, kesho nitakuletea zawadi yako nina mpango wa kukuongezea gari lingine mwezi ujao. Nina amini mafanikio yangu yanapitia mikononi mwako.”
“Nami nitahakikisha huguswi na jini wala wachawi.”
Maneno ya mzee Mukti yalishusha presha ya Subira baada ya kumpanda kutokana na vitu vilivyotokea muda mfupi. Alijikuta akimuona mzee Mukti kama Mungu wake kwa kumtegemea kwa kila kitu na kumsahau aliyemuumba.
***
Siku ya pili kama kawaida Nargis alifika ofisi kwa Thabit, akiwa katika umbile la kibinadamu alitembea taratibu kuingia eneo la ofisi. Alipofika getini alimsalimia mlinzi na kuelekea kwenye ofisi ya mumewe kwa mwendo uliomfanya mlinzi amsindikie kwa macho na kuusifia uzuri wake kimoyomoyo.
Alipofika katika ya uwanja alishtuka kusikia mwili wote ukiwaka moto, kila alipokuwa akikanyaga aliungua na kumfanya apige kelele za maumivu.
“Moto...moto...motoo... nakufa Thabit mume wangu unaniua.”
Sauti yake kali ilimtisha kila mmoja, Subira na Thabit walitoka nje na kumuona Nargis akipiga kelele huku akiungua moto. Kwa vile alikuwa amefika katikati alirudi alipotoka huku akipiga kelele za kuungua moto. Nargis alirukaruka kwa maumivu ya moto kila alipokanyaga aliungua. Alipotoka eneo la ofisi ya Thabit alitoweka ghafla na kuacha wakishangaa.
Mlinzi ndiye aliyesikia maneno ya Nargis na kujiuliza yule mwanamke alikuwa nani, taratibu kumbukumbu zikaanza kumjia na kujiuliza alimuona wapi.
Maneno ya kumwita Thabit mume wake na kusema ana muua yalikuwa na maana gani. Alipanga kumuuliza Thabit kwa wakati wake.
Kwa Subira ilikuwa furaha na kuzidi kumuamini mzee Mukti kwa kazi yake iliyokuwa na majibu ya papo kwa papo. Thabit alichanganyikiwa na kujiuliza kile nini huku akimkumbuka yule mwanamke aliyekuwa akipiga kelele za maumivu ya kuungua moto na kutoweka ndiye aliyekuja jana yake.
“Kile nini?”
“Yule mwanamke si mtu mzuri ndiyo wale wachawi waliotaka kuturudisha nyuma na kutufilisi,” Subira alitengeneza uongo.
“Nimeamini mzee Mukti kazi anaiweza, ndiyo jana nilishangaa mtu kuja kujifanya ananipenda kumbe ana yake,” Thabit aliunga mkono bila kujua kilichokuwa kikiendelea.
***
Nargis alikwenda kujitupa baharini kupunguza mauivu ya moto ambao ulimchoma sehemu kubwa ya mwili wake. Alipogusa maji alipoteza fahamu na kuokotwa na vibwengo ambavyo vilipeleka taarifa chini ya bahari. Walitumwa vijakazi waliomfuata na kumpeleka chini ya bahari mwili wote ukiwa na majeraha makubwa ya moto.
Alipofika tu alipatiwa huduma ya haraka ya kuyatibu madonda makubwa yaliyosababishwa na moto uliomuunguza.
Watoto wake walipomuona walilia sana na kuapa kulipa kisasi kwa mtu aliyemfanya vile mama yao. Lakini bibi yao aliwakataza kwa kuamini wanaweza kupotea kwa vile hawakuwa na nguvu ya kupambana kutokana na kuchanganya damu ya kijini na ya binadamu.
Baada ya kumpatia huduma na kumuacha apumzike, malkia Zabeda alimwita mwanaye wazungumze juu ya hali ya Nargis na jinsi ya kumsaidia.
Inaendelea
 
SEHEMU YA 23

Alipofika tu alipatiwa huduma ya haraka ya kuyatibu madonda ya moto ambayo yalikuwa makubwa. Watoto wake walipomuona walilia sana na kuapa kulipa kisasi kwa mtu aliyemfanya vile mama yao. Lakini bibi yao aliwakataza kwa kuamini wanaweza kupotea kwa vile hawana nguvu kubwa ya kupambana kutokana na kuchanganya damu ya kijini na ya kibinadamu.
Baada ya kumpatia huduma na kumuacha apumzike, Malkia Zabeda alimwita mwanaye wazungumze juu ya hali ya Nargis na jinsi ya kumsaidia.
SASA “Mwanangu naomba tumsaidie mdogo wako hali inatisha.”
“Mama mimi msiniingize mwanao kazidi ubishi na akiendelea watamuua. Moto uliomuunguza si wa mchezo bila nguvu za kijini tungempoteza.”
“Najua, lakini bado yupo chini yetu, lazima tumsaidie.”
“Mama mimi sipo tayari kujiingiza kwenye matatizo, usalama wake ni kuachana na baba Zamzu bila hivyo mwanao atakufa.”
“Kwa ubishi wake siamini kama atakubali, namjua vizuri Nargis, kitendo cha kuumizwa patachimbika bila jembe.”
“Mama mwanao haambiliki, ubishi wake sasa hivi anapotea.”
“Ndiyo hivyo damu nzito kuliko maji hatuwezi kumuacha, basi akitoka mfuate nyuma akizidiwa msaidie.”
“Sawa mama,” Hailat alikubali ili kumfurahisha mama yake lakini aliamini nguvu za wapinzani wao ni kubwa hasa alipouona moto aliochomwa mdogo wake ulimtisha hata chuma kingeyeyuka.
Baada ya kumzuia jini Nargis, Subira kwa furaha alimpelekea zawadi ya gari alilomuahidi na kuzidi kumtia kichaa mzee Mukti.
Kwa furaha aliyokuwanayo, mganga huyo alimuahidi Subira kumpa dawa nzuri zaidi ambayo huwa haitoi ovyo ambayo ilitakiwa kufanywa sehemu saba kwa ajili ya kumficha ili akitafutwa ashindwe kupatikana.
Sehemu ya kwanza aliyopanga kumficha ilikuwa baharini kwenye maji ya shingo, sehemu ya pili kwenye vichuguu, sehemu ya tatu kwenye mti mkavu na sehemu ya nne kwenye jalala.
Sehemu ya tano chooni, sehemu ya sita njia panda na sehemu ya saba kwenye mti mkubwa.
Kukamilisha maandalizi ya dawa hiyo, alipanga kwenda Msumbiji kuongeza vitu vilivyohitajika ambavyo aliamini vingekuwa vya mwisho kumtengenezea Subira.
Mzee Mukti aliamini ndiyo kete ya mwisho ambayo ilikuwa zawadi kwa Subira baada ya kuonesha kumjali kwa kuyabadili maisha yake tofauti na watu wengi aliowasaidia hawakuwa na shukurani baada ya kufanikisha mambo yao.
Alipanga baada ya wiki moja asafiri kwenda Msumbiji ambako angekwenda kuchota mzigo wa nguvu kwani alikuwa na fedha ya kununua dawa nyingi ambazo zingefanya kazi kwa muda mrefu. Subira naye alifurahia maisha ya ndoa baada ya kufanikiwa kumdhibiti jini Nargis.
Mlinzi wa getini alitafuta nafasi ya kuzungumza na Thabit juu ya tukio la mwanamke kuungua moto na kauli zake wakati akipiga kelele kwamba aliungua moto ambao hakuuona zaidi ya kurukaruka kutoka eneo la ofisi ile na alipotoka akatoweka kiajabu. Aliyarudia maneno ya Nargis akilini pale alipokuwa akilalamika huku akiteseka na moto usioonekana:
“Moto...moto...motoo...nakufa Thabit mume wangu unaniua bure bila kujua.”
Alibakia na maswali ambayo aliamini wa kuyajibu ni bosi wake tena angemuuliza akiwa peke yake. Alisubiri siku Subira aliyowahi kuondoka na gari lake na kumuacha mumewe kazini. Thabit alitoka kazini majira ya saa mbili na nusu usiku alipofika getini alimkuta mlinzi.
Alimuaga kama kawaida, lakini mlinzi alimuomba wazungumze kitu, kwa vile Thabit alikuwa hana makuu aliegesha gari pembeni na kuzungumza na mlinzi wake.
“Niambie naona leo una jambo!” Thabit alimuuliza mlinzi.
“Bosi samahani kama nitakalo lizungumza litakuudhi,” mlinzi alijihami.
“Zungumza tu jisikie huru kuzungumza chochote,” Thabit alimtoa hofu.
“Bosi unakumbuka wiki moja iliyopita kuna kitu kisicho cha kawaida kilitokea?”
“Kitu gani?’
“Kuungua moto yule mwanamke mzuri?”
“Yaani yule mwanamke sielewi kwa nini ananifuatafuata!”
“Unajua bosi maneno ya yule mwanamke yamenishtua sana.”
“Maneno gani?”
“Nilimsikia akikuita mume wake na kusema unamuua bure bila kujua.”
“Sasa John mimi nina mke mwingine zaidi ya Subira?”
“Lakini bosi shemu Nargis yupo wapi?”
“Nargis?” Thabit alishtuka.
“Ndiyo, tena yule mwanamke anafanana na Nargis.”
“Kwa nini unasema ni Nargis?”
“Hata alipokuja alinisalimia habari za siku huku akilitaja jina langu.”
“John achana na habari za Nargis, kumbuka alikuwa mke wangu sasa hivi nina mwanamke mwingine.”
“Basi bosi nilitaka kujua hilo tu.”
“Nimekusikia, achana na mawazo ya mtu asiyekuwepo, sasa hivi nina maisha mapya kabisa.”
“Nimekuelewa.”
“Basi tutaonana kesho, usiku mwema na kazi njema.”
“Na kwako pia.”
Thabit aliingia ndani ya gari lake na kuondoka kuelekea nyumbani huku akirudia maneno ya mlinzi na kujikuta akisema mwenyewe:
“Nargis...Nargis...Mmh!“ jina lilikuja lakini lilipotea akilini.
Lakini wazo lile lilipotea baada ya kupigiwa simu na Subira alipokea na kuzungumza:
“Haloo mpenzi.”
“Upo wapi mume wangu?”
“Njiani ndiyo narudi.”
“Wahi basi mume wangu si unajua nipo kama kinda la ndege linalohitaji joto la mzazi wake, wewe ndiyo joto langu.”
Inaendelea
 
