Simulizi ya kweli: Niliishi kuzimu siku saba

SEHEMU YA 63


ILIPOISHIA:
Muda mfupi baadaye, wote tulikuwa ‘saresare maua’, akanisukuma kwa nguvu kwenye uwanja wa fundi seremala, nikaangukia mgongo, akaja juu yangu kwa kasi, maandalizi ya mechi ya kirafiki isiyo na jezi wala refa yakaendelea huku akionesha kunikamia kama Simba na Yanga zinavyokamiana zinapokutana uwanjani.
SASA ENDELEA...
Kipyenga kilipolia tu, Shamila ndiye aliyekuwa wa kwanza kugusa mpira, akawa anabutua mashuti ya nguvu na kunifanya nihisi kama atanielemea na kunishinda ndani ya muda mfupi tu, jambo ambalo kwangu lingekuwa aibu kubwa.
Nikajipanga na kuanza kwenda naye sawa, akawa akipiga mashuti kwa kubutua, mimi naukontroo mpira na kumpiga chenga za mwili, wakati mwingine nikawa natambaa na chaki kama Christiano Ronaldo, jambo lililofanya kibao kigeuke, badala ya yeye kuwa ananishambulia kwa kasi, ikawa mimi ndiyo namshambulia.
Ilibidi nitumie ujuzi wa hali ya juu kuwahi kummaliza nguvu ili nimalize mchezo kwani Junaitha naye alikuwa akinisubiri na sikujua alikuwa na lengo gani. Kutokana na jinsi nilivyokuwa namshambulia Shamila kwa akili, haikuchukua muda mrefu, akatangaza kusalimu amri, akanikumbatia kwa nguvu!
“Nakupenda sana Jamal, nataka unioe, nataka niwe mkeo wa ndoa,” alisema Shamila kwa sauti kama mtoto mchanga, nikamnong’oneza sikioni kwamba asiwe na wasiwasi, nitamuoa, nikamuona akitabasamu na kuangukia upande wa pili kama mzigo. Haikuchukua muda, akawa anakoroma kuonesha kwamba tayari alishapitiwa na usingizi mzito, hakujua kama nilikuwa nacheza na akili yake.
Kwangu mimi ilikuwa ni zaidi ya ushindi kwani nilijua sasa hatanisumbua tena. Harakaharaka nikainuka na kuchukua gwanda zangu na kuzitia mwilini, ikabidi nirudi kwanza kwenye chumba changu. Harakaharaka nikaenda kujimwagia maji huku nikitafakari kilichotokea muda mfupi uliopita.
Kiufupi nilikuwa nimebadilika sana, sikuwa Jamal yule ambaye hata mimi mwenyewe najijua. Awali nilikuwa muoga sana wa wanawake, hata Raya, msichana aliyetokea kunipenda kwa moyo wake wote, ilinichukua muda mrefu sana mpaka kuja kukutana naye kimwili lakini sasa, nilikuwa kama jogoo, kila tetea anayepita mbele yangu sikuwa naona hatari kumpitia. Hata sielewi ujasiri huo niliupata wapi.
Wakati nikiwa naendelea kujimwagia maji, ni kama Junaitha alichoka kunisubiri kule chumbani kwake, nikashtukia akiingia chumbani kwangu. Nilimtambua kuwa ni yeye hata kabla sijamuona kutokana na jinsi alivyoniita.
“Mbona huji jamani, mi nakusubiri mpaka nachoka bwana!” alisema huku akikaa kitandani. Nikamwambia kuwa nilikuwa nasikia sana joto kwa hiyo niliamua kujimwagia maji kabisa.
“Sasa si ungekuja kulekule kwangu uoge?” alisema. Kwa kuwa tayari nilishamaliza, nilijifunga taulo na kutoka.
“Utasababisha hawa watoto wajue siri yetu bure! Nataka nikiingia chumbani na wewe uwe umeshafika,” alisema kwa sauti yenye mamlaka, nikacheka huku nikijifuta maji. Alisimama na kusogea mlangoni, akachungulia huku na kule, alipoona hakuna mtu, alitoka na kuusindika mlango.
Harakaharaka nilivaa nguo zangu, nikatoka na kufunga mlango, nikatembea kwa umakini mpaka kwenye mlango wa chumba cha Junaitha, nikausukuma, ulikuwa wazi, nikaingia mpaka ndani.
Wewe ni mwanaume wa kipekee sana Jamal, samahani usione kama nakufosi kuwa na mimi kwa sababu nimekuzidi kila kitu na hapa upo kwangu, hapana! Ni kwa sababu sijawahi kukutana na mwanaume kama wewe maishani mwangu. Mtu anaweza kukuona mdogo kwa nje lakini una mambo makubwa sana,” alisema Junaitha na kunisogelea, akanikumbatia kwa nguvu, nikalihisi joto la mwili wake kwenye mwili wangu.
Japokuwa nilikuwa nimetoka kwenye mchezo muda mfupi uliopita, kwa jinsi Junaitha alivyokuwa akihamasisha, nilijikuta nikiwa tayari kwa mpambano mwingine, japokuwa hata sheria za mchezo hazikuwa zikiruhusu kilichokuwa kinataka kufanyika.
Haukupita muda mrefu, tuliingia uwanjani tena lakini tofauti na Shamila, Junaitha alikuwa na utaalamu wa hali ya juu. Naye hakuwa na papara kama mimi, maandalizi ya kupasha viungo moto yalienda taratibu, kipyenga kilipopulizwa, kila mmoja akawa anacheza kwa staili ya kumvizia mwenzake, ladha ya mchezo ikawa tofauti kabisa na Shamila.
Mtanange wa kukata na shoka uliendelea, hata sijui nguvu za kuhimili mikikimikiki nilizipata wapi kwa sababu kwa jinsi nilivyomudu kucheza na mpira, hata Junaitha mwenyewe hakugundua kwamba nimetoka kulisakata tena kabumbu muda mfupi tu uliopita.
Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa mpambano huo, Junaitha alikuwa hajitambui, nikajikokota na mpira wangu kwapani kwa sababu kama sheria zinavyosema, mchezaji akipiga hat trick anaondoka na mpira wake, nikavaa gwanda zangu na kurudi chumbani kwangu, nikimuacha Junaitha naye anakoroma.
Nilipofika na kujitupa kitandani, kutokana na jinsi nilivyokuwa nimechoka, sikuelewa tena kilichoendelea mpaka nilipokuja kuzinduka alfajiri ya siku ya pili. Junaitha ndiye aliyekuja kuniamsha, cha ajabu eti akawa ananilaumu kwamba kwa nini sikulala kule kwake, akawa ananiuliza niliondoka muda gani? Nikajua kwamba kwa vyovyote na yeye ndiyo alikuwa amezinduka alfajiri hiyo.
Kwa kuwa siku hiyo tulikuwa na ratiba ngumu sana, tulianza kujiandaa, tukawaamsha watu wengine wote ambapo Shamila alikuwa mgumu sana kuamka kwa madai kwamba bado mwili wake ulikuwa umechoka, ikabidi Junaitha atumie nguvu.
Saa kumi na mbili juu ya alama, wote tayari tulikuwa tumeshajiandaa, tukakaa mezani na kunywa chai iliyoandaliwa na Junaitha kisha baada ya hapo, tukatoka. Ilibidi tutumie gari la Junaitha ambalo kabla ya hapo, sikuwa najua kama anamiliki gari. Lilikuwa ni Toyota Alphard la kisasa, akasema tukitumia ile Noah ya akina Firyaal itakuwa rahisi kutambulika.
Gari tulilopanda lilikuwa na vioo tinted, jambo lililofanya iwe vigumu kwa mtu wa nje kuona kilichokuwa kinaendelea ndani, Junaitha mwenyewe ndiyo akakaa nyuma ya usukani na mimi nikakaa pembeni yake. Kwa jinsi tulivyokuwa tumejikausha, isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuhisi kwamba kuna mchezo ulikuwa ukiendelea kati yetu.
Hata Shamila mwenyewe, japokuwa mara kwa mara alikuwa akinitazama kwa macho ya kuibia, hakuweza kuhisi chochote, achilia mbali mpenzi wangu Raya ambaye muda wote alikuwa ametulia. Tulitoka na breki ya kwanza ilikuwa ni kwenye kituo kikuu cha polisi, Junaitha akatutaka wote tubaki ndani ya gari, akashuka na kuingia kituoni.
Baada ya kama dakika ishirini, alitoka akiwa ameongozana na askari mmoja aliyekuwa na nyota nyingi mabegani, ambaye alionesha ishara tu, askari zaidi ya sita wenye silaha wakaingia ndani ya difenda, Junaitha akarudi kwenye gari letu na yule askari akaungana na vijana wake.
“Kuna watu itabidi tuwapitie, mwanasheria wetu pamoja na yule mwandishi wa habari, nadhani wote tayari watakuwa wanatusubiri sehemu tuliyokubaliana,” alisema Junaitha. Nikamuuliza swali:
“Kwa hiyo hapa tunaelekea wapi?”
“Tulia jamal, mbona una haraka, nimesema leo ndiyo leo na watu wote watatujua sisi ni akina nani. Shenaiza na Firyaal, naomba mkaze mioyo yenu maana kinachoenda kutokea kwa baba yenu siyo kizuri lakini lazima tufanye hivi,” alisema Junaitha, akawasha gari, tukaondoka huku ile difenda ikitufuata kwa nyuma.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEHEMU YA 64


“Tulia jamal, mbona una haraka, nimesema leo ndiyo leo na watu wote watatujua sisi ni akina nani. Shenaiza na Firyaal, naomba mkaze mioyo yenu maana kinachoenda kutokea kwa baba yenu siyo kizuri lakini lazima tufanye hivi,” alisema Junaitha, akawasha gari, tukaondoka huku ile difenda ikitufuata kwa nyuma.
SASA ENDELEA...
Msafara uliendelea na safari mpaka tulipofika Kurasini, tukakata kushoto na kuiacha barabara ya lami, nikaikumbuka vizuri njia hiyo kwani ndiyo tuliyopita siku ile tulipoenda nyumbani kwa akina Shenaiza.
Tulipoingia kwenye barabara hiyo, ile difenda iliyokuwa nyuma, ilituwashia taa, nikamuona Junaitha akipunguza mwendo na kupaki pembeni, ile difenda nayo ikapunguza mwendo na kusimama. Yule askari aliyekuwa na nyotanyota begani akamsogelea Junaitha.
“Kumbe mlikuwa mnamaanisha huyu mzee Loris?”
“Ndiyo, kwani maelezo yote si yanajitosheleza afande?”
“Ni hatari sana kwa kweli, hata sidhani kama itawezekana.”
“Kwani mheshimiwa, wananchi wanapoletamalalamiko kwenu, tena mazito kama haya, wakiwa na ushahidi wa kila kitu, ni nani anayeweza kuwasaidia kama siyo jeshi la polisi?”
“Wewe ni nani unayeuliza maswali ya namna hiyo? Isitoshe sizungumzi na wewe, naongea na huyu mama aliyeleta taarifa.”

“Naitwa Richard Bukos, ni mwandishi wa habari kutoka Kitengo Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM),” majibu yale ya yule mwandishi wa habari ambaye tulikuwa naye ndani ya lile gari, Toyota Alphard, yalimshtua mno yule askari. Ni kama hakutegemea kama kulikuwa na mwandishi wa habari mle ndani, tena akiwa na vitendea kazi vyote.
“Kwa nini mmekuja na waandishi wa habari?” alimgeukia Junaitha na kumuuliza swali hilo, akionesha kutofurahishwa kabisa na uwepo wa Bukos eneo lile.
“Kwani kuna tatizo gani afande? Tunataka Watanzania wote wajue kinachoendelea,” alijibu kwa kujiamini, nikamuona akigeuka na kurudi kule kwa wenzake bila kuzungumza kitu. Shenaiza alinigeukia, tukatazamana kisha wote tukageuka na kumtazama Bukos kisha tukageukia kule kwenye ile difenda. Tukamuona yule askari akijadiliana na wenzake, wakiwa ni kama wanalaumiana kitu.
Muda mfupi baadaye, tulimuona akitoa simu ya upepo (Radio Call), akaibonyeza na kuanza kuzungumza na watu wa upande wa pili. Mpaka muda huo sikuwa nimeelewa ni nini hasa kilichomfanya aonekane kusitasita.
“Kwani kuna nini kinaendelea?”
“Inaonekana wanamjua huyu mzee,” alisema Junaitha, yule askari akawa anazungumza na simu huku akisogea pale kwenye gari. Alipomaliza kuzungumza, alimgeukia Junaitha.
“Huku ni kama mmetuleta uwanja wa vita, hatuwezi kuingia kichwakichwa, hata nyie humo ndani ya gari, itabidi gariligeuzwe na kwenda kupaki kule barabarani, mbali kabisa, tunaenda kuuwasha moto ambao haitakuwa rahisi kuuzima, umenielewa?” alisema askari huyo, sautikutoka kwenye simu yake ya upepo ikawa inasikika, askari wengine wakipeana maelekezo.
Imebidi niombe msaada kutoka makao makuu, kuna wenzetu wanakuja ila nakuonya siku nyingine lazima uwe unatoa taarifa ambazo zimekamilika. Wewe mwandishi wa habari itabidi ukae mstari wa mbele kabisa wa mapambano, si unajifanya unajua kufuatilia matukio magumu?” alisema huku akigeuka na kuondoka.
Kwa muda wote huo, Firyaal na Shenaiza ambao walikuwa wamekumbatiana, walikuwa kimya kabisa, Raya na Shamila nao walikuwa kimya, wakitazama kila kilichokuwa kinaendelea.
“Wasitake kututisha bwana, wanataka tukasimame barabarani ili iweje? Watakuwa wanataka kutuchezea mchezo mchafu hawa.”
“Hapana, alichokisema ni kweli, kule ndani kwetu kuna walinzi wengi wenye bunduki wanamlinda baba na kama amerudi ulinzi huwa unaongezwa zaidi, kuna kamera kila sehemu,” alisema Shenaiza na kuungwa mkono na mdogo wake, Firyaal.
Yule askari ambaye alikuwa amesogea pembeni, alianza kumuonesha ishara Junaitha kwamba ageuze gari, kufuatia maelezo yale ya Shenaiza na Firyaal, ilibidi tugeuze tu, tukaanza kurudi kule tulikotoka ambapo tulilipita lile gari la polisi ambalo lilikuwa limewasha taa za mbele na za juu.
Wale askari waliokuwa ndani ya gari hilo, wote walishashuka na kutawanyika eneo lile na kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele, ndivyo eneo lote lilivyokuwa linaonekana kama uwanja wa vita.
Junaitha aliendesha gari mpaka barabarani, akatafuta sehemu nzuri nakupaki, yule askari akawa anatembea kwa kasi kutufuata.
“Kuna yeyote anayeifahamu vizuri ngome ya Loris na mazingira yake ya ndani?”
“Ndiyo, tuko na binti yake mdogo, yeye anaweza kuwa msaada mkubwa kuwaongoza,” alisema Junaitha akimuonesha Firyaal.
“Basi itabidi tuongozane naye,” alisema, mapigo ya moyo wangu yakanilipuka paah! Yaani wao wenyewe walishasema kwamba pale ni uwanja wa vita halafu safari hii wanataka eti Firyaal ndiyo awaongoze. Wao wamevaa nguo maalum za kuzuia risasi (bullet proof) lakini Firyaal yeye amevaa blauzi tu!
“Haiwezekani.”
“Haiwezekani nini?”
“Haiwezekani Firyaal ndiyo awaongoze, bora hata mimi ndiyo niwaongoze.”
“Kwani wewe unayafahamu mazingira ya mle ndani?”
“Hapana, nitamuuliza akinielekeza na mimi nitawaelekeza.”
“Mbona unataka kuleta mzaha kwenye mambo ‘serious’ we kijana, hebu usiingilie kazi yetu,” alisema yule askarikwa sauti yenye mamlaka, nikageuka na kumtazama Firyaal, tukawa tunatazamana. Sijui kwa nini roho yangu ilikuwa ikinienda mbio kiasi hicho, nilishahisikwamba kuna jambo baya linaenda kutokea mbele yetu.
“Junaitha, do something!” (Junaitha, fanya chochote) nilimwambia Junaithan, akanigeukia na kunitazama.
“Kwani wasiwasi wako ni nini Jamal.”
“Vita haina macho, wanaweza kumpiga risasi Firyaal.”
“Siku zote huwa nakufundisha namna ya kuishinda hofu ndani ya moyo wako, kwa nini ufikirie mabaya tu?”
“Kama wasiwasi wako ni huo, tutamvalisha ‘bullet proof’ na kofia ngumu ya chuma, atakuwa salama,” alisema yule askari, akageuka na kuondoka zake.
“Usiwe na wasiwasi Jamal, nitakuwa sawa. Ni lazima tushirikiane nao ili kukomesha ushetani anaoufanya baba,” alisema Firyaal kwa kujiamini, nikakosa cha kujibu. Ukimya ulitawala mle ndani ya gari, kila mmoja akawa anawaza lake.
Muda mfupi baadaye, tulizinduliwa na ving’ora vya magari manne ya polisi yaliyokuwa yanakuja kwa kasi kubwa, yote yakiwa yamewasha taa za mbele, ndani yake kukiwa na askari wengi wenye silaha.
Yote yakaiacha barabara ya lami na kuingia kwenye barabara ya vumbikwa kasi kubwa, yakaenda kusimama jirani na lile la kwanza na hata kabla hayajasimama, askari wote tayari walikuwa wameshashuka kwa kuruka. Ungeweza kufananisha kila kitunafilamu ya mapigano.
Yule askari aliyekuwa akizungumzana sisi mara kwa mara, alianza kutoa maelezo, akawapanga katika makundi mawili, kila mmoja akiwa na bunduki mkononi, akawa anawaelekeza nini cha kufanya na baada ya kilammoja kujipanga kwenye sehemu yake, alitufuata pale kwenye gari, tulipokuwa tumekaa, tukishuhudia kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
Mkononi alikuwa ameshika koti maalum la kuzuia risasi na kofia ngumu ya polisi kama alivyokuwa ametuahidi, mapigo ya moyo wangu yakawa yanazidi kunienda mbio. Cha ajabu, Firyaal yeye uso wake ulikuwa umejawa na tabasamu pana, akasogea mpaka pale kwenye gari na kutuambia kuwa muda wa kazi umewadia.
“Wewe mpigapicha itabidi ukae kwa mbali maana hatuna vifaa vya kutosha vya kukukinga na risasi, binti njoo nikuelekeze namna ya kuvaa,” alisema akimuoneshea Firyaal, harakaharaka akashuka kwenye gari, ikabidi na mimi nishuke.
“Dont worry Jamal, each and everything is going to be okay!” (Usiwe na wasiwasi Jamal, kila kitu kitakuwa sawa) alisema Firyaal na kunisogelea, akanikumbatia na kunibusu mdomoni huku kila mtu akishuhudia. Sikujali, nilikuwa nampenda sana Firyaal na sikuwa tayari kuona jambo lolote baya linamtokea, hasa kabla ya mimi na yeye kukutana na kumaliza kile tulichokuwa tayari tumekianza.

Je, nini kitafuatia?
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 65
ILIPOISHIA:
“Dont worry Jamal, each and everything is going to be okay!” (Usiwe na wasiwasi Jamal, kila kitu kitakuwa sawa) alisema Firyaal na kunisogelea, akanikumbatia na kunibusu mdomoni huku kila mtu akishuhudia. Sikujali, nilikuwa nampenda sana Firyaal na sikuwa tayari kuona jambo lolote baya linamtokea, hasa kabla ya mimi na yeye kukutana na kumaliza kile tulichokuwa tayari tumekianza.
SASA ENDELEA...
“Inabidi ubaki usaidiane na hawa askari, bado kuna kazi kubwa mbele yetu. Nakukumbusha tu kwamba huonekani na mtu yeyote kwa hiyo utakuwa na nafasi ya kuyafanya hata yale ambayo watu wa kawaida hawayawezi, ni lazima Loris akamatwe, umepigwa risasi na Firyaal naye amepigwa risasi, haiwezekani iwe ni kwa ajili ya kazi bure,” alisema Junaitha, sauti ambayo ilipenya vilivyo masikioni mwangu, akawa ni kama amezidi kuniongezea hasira.
Wale askari walipoingia, wengine ilibidi wabaki nje, wakatawanyika kule ndani kwa tahadhari kubwa na muda mfupi baaddaye, mvua nyingine ya risasi ikaanza kumwagika.
Nilishindwa kuelewa ni kwa sababu gani nyumba hiyo ilikuwa ikilindwa kiasi hicho, nikasikia sauti ya Junaitha masikioni mwangu akinielekeza kusonga mbele haraka mpaka pale walipokuwepo walinzi wengine waliokuwa wakifyatua risasi kwa kasi.
Nilipiga hatua mbili tu, bila kuonekana na mtu nikawa tayari nimeshafika kwenye geti la pili ambalo nalo lilikuwa na vyumba viwili vya walinzi kama kule mwanzo lakini tofauti yao, hawa hawakuwa ghorofani, vyumba vyao vilikuwa vya chini.
Kwenye chumba cha kwanza kilichokuwa upande wa kusini, kulikuwana walinzi wawili ambao tofauti na wale wa nje, hawa walikuwa wamevalia sare maalum, kwa kasi ya ajabu nikawashika vichwa na kuwagonganisha kwa nguvu, wote wakadondoka chini kama mizigo.
Nikainama na kushika shingo ya wa kwanza, nikaigeuza kwa kasi, sauti ya mfupa ukiteguka ikasikika, nikamfuata na yule wa pili, naye nikafanya hivyohivyo! Nikasikia sauti ya Junaitha ikinipongeza na kunielekeza kuelekea upande wa pili ambapo bado risasi zilikuwa zikiendelea kumiminwa.
Nilipoingiatu, kwa mbali nilishuhudia askari wengine wawili wakipigwa risasi na kudondoka chini, kwa jazba nikamshika wa kwanza na kumrushia ukutani na bunduki yake, kwa kuwa alikuwa ameshika sehemu ya kufyatulia risasi ‘trigger’, risasi kadhaa zilimiminika kwenye kifua cha mwenzake, nikammalizia kwa kuvunja shingo yake, eneo lote likawa kimya.
Sikuwa mimi ambaye najijua, roho ya mauti ilikuwa imenijaa kiasi kwamba kupoteza uhai wa mtu niliona kuwa kitu chepesi mno. Mpaka muda huo nilikuwa nimeshawanyonga walinzi kadhaa lakini bado nilikuwa na hamu ya kuendelea kuua tena na tena.
Nikawaona askari wengine wakiburuza miili ya wenzao na kuisogeza pembeni huku wengine wakija kwa kasi kubwa. Kwa muda wote huo hakuna aliyekuwa anajua kwamba mimi ndiyo nilikuwa mstari wa mbele, nikiwasafishia njia, wakawa wanaendelea kukimbilia ndani huku wakifyatua risasi.
Wakafika kwenye geti la pili na kulivunja, wakaingia ndani. Wakati wao wanahangaika kufungua geti, mimi nilikimbia na kuingia mpaka ndani kabisa, nikapigwa na butwaa kwa jinsi jengo hilo lilivyokuwa limejengwa.
Japokuwa kwa nje lilikuwa linaonekana kama jengo la kawaida tu, ndani ilikuwa ni zaidi ya ngome. Kulikuwana nyumba karibu saba, tena zote za kifahari, zikiwa zimejengwa kwa mtindo wa kuzunguka na kutengeneza kama duara hivi, huku kila moja ikiwa imezungukwa na mandhari nzuri sana.
Upande wa Magharibi kulikuwa kama na godauni hivi likiwa limezungushiwa nyaya za umeme, huku mlangoni kukiwa na walinzi wawili wenye bunduki ambao nao waliposikia ile mvua ya risasi, walikaa mkao wa kujihami.
Kwa hesabu za harakaharaka, mle ndani kulikuwa na zaidi ya watu kumi na mbili na miongoni mwao, walikuwepo wanawake watatu ambao kwa kuwatazama tu walikuwa wakifanana sana na Firyaal na Shenaiza, kuanzia rangi ya ngozi zao na watoto wa kiume wawili ambao hata bila kuuliza niligundua kwamba walikuwa ni wadogo zao Firyaal na Shenaiza.
Lakini pia kulikuwa na wanaume wengine kama wanne hivi, wenye miili mikubwa wakiwa na bunduki mikononi, nadhani ndiyo walikuwa walinzi wa mwisho wa familia hiyo. Wakiwa katika hali ya taharuki, walishtukia askari wengi wakiwavamia, wakiwa na silaha na yule kiongozi akasikika akitoa amri kwamba wote wasalimu amri vinginevyo watawapiga risasi.
Kwa jinsi askari walivyokuwa wamefanikiwa kuingia mpaka ndani kabisa, wale walinzi walijikuta wakikosa cha kufanya zaidi ya kusalimu amri, wakainua mikono juu huku wakitupa bunduki zao, wale wanawake nikawaona wote wakiwakimbilia watoto wao na kuwakumbatia, wakajikunyata chini huku wakipiga kelele.
Kwa kuwa askari wote walikuwa na mafunzo ya kazi zao, hawakushughulika sana na wale wanawake na watoto, wakawaweka chini ya ulinzi wale walinzi wote waliokuwa wameinua mikono juu, wote wakafungwa pingu na kulazwa chini.
Bado nilikuwa na shauku ya kutaka kujua mle ndani ya lile godauni lililokuwa likilindwa vikali mlikuwa na nini? Wakati hayo yakiendelea, tulishtushwa ghafla na mlio mkali wa gari lililoonesha kwamba linaondoka kwa kasi kubwa.
Kwa kasi ya ajabu nilianza kukimbia kuelekea kule muungurumo huo ulikokuwa unatokea, baadhi ya askari nao wakafanya hivyo.
Kumbe ile ngome ilikuwa na mlango mwingine wa dharura upande wa nyuma ambako nako kulikuwa na walinzi kadhaa wenye silaha, nikamuona mwanaume mwenye asili ya kiasi, mweupe, mnene, mrefu na mwenye nywele zenye mvi kiasi, akiwa katikati ya mabaunsa wanne, kila mmoja akiwa na bunduki, wakiwa ndani ya gari dogo lakini la kifahari ambalo nyuma lilikuwa wazi, Jeep.
“Mungu wangu,” nilijisemea kwa sababu kwa kumtazama tu, nilijua lazima huyo ndiyo baba yao akina Firyaal na Shenaiza na hapo alikuwa akijaribu kutoroka. Tayari geti lilikuwa limefunguliwa na zilihitajika sekunde chache tu kwa ile kasi yao, wawe tayari wameshatoka nje, jambo ambalo sikuwa tayari kuona likitokea.
Kwa uwezo wa nguvu za kipekee nilizokuwa nazo, niliwahi getini bila kuonekana na mtu yeyote, ndani ya hizo sekunde chache tu na mimi nikalifunga lile geti haraka. Kwa kasi waliyokuwa nayo, dereva alikanyaga breki lakini gari liliserereka na kwenda kulibamiza geti, ukuta wa juu ukabomoka na tofali kubwa likadondokea mbele ya gari hilo, likatua kwenye kichwa cha dereva na kumpasua.
Ungeweza kufananisha kila kitu na movi ya kusisimua ya mapigano, tayari askari nao walishafika na kulizingira lile gari ambalo bado lilikuwa likiendelea kunguruma, huku damu nyingi zikimwagika kutoka kwenye kichwa cha dereva.
Kwa jinsi kila kitu kilivyotokea kwa kasi kubwa, hata wale walinzi wa Loris walishindwa cha kufanya, wakazitupa silaha zao na kujisalimisha, wakawekwa chini ya ulinzi na kufungwa pingu, wote wakalazwa chini isipokuwa Loris ambaye ilibidi askari wawili wenye miili mikubwa wamshike huku na kule, akiwa amefungwa pingu kwani naye hakuwa mtu wa mchezomchezo.
Japokuwa alionesha kuwa umri umeenda, lakini alikuwa na mwili mkubwa wa mazoezi, mikono yake ikiwa na misuli kuonesha kwamba siyo mtu ambaye unaweza kumdhibiti kwa urahisi.
Wale walinzi wengine walirudishwa na kwenda kuchanganywa na wale wenzao, Loris akapelekwa moja kwa moja kwenye gari la polisi chini ya ulinzi mkali, akakalishwa chini.
Kazi iliyokuwa imesalia, ilikuwa ni kuvunja lile godauni kuangalia ndani kulikuwa na nini? Nilikuwa na shauku kubwa ya kujua kilichokuwemo mle ndani kwani kwa jinsi nilivyosikia stori za mzee huyo na mazingira ya ile ngome yake aliyokuwa akiishi, achilia mbali ulinzi wa hali ya juu, ilionesha ana mambo mengi sana maovu.
Je, nini kitafuatia?
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 66
ILIPOISHIA:
Kazi iliyokuwa imesalia, ilikuwa ni kuvunja lile godauni kuangalia ndani kulikuwa na nini? Nilikuwa na shauku kubwa ya kujua kilichokuwemo mle ndani kwani kwa jinsi nilivyosikia stori za mzee huyo na mazingira ya ile ngome yake aliyokuwa akiishi, achilia mbali ulinzi wa hali ya juu, ilionesha ana mambo mengi sana maovu.
SASA ENDELEA...
Askari waliokuwa na silaha, walilizunguka godauni lote na wengine waliokuwa na vifaa maalum vya kuvunjia mageti, walisogelea geti hilo na kuseti mitambo yao, tayari kwa kazi. Kwa muda wote huo, yule mwandishi wa habari alikuwa bize kuhakikisha hakosi picha hata moja.
Alikuwa akichakarika kisawasawa, akawa anapiga picha za mnato na za video, kwa ajili ya kuwajuza wananchi juu ya kilichokuwa kinaendelea. Wakati askari hao wakijiandaa kuvunja godauni hilo, milio ya ving’ora vya magari mengi ya polisi vilisikika.
Kwa kuwa nilikuwa mwepesi, niliweza kupaa juu na kutazama upande wa kule barabarani, nikashtuka kuona magari mengi ya polisi, yakiwa naaskari wengi wenye silaha, yakija kwa kasi eneo lile. Nadhani awali Junaitha alipowapelekea taarifa juu ya oparesheni hiyo, walidhani ni tukio dogo tu lakini kilichotokea, kiliwafanya walipe tukio hilo uzito wa juu.
Binafsi hata sikuona umuhimu wa wao kufika muda huo kwa sababu tayari jeshi la mtu mmoja nilikuwa nimesafisha njia. Wale askari waliendelea na kazi yao na muda mfupi baadaye, walifanikiwa kuvunja geti hilo.
Katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea, milio ya risasi ilianza kusikika upya kutokea ndani ya lile godauni, ikabidi haraka sana niingie mstari wa mbele, nilipigwa na butwaa kwa nilichokikuta mle ndani.
Ilikuwa ni himaya nyingine inayojitegemea kabisa, mlangoni upande wa ndani kulikuwa na walinzi karibu saba, kila mmoja akiwa na bunduki mkononi. Pia kulikuwa na eneo maalum la mapokezi ambapo kulikuwa na wasichana kadhaa waliovalia magauni mekundu yenye mchanganyiko wa rangi nyeupe. Kila kitu kilionekana kuwa rasmi sana kwa sababu hata wale askari walikuwa na sare kabisa.
Baada ya eneo lile la mapokezi, kulikuwa na geti jingine na ofisi ndogondogo zilizokuwa na vifaa vya kisasa kabisa. Taa zote za ndani ya godauni hilo zilikuwa na mwanga mkali kiasi kwamba ukiwa ndani humo, isingekuwa rahisi kutambua kama ni mchana au usiku.
Kwa kasi kubwa niliingia na kuanza kuwaangusha wale walinzi, mmoja baada ya mwingine, nikawa nawavunja shingo kwa kasi kubwa, hali iliyowapa nguvu wale askari ya kusonga mbele, wakafanikiwa kuingia ndani lakini wale waliokuwa wa kwanza kuingia, walionesha kupigwa na mshangao kwa sababu hawakujuani nani aliyekuwa akiwasaidia kuwaangusha maadui zao, tena bila kuwa na majeraha yoyote ya risasi.
Wakafanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi wale wasichana wote na kuwatoa nje. Wakati wakiwatoa nje, wale wengine walikuwa wakihangaika kuvunja lile geti la ndani na hatimaye, walifanikiwa.
Nilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha nakuwa wa kwanza kuona kila kilichokuwa kikitokea. Nilishtushwa sana na nilichokiona, kwani kulikuwa na ngazi zilizokuwa zikielekea upande wa chini ya ardhi, ambako kulikuwa na jengo kubwa mithili ya hospitali, likiwa na vitanda zaidi ya mia moja, kila kimoja kikiwa na mgonjwa juu yake.
Kulikuwa pia na idadi kubwa ya watu waliokuwa wamevalia kama madaktari, waliokuwa wakiendelea na kazi lakini ghafla, kila mmoja aliacha baada ya kuona wakivamiwa na polisi.
Kumbe lile eneo lote ambali kwa juu lilikuwana nyumba na bustani nzuri, chini lilikuwa na handaki hilo kubwa, ambalo hata sikujua niliite hospitali au maabara. Upande wa kaskazini, kulikuwa na maandishi makubwa meusi yaliyokuwa yakisomeka ‘Black Heart’.
Ni hapo ndipo nilipopata picha halisi ya kile kilichokuwa kikiitwa Black Heart. Yale maelezo niliyoyapata kwamba shirika hilo ambalo kwa nje lilikuwa likijitangaza kwamba linasaidia maskini na watu wasiojiweza, kwenda kuwalipia gharama za masomo na matibabu nje ya nchi, kilikuwa kitu kingine tofauti kabisa.
Japokuwa nilishaambiwa kwamba lilikuwa likihusika na usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na viungo vya binadamu, nilikuwa siamini mpaka siku hiyo ambapo kwa macho yangu, nilishuhudia kila kitu. Katika kila kitanda, kulikuwa na mtu aliyelala ambapo wote walionesha kutokuwa na fahamu.
Walikuwepo wengine ambao tayari walikuwa wameshafanyiwa upasuaji wa kutolewa viungo mbalimbali vya miili yao, ambavyo vilihifadhiwa kitaalamu kwenye majokofu makubwa yaliyokuwa mwisho kabisa mwa jengo hilo refu.
Niliwaona askari waliokuwa wameshasambaa kila kona, wakipatwa na kigugumizi cha nini cha kufanya. Amri iliyotoka, ilikuwa ni kuwakamata madaktari wote na kuwatoa nje, huku mipango ya namna ya kuwanusuru wale watu ambao wote walikuwa kwenye usingizi wa kifo, wengine wakiwa wamefungwa mashine za kuwasaidia kupumua, ilianza kufanyika.
Lilikuwa ni tukio la kusisimua mno, nilimuona hata yule mwandishi wa habari tuliyeongozana naye, Richard Bukos akitetemeka kwa hofu. Jengo lote lilikuwa likinukia umauti.
“Inatakiwa usimamie hatua kwa hatua, usikubali mtu yeyote akatibua hii oparesheni, kuwa makini na hao wanaoingia sasa hivi,” alisema Junaitha, sauti ambayo ilisikika vizuri kwenye masikio yangu.
“Vipi huko hospitalini? Sitaki kufa tena wala sikati Firyaal apatwe na tatizo lolote,” nilimwambiaJunaitha ambaye alinitoa wasiwasi, akaniambia nifanye kazi yangu na yeye nimuachie afanye kazi yangu. Kumbuka kwamba kwa kipindi chote hiki, mimi kwa maana ya mwili wangu unaoonekana, na Firyaal, tulikuwa tumepelekwa Hospitali ya Muhimbili baada ya kupigwa risasi kwenye yale mashambulizi.
Nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kufika mwenyewe na kuona jinsi hali ilivyokuwa ikiendelea lakini sikuweza kwa sababu nilikuwa na jambo muhimu sana la kulisimamia kwa wakati huo. Kweli wale madaktari wote walitolewa chini ya ulinzi mkali na kwenda kuunganishwa na wale wenzao waliokamatwa awali.
Mle ndani kukabaki wale wagonjwa tu waliokuwa wamelala, wakiwa hawaelewi chochote kilichokuwa kinaendelea. Ilibidi na mimi nitoke nje kuangalia kilichokuwa kinaendelea, askariwalikuwa wameongezeka zaidi ya mara nne ya wale waliokuwepo awali, tena kila mmoja akiwa na silaha.
Miongoni mwao, nilimuona askari mwingine ambaye alikuwa na nyota nyingi kuliko yule wa kwanza tuliyekuja naye, nikahisi lazima atakuwa na cheo kikubwa zaidi ya yule wa mwanzo, nikawa makini kumfuatilia kila alichokuwa anakifanya.
Nilimsikia akitoa amri ya yule kamanda tuliyefika naye awali aende naye wakazungumze pembeni. Kwa kuwa sikuwa naonekana, na mimi nilisogea pembeni, nikamuona akimpigia saluti na kunifanya niamini kweli kwamba alikuwa na cheo cha juu zaidi yake.
“Nani aliyetoa amri ya kuja kuvamia hapa wakati uongozi wa juu haujui?” nilimsikia akimuuliza, nikapigwa na butwa mno kwani sikutegemea kama anaweza kumuuliza swali kama lile.
Je, nini kitafuatia?
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 67
ILIPOISHIA:
Kwa kuwa sikuwa naonekana, na mimi nilisogea pembeni, nikamuona akimpigia saluti na kunifanya niamini kweli kwamba alikuwa na cheo cha juu zaidi yake.
“Nani aliyetoa amri ya kuja kuvamia hapa wakati uongozi wa juu haujui?” nilimsikia akimuuliza, nikapigwa na butwaa mno kwani sikutegemea kama anaweza kumuuliza swali kama lile.
SASA ENDELEA...
“Mkuu, ni..ni.. ni..liletewa taarifa na msamaria mwema.”
“Lakini si unajua taratibu za kazi kwamba ni lazima uwajulishe viongozi wako kwanza?”
“Ilikuwa ni dharura mkuu, ni..wie radhi.”
“Nikuwie radhi nini? Utaeleza wewe juu ya askari waliopigwa riasi? Utaeleza wewe juu ya hawa watu ambao hatuna hata uhakika kama walikuwa na nia ovu au laa lakini mmewapiga risasi?”
“Mkuu, mbona kila kitu kipo wazi mkuu?”
“Kwa hiyo unabishana na mimi?”
“Hapana afande!”
“Sasa nakuagiza, rudisha vikosi vyako nyuma haraka iwezekanavyo, niachie hii kazi niifanye mwenyewe,” alisema kiongozi huyo na kupiga hatua ndefundefu kuelekea pale kwenye gari alilokuwa amepakizwa Loris, baba yao akina Firyaal na Shenaiza.
Kama nilivyosema tangu awali, kwa kuwa sikuwa naonekana, nilikuwana uwezo wa kujichanganya nakufuatilia jambo lolote ninalolitaka kwa kina bila mtu yeyote kuniona. Nilimfuatilia yule kiongozi mpaka alipolifikia gari ambalo Loris alikuwa ndani yake.
Nikamuona Loris akishtuka baada ya kumuona halafu akageuka huku na kule kutazama kama kuna mtu yeyote alikuwa akiwatazama, alipojiridhisha kwamba hakukuwa na mtu anayewafuatilia, nilimuona akitoa ishara fulani kumpa yule kiongozi wa juu wa polisi, naye akamfinyia jicho moja, nikamuona Loris akishusha pumzi ndefu na kutulia.
Kwa harakaharaka nilichokielewa, ni kama Loris alipomuona tu alitaka kumwambia ‘vipi mbona unaacha nadhalilika kiasi hiki? Nisaidie tafadhali’ kisha yule askari akamwambia ‘nimekuja kwa ajili ya kazi hiyo, usijali’. Ni hapo ndipo nilipoelewa kwa nini Junaitha aliniambia niwe makini sana na kundi hilo la pili la polisi lililofika eneo hilo.
Nikajiapiza kwamba nipo tayari kufanya jambo lolote kuona sheria inafuata mkondo wake. Yaani nipigwe risasi, Firyaal naye apigwe risasi, nikoswekoswe mara kadhaa kuuawa halafu leo nimefanikiwa kumpata mtu aliyekuwa nyuma ya matukio hayo, kisha mtu mwingine anakuja na kutaka kutibua kila kitu kirahisirahisi! Haiwezekani! Nilijisemea moyoni huku nikianza kumfuatilia hatua kwa hatua.
Kwa jinsi roho yangu ilivyokuwa imetawaliwa na harufu ya mauti, nilijiapiza kwamba endapo nitabaini yule askari anataka kumtorosha Loris, nipo tayari hata kumnyonga kwa kumvunja shingo kama nilivyofanya kwa wale mashetani wengine kwa sababu hakuwa na kinga yoyote mwilini mwake licha ya kwamba alikuwa akitembea na bunduki.
Jambo ambalo watu wengi hawalijui ni kwamba katika dunia ya sasa, ni lazima uwe na silaha maishani mwako kwa ajili ya kujilinda. Simaanishi bunduki au panga, namaanisha silaha kubwa zaidi ambazo kila mmoja anazifahamu ingawa wengine huwa wanazipuuza na kujikuta wakiishi maisha ambayo ni rahisi kukumbwa na jambo lolote baya.
Katika maisha, silaha ya kwanza ni kuwa na imani kwa Mungu wako, bila kujali unasali au kuabudu dini gani. Yaani kama wewe ni Mkristo, basi hakikisha unamuamini Mungu wako kwa asilimia 100, kama ni Muislam vilevile, hata kama huna dini lakini ilimradi unaamini Mungu yupo, basi ishimaisha yako kwa ukamilifu.
Wale watu ambao kwa nje anajifanya kuwa mlokole au ‘mswalihina’ lakini kumbe ndani yake anafanya vitendo vichafu kama zinaa, wizi, kula rushwa, dhuluma na mambo mengine machafu, wakiamini kwamba hakuna anayewaona, wanakuwa wanajidanganya wenyewe kwa sababu mwisho wa siku, wanaishi katika maisha ambayo hawana kitu chochote kinachowakinga au kuwalinda maishani.
Kinga nyingine ambayo ndiyo watu wengi wanaipa nguvu kubwa zaidi siku hizi, ni pesa. Ukiwa na pesa, ni ulinzi tosha ingawa katika ngazi za ubinadamu na kujitambua, pesa si chochote zaidi ya mabadilishano tu, lakini kidunia, mtu mwenye pesa anakuwa salama zaidi kwenye baadhi ya mambo, hasa yale ambayo yanahusu mwili na siyo roho.
Yote tisa, kumi ni ulinzi wa nguvu za ndani, ambao katika ngazi za ubinadamu ndiyo unatajwa kuwa ulinzi wa daraja la kwanza kabisa. Hapa kuna matabaka, kuna wengine wanashindwa kuzielewa vizuri nguvu zao za ndani na matokeo yake, wanazihamishia nguvu hizo kwenye vitu kama hirizi, sanamu au uchawi. Wanaamini vitu hivyo kwamba vinawapa ulinzi na kwa kuwa wameweka imani yao hapo, ni kweli vinawapa ulinzi.
Wanaojitambua ambao ndiyo daraja la juu kabisa la ubinadamu, ni wale ambao wanazitumia nguvu zao kujilinda na kuamua nini kitokee kwa wakati gani na kwa namna gani. Haya yote nilikuwa nimefundishwa na Junaitha na nashukuru kwamba ndani ya muda mfupi tu tayari na mimi nilikuwa nimeshaelewa kwa kiasi kikubwa.
Basiniliendelea kumfuatilia yule kiongozi wa polisi, nikamuona akigeuka na kumpa mgongo Loris, akawa anapiga hatua za harakaharaka kuelekea kule kwenye lile godauni tulikokuta watu wengi wakiwa hawana fahamu, wengine wakiwa wameshafanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatoa viungo muhimu kwenye miili yao.
Pale mlangoni bado palikuwa na askari kadhaa, nikamuona akitoa amri kwamba wote waondoke eneo hilo, yule mwingine ambaye naye alikuwa kiongozi mwenye nyota kadhaa begani lakini akionekana kuwa chini kicheo kuliko yule wa mwisho, ambao wote hata sikupata nafasi ya kuyajua majina yao, aliendelea kutoa amri, kwa mdomo na kwa simu za upepo, akiwaamuru vijana wake kurudi nyuma.
Nikamuona kila mtu akishangazwa na amri hiyo lakini kama unavyojua tena, jeshini huwa ni amri tu kwa hiyo mahali popote ukiamrishwa kitu hutakiwi kuhoji. Kwa macho yangu, nilishuhudia hata wale askari waliokuwa wameingia kule chini kwenye lile godauni kubwa, nao wakitolewa kisha geti likafungwa upande mmoja.
Nikajua kama nisipofanya jambo, kweliwanaweza kufanya njama zao na kuhujumu oparesheni ile kubwa tuliyoifanya. Jambo la kwanza nililoona linaweza kuwa msaada mkubwa, ilikuwa ni kwenda kumnyamazisha yule kiongozi wao ingawa sikujua nitamnyamazishaje.
“Katumie mikono yake mwenyewe kumkaba shingoni mpaka apoteze fahamu,” alisema Junaitha, sauti yake ikapenya vizuri kwenye masikio yangu. Kauli hiyo ilinikumbusha tukio la Firyaal kujikaba shingoni kwa nguvu zake zote mpaka kutaka kujitoa roho tukiwa nyumbani kwa Junaitha. Bado sikuelewa nini kinachofanyika.
Hata hivyo, ilibidi tu niende mpaka pale yulekiongozi alipokuwa amesimama, akiwa bize kutoa amri kwa watu waliokuwa chini yake, kwa kasi ya kimbunga nikamshika mkono aliokuwa na radio call, nikautingisha mpaka ikadondoka. Kwa muda wote huo, sauti ya Junaitha ndiyo ilikuwa ikinielekeza nini cha kufanya.
Wakati ukweli ni kwamba mimi ndiyo nilikuwa namtingisha kwa nguvu, kwa kuwa sikuwa naonekana, watu waliokuwa wakimtazama kiongozi huyo wa polisi, waliona kama anatetemeka mikono, kila mmoja akapigwa na butwaa, akiwa haelewi nini kinachoendelea.
Sikuishia hapo, kwa kasi kubwa nilichukua mikono yake na kuipeleka kwenye shingo yake kisha nikafanya kama namkaba hivi, nikamuachia, nikashangaa kumuona akiendelea kujikaba mwenyewe kwa nguvu.
Ndani ya sekunde chache tu, alidondoka chini kama mzigo, mikono bado ikiwa shingoni, macho yakamtoka kama mjusi aliyebanwa na mlango, ulimi wote ukatoka nje na kusababisha kizaazaa kikubwa. Harakaharaka wale askariwaliokuwa chini yake walimkimbilia na kumzunguka, wakawa wanajaribu kumsaidia lakini haikuwa kazi nyepesi, aliendelea kujikaba mpaka akapoteza fahamu.
Kwa mbali vikaanza kusikika ving’ora vya magari mengine yakija kwa kasi eneo lile, sikuelewa ni nani tena aliyekuwa anakuja, nikawana shauku kubwa ya kutaka kuona ni nani maana tayari kengele ya hatari ilishalia ndani ya kichwa changu.
Je, nini kitafuatia?
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 68
ILIPOISHIA:
Harakaharaka wale askari waliokuwa chini yake walimkimbilia na kumzunguka, wakawa wanajaribu kumsaidia lakini haikuwa kazi nyepesi, aliendelea kujikaba mpaka akapoteza fahamu.
Kwa mbali vikaanza kusikika ving’ora vya magari mengine yakija kwa kasi eneo lile, sikuelewa ni nani tena aliyekuwa anakuja, nikawa na shauku kubwa ya kutaka kuona ni nani maana tayari kengele ya hatari ilishalia ndani ya kichwa changu.
SASA ENDELEA...
“Mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani amekuja!” nilimsikia mmoja kati ya wale askari akimwambia mwenzake. Moyoni nilifurahi sana kwa sababu kwa jinsi nilivyokuwa namjua waziri huyo alivyo mkali kwenye kazi, niliamini lazima atasimamia ukweli.
Wale askari wengine waliendelea kuhangaika na yule kiongozi wao, wakampakiza kwenye garila polisi na kuondoka kwa kasi eneo hilo, kila mmoja akiwa haelewi ni nini hasa kilichotokea.
Gari lililombeba lilipishana mlangoni na msafara wa mheshimiwa waziri ambaye alikuwa akiingia eneo hilo. Muda mfupi baadaye, tayari alikuwa ameshashuka kwenye gari lake, walinzi wake waliokuwa kwenye magari yaliyokuwa kwenye msafara huo, wakateremka harakana kuhakikisha kiongozi huyo yupo salama.
Alimuita kiongozi wa oparesheni na kwa sababu yule ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi alikuwa amepata matatizo, ilibidi aende yule kamanda ambaye ndiye tuliyetoka naye kituoni, nikamuona akimpigia saluti na kusalimiana naye.
Nilijisogeza karibu, nikamsikia mheshimiwa waziri akiuliza nini kilichotokea ambapo yule kamanda alianza kueleza kila kitu, kuanzia mwanzo alipopokea taarifa kutoka kwa Junaitha, tulivyoongozana mpaka eneo hilo na jinsi tulivyoshambuliwa vikali kabla ya baadaye kufanikiwa kuwadhibiti wahalifu wale.
Alieleza na jinsi kiongozi wake alivyokuja kumuingiliakwenye kazi yake na kutaka kukwamisha kila kitu, mheshimiwa waziri akaonesha kushtushwa mno, akataka ufafanuzi zaidi lakini hakuna aliyeweza kumfafanulia kwa sababu mhusika tayari alikuwa ameshapoteza fahamu.
Alichoagiza ni kwamba Loris na watu wake wote watolewe haraka eneo hilo na kupelekwa kituo kikuu cha polisi na timu ya madaktari na askari wenye silaha waungane pamoja kuangalia namna ya kuwasaidia watu wale na kujua nini kilichowasibu. Aliagiza pia kwamba eneo hilo lilindwe kwa muda wote mpaka atakapoagiza vinginevyo. Ilibidi na yeye aombe kutembezwa kwenye maeneo mbalimbali ya ngome hiyo.
Alipomaliza kufanya ziara hiyo, alishindwa kuyazuia machozi, akawa analia kama mtoto mdogo. Yulemwandishi wa habari naye aliendelea na kazi ya kumpiga picha za kutosha. Aliguswa mno na alichokiona kule chini kwenye handaki, akashindwa kuelewa kwa nini ukatili mkubwa namna hiyo ulikuwa ukitokea kwenye nchi ambayo kila mmoja anajua kwamba ni kisiwa cha amani.
Huku akiwa anaendelea kutokwa na machozi, mheshimiwa waziri aliondoka eneo hilo huku akiwaonya watu aliowaacha eneo hilo, kuanzia yule kiongozi wa polisi na wenzake wote kwamba yeyote atakayethubutu kutaka kuleta ‘figisu’ za aina yoyote, hatamvumilia.
Baada ya nafsi yangu kuridhika kwamba sasa kila kitu kilikuwa kwenye mikono salama, niliona huo ndiyo muda muafaka wa mimi kurudi kwenye mwili wangu ambao bado ulikuwa hospitali. Nikafumbamacho na kusema kile nilichokuwa nakitaka, nikajihisi nikivutwana kitukama kimbunga kikali.
Nilipokuja kushtuka, tayari nilikuwa ndani ya wodi ambayo ilikuwa na madaktari wanne na manesi wawili, wakihangaika kumtibu mgonjwa aliyekuwa amelala kwenye kitanda, mdomoni akiwa amefungwa mashine maalum ya kumsaidia kupumua.
Hakuwa mwingine bali mimi, niliwaona madaktari wakihangaika kunitoa risasi ambayo ilikuwa imenipiga upande wa kulia wa kifua changu. Kwa kuwa hii haikuwamara ya kwanza kutokewa na hali hiyo ambayo baadaye nilikuja kujua kwamba inaitwa Out of Body Experience au O.B.E., sikushtuka sana.
Nifafanue kidogo kuhusu hali hii kama utakuwa umesahau nilichoeleza mara ya kwanza. Ni hivi, kila mtu unayemuona akiishi duniani, ana miili ya aina mbili, kuna huu mwili unaoonekana na kuna mwili usioonekana ambao wengine huuita aura.
Hata wale wachawi wanaoweza kupenya kwenye ukuta na kuingia ndani ya nyumba bila kipingamizi chochote, huwa wanatumia mwili usioonekana. Yapo mazoezi maalum ambayo mtu akiyafanya kwa muda mrefu na akafuzu, anaweza kuutenganisha mwili unaoonekana na ule usioonekana, wengine wanaitwa wachawi lakini ukweli ni kwamba kinachofanyika siyo uchawi wa moja kwa moja, bali ni sayansi ya giza.
Zoezi ambalo hutumika zaidi na watu wengi dunia nzima, huwa ni tahajudi (meditation) lakini lazima mtu awe ameshaiva vya kutosha.
Inawezekana kabisa ukaingia ndani ya chumba kilichotulia, ukafanya tahajudi na kwa mfano kama unataka uone kinachoendelea Mbeya na wewe upo Dar es Salaam, ukituliza akili yako mpaka kiwango cha mwisho kabisa, utaweza kusafiri kwa mwili usioonekana, kwa kasi kama ya mwanga au sauti, ukafika eneo unalotaka kuwepo, na ukashuhudia kila kitu kinachoendelea kwa muda unaotaka.
Ukiwa nje ya mwili wako, huu mwili wako unaoonekana, hubaki kama gogo, kwamba hata mtu aje autingishe namna gani, huwezi kuzinduka mpaka ulemwili usioonekana utakaporejea. Ni suala ambalo kwa maelezo ya mdomo linaweza kuonekana gumu na la kushangaza au lisilowezekana lakini kwa wanaojua, watakubaliana na mimi kwamba kila kitu kinawezekana na hata unaposikia watu wakisema hakuna kinachoshindikana chini ya jua, huwa wanamaanisha matukio kama haya.
Basi niliendelea kuwatazama wale madaktari walivyokuwa wananihangaikia, nikasikia sauti ya Junaitha ikiniambia kwamba kama nataka kurudiwa na fahamu zangu haraka na kupona, ni lazima nikubali kurudi kwenye mwili wangu unaoonekana, akaniambia kwamba nitasikia maumivu makali lakini yatakaa kwa muda na baadaye yatapotea.
“Vipi kuhusu Firyaal?”
“Shughulikia uhai wako kwanza, mengine yatafuata,” alisema Junaitha, kauli ambayo kiukweli sikuielewa. Hata hivyo, sikutakakubishana naye, nikaamua kufanya kile alichoniambia.
Nikajisogeza katikati ya wale madaktari na kulala juu ya mwili unaoonekana, kwa namna ambayo nilifanana kwa kila kitu, nikafumba macho na kunuia ndani ya moyo wangu kwamba nataka kurudi kwenye mwili wangu.
Kufumba na kufumbua, nilihisi kama giza nene likiuzingira uso wangu, kwa mbali nikaanza kuhisi maumivu makali upande wa kulia wa kifua changu ambapo kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele ndivyo yalivyokuwa yakizidi kuongezeka. Visu na mikasi vya madaktari walivyokuwa wakitumia, wakihangaika kutoa ile risasi, nilivisikia ‘moja kwa moja’.
Nikiri kwamba sijawahi kusikiamaumivu makali kiasi hicho, basi nikawa nahangaika kupambana na lile giza lililokuwa limenizingira kwenye uso wangu, kiasi cha kushindwa kuelewa kilichokuwa kikiendelea kwenye ulimwengu wa kawaida. Nikiwa kwenye haki hiyo, nilisikia kitu kama chuma kikidondokea kwenye karai la kidaktari, kisha madaktari wote wakawa wanapongezana kwa kazi waliyoifanya.
Nilizidi kujikakamua na katika hali ambayo sikutegemea, nilifumbua macho yangu na kujikuta tayari nimesharudi kwenye mwili wangu wa asili, nikawasikia madaktari wakiambizana: “Amerejewa na fahamu zake! Ana roho ngumu sana huyu!” wakawa wanahangaika kuzuia damu zisiendelee kuvuja kwenye lile jeraha langu.
“Inabidi aendelee kupumzika, lete dawa ya usingizi,” alisema daktari mmoja na muda mfupi baadaye, nesi mmoja alinidunga sindano na uso wangu ukaanza kuwa mzito tena, nikapitiwana usingizi mzito.
Je, nini kitafuatia?
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 69
ILIPOISHIA:
“Amerejewa na fahamu zake! Ana roho ngumu sana huyu!” wakawa wanahangaika kuzuia damu zisiendelee kuvuja kwenye lile jeraha langu.
“Inabidi aendelee kupumzika, lete dawa ya usingizi,” alisema daktari mmoja na muda mfupi baadaye, nesi mmoja alinidunga sindano na uso wangu ukaanza kuwa mzito tena, nikapitiwa na usingizi mzito.
SASA ENDELEA...
Sikuelewa tena ikilichoendelea, siyo katika ulimwengu wa kawaida wala ulimwengu wa nguvu za kipekee, kwa kifupi nililala usingizi halisi. Nilipokuja kuzinduka baadaye, nilijikuta nikiwa kwenye wodi nyingine tofauti na ile ya awali, niligeuka huku nakule, maumivu makali ya pale kifuani yakawa yananirudisha kitandani.
Niligundua kwamba nilikuwa kwenye wodi ya kawaida ya wanaume lakini mle ndani hakukuwa na mgonjwa mwingine zaidi yangu. Muda mfupi baadaye, nikiwa bado nashangaashangaa, nilisikia mlango wa wodi ukifunguliwa, mwanaume mmoja aliyekuwa amevaa koti la kidaktari, akiwa ameshika faili aliingia akiwa ameongozana na wanaume wengine wanne.
Wakaja mpaka pale kwenyekitanda changu na kunizunguka, daktari akawa ananiuliza maendeleo yangu, nikamjibu kwa taabu kwamba naendelea vizuri. Midomo yangu ilikuwa mizito sana nadhani kwa sababu ya zile dawa za usingizi nilizochomwa.
“Halafu sura yako siyo ngeni machoni mwangu, hujawahi kulazwa hapa wewe?” aliniuliza yule daktari akiwa ni kama ameshtuka jambo fulani. Mapigo ya moyo yalinilipuka na kuanza kunienda mbio kwa sababu nilikuwa najua vizuri kwamba mara ya mwisho kuondoka hospitalini hapo, tuliondoka kimafia kwa kutoroka usiku tukiwa na Shenaiza ambaye alikuwa hajitambui.
“Ndiyo, nimewahi kulazwa tena siku siyo nyingi,” nilimjibu huku nikijaribu kukwepesha uso wangu lakini tayari nilikuwa nimechelewa, alishanikumbuka.
“Si unaitwa Jamal? Ulilazwa kule kwenye wodi za private?” aliniuliza, nikatingisha kichwa kumkubalia, nikamuona akiwavuta wale wenzake pembeni wakaanza kujadiliana jambo ambalo sikulielewa.
“Huna haja ya kuogopa chochote, kwanza unao uwezo mkubwa ambao hata ukiamua kupotea hapohapo kitandani unaweza, unaogopa nini sasa?” sauti ya Junaitha ilisikika masikionimwangu, nikajikuta nikitabasamu, ile hofu niliyokuwa nayo iliyeyuka kama barafu ndani ya moyo wangu.
Baada ya majadiliano ya dakika kadhaa, niliwaona yule daktari na wenzake wakitoka mle wodini bila kusema chochote, wakaniacha nimelala pale kitandani kwangu, bado nilikuwa nikiendelea kutabasamu kwa sababu sasa maisha yalikuwa yamebadilika sana kwa upande wangu kiasi kwamba hakukuwa tena na kitu cha kuhofia.
Nilijivuta kidogo na kuinuka, nikaegamia mabomba ya kitanda na kuanza kujitazama pale kifuanikwangu. Nilikuwa nimefungwa bandeji upande wa kulia wa kifua changu lakini halikuwa jeraha kubwa kama lile ambalo sasa lilishapona la upande wa kushoto.
Nilipokumbuka kwamba Junaitha anazo dawa za kuweza kunisaidia kupona ndani ya muda mfupi, wala sikuwa na wasiwasi kabisa ndani ya moyo wangu. Swali kubwa ambalo lilibaki ndani ya moyo wangu, ilikuwa ni hali ya Firyaal.
Nilitamani japo kusikia hali yake inaendeleaje lakinihakukuwa na wa kunipa majibu. Ikumbukwe kwamba mpaka muda huo hakuna mtu yeyote aliyekuwa amekuja kunijulia hali pale wodini nilipokuwa nimelazwa, jambo lililozidi kunipa maswali mengi ndani ya kichwa changu.
Niliendelea kutafakari mambo mbalimbali yaliyotokea mpaka muda huo, moyoni nikawa najiona kama shujaa kwa sababu kwa mambo niliyopitia, kama angekuwa ni mtu mwingine huenda tayari angeshakuwa marehemu lakini kwangu haikuwa hivyo.
Dakika kadhaa baadaye, nilisikia mlango ukifunguliwa tena, nikamuona yule daktari akiingia tena lakini safari hii alikuwa ameongozana na maafisa kadhaa wa jeshi la polisi, ambapo mmoja kati yao niliweza kumtambua vizuri, alikuwa niyule kamanda mwenye nyota kadhaa begani tuliyekuwa naye eneo la tukio wakati wa kuvamia kambi ya Loris.
“Aah! Kumbe kijana mwenyewe ndiyo huyu,” alisema mmoja kati yao, yule kamanda mwenye nyota nyingi akawa anatingisha kichwa kama ishara ya kumjibu kwamba ‘ndiye mwenyewe’. Wakasogea mpaka pale kwenye kitanda changu, yule kamanda akaniinamia na kunipa mkono wa pole ulioambatana na pongezi nyingi.
“Tunatambua kwamba wakati ukihangaika kukamilisha kazi yako kuna makosa mengine madogomadogo uliyafanya lakini usiwe na wasiwasi wewe na watu wako, tutawasimamia na kuhakikisha mnapata kile mlichostahili kwa kazi nzuri mliyoifanya,” alisema, kauli ambayo ilinipa nguvu za ajabu.
Nikamshukuru sana lakini bado nilikuwana swali moja kuhusu Firyaal pamoja na wale askari wengine waliopigwa risasi eneo la tukio. Nilipomuuliza swali hilo, naye alinikwepa na kukataa kabisa kunijibu chochote, akaniambia sanasana natakiwa kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyoniokoa mpaka muda huo, akarudia kunipongeza kwa ukakamavu mkubwa niliouonesha na akaniambia kwamba kuna salamu zangu kutoka ikulu, nitakaporuhusiwa kutoka hospitalini nitazipata.
“Huyu ni Inspekta Ismail Lauden, ndiye atakayesimamia suala la ulinzi wako na watu wako mpaka hapo mambo yatakapotulia,” alisema yule kamanda huku akinikabidhi kwa askari mwingine mwenye mwili mkubwa wa mazoezi, akatabasamu na kuinama kidogo kama ishara ya kuonesha heshima kwangu.
Aliniambia kwamba kuanzia muda huo, watu wangu wa karibu waliruhusiwa rasmi kuja kuniona kwa hiyo nisiwe na wasiwasi,” alisema, kauli ambayo iliniacha namaswali mengi, nikajiuliza ina maana kumbe watu walikuwa wamezuiwa kuja kuniona?
Nikapata majibu kwamba kumbe ndiyo maana tangu nifikishwe hospitalini hapo hakuna mtu yeyote aliyekuja kuniona zaidi ya Junaitha ambaye naye tulikuwa tukiwasiliana katika ulimwengu wa nguvu pekee.
Aliniaga na kuniambia kwamba ataendelea kuja mara kwa mara kunijulia hali, akamwambia na yule daktari kwamba wahakikishe napewa huduma za kiwango cha juu, moyoni nikamshukuru sana Mungu kwani nilijua hata lile suala la nesi Shenaiza kututorosha hospitalini hapo litamalizwa vizuri.
Alipotoka na watu aliokuwa ameongozana nao, mtu wa kwanza kuingia wodini alikuwa ni Raya ambaye alikimbia mpaka pale kitandani kwangu, akapiga magoti na kunikumbatia kwa tahadhari ili asije akanitonesha kidonda changu.
“Pole sana mume wangu, jamani Mungu mkubwa, nilijua nimeshakukosa,” alisema huku machozi mengi yakimtoka na kuulowanisha uso wake, nikawa na kazi ya kumtuliza ambapo aliinuka pale chini na kukaa pembeni ya kitanda changu.
Akaniambia kwa muda wote huo walikuwa wamezuiwa kabisa kuingia kwenye wodi niliyokuwa nimelazwa, nikajuanilichokiwaza kumbe kilikuwa kweli. Nilimuuliza kuhusu Firyaal lakini badala ya kunijibu, alianza kuangua kilio kwa nguvu, nikajua lazima kuna tatizo kubwa limetokea.
Akiwa anaendelea kuangua kilio, nilisikia mlango ukifunguliwa, nikamuona Shenaiza na Shamila nao wakiingia, nyuso zao zikionesha kabisa kwamba kulikuwa na tatizo kubwa limetokea. Nao walinikimbilia mpaka pale kitandani, wakanikumbatia huku nao wakiangua kilio kwa nguvu, wakawa wanamshukuru Mungu eti kwa kuninusuru kutoka kwenye mdomo wa mauti. Bado swali langu lilikuwa palepale, Firyaal yuko wapi? Hakuna aliyekuwa na majibu, wote wakawa wanalia kwa sauti za juu, nikashindwa kabisa kuelewa kilichokuwa kikiendelea.
Wakati wote wakiendelea kulia, nilisikia mlango ukifunguliwa tena, nikamuona Junaitha akiingia lakini tofauti na wengine, yeye uso wake ulikuwa mkavu kabisa, akatembea harakaharaka mpaka pale nilipokuwa nimelala, akanitazama usoni, na mimi nikamtazama, tukawa tunatazamana huku nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia ataniambia nini.
Je, nini kitafuatia?
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 70
ILIPOISHIA:
Wakati wote wakiendelea kulia, nilisikia mlango ukifunguliwa tena, nikamuona Junaitha akiingia lakini tofauti na wengine, yeye uso wake ulikuwa mkavu kabisa, akatembea harakaharaka mpaka pale nilipokuwa nimelala, akanitazama usoni, na mimi nikamtazama, tukawa tunatazamana huku nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia ataniambia nini.
SASA ENDELEA...
“Najua unataka kujua kuhusu Firyaal!” alisema na kabla sijamjibu chochote, akaniambia kwamba kulikuwa na habari mbaya kwa sababu inaonekana maisha yake yanashikiliwa na uzi mwembamba sana unaotenganisha kati ya uhai na kifo. Kwa maelezo yale, nilielewa kwamba anamaanisha kwamba tayari Firyaal alishatoka kwenye ulimwengu wa kawaida, hakuwa na uhai tena.
“Tunaweza kumuokoa kutoka kwenye mdomo wa mauti lakini itatugharimu kukaa siku saba kuzimu,” alisema Junaitha, kauli ambayo ilitufanya wote ndani ya wodi ile tubaki tukimshangaa.
“Inabidi kwanza tuhakikishe wewe umerejewa na nguvu zako kwa sababu unahitajika sana kwenye kazi ya kukata minyororo ya kuzimu ambayo tayari Firyaal ameshafungwa. Nilishusha pumzi ndefu na kutulia pale kitandani.
Akaanza kutupa maelekezo kwamba, nikisharejewa na nguvu zangu, tutaomba ruhusa ya kutoka hospitalini hapo kwa sababu za kiusalama, kisha tutaomba kuondoka na Firyaal kwa ajili ya taratibu nyingine.
“Kuna kitu sijaelewa.”
“Hujaelewa nini?”
“Umesema itatulazimu kukaa siku saba kuzimu?”
“Utaelewa tu,” alijibu Junaitha huku akigeuka na kutoka, akatutaka wote tutulie pale wodini na kama akina Shamila wakitolewa, basi wasiende mbali na mlango wa kuingilia kwenye ile wodi niliyokuwa nimelazwa kwa sababu za kiusalama.
Sikukaa muda mrefu sana, Junaitha alirudi na kunisogelea pale kwenje jeraha langu, akalishika kwa kulikandamiza huku akiongea maneno ambayo hakuna aliyeyaelewa, kisha akato kichupa kilichokuwa na ungaunga fulani, akafungua bandeji upande mmoja na kunyunyizia ule unga kwenye jeraha lango.
Hapohapo nikaanza kuhisi kama moto mkali unawaka kifuani na kadiri ulivyokuwa unaongezeka, maumivu nayo yalikuwa yakipungua na mwili wangu ukaanza kurejewa na nguvu zake.
“Nashughulikia usafiri, kaeni tayari,” alisema kisha akatoka tena, wote wakawa wananitazama kwa makini usoni kuona hali yangu inaendeleaje, kwa mbali nikaanza kutoa tabasamu hafifu lililoamsha matumaini mapya kwenye moyo wa kila mmoja.
Baadaye, Junaitha alirudi tena, safari hii akiwa ameongozana na manesi ambao waliniandaa vizuri, tayari kwa kuondoka. Wakanisaidia kuninyanyua pale kitandani, na kunitoa mpaka kwenye maegesho ya magari, wote tukaingia ndani ya gari na kushtuka kugundua kwamba mwili wa Firyaal pia ulikuwa ndani ya lile gari, akionesha kutokuwa na uhai kabisa.
Akawasha gari na kutusisitiza kwamba hatutakiwi kumgusa Firyaal wala kuzungumza chochote kumhusu mpaka atakapotuambia, akabadili gia na kukanyaga mafuta, gari likawa linaondoka, tukaenda mpaka kwenye geti la kutokea ambapo alizungumza na wale walinzi, wakamfungulia geti.
Tukatoka ambapo alizidi kukanyaga mafuta, gari likawa linakimbia kwa kasi kubwa.
Tuliendelea na safari huku wote tukiwa kimya kabisa ndani ya gari, kila mtu akiwaza lake lakini kubwa tukifikiria hatma ya Firyaal. Safari iliendelea na hatimaye tulifika nyumbani kwa Junaitha, akaingiza gari mpaka ndani ya geti, wote tukashuka huku tukionesha dhahiri kuchoka.
Mimi ndiyo nilionekana kuchoka zaidi kwa sababu bado mwili wangu haukuwa na nguvu kutokana na kupoteza damu nyingi kwenye lile tukio la kupigwa risasi, sambamba na maumivu ambayo yalikuwa yakizidi kupungua kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Shamila na Raya walisaidiana kunishika huku na kule kama ilivyokuwa kule mwanzo, tukaingia ndani na kwenda moja kwa moja kukaa sebuleni. Shenaiza na Junaitha wao walisaidiana kumbeba Firyaal na kumpitisha moja kwa moja mpaka kwenye kile chumba ambacho ndiyo huwa tunafanyia shughuli mbalimbali pale ndani.
Muda mfupi baadaye, Shenaiza alirudi na kujumuika na sisi pale sebuleni, akaenda kuwasha runinga na kwenda kutoa chupa ya maji ya kunywa kwenye friji, akanimiminia kwenye glasi na kuniletea, wote watatu wakakaa pembeni yangu.
Junaitha yeye aliendelea kubaki kwenye kila chumba akiwa na Firyaal, hatukujua anafanya nini kwa sababu yeye ndiye aliyetoa maagizo kwamba sote tubaki sebuleni. Bado ukimya ulikuwa umetawala nyumba nzima, sauti pekee iliyokuwa inasikika ilikuwa ni ya TV tu ambayo hata hivyo hakuna aliyekuwa akiitazama.
Kila mmoja alikuwa akiwaza lake lakini ghafla tulishtushwa na kiashirio cha ‘breaking news’ kwenye runinga, wote tukainua vichwa vyetu na kuanza kuitazama runinga hiyo kubwa na ya kisasa, iliyokuwa imebandikwa ukutani.
“Mungu wangu,” nilisema baada ya kushuhudia picha zetu tukiwa pale hospitalini zikioneshwa, zikifuatiwa na maelezo kwamba sisi ndiyo tulikuwa mashujaa wa lile sakata ambalo sasa lilikuwa limebatizwa jina jipya la Kurasini Scandal, likiwa na maana ya skendo ya Kurasini.
Mtangazaji aliwaambia watazamani kwamba hatimaye walikuwa wamefanikiwa kupata picha za watu ambao ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kufichua uovu mikubwa uliokuwa ukifanywa na mfanyabiashara mkubwa mwenye asili ya Uturuki, Loris kwa kivuli cha Shirika la Black Heart.
Alitumwagia sifa kedekede kisha baada ya hapo, alisema kwamba mheshimiwa rais alikuwa na maneno ya kuzungumza na wananchi wake ana kwa ana muda huo, ukapigwa wimbo wa taifa kisha mheshimiwa rais akaonekana, akiwa amesimama kwenye viunga vya hospitali alianza kuzungumza na wananchi moja kwa moja kupitia runinga.
Alianza kwa kueleza kuhusu mtikisiko mkubwa uliolikumba taifa baada ya kugundulika kwa kile mwenyewe alichokiita machinjio ya binadamu eneo la Kurasini, akafafanua kwamba mtu aitwaye Loris, ambaye serikali ilimuamini na kumpa kibali cha kuendesha Shirika la Black Heart, ambalo alilisajili kama shirika la kusaidia jamii, alivyogundulika kwamba anafanya biashara nyingine haramu na hatari mno kwa maisha ya wananchi.
Alieleza kila kitu, akasema wamegundua kwamba kumbe Black Heart, kazi yake ilikuwa ni kuwasafirisha watu kwenda nje ya nchi ambako wengi wao walikuwa wakienda kuuawa kisha kutolewa viungo muhimu kwenye miili yao, huku wengine wakiuawa hapahapa nchini na viungo vyao kwenda kuuzwa nje ya nchi.
Alionesha kusikitishwa mno na kugundulika kwa sakata hilo ikiwa ni muda mrefu umepita tangu kuundwa kwa shirika hilo, jambo ambalo lilimaanisha kwamba wananchi wengi tayari walishatolewa sadaka kwa sababu ya dhiki zao.
“Najua ni watu wengi ambao walienda kuonana na Loris kwa lengo la kuomba misaada, iwe ni kwenda kusomeshwa nje ya nchi, kufadhiliwa matibabu nje ya nchi au kutafutiwa kazi lakini wakaishia kutolewa kafara,” alisema mheshimiwa rais na alipofika eneo hilo, alishindwa kuzuia machozi yasimtoke, akavua miwani yake na kutoa kitambaa, akajifuta machozi na kuendelea kuzungumza.
Mwisho alitutaja majina, akianza na Junaitha, akaja mimi, Raya na Shamila huku akiwataja Shenaiza na Firyaal kwa utambulisho wa juujuu, nadhani alifanya hivyo kwa sababu za kiusalama, akasema anahitaji kuonana na sisi ikulu na kutoa maagizo tutafutwe mahali popote tulipo ili akatupongeze kwa kazi nzuri tuliyoifanya.
Alieleza kwa kirefu jinsi tulivyofanikisha suala hilo na vikwazo ambavyo tulikumbana navyo, akasema kwamba anajua tulipingwa sana lakini kwa sababu ya ushujaa wetu, tumefanikisha kufichuka kwa sakata hilo kubwa. Akatupa pole kwa yote na kutupongeza sana.
Alipofikia hapo, picha zetu zilirushwa tena runingani tukiwa tunatoka hospitalini kisha wimbo wa taifa ukapigwa tena na huo ukawa mwisho wa habari hiyo. Kwa muda wote huo tulikuwa kimya kabisa, tukiwa ni kama hatuamini tulichokuwa tunakiona.
Kwangu mimi kila kitu kilikuwa zaidi ya muujiza, yaani sisi ndiyo tulikuwa tukitangazwa na mheshimiwa rais mwenyewe kwamba ni mashujaa wa nchi? Hakika ilikuwa ni zaidi ya muujiza. Nilijikita nikishindwa kuyazuia machozi ya furaha yasiulowanishe uso wangu, hali ilikuwa hivyohivyo kwa wenzangu wote, hakuna ambaye hakutoa machozi ya furaha.
“Tunastahili, uwezo wetu wa kutumia nguvu za ndani ndiyo uliotufikisha hapa,” alisema Junaitha, wote tukageuka na kumtazama, hatukuwa na habari kwamba kumbe na yeye alikuwa akiitazama taarifa hiyo ya habari, akaja pale tulipokuwa tumekaa, tukakumbatiana huku wakiwa makini wasinitoneshe kidonda changu.
“Nimeshamaliza kumuandaa Firyaal twendeni tukamalizie kazi iliyosalia,” alisema Junaitha, tukainuka na kuanza kutembea taratibu kuelekea chumbani, kila mmoja akiwa na furaha kubwa sana ndani ya moyo wake.
“Niliwaambia lakini, bila shaka sasa mnaamini,” alisema Junaitha, wote tukamuunga mkono kwa sababu ni kweli alituambia kwamba tukifanikisha suala lile, nchi nzima itatujua sisi ni akina nani na kutupa heshima tuliyokuwa tukistahili.
Tulienda mpaka chumbani ambako Firyaal alikuwa amelazwa chini huku mishumaa saba ikiwa imewashwa na kuzungushiwa pande zote, kuanzia kichwani mpaka miguuni. Alikuwa amemfunga kwa sanda nyeupe ambayo hata sikujua ameipata wapi lakini eneo la usoni lilikuwa wazi.
“Mpendwa wetu Firyaal amelala usingizi wa kifo, kuna uwezekano wa asilimia 50 kwa 50 wa kumrudisha duniani lakini hata ikitokea tumeshindwa, bado kwetu hayo yatakuwa ni mafanikio makubwa kwa sababu kwa kipindi kifupi alichoishi duniani, Firyaal alikuwa ameishi kikamilifu.
Alituelekeza nini cha kufanya, wote tukakaa chini kwa mtindo wa tahajudi, mimi nilikaa upande wa kichwa cha Firyaal, Junaitha yeye alikaa upande wa kushoto wa kifua chake, jirani kabisa na moyo wake, Shamila alikaa upande wa miguuni kwa namna ambayo mimi na yeye tulikuwa tukitazamana, Raya na Shenaiza wao wakakaa upande wake wa kulia.
“Inatakiwa wote tuanze kwa kufanya tahajudi ya pumzi huku tukiunganisha nguvu, kila mmoja akitulia kwa kadiri ya uwezo wake na kuweka uzingativu, tunaweza kuiamsha upya pumzi ya Firyaal, akaanza upya kupumua na kurejea duniani,” alisema, akaanza kutuelekeza nini cha kufanya lakini mwisho alitoa angalizo:
“Kazi haitakuwa nyepesi kwa sababu tayari pumzi zake zimeshahama upande na kuelekea upande wa pili ambao ni kuzimu, kwa hiyo suala la kuzirudisha lilikuwa ni lazima lihusishe safari ya kuelekea kuzimu, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa changu.
Je, nini kitafuatia?
 
Leta vitu
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 70
ILIPOISHIA:
Wakati wote wakiendelea kulia, nilisikia mlango ukifunguliwa tena, nikamuona Junaitha akiingia lakini tofauti na wengine, yeye uso wake ulikuwa mkavu kabisa, akatembea harakaharaka mpaka pale nilipokuwa nimelala, akanitazama usoni, na mimi nikamtazama, tukawa tunatazamana huku nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia ataniambia nini.
SASA ENDELEA...
“Najua unataka kujua kuhusu Firyaal!” alisema na kabla sijamjibu chochote, akaniambia kwamba kulikuwa na habari mbaya kwa sababu inaonekana maisha yake yanashikiliwa na uzi mwembamba sana unaotenganisha kati ya uhai na kifo. Kwa maelezo yale, nilielewa kwamba anamaanisha kwamba tayari Firyaal alishatoka kwenye ulimwengu wa kawaida, hakuwa na uhai tena.
“Tunaweza kumuokoa kutoka kwenye mdomo wa mauti lakini itatugharimu kukaa siku saba kuzimu,” alisema Junaitha, kauli ambayo ilitufanya wote ndani ya wodi ile tubaki tukimshangaa.
“Inabidi kwanza tuhakikishe wewe umerejewa na nguvu zako kwa sababu unahitajika sana kwenye kazi ya kukata minyororo ya kuzimu ambayo tayari Firyaal ameshafungwa. Nilishusha pumzi ndefu na kutulia pale kitandani.
Akaanza kutupa maelekezo kwamba, nikisharejewa na nguvu zangu, tutaomba ruhusa ya kutoka hospitalini hapo kwa sababu za kiusalama, kisha tutaomba kuondoka na Firyaal kwa ajili ya taratibu nyingine.
“Kuna kitu sijaelewa.”
“Hujaelewa nini?”
“Umesema itatulazimu kukaa siku saba kuzimu?”
“Utaelewa tu,” alijibu Junaitha huku akigeuka na kutoka, akatutaka wote tutulie pale wodini na kama akina Shamila wakitolewa, basi wasiende mbali na mlango wa kuingilia kwenye ile wodi niliyokuwa nimelazwa kwa sababu za kiusalama.
Sikukaa muda mrefu sana, Junaitha alirudi na kunisogelea pale kwenje jeraha langu, akalishika kwa kulikandamiza huku akiongea maneno ambayo hakuna aliyeyaelewa, kisha akato kichupa kilichokuwa na ungaunga fulani, akafungua bandeji upande mmoja na kunyunyizia ule unga kwenye jeraha lango.
Hapohapo nikaanza kuhisi kama moto mkali unawaka kifuani na kadiri ulivyokuwa unaongezeka, maumivu nayo yalikuwa yakipungua na mwili wangu ukaanza kurejewa na nguvu zake.
“Nashughulikia usafiri, kaeni tayari,” alisema kisha akatoka tena, wote wakawa wananitazama kwa makini usoni kuona hali yangu inaendeleaje, kwa mbali nikaanza kutoa tabasamu hafifu lililoamsha matumaini mapya kwenye moyo wa kila mmoja.
Baadaye, Junaitha alirudi tena, safari hii akiwa ameongozana na manesi ambao waliniandaa vizuri, tayari kwa kuondoka. Wakanisaidia kuninyanyua pale kitandani, na kunitoa mpaka kwenye maegesho ya magari, wote tukaingia ndani ya gari na kushtuka kugundua kwamba mwili wa Firyaal pia ulikuwa ndani ya lile gari, akionesha kutokuwa na uhai kabisa.
Akawasha gari na kutusisitiza kwamba hatutakiwi kumgusa Firyaal wala kuzungumza chochote kumhusu mpaka atakapotuambia, akabadili gia na kukanyaga mafuta, gari likawa linaondoka, tukaenda mpaka kwenye geti la kutokea ambapo alizungumza na wale walinzi, wakamfungulia geti.
Tukatoka ambapo alizidi kukanyaga mafuta, gari likawa linakimbia kwa kasi kubwa.
Tuliendelea na safari huku wote tukiwa kimya kabisa ndani ya gari, kila mtu akiwaza lake lakini kubwa tukifikiria hatma ya Firyaal. Safari iliendelea na hatimaye tulifika nyumbani kwa Junaitha, akaingiza gari mpaka ndani ya geti, wote tukashuka huku tukionesha dhahiri kuchoka.
Mimi ndiyo nilionekana kuchoka zaidi kwa sababu bado mwili wangu haukuwa na nguvu kutokana na kupoteza damu nyingi kwenye lile tukio la kupigwa risasi, sambamba na maumivu ambayo yalikuwa yakizidi kupungua kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Shamila na Raya walisaidiana kunishika huku na kule kama ilivyokuwa kule mwanzo, tukaingia ndani na kwenda moja kwa moja kukaa sebuleni. Shenaiza na Junaitha wao walisaidiana kumbeba Firyaal na kumpitisha moja kwa moja mpaka kwenye kile chumba ambacho ndiyo huwa tunafanyia shughuli mbalimbali pale ndani.
Muda mfupi baadaye, Shenaiza alirudi na kujumuika na sisi pale sebuleni, akaenda kuwasha runinga na kwenda kutoa chupa ya maji ya kunywa kwenye friji, akanimiminia kwenye glasi na kuniletea, wote watatu wakakaa pembeni yangu.
Junaitha yeye aliendelea kubaki kwenye kila chumba akiwa na Firyaal, hatukujua anafanya nini kwa sababu yeye ndiye aliyetoa maagizo kwamba sote tubaki sebuleni. Bado ukimya ulikuwa umetawala nyumba nzima, sauti pekee iliyokuwa inasikika ilikuwa ni ya TV tu ambayo hata hivyo hakuna aliyekuwa akiitazama.
Kila mmoja alikuwa akiwaza lake lakini ghafla tulishtushwa na kiashirio cha ‘breaking news’ kwenye runinga, wote tukainua vichwa vyetu na kuanza kuitazama runinga hiyo kubwa na ya kisasa, iliyokuwa imebandikwa ukutani.
“Mungu wangu,” nilisema baada ya kushuhudia picha zetu tukiwa pale hospitalini zikioneshwa, zikifuatiwa na maelezo kwamba sisi ndiyo tulikuwa mashujaa wa lile sakata ambalo sasa lilikuwa limebatizwa jina jipya la Kurasini Scandal, likiwa na maana ya skendo ya Kurasini.
Mtangazaji aliwaambia watazamani kwamba hatimaye walikuwa wamefanikiwa kupata picha za watu ambao ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kufichua uovu mikubwa uliokuwa ukifanywa na mfanyabiashara mkubwa mwenye asili ya Uturuki, Loris kwa kivuli cha Shirika la Black Heart.
Alitumwagia sifa kedekede kisha baada ya hapo, alisema kwamba mheshimiwa rais alikuwa na maneno ya kuzungumza na wananchi wake ana kwa ana muda huo, ukapigwa wimbo wa taifa kisha mheshimiwa rais akaonekana, akiwa amesimama kwenye viunga vya hospitali alianza kuzungumza na wananchi moja kwa moja kupitia runinga.
Alianza kwa kueleza kuhusu mtikisiko mkubwa uliolikumba taifa baada ya kugundulika kwa kile mwenyewe alichokiita machinjio ya binadamu eneo la Kurasini, akafafanua kwamba mtu aitwaye Loris, ambaye serikali ilimuamini na kumpa kibali cha kuendesha Shirika la Black Heart, ambalo alilisajili kama shirika la kusaidia jamii, alivyogundulika kwamba anafanya biashara nyingine haramu na hatari mno kwa maisha ya wananchi.
Alieleza kila kitu, akasema wamegundua kwamba kumbe Black Heart, kazi yake ilikuwa ni kuwasafirisha watu kwenda nje ya nchi ambako wengi wao walikuwa wakienda kuuawa kisha kutolewa viungo muhimu kwenye miili yao, huku wengine wakiuawa hapahapa nchini na viungo vyao kwenda kuuzwa nje ya nchi.
Alionesha kusikitishwa mno na kugundulika kwa sakata hilo ikiwa ni muda mrefu umepita tangu kuundwa kwa shirika hilo, jambo ambalo lilimaanisha kwamba wananchi wengi tayari walishatolewa sadaka kwa sababu ya dhiki zao.
“Najua ni watu wengi ambao walienda kuonana na Loris kwa lengo la kuomba misaada, iwe ni kwenda kusomeshwa nje ya nchi, kufadhiliwa matibabu nje ya nchi au kutafutiwa kazi lakini wakaishia kutolewa kafara,” alisema mheshimiwa rais na alipofika eneo hilo, alishindwa kuzuia machozi yasimtoke, akavua miwani yake na kutoa kitambaa, akajifuta machozi na kuendelea kuzungumza.
Mwisho alitutaja majina, akianza na Junaitha, akaja mimi, Raya na Shamila huku akiwataja Shenaiza na Firyaal kwa utambulisho wa juujuu, nadhani alifanya hivyo kwa sababu za kiusalama, akasema anahitaji kuonana na sisi ikulu na kutoa maagizo tutafutwe mahali popote tulipo ili akatupongeze kwa kazi nzuri tuliyoifanya.
Alieleza kwa kirefu jinsi tulivyofanikisha suala hilo na vikwazo ambavyo tulikumbana navyo, akasema kwamba anajua tulipingwa sana lakini kwa sababu ya ushujaa wetu, tumefanikisha kufichuka kwa sakata hilo kubwa. Akatupa pole kwa yote na kutupongeza sana.
Alipofikia hapo, picha zetu zilirushwa tena runingani tukiwa tunatoka hospitalini kisha wimbo wa taifa ukapigwa tena na huo ukawa mwisho wa habari hiyo. Kwa muda wote huo tulikuwa kimya kabisa, tukiwa ni kama hatuamini tulichokuwa tunakiona.
Kwangu mimi kila kitu kilikuwa zaidi ya muujiza, yaani sisi ndiyo tulikuwa tukitangazwa na mheshimiwa rais mwenyewe kwamba ni mashujaa wa nchi? Hakika ilikuwa ni zaidi ya muujiza. Nilijikita nikishindwa kuyazuia machozi ya furaha yasiulowanishe uso wangu, hali ilikuwa hivyohivyo kwa wenzangu wote, hakuna ambaye hakutoa machozi ya furaha.
“Tunastahili, uwezo wetu wa kutumia nguvu za ndani ndiyo uliotufikisha hapa,” alisema Junaitha, wote tukageuka na kumtazama, hatukuwa na habari kwamba kumbe na yeye alikuwa akiitazama taarifa hiyo ya habari, akaja pale tulipokuwa tumekaa, tukakumbatiana huku wakiwa makini wasinitoneshe kidonda changu.
“Nimeshamaliza kumuandaa Firyaal twendeni tukamalizie kazi iliyosalia,” alisema Junaitha, tukainuka na kuanza kutembea taratibu kuelekea chumbani, kila mmoja akiwa na furaha kubwa sana ndani ya moyo wake.
“Niliwaambia lakini, bila shaka sasa mnaamini,” alisema Junaitha, wote tukamuunga mkono kwa sababu ni kweli alituambia kwamba tukifanikisha suala lile, nchi nzima itatujua sisi ni akina nani na kutupa heshima tuliyokuwa tukistahili.
Tulienda mpaka chumbani ambako Firyaal alikuwa amelazwa chini huku mishumaa saba ikiwa imewashwa na kuzungushiwa pande zote, kuanzia kichwani mpaka miguuni. Alikuwa amemfunga kwa sanda nyeupe ambayo hata sikujua ameipata wapi lakini eneo la usoni lilikuwa wazi.
“Mpendwa wetu Firyaal amelala usingizi wa kifo, kuna uwezekano wa asilimia 50 kwa 50 wa kumrudisha duniani lakini hata ikitokea tumeshindwa, bado kwetu hayo yatakuwa ni mafanikio makubwa kwa sababu kwa kipindi kifupi alichoishi duniani, Firyaal alikuwa ameishi kikamilifu.
Alituelekeza nini cha kufanya, wote tukakaa chini kwa mtindo wa tahajudi, mimi nilikaa upande wa kichwa cha Firyaal, Junaitha yeye alikaa upande wa kushoto wa kifua chake, jirani kabisa na moyo wake, Shamila alikaa upande wa miguuni kwa namna ambayo mimi na yeye tulikuwa tukitazamana, Raya na Shenaiza wao wakakaa upande wake wa kulia.
“Inatakiwa wote tuanze kwa kufanya tahajudi ya pumzi huku tukiunganisha nguvu, kila mmoja akitulia kwa kadiri ya uwezo wake na kuweka uzingativu, tunaweza kuiamsha upya pumzi ya Firyaal, akaanza upya kupumua na kurejea duniani,” alisema, akaanza kutuelekeza nini cha kufanya lakini mwisho alitoa angalizo:
“Kazi haitakuwa nyepesi kwa sababu tayari pumzi zake zimeshahama upande na kuelekea upande wa pili ambao ni kuzimu, kwa hiyo suala la kuzirudisha lilikuwa ni lazima lihusishe safari ya kuelekea kuzimu, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa changu.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 43

ILIPOISHIA:
Kauli yake hiyo ilitufurahisha sana mimi na Shamila, tukawa na uhakika kwamba sasa kazi itakuwa nyepesi kwa sababu tayari tutakuwa na mtu kutoka ndani kabisa, ambaye angetusaidia kutimiza lengo letu la kupambana na mtu huyo hatari.
SASA ENDELEA…
“Kwa hiyo tunaanzia wapi?” nilimuuliza Shamila, akawa ni kama anayetafakari kitu kisha akaniambia ameshapata majibu.
“Ngoja niende kwanza na huyu binti nikampe hiyo hard disk yake,” alisema Shamila.
“Utaweza kuichomoa kwenye kompyuta?”
“Mimi naweza, nasomea Information Technology niko mwaka wa pili,” alisema Firyaal ambaye alikuwa amefanana sana na Shenaiza, yaani hata bila kuuliza ungemjua tu kwamba ni ndugu yake.
“Sijamaliza kukopi data ninazozihitaji lakini.”
“Nitakusaidia pia, ninayo ‘back up’ kubwa tu nyumbani, naweza kuhamisha data zote na kukuletea,” alisema msichana huyo, nikawa namtazama usoni kwani aliyokuwa akiyasema hayakuwa yakifanana na umri wake.
Kwa kumtazama alionekana kama msichana mdogo ambaye kwa makadirio ungeweza kudhani yupo kidato cha pili au cha tatu lakini kumbe tayari alishafika kidato cha sita na sasa alikuwa chuoni.
“Nitashukuru sana ukinisaidia dada’angu,” nilisema kwa sauti ya kiungwana, Firyaal akanitazama usoni, na mimi nikamtazama, macho yetu yakagongana, harakaharaka akakwepesha macho yake huku aibu za kikekike zikiwa zimemtawala.
“Basi usitoke kwenda sehemu yoyote, mimi ngoja niende naye nyumbani,” alisema Shamila, akanisogelea pale kitandani na kunibusu kisha harakaharaka akamshika mkono Firyaal na kuanza kutoka naye nje.
>>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Walipofika mlangoni, nilimuona Firyaal akigeuka na kunitazama, na mimi nikamtazama, macho yetu yakagongana kwa mara nyingine. Tofauti na mwanzo, safari hii hakukwepesha macho yake, tukaendelea kutazamana mpaka walipotoka nje. Sikuelewa sababu iliyofanya awe ananitazama vile kwa sababu kimsingi hiyo haikuwa mara ya kwanza mimi na yeye kuonana.
Ilikuwa ni mara ya pili. Hata hivyo sikutilia sana maanani, nikampotezea.
Nikashusha pumzi ndefu na kutulia kitandani, mawazo mengi yakiendelea kupita ndani ya kichwa changu. Ni kweli nilikuwa bado sijapona vizuri lakini ilikuwa ni lazima niondoke hospitalini hapo kabla mambo hayajaharibika. Kutokana na sifa nilizokuwa nazisikia, nilijikuta nikimuogopa mno baba yake Shenaiza kama malaika mtoa roho.
Niliendelea kutulia pale kitandani, japokuwa Shamila aliniambia nisitoke, nilipata wazo la kwenda kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Shenaiza kwenda kuangalia anaendeleaje. Hata hivyo, nilipomkumbuka yule mtu aliyekuwa akinitazama sana kwa makini mle ndani ya wodi ya vichaa, nilijikuta nikipatwa na hofu moyoni, nikaghairi.
Kwa hesabu zangu za harakaharaka ukichanganya na maelezo niliyoyapata kutoka kwa Shamila, nilikuwa nimekaa hospitalini hapo kwa wiki mbili mfululizo, huku kati ya hizo, siku saba nikiwa nimepoteza kabisa fahamu.
Nilijaribu kuvuta kumbukumbu ya mambo yote yaliyotokea ndani ya kipindi hicho nilichokuwa hospitalini hapo, ungeweza kudhani kama nimekaa hospitalini kwa kipindi cha mwaka mzima. Kila kitu kilikuwa kikitokea kwa kasi kubwa mno kiasi cha kufanya hata akili yangu isipate muda wa kupumzika.
Kitu ambacho kilinipa faraja kubwa ndani ya moyo wangu, ni kuona jinsi wafanyakazi wenzangu pamoja na bosi wetu walivyokuwa wakinijali. Japokuwa nilikuwa chini ya uangalizi maalum ambapo watu hawakuwa wakiruhusiwa kuja mara kwa mara kunitazama, Raya alinihakikishia kwamba katika zile siku nilizokuwa nimepoteza fahamu karibu kila siku watu kutoka kazini walikuwa wakija kunitazama.
Baada ya kama dakika arobaini tangu Shamila na yule mdogo wake Shenaiza waondoke, Raya alikuja tena. Kiukweli japokuwa nilikuwa nikimuendea kinyume, Raya alikuwa akijitahidi sana kuwa karibu na mimi.
>>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Muda wote yeye alikuwa akinifikiria mimi tu kiasi cha kumfanya kazini asiwe anaenda wala nyumbani kwao asiwe anatulia, muda wote ilikuwa ni kiguu na njia, kuja hospitali na kurudi kwao.
“Vipi unaendeleaje mume wangu,” alisema Raya kwa sauti ya chini, akionesha kuwa na mawazo lukuki ndani ya kichwa chake.
“Naendelea vizuri mke wangu, vipi mbona nakuona kama mudi yako iko chini sana, nini kinakusumbua,” nilimwambia Raya kwa upole, akajisogeza na kupitisha mkono wake mmoja shingoni kwangu, akanibusu kwenye paji langu la uso na kuanza kuniambia kwamba tangu nilipomweleza ukweli wa kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia, alikosa raha kabisa.
“Nahisi kama nitakupoteza mpenzi wangu na mimi siwezi kuishi bila wewe, hata sijui itakuwaje,” alisema kwa huzuni, nikashusha pumzi ndefu na kuanza kumtuliza. Nikamwambia asiwe na wasiwasi, hakuna jambo lolote baya litakalotokea nakuhakikishia,” nilimwambia.
Kidogo kujiamini kwangu kulimfanya naye aanze kuona kwamba kumbe halikuwa tatizo kubwa mbele yetu, nikamueleza pia juu ya mipango ya kutoroka tuliyokuwa tumeipanga kwa ajili ya kumkimbia baba yake Shenaiza. Nilimuona naye akiniunga mkono, nadhani hata yeye hakuwa na imani kabisa juu ya usalama wangu hospitalini hapo.
Tulizungumza mambo mengi, Raya akawa ananisisitiza kwamba yeye amejitoa kwa asilimia mia moja kunisaidia, isije ikatokea kwamba nikamgeuka na kumuona hana maana tena. Kauli yake iliugusa sana moyo wangu kwa sababu ni kweli Raya alikuwa amejitoa kwa kila kitu lakini kwa bahati mbaya sana shetani alionekana kunizidi nguvu.
Nikawa namhakikishia kwamba asiwe na wasiwasi lakini ukweli, sikuwa namaanisha kile nilichokuwa nakisema. Akaniambia kwamba atashirikiana na Shamila kuhakikisha wananitorosha hospitalini hapo usiku bila mtu yeyote kujua, swali likawa nikishatoroshwa nitaenda kukaa wapi?
Raya alisema anataka nikakae nyumbani kwao kwa sababu pale kuna usalama zaidi, nikamwambia ni rahisi wabaya zangu kujua kwamba niko pale kwa sababu kuna baadhi ya watu walikuwa wakijua kuhusu uhusiano wetu wa kimapenzi. Nikatumia nafasi hiyo kumpigia chapuo Shamila, nikamwambia Raya kwamba amesema yupo tayari kunificha nyumbani kwake.
Nilimuona Raya akishtushwa kidogo na nilichokisema lakini nikamtoa wasiwasi na kumwambia kwamba mimi na yeye tutakuwa pamoja kwa hiyo asiwe na wasiwasi wowote. Akakubali kwa shingo upande, nadhani bado alikuwa na wivu juu ya ukaribu wangu na Shamila.
Muda ulizidi kuyoyoma, baadaye Shamila alirudi akiwa peke yake, akaniambia kwamba kila kitu kimeenda kama tulivyokubaliana, akaniambia kwamba Firyaal alikuwa mtundu sana kwenye mambo ya kompyuta na kwamba tayari alishanikopia data zote na kuziacha pale nyumbani kwake kama tulivyokubaliana, tukaanza kupanga mipango ya namna ya kutoroka usiku huku Raya naye akiwepo.
Jambo ambalo kuanzia mwanzo Raya hakuwa akilijua, ni kwamba katika mpango wetu huo ilikuwa ni lazima pia tumtoroshe na Shenaiza, akashtuka kusikia hivyo.
Bado nikaendelea kumsisitiza kwamba ilikuwa ni lazima tuondoke na Shenaiza kwa sababu bila yeye mimi nisingeingia kwenye mtego huo na kuanzia mwanzo alikuwa akinisisitiza kwamba mimi ndiye mtu pekee ninayeweza kumsaidia.
“Usiwe na wasiwasi, hawa wote wataenda kukaa nyumbani kwangu, mimi nina nyumba kubwa, hata na wewe ukitaka tukae pamoja tusaidiane kuwahudumia wagonjwa haina shida,” alisema Shamila, nikamuona Raya akishusha pumzi ndefu na kunitazama, akatingisha kichwa kama ishara ya kukubaliana na mimi.
Ilibidi Raya abaki palepale hospitalini mpaka usiku ili iwe rahisi kufanya kazi yetu, muda ukazidi kuyoyoma na hatimaye giza likaingia, ule muda tuliokuwa tukiusubiri kwa hamu ukawa umewadia.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
kidonda cha kisu cha kifua tena cha wiki mbili!!!!.......ukaweza kupiga KOKROCH DETH....tena bila kujitonesha!!!....mwanangu we mkali
 

Similar Discussions

23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom