Simulizi ya kweli inayomuhusu mwanamke Anna Ecklund na Padre Theophilus Riesinger

Polycarp Mdemu

Senior Member
Jun 2, 2019
165
209
+ Hii ni Simulizi ya kweli Inayomuhusu mwanamke ANNA ECKLUND Na Padre Theophilus Riesinger.

+ Simulizi ya kusikitisha ya Anna ni moja ya simulizi za kweli maarufu huko Amerika, kuna vitabu kadhaa vimechapisha simulizi hii kikiwemo kitabu cha Begone Satan kilichoandikwa na Carl Vogl mwaka 1935 na baadaye kuandikwa tena na mchungaji Celestine Kaspsner wa UK mwaka 1973.

+ Anna Alizaliwa huko mjini Wisconsin mnamo March 23 mwaka 1882 na kukulia akitunzwa katika Nyumba ya Watawa Mjini Marathon, Kulingana na vyanzo vya vyeti vya kuzaliwa mjini hapo Inaonyesha Wazazi wa Anna wote walikuwa ni Wahamiaji kutoka Ujerumani.

+ Akiwa na Umri wa Miaka 14 tuu Alianza Kuandamwa na Roho Chafu za Ndugu Zake Waliofariki. Marehemu Baba Yake Alikuwa Anamuingilia Kingono Na Hakuna Aliyeweza Kumsaidia. Chakushangaza Mwanamke huyu Bado Yuko Hai Hadi Leo.

+ Inasemekana chanzo cha Mambo haya yote ni Shangazi yake Anna Ambaye aliitwa Mina, Mina Alikuwa mshirikina Enzi za uhai wake, baada ya kufa walihitaji kumtesa Anna ili warejee kuwa na nguvu za giza tena hata baada ya kufa kwakua inaaaminika Mshirikina akirudi huwa na nguvu zake zinakuwa kubwa mara saba zaidi ya zile za awali.

+ Paranormal Investigators wanaeleza kuwa kilichowaudhi sana ndugu zake hao kabla ya kufariki ilikuwa ni kitendo cha Anna kupenda Imana na Kuwa na Imani sana, alikuwa ni mtoto mwenye imani kitendo kilichowaudhi sana hao ndugu zake.

+ Anna alikuwa anaishi na roho nyingi katika mwili wake zikiwa zinamsumbua, na moja ya roho hizo zilikuwa ni roho za marehemu baba yake Jacob Ecklund, marehemu shangazi yake Mina na marehemu Bibi wa baba yake Mina, wote walifariki, lakini bado roho zao zimekuwa zikiishi ndani yake.

+ Hali hii iliendelea katika maisha yake yote na alipofikisha umri wa miaka 26 alikuwa ameshamilikiwa kwa asilimia 100% na roho hizo mbaya.

+ Mwaka 1911 Padre Theophilus Riesinger Wa Shirika La Ndugu wadogo Wafransiscan (Mkapuchini) Aliyekuwa akihudumu mjini Wisconsin wakati huo aliamua kufanya uchunguzi juu ya Anna, Juni 18, 1912 alikua amemaliza kufanya uchunguzi huo. Hata hivyo kwa bahati mbaya inaelezwa kuwa uchunguzi huo wa baba Padre uliokuwa na lengo na kumsaidia Anna kutoka katika mateso hayo haukufanikiwa kabisa kutokana na roho hizo kuwa 'zimeota mizizi' na zimeanza kumuachia laana Anna. Roho zilitoa laana kwa chochote ambacho Anna angepatiwa na watu wadini ili kisifanye kazi, zilitoa laana kwa yeyote aliyejifanya mstaari wa mbele kumsaidia Anna kutoka katika hali hiyo.

+ Mwaka 1928 Padre Theophilus alianza mchakato wa kumsaidia Anna kuondokana na roho hizo zilizokuwa zikimtesa maisha yake yote, Wakati huu alisaidiana na Padre Joseph Steiger wa mjini Earling, Padre Joseph Alishauri wakati huu utoaji wa Mapepo kwa Anna (exorcism) inabidi ufanyika katika nyumba ya Watawa (convent) iliyomilikiwa na Franciscan Sisters.

+ Kwahiyo Anna Alipelekwa Kwenye nyumba ya Watawa tarehe 17 August 1928 inaripotiwa baada ya kuingia tu katika Nyumba ya Watawa, Basi Alianza Kuwa na hasira na Kulia kama Paka. Kwa usaidizi wa Masista Wafransiscan Utoaji wa Rohi hizo chafu ulianza Tarehe 18 (siku ya pili yake) kazi hii ikifanyika kwa siku nane, Na Anna afya yake ilizorota zaidi, Kwani akikataa kula chakula Cha hapo Conventini, Labda kitoke nje ya hapo, Pia alitapika mfululizo uchafu usioeleweka, Pengine hata Majani ya Tumbaku.

+ Kelele zilikuwa nyingi katika Nyumba hiyo, Mpaka Watawa wakaomba pengine Kazi hiyo Padre akaifanyie Pahala Pengine, Anna akiongea lugha nyingi ambazo hata yeye hakuzijua, Mara nyingine aliongea wazi kuwa Ile ilikuwa laana ya Baba yake mzazi kwa Mina ambaye alikataa kufanya Mapenzi naye wakati wa kupevuka, Lakini yalipotoka maneno haya ndipo Padre Riesinger alipogundua kuwa anayeongea si Anna Bali ni Mina (Shangazi wa Anna).

+ Tarehe 23 ambayo Padre Riesinger alisema itakuwa ni mwisho wa Utoaji wa Roho hizo, Padre Riesinger aliamuru tu Roho hizo kutoka kwa Jina la Baba, Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu, Na kupitia maombezi ya Bikira Maria "Blessed Virgin Mary to depart to Hell" Anna Alipoteza nguvu katika mwiki kabisa kisha kutaja majina kadhaa ya Ndugu zake katika sauti yake Halisi, Kisha alifumbua macho na Kusema " "My Jesus, Mercy! Praised be Jesus Christ!"

+ Kutoka Hapo Padre Riesinger akawa Amefanikiwa Kutoa roho hizo, Na ushuhuda huo ukawekwa katika Viwakilishi katika nchi ya Marekani.

+ Baada ya Kazi hii kufanikiwa Padre Theophilus alisema kuwa kuna muda alikuwa akiwaona watu wawili wa ajabu katika kona ya chumba cha Anna, mmoja alimuelezea kuwa ni mrefu sana, mwenye manyoya meusi, alikuwa anamtazama sana kwa hasira mchungaji huyo aliyekuwa akijitahidi kumsaidia Anna bila mafanikio.

+ Kumbuka Padre Riesinger hudai hii sio kazi ngumu kati ya zile alizowahi aombwe afanye,
Riesinger alikufa mwaka 1941 akiwa na umri wa miaka 73 na Anakumbukwa zaidi katika kazi zake hizo, Na kuna Movie zilizotoka zikiwaonyesha Watu wakibeba uhusika wake Kama ile iitwayo THE EXORCIST yule mtoaji wa Mapepo ndio huonyesha kazi ya Padre Riesinger.

+ Anna yupo hai mpaka leo ana umri wa miaka 138, anaendelea kusaidiwa katika Nyumba za Watawa mjini Early, Lowa, Ni vitabu na movie nyingi sana zimetoka hadi sasa kuielezea story hii ya kusikitisha ya Anna, mwaka 2016 ilitoka movie ya THE EXORCISM OF ANNA ECKLUND.

*****************MWISHO*********************

(Picha za Wahusika na Cover's za Movies za wagusika katiaka Picha)

Polycarp Mdemu
https://t.co/xLLbOpNOL9

Ahsante.
IMG_20200805_130530.jpeg
96bfdda88343850a0b53c4172f2583ab.jpeg
94583bd100379c0fac59dbcff93cf4ae.jpeg
a73283279ad17d6697706631a9573b9e.jpeg
 
Back
Top Bottom