SEHEMU YA 24

“Nargis...Nargis.. Mmh!“ jina lilikuja lakini lilipotea akilini.
Lakini wazo lile lilipotea baada ya kupigiwa simu na Subira alipokea na kuzungumza:
“Haloo mpenzi.”
“Upo wapi mume wangu?”
“Njiani ndiyo narudi.”
“Wahi basi mume wangu si unajua nipo kama kinda la ndege linalohitaji joto la mzazi wake, wewe ndiyo joto langu.”
SASA ENDELEA...“
Usihofu nakuja mpenzi wangu.”
“Leo nimekupikia chakula ukipendacho cha tambi na nyama.”
“Ndiyo maana nakupenda, na ile ahadi ya nyumba ya ghorofa ujenzi unaanza wiki ijayo.”
“Jamani mume wangu nakupendaje!”
“Asante mume wangu.”
“Basi tusimalize maneno yote nikakosa ya kuongea nikiwa pembeni yako.”
“Haya mpenzi ufike salama.”
“Amina.”
Baada ya kukata simu alijikuta mawazo yake yamehamia kwa mkewe na kusahau kuhusu mkewe NargisNargis baada ya kupata nafuu alirudiwa na fahamu na kujitambua baada ya kupoteza kwa wiki nzima.
Kila alipojiangalia mwili wake ulivyoharibika kwa moto alilia na kuapa kufa na mtu. Hakukubali kushindwa kwa haki yake, suala lake hakutaka kuwashirikisha familia yake kwa vile aliamini vita ile ni kubwa hivyo aliamini kabisa kama akishindwa basi afe peke yake.
Wanaye mapacha Zumza na Zamzu baada ya mama yao kupata nafuu waliomba wamsaidie kwenye vita ile.
“Mama ukiondoka tunaondoka wote,” Zumza (Kulwa) alimwambia mama yake aliyekuwa akijiandaa kuondoka.“Hapana wanangu ninyi bado wadogo, tutaondoka siku nyingine kwanza sasa hivi usiku.”
“Hata kama ni wadogo tutakufa na wewe,” Zamzu (Doto) alimwambia mama yake.
“Mama ukifa tutabaki na nani hatukubali? Ukiondoka tunakufuata,” Zumza alimuunga mkono mdogo wake. “Sikilizeni watoto wangu wapenzi, najua mnanipenda sana mama yenu, nakuombeni kitu kimoja, kwa vile mmejitolea kunisaidia mama yenu nimepanga kwenda kwenye mapambano mpaka nipone kabisa,” Nargis aliwadanganya wanaye.
“Mama, kwa baba tunakwenda lini?” Zamzu aliuliza.
“Kuna safari nakwenda nikirudi tutakwenda kwa baba yenu, sawa wanangu?”
“Sawa mama,” walikubali kwa pamoja.
Kwa vile ulikuwa usiku wanafamilia yake wakiwa wamelala, alitoka kwenda kujaribu tena huku ajiuliza amekosea wapi kwani aliamini alichokuwa akikipigania ni haki yake hata kama akifa angekuwa amekufa kwa haki yake ya msingi.
Alijua majini na binadamu wote ni viumbe wa Mungu na ndoa yake aliyofunga na Thabit ilifuata taratibu zote hivyo alitambulika mbele ya Mungu.
Alitoka kwa kuibia kuelekea nje ya maji, kabla hajatoka alishtuka kuitwa nyuma yake.
“Mwana wa malkia.”
“Kun’za unasemaje?” alishangaa alimuuliza Kun’za mtwana mwenye kibyongo ambaye alikuwa mkongwe kuliko wote na ndiye aliyekuwa mtiifu kuliko wote.
“Binti mfalme najua una matatizo mazito kutokana na vita yako na wanadamu.”
“Umejuaje?” Nargis alishtuka sana.
“Najua tu binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu,” Kun’za alijibu kwa utulivu kama kawaida yake.
“Nani kakuambia?” alizidi kumuuliza.
“Hata bila kuambiwa uso wako unaonesha kila kitu na safari yako inaonesha si njema kwako.”
“Wewe umejuaje?” Nargis alizidi kumuuliza.
“Najua kwa kukutazama.”
“Wewe Kun’za mtwana umetoa wapi uwezo wa kufahamu mambo ya wakubwa?”
“Babu yangu ni mchawi aliyefukuzwa kwenye anga za majini na kwenda kukaa kwenye miamba myeusi ambayo hakuna jini wala kiumbe chochote kilichowahi kufika huko. Mimi nilifika baada kuelekezwa na marehemu mama yangu ambaye alinielekeza nimtafute babu yangu alipo na alinilazimisha lazima nifike japokuwa sehemu yenyewe ni mbali sana.
“Baada ya kuelezwa hivyo nilitoka nyumbani kuelekea kwenye miamba myeusi, huwezi kuamini nimetumia miaka mia mpaka kufika kwenye miamba hiyo. Sehemu yenyewe ina kiza cha ajabu inataka moyo kuvuka miamba mpaka kuupata mlango wa kuingia ndani ya mwamba wa kiza ambamo yumo yeye.”
“Kun’za nimekusikiliza, sijui babu yako mchawi, sijui anakaa kwenye miamba myeusi katika mwamba wa kiza, una maanisha nini?”
“Shida yangu nikupeleke kwa babu yangu akusaidie, katika viumbe wenye huruma kama wewe .”
“Kun’za toka nizaliwe kwanza leo ndiyo nasikia hiyo miamba myeusi, katika utundu wangu toka utotoni nimeishafika kila kona ya bahari lakini sijawahi kuona wala kusikia miamba hiyo. Hiyo miamba ipo bahari gani?”
“Hiihii ya dhahabu.”
“Kun’za hakuna kitu kama hicho!” Nargis alibisha.
“Binti mfalme, bahari hizi hata baba yako nina imani hazijui, mzee Dudumizi huu ni mwaka wa mia tatu yapo huko. Siri hii naijua mimi peke yangu na alinikanya nisimwambie mtu. Lakini kutokana na matatizo yako lazima nikupeleke najua utafanikiwa na utampata mumeo.”
“Kun’za unaniambia kweli au unanitania?” Nargis hakumuamini.
“Binti mfalme wa bahari sijawahi kukudanganya, najua katika watwana wako mimi ndiye mtiifu kuliko wote.”
“Najua, pamoja na kukuamini sana Kun’za lakini kwa hili mbona linanitia shaka?”
“Naomba uniamini, nakuapia utampata mumeo ila nakuomba kitu kimoja ukirudi kwa mumeo naomba niwe mlinzi wako mkuu.”
“Hilo halina shida, lakini mbona kufika huko ni miaka mingi, miaka mia ni mingi sana heri niendelee kupigana mpaka nijue hatima yangu.”
“Baada ya kufika kule alinipa dawa ya kuweza kufika kwa siku moja tena kwa saa chache.”
“Huyu babu yako ana miaka mingapi?”
“Mia saba.”
Itaendelea
 
SEHEMU YA 25
“Hilo halina shida, lakini mbona kufika huko ni miaka mingi, miaka mia ni mingi sana heri niendelee kupigana mpaka nijue hatima yangu.”
“Baada ya kufika kule alinipa dawa ya kuweza kufika kwa siku moja tena kwa saa chache.”
“Huyu babu yako ana miaka mingapi?” “Mia saba.
ENDELEA...
“Duh! Sasa tutakwenda lini?”
“Nataka tuondoke usiku huu, mpaka kunakucha tuwe tumerudi.”
Kwani alifanya kosa gani lililosababisha kufungwa huko?”
“Kwa kweli sijui, nilijaribu kumdodosa aliniambia niachane nayo bali nifuate kilichonipeleka.”
“Basi tuondoke.”
Kun’za alimshika mkono Nargis na kuzama chini ya bahari kwa kutembea kwa kasi ya ajabu ambayo ilimtisha Nargis. Ilikuwa kasi ya ajabu ambayo hakuwahi kwenda nayo katika maisha yake. Walitembea kwa saa saba na kufika kwenye miamba myeusi.
Sehemu yenyewe ilikuwa na kiza cha ajabu ambacho kilimtisha Nargis, lakini alificha hofu yake.
Pamoja na kuwa yeye ni jini kwa mara ya kwanza woga ulimtawala kutokana na kiza cha ajabu cha eneo lile. Hali ya ukimya nayo ilizidisha kuogopesha kama angekuwa peke yake angekufa kwa hofu. Lakini alimshangaa Kun’za ambaye hakuonesha wasiwasi wowote, alimshika mkono na kutembea naye kwenye miamba ya barafu yenye kugandisha damu.
Kila walivyotembea ndivyo baridi kali lilivyozidi kuongezeka baada ya muda Nargis alianza kusikia ganzi kali mwilini na kuwa na wasiwasi labda Kun’za kampeleka kule kumuua. Moyoni alijiapia watakufa wote hawezi kukubali kufa peke yake, siku zote alikuwa hakubali kushindwa.
“Kun’za mbona hatufiki? Nasikia ganzi ikisambaa mwili mzima nahisi damu kuanza kuganda.”
“Tutafika sasa hivi.”
Ghafla ubaridi ulipotea na kuanza kusikia joto ambalo kila walivyokwenda ndiyo lilivyoongezeka.
“Kun’za huku wapi tena?”
“Tunaingia mwamba wa moto.”
Baada ya mwendo kidogo walifika kwenye miamba wa moto, walipoanza kukanyaga barafu yote iliyokuwa imewaganda iliyeyuka na kuanza kuhisi joto kali. Hali ile ilizidi kumtisha na kuona ameingia dunia nyingine kabisa ambayo hakuwahi kuiota wala kuisikia.
Baada ya mwendo wa saa moja walifika kwenye mwamba wa giza ambao lilikuwa zito mpaka hewa ikawa shida kupatikana. Nargis alijuta kwenda sehemu ile kwani aliamini kabisa Kun’za alimpeleka kule kumuua. Baada ya muda alihisi baridi kali na hewa nzuri kisha mwanga mkali ulioyachoma macho yake.
Baada ya mwendo wa kutembea juu ya miamba alitokea kwenye mwamba mmoja uliokuwa na mlango.
“Tumefika,” Kun’za alimwambia waingie ndani.
Waliingia na kufika kwa kiumbe kilichokaa kama mdudu Karugu yeye kwa mwili wake wote kufunikwa na miba midogodogo na manyoya na kufanya uso wala viungo vingine visionekane. Yule ndiye aliyekuwa babu yake Kun’za babu Dumidumzi.
“Karibu Nargis mwana wa mfalme wa bahari ya dhahabu,” baba Dumidumzi alisema huku akijilaza kifudifudi kuonesha heshima kwa mwana wa mfalme.
“Asante mzee Dumidumzi.”
“Nina imani Kun’za ana mapenzi makubwa kwako mpaka kukuleta huku, poleni na misukosuko ya safari hiyo ndiyo inayonifanya nisifikiwe na kiumbe chochote. Kiumbe kinachokuja huku basi huwa kimedhamiria nami sitakiacha kiondoke mikono mitupu lazima nikipe zawadi kubwa.”
“Nitashukuru mzee wangu.”
“Mshukuru sana Kun’za kwa kukuponya kwani safari yako ilikuwa ya kifo usingerudi salama kwa vile adui yako kajipanga na anaendelea kujiimarisha. Kwa nguvu za kijini za kawaida hamumuwezi.”
“Naomba msaada wako mzee Dumidumzi.”
“Sasa unataka msaada gani mkubwa toka kwangu?”
“Kumpata mume wangu.”
“Kwa njia gani?”
“Utakayoitaka lakini nimpate mume wangu.”
“Mbona moyo wako hautaki shari sasa unataka nimtie adabu anayekusumbua, nina uwezo wa kumfanya chochote unachotaka. Nimgeuze funza wa chooni au nimuozeshe mwili mzima?”
“Mzee nataka unipe uwezo wa kumpata mume wangu bila kumwaga damu.”
“Nitakupa uwezo wa kufika popote bila kizuizi, hiyo itakuwezesha kukutana na mganga uso kwa uso na kumwambia amrudishe mumeo kwa hiyari yake akikataa rudi nitakupa kitu kimoja kitakuwa na uwezo robo ya muumba. Kwanza nitakupa uwezo wa kufanya kiini macho kitakachomkimbiza yule mwanamke mwenyewe kama hasikii mfuate mganga akileta kiburi njoo tumalize kazi. Kuna kitu anajivunia kazi ya kukichukuwa nitampa Kun’za akikichukuwa basi kila kitu kimeisha.”
“Nitashukuru mzee wangu, nitafurahi sana sijui nitakupa zawadi gani.”
“Zawadi yangu kubwa wewe ulipokuja kunitembelea.”
“Sawa babu.”
“Mnaweza kwenda ili alfajiri iwakute nyumbani kwenu, sasa hivi mtatumia muda mfupi zaidi.”
Baada ya kusema vile waliruhusiwa kuondoka, walishikana mikono na kutoweka ghafla. Nargis aliposhtuka usingizini alijikuta kitandani kwake mwili wake ukiwa hauna kovu lolote na kuwa mzuri mara dufu. Baada ya kuamka alijikuta akijiuliza kilichotokea kilikuwa ndoto au kweli kwani aliamka kitandani kwake.
Alitulia na kujifikiria jana usiku alipanga kutoroka kwenda kupambana kumrudisha mumewe mikononi mwake. Kumbukumbu zilimuonesha alikutana na jini mtwana Kun’za aliyezungumza naye na kusafiri naye kwenda kwa babu yake kwenye miamba myeusi kisha walisafiri.
Alikumbuka adha walizokutana nazo kwenye safari yao mpaka kufika kisha kukutana na babu Dumidumzi na kumpa uwezo wa kumrudisha mumewe. Akiwa katikati ya mawazo mwanaye wa kike alimshangaa mama yake kuwa na ngozi nzuri.
“Ha! Mama umepona ulikwenda wapi, sasa hivi huna makovu hata moja!”
Kauli ya mwanaye ilimfanya ajichunguze na kugundua hana kovu na ngozi yake ilikuwa nzuri sana.
Inaendelea
 
SEHEMU YA 26

Alikumbuka adha walizokutana nazo kwenye safari yao mpaka kufika kisha kukutana na babu Dumidumzi na kumpa uwezo wa kumrudisha mumewe. Akiwa katikati ya mawazo mwanaye wa kike alimshangaa mama yake kuwa na ngozi nzuri.
“Ha! Mama umepona ulikwenda wapi, sasa hivi huna makovu hata moja!”
Kauli ya mwanaye ilimfanya ajichunguze na kugundua hakuwa nna kovu na ngozi yake ilikuwa nzuri sana. ENDELEA...“
Kaniitieni Kun’za,” aliwatuma wanaye kwenda kwa mtwana Kun’za.
Walitoka na kumfuata na kumkuta akiendelea na kazi na kumweleza anaitwa na mama yao. Aliacha kazi na kwenda kumsikiliza binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu. Alipofika alikaribishwa chumbani kwake kwa mara ya kwanza.
“Naam binti mfalme.”
“Eti jana kuna sehemu tulienda pamoja?”
“Ndiyo binti mfalme, tulienda kwa babu kwenye miamba myeusi.”
“Ooh! Kwani unafanya kazi gani?”
“Ya usafi.”
“Sasa hivi utahamia kwenye bustani kuwasimamia wenzako nami nakuja kutoa amri.”
Baada ya kusema vile alitoka hadi kwenye bustani na kuwaita watwana na vijakazi wote na kuwaeleza kuanzia siku ile kiongozi wao atakuwa Kun’za kwa kuwasimamia bila kufanya kazi yoyote na walipiga magoti kukubaliana na agizo la binti mfalme.
Baada ya kupata uhakika alipanga kuanza vimbwanga vyake usiku vya kumtisha mke wa Thabit ili aikimbie nyumba na yeye kurudi kwenye nyumba yake. Moyoni alipanga kumpa zawadi kubwa Kun’za siku atakapomrudisha Thabit mikono mwake.
Kwa vile alitaka kutumia njia ya kistaarabu alipanga kwenda siku ya pili asubuhi ofisini na kuonana na Subira uso kwa macho. Siku ya pili asubuhi alikwenda ofisini kwa Thabit, akiwa katika vazi lake la heshima kama ilivyokuwa kawaida. Alivalia gauni refu jekundu lililokuwa limempendeza sana, chini alivaa viatu vyeupe vyenye mchuchumio mrefu na juu alijitanda mtandio wa hariri.
Kwa kujiamini aliingia getini kama ilivyokuwa kawaida yake alikwenda kumsalimia mlinzi ambaye alishtuka kumuona tena.
“Za asubuhi John?”
“Nzu..nzuri dada.”
“Niite Nargis.”
“Ooh! Si...si...wewe u...uli...kuwa m...m...ke wa...wa..”
“John kigugumizi cha nini, ndiye mimi shemeji yako wa ukweli!”
“Mmh! U...u...likuwa wa...wapi?”
“Utajua muda si mrefu, Thabit yupo?” Nargis alijifanya hajui kitu.
“Ha...ha...jafika.”
“Mkewe?”
“Yu...yu...po.”
“Naweza kwenda kuonana naye?”
“Ndi...ndi...yo.”
Nargis pamoja na uwezo wake wa kuweza kuingia popote bila mtu kumuona siku ile hakutaka kutumia nguvu za kijini bali busara ya kibinadamu ili waelewane. Lakini kama ingeshindikana angetumia nguvu za kijini tena zilizoongezwa nguvu na mzee Dumidumzi.
Alitembea kama kawaida yake kwa madaha kama hakuna mwanamke mwingine mzuri chini ya jua kama yeye. Mlinzi alibakia amepigwa na butwaa huku akihofia kutokea yaliyotokea siku chache zilizopita. Lakini siku ile ilikuwa tofauti, kwani Nargis alitembea taratibu mpaka alipoufikia mlango wa ofisi na kuingia ndani.
Alimkuta Subira akiwa bize macho yake kwenye kioo cha kompyuta, harufu nzuri ya manukato aliyojipulizia Nargis yalimfanya anyanyue uso wake na kukutana na uso wa Nargis wenye tabasamu pana.
“He!” alishtuka kumwona mbaya wake.
“Subira unashtuka nini?” alimuuliza huku akimtazama usoni.
“Ha...ha...pana,” Subira alibabaika kumwona kiumbe aliyeambiwa hawezi tena kumsogelea. Kwake aliona kama alikuwa kwenye njozi, alifikicha macho yake ili kupata uhakika kwa kile alichokiona mbele yake.
“Subira usisumbuke kuutafuta ukweli juu ya mimi kusimama mbele yako, ni kweli nipo mbele yako pamoja na dawa ulizopewa na mganga Mukti. Siku zote haki ya kiumbe huchelewa lakini haipotei kamwe. Umejitahidi kuchukua mali yangu kwa nguvu, nina imani siku niliyounguzwa na moto mliamini kabisa mmenimaliza.
“Ni kweli mliniweza lakini bado nakueleza haki ya kiumbe haipotei bali huchelewa, sasa nakuomba kwa hiyari yako nirudishie mume wangu. Ningeweza kukufanya kitu kibaya lakini nimechoka kupata dhambi za wanadamu, nataka njia uliyotumia kumchukuwa mume wangu uitumie kunirudishia.
“Nataka usiku wa leo nilale kwangu hujui gharama ya nyumba ile wala thamani na mali zote hujui vimepatikana vipi. Kwa hiyo kwa kauli ya kistaarabu nakuomba kuanzia sasa hivi nenda kwa mganga wako mweleze mwenye mali amerudi.
“Nina imani nimeongea kwa kauli ya kistaarabu isiyo na ghadhabu hata chembe japokuwa nazungumza na adui yangu mkubwa. Naondoka, usiku narudi kwangu rasmi hivyo sitaki nikukute, nikikukuta sitataka lawama na mtu japokuwa akili yako imejaa kiburi.”
Nargis baada ya kusema vile aligeuka na kuondoka na kumuacha Subira bado kapigwa butwaa bila kujua kilichotokea mbele yake ni kweli au aliota. Alifikicha macho tena bado hakuamini alijitandika makofi na kuhisi maumivu hapo ndipo aliporudi katika akili ya kawaida.
Alinyanyuka na kutoka nje ya ofisi na kwenda hadi getini kumuuliza mlinzi, alipofika alionekana amechanganyikiwa.
“John!”
“Naam mama.”
“Eti kuna mtu kapita muda huu?”
“Wa aina gani kwa vile wamepita wengi.”
“Mwanamke mmoja mzuuuri kavaa gauni jekundu.”
“Ooh! Ndiyo.”
“Mmh! Kazi kwelikweli,” alisema huku akishusha pumzi kijasho chembamba kikitoka.
“Kwani vipi?” mlinzi alimuuliza.
“Mmh! Sijui, hebu ngoja.”
Subira alichanganyikiwa baada ya kumuona kiumbe aliyeambiwa hawezi kufika popote alipo yeye.
Itaendelea
 
SEHEMU YA 27

Lakini aliweza kufika bila kizuizi cha aina yoyote ikiwa tofauti na maelezo ya mzee Mukti. Alijiuliza mpaka ameweza kufika mbele yake na kutoa onyo kwake aliamini hali ni mbaya. Maneno aliyoambiwa yalimtisha mpaka kufikia usiku awe amemrudisha mumewe mikononi mwake na yeye anarudi rasmi kwake.
Aliona haelewi kitu jibu angelipata kwa mzee Mukti, alijikuta akiamua kuondoka muda uleule bila kupanga vitu alivyokuwa ameanza kuvifanyia kazi wala kuzima kompyuta alitoka kwenda kwa mzee Mukti kumpa kilichomkuta asubuhi ile. Aliendesha gari kwa mawenge kidogo agonge kutokana na kuchanganyikiwa.
Lakini alifika salama Kigamboni kwa mzee Mukti ambaye alishtuka kumwona asubuhi ile huku uso wake ukionesha sintofahamu.“Mjukuu mbona hivyo kuna nini?” mzee Mukti alimuuliza huku akimshangaa.
“Babu hali ni mbaya,” Subira alijibu huku akihema kama aliyetoka kupanda mlima.
“Unaumwa?”
“Heri ningeumwa babu.”
“He! Tatizo nini?”
“Yule mwanamke amekuja.”
“Mwanamke! Mwanamke gani?”
“Jini.”
“Wapi?”
“Ofisini na kunieleza kuwa leo anarudi kwake hivyo nimrudishe mumewe.”
“Umrudishe wapi?”
“Mzee Mukti ina maana hunielewi, nimekuambia leo anarudi kwake hivyo usiku wa leo anataka kulala na mumewe.”
“Kwanza sijakuelewa kaja wapi?” mzee Mukti alimsikia lakini hakumuelewa.
“Mzee Mukti ina maana yote ninayozungumza hunielewi au unafanya makusudi?” Subira alimshangaa mzee Mukti.
“Kwanza hebu tulia maana nakuona unanichanganyia maneno mara amefika ofisini mara anataka kurudi kwake mara leo anataka kulala na mumewe sasa nisikilize lipi?”
“Mzee Mukti yote niliyosema, kumbuka ulisema akigusa tena lazima afe mbona leo kaja kama kwake tena kwa kujiamini, huoni kama hiyo ni hatari angeweza kunifanya kitu chochote kibaya?”
“Unajua mpaka sasa sielewi unachokizungumza, umeota au ni kitu cha kweli?”
“Mzee wangu mbona leo nakuona kama unanigeuza kituko, nimekueleza asubuhi hii yaani nimefika hata sijaanza kazi vizuri na kunieleza niliyokueleza eti njia niliyotumia kumchukua mumewe ndiyo niitumie kumrudisha kwake.”
“Kwa hiyo kaingia ofisini?”
“Mbona leo nimekuwa kama mwalimu wa chekechea nikueleze kwa kurudia neno moja mara kumi, ina maana kila ninalolizungumza linapita halikai kichwani?”
“Hawezi kuingia ofisini nakataa utakuwa umeota tu mjukuu wangu.”
Mzee Mukti kutokana na zindiko alilolifanya aliamini hakuna kiumbe chochote kibaya kinaweza kuingia kwenye ofisi na nyumba za Thabit na kuwadhuru. Kusikia vile aliamini alichokisema Subira kilikuwa ni ndoto.
“Sasa babu nimekuja kubishana na wewe au unisaidie maana amesema anakuja usiku nitamdhibiti vipi?”
“Hawezi.”
“Hawezi vipi ikiwa ofisini ameingia na kutoka tena amesema kaonesha ustaarabu wa hali ya juu japokuwa mimi ni adui yake. Na amesema nikikaidi atakachonifanya Mungu anajua.”
“Hebu twende ndani,” waliongozana hadi ndani ya kilinge ili mzee Mukti aangalie kuna nini.
Baada ya kuangalia kwenye setilaiti zake aliona kila kitu kipo sawa na kuamini kabisa anachokizungumza kilikuwa cha ndotoni. Lakini hakutaka kumnvunja nguvu kutokana na kumuamini sana. Alichukua maji ya manukato na kumpatia ili usiku ukiingia ajipake kufukuza nguvu za kijini.
“Hii itanisaidia?”
“Ndiyo.”
“Kwani babu tumekosea kitu gani mpaka leo kaja kama kwake?”
“Hatujakosea popote zile ni nguvu za kijini lakini hazina ubaya wowote. Kuja kwake pale ni kwa vile hakuwa na madhara kama angekuwa na madhara angekufa kabla hajakufikia. Aliyosema ni mkwara wa kukutisha ili uondoke lakini hawezi kufanya chochote.”
“Mmh! Afadhali, maana nilichanganyikiwa nilijua nimekwisha.”
“Pole mjukuu.”
“Asante.”
Baada ya kupewa moyo na mzee Mukti Buguju, Subira alirudi ofisini kuendelea na kazi lakini akiwa na wasiwasi wa usiku japokuwa maneno ya mzee Mukti yalimpa moyo.
***
Majira ya usiku baada ya chakula Subira alijipaka maji ya manukato aliyopewa mzee Mukti kisha alipanda kitandani.
Baada ya usingizi kumpitia alishtuka baada ya kumsikia mtu akimtikisa, alifumbua macho kuangalia ni nani alimtikisa. Alijikuta akishtuka baada ya kumuona Nargis akiwa katika vazi la kulalia amesimama pembeni ya kitanda. Alipoangalia pembeni Thabit alikuwa amepitiwa na usingizi.
“Nilikueleza nini?” Nargis alimuuliza kwa sauti ya upole.
Subira alibakia macho yamemtoka pima asijue ajibu nini, macho yake yake yalikataa yalichokiona na kuamini aliota ndoto. Sauti ya Nargis ilimrudisha kwenye akili yake halisi baada ya kuitwa jina lake.
“Subira, inawezekana hunijui ila kuanzia sasa utanitambua mimi ni nani,” bado Nargis alizungumza kwa sauti ya upole.
“Ni...ni...sa...”
“Subira naomba nikuulize swali jepesi, unanijua mimi?”
“Ndi...ndi...yo.”
“Kama nani?”
Itaendelea.
 
SEHEMU YA 28

Subira alibakia macho yamemtoka pima asijue ajibu nini, macho yake yalikataa yalichokiona na kuamini aliota ndoto. Sauti ya Nargis ilimrudisha kwenye akili yake halisi baada ya kuitwa jina lake.
“Subira, inawezekana hunijui ila kuanzia sasa utanitambua mimi ni nani,” bado Nargis alizungumza kwa sauti ya upole.
“Ni...ni...sa...”
“Subira naomba nikuulize swali jepesi, unanijua mimi?”
“Ndi...ndi...yo.”
“Kama nani?” endelea...“
M...m...ke wa Thabit.”
“Nilikuambia nini asubuhi?”
“Ni...ni...ni..”
“Sikiliza kwa vile leo nimerudi kwa mume wangu naomba leo nikuoneshe sehemu ya kulala ambayo utalala siku zote.”
Baada ya kutoa kauli hiyo, alinyanyua mkono juu ghafla lilitokea jeneza pembeni ya kitanda. Aliliamuru kufunguka, likawa wazi.
“Naomba uingie ndani ya jeneza nakwenda kukuzika ukiwa hai.”
“Ni...ni...samehe...ni...ni...”
“Nilikueleza kiustaarabu lakini husikii sasa haya ni manyunyu tu ukizidisha ukaidi mvua ya mawe itakunyeshea. Ulidhamiria kuniua lakini mmeshindwa, nilikuwa na uwezo wa kukuua lakini siitaki dhambi ya kuua. ”
“Na...na...jua ni...ni...”
“Subira mimi ni jini, naweza kukufanya lolote pamoja na kujitahidi kunizuia kwa haki yangu, hivi kwa hali ya kawaida ungekuwa wewe umesafiri kwenda kwenu kujifungua halafu unarudi unakuta mumeo katekwa na mwanamke mwingine ungejisikiaje?
“Inawezekana upole wangu ndiyo unaokutia kiburi, sasa leo utanijua mimi ni nani.”
Alinyanyua tena mikono juu, ghafla sanda ilitua mikononi, alinyoosha mkono na kumpa Subira.
“Hii ndiyo shuka yako utakayojifunika huko utakapokwenda kulala.”
Alimuamuru avue nguo alizovaa wakati wa kulala, alimpa sanda na kujifunga kisha alimuamuru aingie kwenye jeneza. Subira huku akitetemeka alitembea taratibu kulifuata jeneza, alimwangalia mumewe aliyekuwa kwenye usingizi mzito bila kujua kilichokuwa kikiendelea muda ule.
Alitanguliza mguu mmoja ndani ya jeneza kisha aligeuza shigo kumwangalia Nargis ambaye wakati huo alikuwa amekaa kitandani akifikiri atamuonea huruma. Gauni alilovaa lilionesha mpaka ndani kuonesha hakuvaa nguo nyingine.
Huku machozi yakimtoka alitaka kuomba msamaha lakini jicho kali la mbaya wake lilimtisha. Nargis alimuonesha kwa ishara ya mkono aingie ndani ya jeneza huku akimweleza muda ulikwenda alitaka kulala. Subira aliingiza na mguu wa pili kisha alikaa na kujilaza chali.
Baada ya kujilaza, Nargis aliliamuru jeneza kujifunga kisha alilisafirisha hadi makaburini ambako kulikuwa na kaburi limechimbwa tayari.
Baada ya kufikishwa alitolewa ndani ya jeneza na kubebwa na viumbe wanne wa ajabu mpaka kwenye mwana ndani na kulazwa ndani yake kisha alisikia akiwekewa ubao na baada ya muda alisikia vishindo vya udongo kumjulisha alikuwa ndiyo anazikwa. Subira alijikuta akijilaumu kwa kudhulumu mume wa mtu na kukubaliana na usemi wa cha mtu sumu.
Baada ya vishindo vya muda ghafla hali ilikuwa kimya huku kiza kinene kikiwa kimetawala na kuamini ule ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yake ya duniani kwa kuzikwa akiwa hai. Kizunguzungu kikali kilimshika na kupoteza fahamu, kilichoendelea hakukijua tena.
Nargis baada ya miaka kumi na ushee alilala na mumewe kwa mara ya kwanza, lakini hakuyafurahia mapenzi kwa vile alikuwa na mumewe kama mtu aliyekuwa msukule usiyojua kitu chochote. Roho ilimuuma kwa vile uwepo wake pale Thabit hakuujua.
Alipata wazo la kurudi kwa mzee Dumidumzi kumweleza alichokikuta kwa mumewe, lakini aliona kwenda huko ni kutumia njia ndefu. Aliamini njia rahisi ni kurudi kwa mganga wa Subira mzee Mukti kuzungumza naye ili amrudishie mumewe kwa gharama yoyote kuliko kurudi katika miamba myeusi ambako hakuyapenda mateso yake mpaka kumfikia mzee Dumidumzi ilitakiwa moyo wa ziada.
Aliondoka alfajiri kwenda kwa mganga katika umbile la kibinadamu, alikuta wagonjwa waliolala pale wakipata tiba. Naye aliungana nao katika foleni ya kwenda kuonana na mganga, yeye alikuwa mtu wa nne. Baada ya wagonjwa waliotangulia kuingia Nargis naye akaingia baada ya saa nzima kupita tangu alipofika.
Aliingia kama mtu wa kawaida na kumkuta mzee Mukti amekaa kwenye kigoda chake cha kuagulia. Mpaka anaingia netiweki yake ilikuwa bado haijasoma kaingia nani, kwa kuwa Nargis alikuwa amejitanda ushungi aliuondoa na kubaki kichwa wazi na uso wake kuonekana uwazi.
Nargis alitikisa nywele na kumfanya aonekane kiumbe mrembo, ghafla nywele za Mukti zilianza kumsimama na kujikuta akishtuka alipomwangalia vizuri mteja wake aliona pembe ndogo katikati ya kichwa. Aligundua aliyekuwa mbele yake ni jini aliyekuwa akipigana naye ambaye jana yake alipata taarifa zake. Alijiuliza aliwezaje kuingia kwenye kilinge chake!
Kwa chati huku macho yake yakimwangalia usoni jini Nargis, alipeleka mkono kwenye dawa ili amzuie. Lakini kabla hajaishika Nargis alikinyooshea kidole kikopo chenye dawa ghafla kilianza kuwaka moto. Mzee Mukti alishtuka na kuona kapatikana kwa vile tangu aujue uganga hakuwahi kuchezewa kilinge chake na kiumbe chochote.
Kitendo cha jini Nargis kuingia ofisini kwake na kufanya dawa zake zishindwe kufanya kazi kilimchanganya sana na kuona amewahiwa. Aliona kilichokuwa kikitokea muda ule ni kama ndoto si kitu cha kweli. Alijifikisha macho ili apate ukweli kilichotokea kama kina ukweli na tukio lililotokea mbele yake. Baada ya tukio lile Nargis alicheka sana kisha alisema:
“Hongera umejitahidi lakini hapa ndipo mwisho wa matatizo, ila leo sikuja kwa shari nami nimekuja kama wateja wengine hivyo nataka msaada wako,” Nargis alisema kwa sauti ya upole.
Inaendelea
 
SEHEMU YA 29

Alijifikisha macho ili apate ukweli kama tukio lililotokea mbele yake lilikuwa la kweli. Baada ya tukio lile Nargis alicheka kisha kwa upole alisema:
“Hongera umejitahidi lakini hapa ndipo mwisho wa matatizo, ila leo sikuja kwa shari nami nimekuja kama wateja wengine hivyo nataka msaada wako.” SASA ENDELEA...
Mzee Mukti akiwa bado mapigo ya moyo yapo juu na kijasho kiliendelea kumtoka, alijiuliza Nargis anataka msaada gani ikiwa tayari ameonesha ana uwezo mkubwa kuliko yeye. Huku akijitahidi kuficha hofu yake alimuuliza.
“U...u...una...taka m...m...saada gani ewe jini mwana wa mfalme wa bahari ya dhahabu?”
“Naomba kwanza suala la ujini liweke pembeni nami nakuja kama Subira alivyokuja, naitwa Nargis mke halali wa Thabit. Kwa hiyo nisaidie kama mwanadamu mwenye matatizo na si jini ndiyo maana nipo mbele yako kama mwanadamu.”
“U...unataka msaada gani?”
“Nataka unirudishie mume wangu mikononi mwangu.”
“Nimrudishe vipi?”
“Kama ulivyomtoa, najua umepewa fedha nyingi baada ya kuninyang’anya mume wangu. Nataka kukuambia ulichopewa na Subira, mimi nitakupa mara mia ili tu unirudishie mume wangu. Mimi kweli ni jini lakini nina haki ya kuishi maisha nitakayo bila kumdhuru kiumbe yeyote.
“Ni kweli mwanzo kabla ya kuwa mzazi nilikuwa sikubali kushindwa, nilipata dhambi nyingi kwa ajili ya kutoa roho za watu na majini kwa ajili ya kumlinda mume wangu. Lakini nimeona si lazima kutumia nguvu au kutoa uhai wa kiumbe kumlinda mume wangu.
“Kipindi hiki cha kumtafuta mume wangu nimekutana na vikwazo vingi toka kwako nina imani uwezo wako ndiyo uliomfanya Subira akupe zawadi nyingi za nyumba na magari. Nilikuwa na uwezo wa kuviteketeza vyote ulivyopewa lakini sikutaka kufanya hivyo kwa vile kwangu mali si muhimu kama mume wangu.
“Mali aliyokupa Subira ni yangu kwa vile hajui imepatikana vipi, mimi ndiye mmiliki wa mali yote aliyonayo Thabit. Kumbuka mali zote ziliteketezwa pamoja na uganga wako hukuweza kuzirudisha lakini nilizirudisha. Hata mume wangu alipopata matatizo usingeweza kumtibu, nilimtibu mwenyewe.
“Huoni jinsi gani ninavyomjali mume wangu pia ni mzazi mwenzangu, kwa hiyo ninacho kuomba kikubwa nirudishie mume wangu. Sema unataka nikupe kitu gani ili unirudishie mume wangu.
Hata wewe kama unasafiri kwenda nyumbani ukirudi ukute mkeo kipenzi kaolewa na mtu mwingine utajisikiaje tena kwa hila za huyo mwanaume? “Nina imani unajua maumivu yake kingine nimeteswa kwa haki yangu hivi hapa jini na mwanadamu nani mbaya?” Nargis aliuliza huku machozi ya uchungu yakimtoka na kuongeza uzuri wake mara kumi.
“Mzee Mukti kwa nini unamlisha chakula asichokipenda mume wangu? Kwa nini unamlisha haramu? Subira yupo na mume wangu kwa nguvu za dawa yupo kama ndondocha. Sitaki nirudi nilipotoka kwani uvumilivu una kikomo, waganga wengi walikufa kwa ubishi hivyo sitegemei na wewe kuwa hivyo.
“Lakini leo nimekuja kistaraabu, hivi mtu aliyedhamiria kukuua unaweza kuzungumza naye hivi?” Nargis alimuuliza mzee Mukti aliyekuwa amepigwa na butwaa macho yamemtoka pima.
“Nakuuliza mzee wangu, mara ngapi mmepanga mipango ya kuniua lakini mmeshindwa. Lakini leo nakuja kwako kistaraabu hivi, kweli?”
“Najua nazungumza maneno mengi bila vitendo,” Nargis alisema huku akinyanyuka kitendo kilichoongeza wasiwasi kwa mganga na kujua kumekucha.
Lakini ilikuwa tofauti kwa Nargis ambaye alishika mkono kichwani kwa muda kisha alipiga kofi. Ghafla walitokea viumbe wawili wamebeba mabegi mawili makubwa na kuyaweza mbele ya mganga. Baada ya kuweka Nargis alipiga kofi jingine lililowafanya viumbe wale kuyeyuka. Baada ya kutoweka Nargis alisema:
“Mzee wangu, huu ni utajiri ambao utautumia mpaka kufa kwako hata kizazi chako kitakufa na kuuacha. Nina imani njaa ndiyo inayowafanya waganga wengi wawadhuru wasio na hatia. Nina imani nimeona jinsi gani ninavyompenda mume wangu.”
Nargis alisema huku akifungua yale mabegi, moja lilikuwa limejaa fedha za mataifa mbalimbali na lingine lilikuwa na mchanganyiko wa madini yote ya thamani.
“Sasa mama unataka msaada gani?” Mzee Mukti alichanganyikiwa na mali iliyokuwa mbele yake.
“Kunirudishia mume wangu.”
“Unataka nimfanye nini Subira?”
“Sitaki umfanye kitu chochote kibaya, ninachotaka liondoe tandaburi ulilomvilingishia mume wangu ili arudi kwenye akili yake ya kawaida anitambue kama mimi ni mkewe wa halali. Najua kwa sasa umeifunga akili yake asinikumbuke na kufanya aamini kabisa mkewe ni Subira.”
“Nitafanya hivyo, nakuahidi kazi hiyo nitaifanya mwenyewe.”
“Sitaki uifanye wewe, nataka aifanye Subira mwenyewe kama alivyofanya mwanzo.”
“Sawa nimekuelewa.”
“Nina imani tutakwenda vizuri kama utafanya ninavyotaka.”
“Nakuahidi kufanya kila ulichonieleza.”
“Nitashukuru, naomba nikuache uendelee na wateja wengine.”
“Hapana leo nitakuwa na kazi yako tu.”
“Kuja kwangu kusiwe chanzo cha wengine kukosa huduma, najua lazima Subira atakuja hivyo utaanza hapo ila sasa hivi wahudumie wagonjwa wengine.”
“Nashukuru kwa huruma yako.”
Kama alivyoingia ndivyo alivyotoka katika umbile la kibinadamu na kuwaaga wagonjwa wengine waliokuwa kwenye foleni. Baada ya kutoka Mukti alishusha pumzi ndefu asiamini kilichotokea.
Itaendelea
 
SEHEMU YA 30

Kama alivyoingia ndivyo alivyotoka katika umbile la kibinadamu na kuwaaga wagonjwa wengine waliokuwa kwenye foleni. Baada ya kutoka Mukti alishusha pumzi ndefu asiamini kilichotokea.
ENDELEA...
Alivuta begi kubwa na kuliangalia vizuri na kukuta limejaa fedha mchanganyiko za mataifa makubwa na za Tanzania.
Alifungua begi la pili lililokuwa limejaa madini mchanganyiko na kumfanya mzee Mukti kupiga kelele za kupagawa na kuanza kujimwagia kitu kilichowashtua wasaidizi wake walioingia ndani na kukuta fedha na madini yametawanyika.
“Nini mzee?” wasaidizi walimshangaa.
“Sasa hivi mimi ni tajiri wa maisha.”
“Hizi fedha na madini umetoa wapi?”
“Ni Mungu tu.”
Ghafla alitokea Nargis mbele yake na kumweleza afanye kazi kwanza, aliwaomba watoke na kuyaweka pembeni yale mabegi yenye fedha kisha aliendelea na kazi yake kama kawaida ya kuwahudumia wateja. Alijikuta akili yake ikimuwaza Subira na kutaka afike mapema.
Alijikuta akimshangaa jini Nargis kuonesha huruma ya ajabu, lakini ingekuwa hiyari yake na utajiri kama ule angemfanya kitu kibaya kama si kumpa sumu ili kuwaacha Nargis na mumewe wafurahie ndoa yao. Lakini hakutaka kumfanyia baya lolote zaidi ya kurudi katika ndoa yake.
***
Kibaridi kikali cha alfajiri kilimwamsha Subira ambaye alipojigeuza alishangaa kujiona amebanwa na kitu. Alipofumbua macho alikutana na mwanga mkubwa ukitoka juu kuonesha yumo shimoni. Alipojitahidi kunyanyuka alishindwa kutokana na sehemu aliyowekwa ilikuwa ndogo na kumfanya asiweze kujitikisa.
Ili apate msaada ilibidi apige kelele kuomba msaada kwa wapita njia, baada ya muda watu walikusanyika juu ya kaburi. Walishangaa kumwona mtu amelala kaburini akiwa amelazwa kwenye mwana ndani akiwa amefungwa sanda lakini pembeni ya kaburi hakukuwa na udogo.
Waliingia ndani ya kaburi na kumtoa nje, watu wote walimshangaa na kutaka kujua kipi kilimsibu. Subira alishindwa kusema alikuwa akilia tu, kurudi nyumbani aliogopa aliomba msaada wa nguo. Baada ya kupatiwa pande mbili za kanga, aliomba msaada wa gari mpaka kwa rafiki yake ambaye alimshangaa kumwona yupo vile.
Alimuomba kwanza ampe nguo zake kisha amuazime fedha ili aende Kigamboni kwa mzee Mukti kwani aliamini bwawa liliishaingia ruba lilikuwa haliogeki tena. Shoga yake alimpatia nguo baada ya kuoga. Kutokana na kuchanganyikiwa hata kula hakutaka.
Alikodi gari hadi Kigamboni kwa mzee Mukti, kama kawaida alikuwa hakai foleni alikuwa akipitiliza na kwenda kukaa kwenye chumba maalumu alichotengewa na mganga kisha aliwatuma vijana wa mzee Mukti wakamwite kwani alionekana amechanganyikiwa.
Mzee Mukti alikwenda kwenye chumba maalumu alichotenga kwa ajili ya kukutana na Subira kutokana umuhimu wake katika kuyabadili maisha yake. Lakini siku ile alimuona kama adui, bila Nargis angemfanya kitu kibaya baada ya akili yake kufikiria utajiri aliopewa.
“Karibu,” mzee Mukti alificha chuki yake.
“Asante.”
“Mbona upo hivyo?”mzee Mukti alimshangaa jinsi alivyovaa na mwonekano wake kuonesha ana matatizo makubwa hakuwa Subira aliyemzoea kujiremba lakini siku ile alikuwa vululuvululu.
“Babu mambo ni mabaya kuliko ulivyofikiria.”
“Tatizo nini?”
“Huwezi kuamini kilichonitokea, mimi wa kulala kaburini nimevishwa sanda?” Subira alisema huku akilia.
“Sijakuelewa una maanisha nini?”
Subira alimweleza kilichotokea usiku wakati akiwa kitandani alipotokewa na jini Nargis ambaye alimvisha sanda kama maiti na kupelekwa kulala ndani ya kaburi tena kwenye mwana ndani na jinsi alivyookolewa na watu na kutolewa ndani ya kaburi.
“Duh!” mzee Mukti alishtuka baada kusikia uwezo mkubwa wa Jini Nargis kwa kuvunja nguvu zake zote alizoweka na kufanya anavyotaka.Kwa mara ya kwanza aliamini uchawi unazidiana na kushangaa kama Nargis alikuwa na uwezo wa kuingia kila kona na kufanya aliyoyafanya kulikuwa na umuhimu gani wa kumpa utajiri ili amrudishie mumewe mkononi mwake. Wasiwasi wake alijua lazima alikuwa akimtega kama akikaidi basi naye amtie adabu.
“Mzee wangu naumbuka kwani tumekosea wapi mpaka imekuwa hivi?”
“Mmh! Hebu subiri.”Mzee Mukti alitoka na kumwacha Subira akiwa ameshika tama asijue hatima yake, mzee Mukti aliamini ile ndiyo ilikuwa nafasi yake ya kulirudisha penzi la Nargis kwa mumewe. Alitumia nafasi ile kufungua vifungo vyote alivyomfunga Thabit, baada ya kuandaa dawa ya kuvunja kila alichokifanya ili Thabit ampende Subira.
Baada ya kuandaa dawa alirudi chumbani na kumpa Subira, alipofika alimpa dawa za kuoga, kuweka katika chakula, kinywaji na kuweka katika maji ya kunyunyizia kuzunguka nyumba nzima.
“Hebu kafanye hivi.”
“Mzee wangu mbona kama dawa ulizokuwa ukinipa zamani, zitaweza kweli?”
“Mama, mimi ndiye mganga, hebu kafanye niliyokuelekeza.”
“Mmh! Sawa, naweza kurudi nyumbani kwangu?” Subira aliisha ingia woga.
“Nenda tu wala usiogope.”
“Yaani nakwenda lakini nimeingiwa woga kweli.”
“Ukiingia vitani usiogope kupigwa lazima upambane na si kuogopa.”
“Kwa nini tusiende wote, yaani naogopa.”“Hakuna kitu we nenda tu.”
“Mmh! Sawa,” Subira alisema na kunyanyuka kuelekea nje ili aelekee kwake ambako alipaona panawaka moto.
Inaendelea
 
SEHEMU YA 31
“Mmh! Sawa, naweza kurudi nyumbani kwangu?” Subira aliisha ingia woga.
“Nenda tu wala usiogope.”
“Yaani nakwenda lakini nimeingiwa woga kweli.”
“Ukiingia vitani usiogope kupigwa lazima upambane na si kuogopa.”
“Kwa nini tusiende wote, yaani naogopa.”
“Hakuna kitu we nenda tu.”
“Mmh! Sawa,” Subira alisema na kunyanyuka kuelekea nje ili aelekee kwake ambako alipaona panawaka moto.
SASA ENDELEA...
Subira alirudi nyumbani akiwa hajiamini kwani wasiwasi wake wote ulikuwa kwa Jini Nargis mwanamke halali wa Thabit aliyempindua. Alikodi gari hadi nyumbani kwake, bahati nzuri alimkuta mumewe Thabit bado yupo nyumbani.
Alimshangaa mkewe mavazi aliyovaa na asubuhi ile alikuwa akitoka wapi.
“Mke wangu unatoka wapi asubuhi yote hii na ulikuwa wapi?”
“Mume wangu nitakueleza naomba uniache nipumzike kwanza mengine tutazungumza baadaye.”
“Sawa, vipi kazini huendi?”
“Naenda.”
“Basi fanya haraka tuondoke mengine tutazungumza jioni tukirudi.”
“Sawa mume wangu, naomba nikaoge ili nikuandalie kifungua kinywa.”
“Sawa mke wangu fanya haraka.”
Subira alishangaa Thabit kuendelea kumwita mkewe pamoja na kulala na mkewe jini, alikwenda kuoga maji aliyochanganya dawa aliyopewa na mzee Mukti. Baada kuoga alimwita na Thabit kuoga maji ya dawa. Mumewe aliingia bafuni na kuoga bila kujua maji aliyokuwa akioga yalikuwa na dawa.
Baada ya kuoga alimwandalia kifungua kinywa kama kawaida na kuweka dawa kwenye chakula. Baada ya kuweka dawa alimpelekea chakula ambacho walikula pamoja. Kila alivyokuwa akila na kunywa alihisi kuona kama maluweluwe machoni mwake.
“Subira,” alimwita baada ya kushindwa kujielewa.
“Nini mume wangu?”“Au basi,” alijibu baada ya hali kutulia.
“Niambie mume wangu kuna nini?”
“Walaa, tuwahi kazini.”
“Sawa.”
Kabla ya kuondoka Subira alimuacha ndani Thabit na kuzunguka nyumba kunyunyuzia dawa aliyopewa na mganga. Alifanya kwa haraka kisha alirudi ndani na kumweleza mumewe.
“Mume wangu twende zetu,” Subira alisema huku akimshika mkono wawahi kazini.
Walitoka pamoja na kuingia ndani ya gari kuwahi kazini, walipofika waliendelea na kazi kama kawaida huku Thabit akiwa hajielewi baada ya kuingiwa na kumbukumbu ya ghafla ya Nargis.
“Mmh! Nargis...Nargis...ni...ni...nani? Hapana si...si mke wangu..Mungu wangu na...na Subira ni nani yangu? Hebu,” alinyanyua simu na kubofya namba kisha alizungumza.
“Subira.”
“Abee.”
“Njoo mara moja.”
“Nakuja.”
Baada ya muda Subira aliingia ofisini kwa Thabit na kusimama mbele kusikiliza wito.
“Subira.”
“Abee.”
“Eti wewe hapa ofisini ni nani?”
“Mume wangu, swali gani hilo?”
“Umeniitaje?”
“Mume wangu.”
“Mimi mumeo! Tokea lini?”
“Thabit mume wangu upo sawa?”
“Nipo sawa.”
“Kwa nini unaniuliza swali hilo?”
“Kuna kitu kinanichanganya!”
“Kitu gani hicho?”
“Kwanza kuna pete niliyokuwa navaa ipo wapi?”
“Si...si...jui!”
“Halafu wewe ni msaidizi wangu, mke na mume imeanza lini?” Thabit alishangaa.
“Thabit mume wangu wewe ndiye uliyeniomba niwe mkeo na kufuata taratibu zote nashangaa leo kuniuliza hivyo?”
“Mimi nilikuoa wewe?”
“Ndiyo.”
“Mimi kweli! Thabit nilikuoa wewe na kuwa mke na mume?” Thabit alizidi kushangaa.
“Ndiyo na sasa hivi tuna miaka zaidi ya mitano.”
“Mmh! Siamini...siamini, mimi nina mke.”
“Ndiye mimi.”
“Hapana mke wangu anaitwa Nargis.”
“Mume wangu leo umekuwaje?” Subira alisema huku akitoka ofisini na kurudi na picha iliyokuwa kwenye flemu ya siku yao ya harusi wakiwa wamepozi na kuipeleka mbele ya Thabit.
“Mume wangu hii nini?” Subira alimuonesha Thabit picha yao ya harusi.
“Mmh! Hii harusi ulifunga na mimi?” Thabit alizidi kushangaa huku akitazama picha ya harusi yao kama ndiyo siku ya kwanza kuiona.
“Thabit mume wangu umekuwaje leo, asubuhi tumetoka pamoja na siku zote tupo pamoja kipi cha ajabu kwa leo?” Subira alizidi kushangaa mabadiliko ya ghafla ya mume wake.
“Bado naona mauzauza.”
“Mauzauza gani jamani?’
“Naomba uniache kwa muda nitakupigia baadaye.”
Subira alitoka ofisini kwa Thabit akiwa amechanganyikwa asijue nini kimetokea kwani kila dakika mambo yalizidi kumchanganya. Kwa haraka alichukuwa simu kumpigia mzee Mukti ili amweleze kilichotokea kwani ni muda mfupi toka atoke kwake na kupewa dawa ambayo badala ya kupunguza imeongeza matatizo.
Baada ya kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili:
“Haloo.”
“Haloo babu mbona mambo huku yanazidi kuwa magumu?”
“Kivipi?” Mzee Mukti alijifanya hajui kitu.
Subira alimweleza kilichotokea muda mfupi, mumewe kumshangaa na kumwona si mkewe. Mzee Mukti aliamini kazi aliyotumwa na Nargis ilikuwa imekwisha, alishusha pumzi na kusema:
“Mmh! Mambo mazito, inaonekana uwezo wangu umefikia mwisho.”
“Mungu wangu sasa itakuwaje?”
Itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom