Simulizi ya kijasusi- Nilimdhania kahaba kumbe bikra

singanojr

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
569
2,792
SEHEMU YA 176

Roma alijikuta akitabasamu na kupenda kwa wakati mmoja kwa namna ambavyo Goodman alikuwa vizuri katika kazi yake , kwani kwa jinsi alivyomuona aliona kabisa ni sehemu ya kazi yake anapokutana na watu wakubwa kujenga konekesheni.

“The Cromwell Family…Goodman, are you saying that they’re the descendants of the Lord Protector?”

”Ukoo wa Cromwell…Goomna unamaanisha kwamba hawa ni mwendelezo wa uzao wa The Lord Protector?”

“Yes Exactlly! This gentleman here Mr Stern is the heir apparent of the Lord Protector title in the Cromwell clan while Miss Alice is his younger sister given birth by the same mother.”

“Ndio! Hakika , huyu Stern unaweza kusema ndio mrithi mkuu wa Familia ya Cromwell na huyu Alice ni mdogo wake kutoka kwa mama mmoja”Aliongea huku akiwa na mchecheto wa hali ya juu na hata uwoga ulikuwa umepungua.

Lord Protector ni jina la kikatiba alilokuwa akipewa mkuu wa nchi katika kipindi cha ‘Common Wealth of England’ kwa kuzingatia nguvu ya kikanisa enzi hizo , sasa basi katika historia ya Uingereza , Oliver Cromwell ndio mtu wa kwanza kupewa cheo hiko cha Lord Protector baada ya kushinda vita (War of Three Kingdoms),Vita vilivyokuwa vikipiganwa na mataifa matatu yaani Scotland , Ireland na England na Cromwell alitawala kama Lord Protector mpaka pale alipokuja kushindwa katika vita vingine na Charles Mfalme wa pili na kuchukua utawala na kuanzia hapo jina la Lord Protector halikutumika sana na ndio maana ni ngumu sana kulisikia huko duniani, kwani lilibakia katika historia , lakini hio sio kweli kulingana na vitabu vya kihistoria vya Uingereza , ukweli ni kwamba licha ya kwamba Cromwell aliuliwa kipindi hiko lakini ukoo wake haukuangamizwa , Ukoo wa Cromwell ulibakia na kuendesha Maisha yao pasipo kuwa na uongozi wa juu ndani ya serikali lakini kutokana na kwamba hapo mwanzo Oliver alikuwa mkuu wa nchi basi utajiri wake haukupotea na ulienda moja kwa moja kwa familia yake, na kwanzia kipindi hiko Cromwell Familly wakaanza kujitengenezea koneksheni ndani ya taifa la Uingereza na hata kuendesha taasisi za siri sana na unachotakiwa kuelewa pia ni kwamba hii familia ndio wenye nguvu katika kanisa la Pretsbyrean Church, hapa kumbuka Archimonde wakati akiwa ameshikilia Holy Grail alivyokuwa akiongea na Moses na kusema wanapaswa kufikisha kikombe kwenye kanisa la Pretsbyrean Church.

Kuhusu hili kanisa nitaelezea mwishoni kama kujazia , lakini unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba kupitia Pretsbyirean Church ndio kulitokea makanisa ya waprotestant waliosambaa huko Marekani na kuna kitu kinaitwa ‘Five Solas’, kuna mambo mengi hapa ya kuelezea ndugu msomaji ambayo yanawaunganisha Cromwell na Dark Parliament.

Hivyo Edna kusomea Oxford Uingereza ni lazima angeweza kusikia kuhusu historia ya ukoo wa Cromwell, kwahio haikumshangaza Roma kwa Edna kuifahamu familia hio.

“Kwahio kumbe wewe ndio mrembo Edna kutoka kampuni ya Vexto kutokaTanzania?, Umrembo kama nilivyoweza kusikia Habari zako”aliongea Alice na kumfanya Edna kushangaa inawezekanaje watu kutoka ukoo wa Cromwell kumfahamu.

“Kwenye macho yangu wewe ndio mwanamke mrembo kuliko wote ndan ya dunia hii”Aliongea Stern na walianza kubusiana , kitu na dada yake na hilo wala halikumshangaza Roma ila kwa Edna lilimshangaza.

“Umesema hawa ni ndugu kwanini ni wapenzi?”Aliuliza Edna akimwangalia Goodman.

“Ni wapenzi ndio na inafahaika ndani ya uingereza yote na hata familia yao haipingi hili swala na wanabaraka zote,hivyo sio siri,nadhani ushawahi kusikia msemo wa ‘Maintaining the Pure Blood’?”Aliongea Goodman na kumfanya Edna kutingisha kichwa kwa kuelewa

“Bebi Edna usishangae sana , hili sio jambo jipya , ukweli nishaona mambo kama haya yakitokea , hata hivyo sioni ubaya kwa kaka kumtamani dada yake kisa ni mrembo”Aliongea Roma huku akitoa cheko la kinafiki.

“Unaonekana kujua mengi?”Aliongea Edna huku akimfinya Roma mkononi kiasi cha koti kutaka kumdondoka na Roma alimvalisha vizuri na kisha akachuchumaa na kuwamulika tena usoni.

“Mnaonaje sasa mkiacha kuvyonzana , na mkatueleza mmefikaje hapa , na hali yote kwa ujumla?”Aliongea Roma.

Baada ya Roma kuuliza , Stern alimuachia dada yake na kisha kumwangalia Roma.

“Hata sisi hatujui hali inayoendelea hapa , ukweli ninachojua tulitekwa mchana kweupe wakati tukiwa tunatoka hotelini na tulifunikwa na vitambaa na ninachojua tu ni kwamba hapa hata simu mawasiliano hakuna kabisa ,Halafu nimekumbuka pia inaonekana kuna vyumba vingine , kwani niliweza kusikia sauti ya mwanamke ikitoa kilio ikiomba msaada naamini kuna wenzeru pia”Aliongea .

“Unamaanisha zile tetesi za watu matajiri kutekwa ndani ya jiji la Parisi ni za kweli?”Aliuliza Goodman.

“Nani anaweza kujua,Sisi tumekuja hapa Paris kwa ajili ya kuhudhuria maonyesho ya wiki ya Fasheni na hatujui kitatokea nini baada ya hapa , lakini mimi sijali sana , ilimradi nipo na mpenzi wangu Alice”Aliongea Stern na kumwangalia Alice na wakaanza kudendeka tena.

Roma aliwapuuza na kuwaza kutumia uwezo wake kujua mazingira yote ya hili eneo na aliweza kushuhudia watu wengi waliokuwa kwenye vyumba vingine kama walichokuwepo na kushangaa lakini pia kujiuliza kwa Pamoja , kwanini watu hawa wameletwa hapa na waliowaleta hawafanyi chochote.

“Stern Mpenzi nanuka jasho nataka nikaoge , ongea na hao walinzi basi”Aliongea Alice baada ya kujitoa kwenye mwili wa Stern huku akijidekeza,

“Miss Alice huu sio muda wakufikiria kuoga , tunapaswa kufikiria njia za kujikoa”Aliongea Goodman

“Kwanini siruhusiwi kuoga kisa nimetekwa?” Alice alimjibu huku akisimaa na kusogelea upande wa mlangoni.

“Kitendo unachotaka kufanya ni Harari Alice”Aliongea Goodman

“Usijali hakuna cha kunipata kwa urembo wangu huu niliokuwa nao”Aliongea akitabasamu kwa namna ya kushawishi na kumfanya Goodman ameze mate, maana ni kama kahaba aliekuwa kazini.

“Bam,Bam Bam”

“Jamani hebu mkuje hapa , ninataka Kwenda kuoga mimi”Aliongea Alice huku akigonga chuma kwa nguvu na sauti kusambaa.

“Wanaonekana kama hawana akili vizuri wewe huwaoni , inakuaje mtu tupo kwenye hali kama hii halafu akafikiria kuoga?”Aliuliza Edna kwa Kiswahili.

“Usiwajali sana , waone tu kama watu wa kawaida”Alijibu Roma kwa Kiswahili.

Mshindo wa viatu uliwasogea na ndani ya sekunde alionekana mwanajeshi aliekuwa ameshikilia bundui lake na akamwangalia Alice.

“Hatuna huduma ya kukuogesha humu , tunaweza kukupa maji tu na chakula”

“Mhmh jamani kaka jambazii… mbona unakuwa na roho mbaya hivyo, nataka Kwenda kukojoa na kujisafisha mwili , usiniambie unataka mwanamke mrembo kama mimi nikojoe hapa ndani”Aliongea Alice kwa kujidekeza kwa kaka jambazi.

“Hahaha… Stern dada yako bwana.. hahaha ila ni mcute hatari”Aliongea Roma huku akicheka.

“Roma umeona eh , ndio maana nampenda , huwa namuona Alice kuvutia sana kwa vitendo vya kitoto”Aliongea Stern na Edna aliwaangalia Roma na Stern na kisha akabinua midomo, aliona hao wanaume wanaongea upuuzi.

“Rudi ukae ukatulie usinipigie kelele tena , la sivyo nitakufumua na hii bunduki”

“Usinifanyie hivyo jamani.. kaka Jambazi”

“Usinijaribu Rudi ndani”

“Bebi hawataki ,napaswa kufanya nini mimi nataka kuoga ..”

“Hata mimi mpenzi siwezi kujua ni nini tunapaswa kufanya, Labda Roma na Edna wana njia ya kukusaidia mpenzi”Aliongea Stern.

“Okey!Mimi nitawasaidia”Aliongea Roma akijitolea na yule mwanajeshi hakuwa hata na muda nao na hakujali wanachoongea.

“Hey! Unaonaje mkamsaidia huyu mrembo akatoka kujisaidia?”Aliongea Roma.

“Acha upuuzi tuliza mbupu zako , unakitafuta kifo eh”Aliongea mwanajeshi kwa hasira na kumuwekea mdomo wa bunduki kwenye paji la uso na kumfanya Edna awe na wasiwasi na kutaka Kwenda kumzuia Roma , alikuwa ashasahu kabisa kuwa Roma alikuwa na uwezo wa kimaajabu , na alijawa na wasiwasi.

“Usisogee Edna”Aliongea Goodman akimzuia kwa mkono lakini Edna alimkwepa Goodman , lakini kabla hajafikia mlango mara giza lilitawala kwani simu ya Roma tochi aliizima na kiza kiliendana na milio ya Bunduki ikikohoa risasi kama tatu hivi

‘Bang ..Bang ..Bang’

“Romaa.. Romaa”Aliita Edna kwa wasiwasi kweli baada ya kusikia mlio wa riasisi baada ya kufumba masikio Pamoja na macho kwa sekunde kadhaa na ile anafumbua macho yalikuwa na machozi tayari huku akitetemeka.

Stern alitoa simu yake kubwa na kuwasha tochi na hapo hapo ndipo Edna aliweza kushuhudia mlango ushafunguliwa muda na Roma hakuonekana kabisa ni kufuri pekee lililokuwa limedondoka chini.

Stern baada ya kuona mlango upo wazi alitabasamu na kisha akamshika mkono mchumba wake.

“Stern msisogelee geti mtapigwa risasi na nyie , Roma ashadhurika , hatutakiwi kufanya kosa tena”Aliongea Goodman akiwa anatetemeka akitaka kuwazuia.

“Hey Goodman naona unaniwangia sasa , nani kadhurika?”Ilisikika sauti ikitokea upande wa kona kwenye njia ndefu ya handaki , huku Roma akiwa na Bunduki begani huku mkononi akiwa na ile sigara kubwa aliokuwa nayo kwenye gari na alikuwa akivuta na kutoa moshi kwa wakati mmoja.

SEHEMU YA 177

Sasa Goodman hakuangalia vizuri , ila alipoangalia chini ndipo aliweza kushuhudia Roma akiwa ameegemeza mguuu wake kwenye kichwa cha yule Jambazi Mwanajeshi na Damu zilikuwa zimetapaa chini.

“Wewe..we.. umewezajee!!?”Aliongea Goodma huku akijivuta kwa wasiwasi na kuangalia maiti iliokuwa chini kwenye sakafu.

“Mr Roma nimekukubali sana… nadhani ni muda wa sisi kuondoka , ili nirudi hotelini nikaoge,Ila hao Majambazi wengine unadili nao vipi”Aliongea Alice huku furaha ikiwa kwenye macho yake , hakuona woga maiti iliokuwa chini yake kama ilivyokuwa kwa Edna ambaye alikuwa akiangalia kiatu cha Roma kilivyokanyyaga kichwa cha Maiti.

“Hehe.. hata usijali mpaka sasa hivi nimeua watatu,Toka uwaangalie nilichokifanya nikuvuta Triger tu na nikashangaa wanadondoka wenyewe”Aliongea Roma huku akitabasamu na Alice Pamoja na Goodman walitoka na hapo ndipo waliposhuhudia majambazi matatu yakiwa chini , na wote walionekana kupigwa risasi za Koromeo .Goodman alimwangalia Roma kwa mshangao na kujiuliza huyu Roma ni nani haswa , wakuweza kufanya yote hayo kwa sekunde tu.

“Hapana haiwezekani?”Aliongea kwa sauti Goodman.

“Kwanini isiwezekane Mdogo wangu Goodman , ngoja nikuonyeshe tena ninavyoweza”

Bang! Bang Bang!

Roma alisambaza Riasi upande wa kulia kwake kwenye kiza kwa spidi .

“Haha ..Mdogo wangu Goodman iko hivyo , ni rahisi sana”kusema ukweli hapa Goodman alimuona Roma yeye ndio kama Jambazi , kwa jinsi alivyokuwa akitoa moshi wa sigara na pua zake , aliona kinachomtofautisha Roma na Jambazi ni nguo safi pekee alizovaa.

“Halafu mimi sio mdogo wako”Aliongea Goodman.

Wakati huu Edna na yeye alisogea taratibu mpaka aliposimama Roma huku akiwa na uso wa ukauzu hatari , lakini licha ya hivyo machozi hayakujificha kwenye macho yake , alimkata jicho Roma.

“Edna kwani…”

“Unaona ni sifa sio , kisa umeua majambazi Eeh, unajiona mwamba sana hapa ndani na unatufanya tuogope…Unapenda kufanya wenzako tuwe na wasiwasi kwa ajili yako..?,Nakuuliza?”

“Aa…!”Roma alishindwa hata kujitetea , maana Edna licha ya kuwa na machozi , lakini Jazba yake ilikuwa waziwazi., na Edna hakutaka hata jibu alitoa simu yake kwenye mfuko wa suruali ya Jeansi na kisha akawasha tochi na kuanza kupiga hatua kusonga mbele.

“Edna kuwa makini , utawashitua walinzi”Aliongea Goodman huku akimsogelea kwa spidi , akiwa na wasiwasi.

“Nitakuwa sawa”Aliongea Edna akizidi kusonga

“Acha kelele hakuna wa kumdhuru”Aliongea Roma akimuongelesha Goodman.

“Kwanini unasema hivyo?”

“Kwasababu wote washakufa”Aliongea Roma na kumfanya Goodman asimame , ni kama hajaelewa vizuri ila Roma hakumjali alimpita kumuwahi Edna na Alice na Stern pia wakampita na kumfanya Goodman na yeye atoe simu yake na kuanza kuwakimbilia kutoka kwenye pango.

Roma alikuwa ashamfikia Edna tayari na walikuwa wakitembea kiupande upande na Roma alitupa siraha upande wa ushoto na kisha akamshika Edna mkono.

“Unafanya nini..?”

“Nakuongoza njia ya kutokea”

“Niachie hata huna haja ya kunijali”Aliongea kwa hasira

“Mke wangu mtiifu usiwe na hasira bhana , nisamehe kwa kukufanya uwe na wasiwasi , sitorudia tena na kila nitakachofanya nitahakikisha na kushirikisha , nikiua tutaenda wote kuua , ..Enhee hata pia nikienda kutafuta warembo”Aliongea Roma na kumfanya Edna Asimame na kummulika Roma usoni huku akimwangalia na Roma aliweka tabasamu la Kifisi na kumkonyeza na kumfanya Edna ashinwe kujizuia kutabasamu.

“Fanya mambo yako mwenyewe , Acha kujimwambafai”Aliongea

“Hehe .. nitafanya chochote ili mradi usikasirike”Aliongea Roma huku moyo wake ukiwa na amani maana alijiambia kumfanya mwanamke kauzu kama Edna kutabasamu ni shughuli kweli kweli., Wengine hawakueweza kuwaelewa kwa lugha waliokuwa wakiongea , lakini Alice na Stern waligundua kitu kutokana na matendo ya Edna na Roma na waliangaliana na kukonyezana na kisha wakatabasamu.

“Jamani eh , hatutakiwi Kwenda moja kwa moja mpaka nje kule , tunapaswa kwanza kutafuta magari yetu kwanza hapahapa ndani kwenye maeneo ya karibu , watakuwa wameyahifadhi huku”Aliongea Roma na Edna aliona Roma kaongea Pointi.

“Aiiii..Jamani nisaidieni”Goodman aliekuwepo nyuma alipika ukulele na kuwafanya wote wageuke na kumwangalia na walipomulika waliona Goodman akiwa ameshikiliwa na Jambazi na mkono kwenye mguu wake na pale pale lile jambazi likamwamchia na kulala tena , lilionekana lilikuwa likikata Roho na hata Edna hakuelewa ni namna gani Roma aliweza kuua watu wote kwa wakati mmoja , ila hakutaka hata kuuliza , ilimradi walikuwa salama.

“Goodan ashakufa huyo”Aliongea Edna na Goodman alinyanyua macho yake na kuangalia na kweli yule Jambazi alikuwa ameshakufa,lakini Roma baada ya kuangaza macho upande wa kushoto alijikuta akitabasamu baada ya kuona gari lao walilokuja nalo , na kufanya kila mtu kutabasamu akiwemo Alice alieshangilia kabisa na kuonekana kama mtoto alieharibiwa kwa kudekezwa.

“Edna usikae huko , njoo tukae mbele na mimi, Goodman atakupigia makelele ya ajabu ajbu”Aliongea Roma na kumkonyeza Edna na kisha akafungua mlango na kumvuta Edna na kuingia na yeye akizunguka na kuingia ,na ndani ya dakika nne wote walikuwa kwenye gari na Roma aliwasha taa za gari baada ya kufanya mautundu yake na eneo lote la msituni kuwa na mwanga.

Lakini ajabu ni kwamba eneo lote lilikuwa na miili ya wanajeshi waliokufa na kumfanya Goodman kushaangaa,

“Nani alikuja kuwaaua?”Aliuliza Goodman akimwangalia Stern na Alice.

“Goodman unasahau haraka , Si Mr Roma alisema ndio kawaua wote, Bebi tuachane nae bwana anasumbua hadi anakera”Aliongea Stern akimvuta Alice kifuani,..

Edna na yeye aliekuwa amekaa upande wa Dereva na Roma alishuhudia miili hio na kumwangalia Roma.

“Wakati unaua watu wote hawa na giza totoro ulikuwa ukiwaona mmoja baada ya mwingine?”

“Mke wangu haijalishi na namna gani nilivyowaua , ila washakufa tayari na hawana thamani tena”Aliongea Roma na Edna alinyamaza.

“Tunaelekea uelekeo wa wapi sasa kutoka hapa?”

“Tutaelekea Parisi mke wangu”

“Unajua hapa tuko wapi na njia ya kuturudisha unaijua maana naona msitu tu mbele”

“Hapa tupo kaskazini mwa Paris msitu wa Romilly-sur-Seine,kutoka hapa mpaka mjini ni kama masaa mawili , ngoja tuwahi tukapige msosi wa maana mke wangu”Aliongea Roma na kukanyaga pendeli ya spidi kwa nguvu na gari ikanguruma kama Simba na kufyatuka Kwenda mbele.

“Punguza mwendo Romaa..”

“Hahaha…Funga mkanda nina njaa nataka niwahi”Aliongea Roma na kumfanya Edna azidi kuwa na wasiwasi na sekunde tu kama mshale waliingia kwenye barabara ya Rami , na Roma aliona hii ndio raha ya kuwa kwenye mataifa makubwa kwani Rami ni mpaka misituni.

“He is Crazy ….”Aliongea Goodman kwa sauti , huku akiogopa mwendo wa Gari maana alishuhudia vimiti vikipishana kwa kasi, lakini kwa Stern na Alice waliinua Glasi za Wine juu.

“Cheers!!”Waligongesheana kwa kujipongeza na kisha kupeleka kinywani na kunywa kwa furaha, yaani hawakujali kabisa kinaochendelea kwao kila jambo ni fursa na walionekana kutimiza Fantansy zao , Kwanza walishatimiza Fantansy ya kufanya mapenzi wakiwa wametekwa jambo ambalo walikuwa wakiliota kwa muda mrefu , lakini sasa hivi Roma anawakamilishia Fantansy yao nyingine ya kunywa Wine kwenye gari iliokuwa kwenye mwendo kama wa mashindano.,watake nini , Pesa kwao haikuwa tatizo , Mapenzi wanayo ya moto moto na isitoshe ni kaka na dada , wasingeweza kuachana.

Dakika chache mbele Edna aliweza kushuhudia mto maarufu ufahamikao kwa jina la Seine , na kwa mbaali akiliona jiji la Parisi likionyesha mataa , na wakati akiendelea kushangaa , mara gari ilisimama na Roma alifunuga mlango na kutoka.

“Unafanya nini tena Roma?”

“Mke wangu nimesahau kuripoti kwako , nadhani unakumbuka kuwa mle ndani hatukua peke yetu , nataka niwe msamalia mwema leo kwa kuwasiaida”Aliongea Roma na kutoa simu yake mfukoni na kubonyeza bonyeza na kisha akaweka sikioni

“Anafanya nini tena?”

“What is he doing?!”

“Mr Goodman, it looks like you have night blindness. Isn’t Mr Roma making a call?”Aliongea Alice huku akimpuuza kwa kumwambia atakuwa na upofu wa kuona kwenye giza.

“Look at the situation! Why is he making a call now?!”

“The signal was jammed inside the Cave. I guess it’s an urgent one.”Aliongea Akimaanisha kuwa ndani ya lile pango kulikuwa hakuna mtandao ndio maana.

Lakini sasa muda huo huo wakati wakiwa ndani ya eneo hili la msitu , mara mivumo ya gari kutoka upande wa kulia ziliwashataa huku zikija kwa kasi.

“Damn it , Their Backups are here”Aliongea Goodman kwa hasira ,ila kwa upande wa Roma baada ya kuona taa za gari hizo zilizokuwa mita kama mia tatu , alifungua tena mlango na kutoa bunduki aliokuwa ameiweka juu ya Dashboard na kutoka nayo huku akiendelea kupiga simu.

Na dakika cheche mbele Roma aliweza kushuhudia wanajeshi waliokuwa kwenye gari aina ya Pickups kampuni ya Jeep zote zikiwa na mabaka baka ya kijeshi huku nyuma yake walikuwepo wanajeshi , na wawili walionekana kubeba Kombola aina ya RPG huku wakilengesha upande wao.

Roma aliangalia gari ya nyuma na ya mbele na kisha lile bunduki akaliweka Begani na kusogea kwa kupiga hatua kadhaa mbele , na kisha akatoa tabasamu la Kifedhuli.

“Nimemisi sana haya mambo, kwa muda mrefu”Aliongea Roma pasipo kuwa na wasiwasi na Gari iliokuwa mbele yake ilizidi kumsogelea kwa spidi kubwa na ni kama ilikuwa ikitaka kumgonga , lakini Roma aliendelea kuiangalia huku akiweka kisimu chake mfukoni.
 

singanojr

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
569
2,792
SEHEMU YA 178“Swaaaashiii..!!” Ulikuwa ni mlio wa breki uliosikika baada ya gari zote mbili kupiga msele na breki kukanyagwa kwa nguvu na zikasimama na pale pale risasi zikaanza kulindima mfululizo huku nyingi zikigonga kwenye ubavu wa gari na kwenye Dirisha la kioo.

Edna katika Maisha yake yote hakuwahi kushuhudia tukio kama hilo la kushambuliwa risasi mfululiizo , kwa mara ya kwanza kwenye Maisha yake alikuwa kwenye vita, aliishia kuziba masikio yake na kulala chini kwa woga huku akishindwa kuangalia kile kinachoendelea mbele.

Hivyo hivyo kwa Goodman na yeye alikuwa kwenye hali mbaya , licha ya kwamba walikuwa wamefunga vioo vya gari lakini sauti ziliweza kupenya kwa ndani , aliishia kulala chini ili asiweze kushuhudia kile kinachoendelea huku pia akiwa na mawazo ya kutoka kwenye gari na kukimbia , ila ujasiri huo hakuwa nao.

“BOOM’ ulikuwa ni mlipuko mkubwa uliotokea eneo ambalo alikuwa amesimamama mita moja kutoka ilipokuwa gari kiasi kwamba Presha ya Bomu lililorushwa na RPG kurudisha gari nyuma , huku pasipo ya Roma kuonekana kutokana na moshi mzito kutanda.

“Cheeers” Stern na Alice baada ya kushuhudia mlipuko mkubwa waligongesheana glasi zao wakiendelea kufurahia mvinyo, hawakuwa na wasiwasi hata kidogo na kilichokuwa kikiendelea huko nje hakikuwashitua wala kuwafanya kuwa waogope kama ilivyokuwa kwa Edna na Goodman.

Sasa basi wale wanajeshi baada ya kuachia lile bomu kwa kutumia RPG na kulipuka mita kadhaa kutoka lilipokuwa gari , walijikuta wakiacha kufyatua Risasi kwa mshangao , ukweli hawakua wakielewa nini kimetokea , kwani shabaha yao ilikuwa ni kumaliza kila kitu kwa kutumia RPG , lakini sasa Gari walilokusudia lilikuwa halijaguswa kwa maana hio bomu lililipukia njiani jambo ambalo kwa uzoefu wao ni swala ambalo halikuwa likiwezekana hata kidogo.

Wakati wakiendelea kushangaa eneo ambalo Bomu limelipuka na kutawaliwa na moshi mara walianza kushuhudia kivuli cha mtu kikijitokeza katikati ya Moshi na kuwafanya watumbue macho.

“Inawezekanaje hii….”Kabla hajamaliza kuongea alifumuliwa kichwa na wanajajeshi waliokuwa upande wa gari lingine waliinua siraha zao kwa ajili ya kushambulia , lakini walikuwa wamechelewa sana kwani haikueleweka Roma alikuwa akitumia spidi ya uwezo gani , kwani mkono wake ulionekana kama kivuli kikicheza cheza huku Risasi zikitoka mfululizo na hakuna hata Risasi moja iliomkosa mtu tena mbaya Zaidi Alitumia mkono mmoja tu kushika ‘Assault Riffle, waliokuwa ndani ya Gar,i ile wanajiandaa kutoka walikuwa wamechelewa kwani Roma alipiga Risasi tatu mfululizo kwenye Tanki la mafuta.

“Boom , Boom”

Jeep Zote mbili ziliripuka kwa wakati mmoja na kusababisha eneo lote litoe mwanga wa moto mara moja na kurudi katika hali yake huku moshi ukisambaa na Gari zile kutupiwa pembeni ya barabara.

“Haha…”Roma alicheka baada ya kushuhudia mlipuko huo , huku akitupia ile Siraha pembeni na kuingiza mkono wake kwenye mfuko na akatoa simu na kuweka sikioni , na midomo yake ilionekana kucheza cheza ikimaanisha alikuwa akiongea na baada ya hapo aliirudisha simu mfukoni na kurudi kwenye gari na baada ya mlango kufunguliwa Edna alieijiinamia chini aliinua macho kwa woga na baada ya kuona aliefungua mlango ni Roma , alivuta pumzi ndefu ya ahueni , ila Roma hakumjali , alichukua Sigara na kuiwasha na kuvuta kidogo na kupuliza moshi wa sigara nje.

“Nini kinaendelea….?”Aliuliza Goodman baada ya kuona hali imetulia na kuinua kichwa chake na kuwaangalia Alice na Stern waliokuwa wakiendelea na burudani yao.

“Mr Goodman, you looked just like a penguin just now. That’s so adorable. Those people have been dealt with by Mr Roma. Haven’t you noticed up until now?”Aliongea Alice Akimfananisha Goodman na ndege flani wa baharini wanaofahamika kwa jina la Pengwini.

Goodman alijikuta akijionea aibu kwa namna alivyokuwa muoga na alinyanyuka na kuweka suti yake vizuri na kisha akakohoa kidogo.

“Ni vyema kila mtu yupo salama”Aliongea Goodman na wala Stern na Alice hawakumjali.

Roma aliondoa gari kwa spidi huku akiendesha kwa kutumia mkono mmoja,huku mkono mwingine ukiwa umeshikilia Sigara na alikuwa akivuta na kutolea moshi nje na baada ya kutembea umbali mrefu kidogo aligeuza macho yake na kumwangalia Edna na alishangazwa na ukauzu wa mke wake na Edna aliishia kumwangalia Roma kwa macho makali na kisha akageuza macho yake upande wa nje.

“Mke wangu kuna tatizo?”Aliuliza Roma lakini Edna hakujibu na haikueleweka alikuwa akifikiria nini.

Na Roma aligeuza macho yake barabrani na kuendelea kuendesha kwa muda huku akishindwa kujua ni namna gani ya kurudisha hali ya Edna kuwa sawa na waendelee kuongea.

“Edna najua matendo yangu yanaweza yasikuridhishe lakini pia ni mambo mengi hauyafahamu kuhusu mimi mpaka sasa, lakini pia kadiri tunavyoishi unaweza usiridhishwe na matendo yangu , lakinii jambo moja tu kwenye moyo wangu unatakiwa kulielewa ni kwamba siwezi kukuona ukidhurika kwa namna yoyote hio ,nitaishi kwa kanuni hio moja tu , kukulinda kwa namna yoyote”Aliongea Roma ila Edna aliishia kuinua macho juu kama mtu anaehesabu nyota ni kama vile hakuwa amesikia kitu..

“Ule muda wakati tunafikishwa pale nilichoweza kugundua ni kwamba wale Majambazi walikuwa wameshikilia Bunduki G36 Model , Siraha inayozalishwa na kampuni ya Kijerumani inayofahamika kwa jina la Heckler and Coch , Ni ‘Automatic Riffle’ ambayo inaongoza kwa teknolojia kubwa duniani,,Kuhusu Mavazi yao ya kijeshi yale ni mavazi feki tu ambayo yametengenezwa kwa makusudi maalumu na wanaonekana kuwa ni magaidi, na linapokua swala la magaidi mara nyingi wanapigana kufa na kupona hivyo usipo wahi wewe kuua watakuua wewe, Hawa ambao wametushambulia sasa hivi walikuwa wamejificha njiani kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na nilikuwa nishafahamu mtego wao tokea tunatoka pale hivyo kusimamisha gari psikutaka kuingia kwenye mtego wao na pia nilitaka kuwasaidia wenzetu ,japo sijui nia zao , lakini nahisi wanachokifanya ni kuteka matajiri ambao wamekuja ndani ya Paris kwa ajili ya kuhudhuria maonyeshi ya wiki ya Fasheni yanayofanyika kila mwaka.”Aliongea Roma kwa kujielezea , aliona aimize ahadi yake ya kueleza kila kitu anachokifanya, Edna alijikuta baada ya kusikia maelezo hayo kugeuka na kumwangalia Roma.

“So ulivyoniona na piga simu nilikuwa nikipigia Polisi, tusingeweza kuwatoa watu wote pale na isitoshe usafiri haukuwepo na ingekuwa hatari Zaidi na kwasababu polisi washasikia mlipuko watakuja mara moja , lakini uzuri ni kwamba nishamaliza magaidi yote”Aliongea.

“Lakini si lazima watachunguza namba yako baada ya kukuta vile vifo cya majambazi?”Aliuliza Edna.

“Hawawezi kwasababu sijatumia mtandao wa simu wa kawaida kuwasiliana nao , bali nilitumia namba maalumu inayoweza kufanya mawasiliano kwa kupitia Satilaiti”

“Mambo unayofanya yanaogopesha na kufanya tuwe na wasiwasi”

“Bebi Wife ijapukuwa nimekuambia nitaripori kila kitu , lakinni pale hakukuwa na muda”Aliongea Roma akirudi kwenye hali yake ya kawaida na kumfanya Edna atabasamu , kidogo alijisikia vizuri baada ya kupata maelezo kwa Roma huku akigeuka pembeni , lakini wakati huo huo Roma kwa kutumia mkono mmoja alimgusa Edna kwa kuweka mkono kwenye paja lake na kumfanya Edna amwangalie Roma na kuutoa mkono wake huku akiona aibu za kike.

“Unafanya nini …”Aliongea Edna , ila Roma hakumzingatia.

“Mke wangu angalia ndio tunaingia mjini,unataka tukale nini usiku wa leo ,Mcdonald , Wendy`s au Burger King unapendelea Fastfood zipi , Tupo Paris lazima tujaribu aina ya vyakula vya nchi hii”Aliongea Roma na kumfanya Edna aone Roma anapotezea topiki kwa kitendo alichokifanya.

“Ulijuaje haya maneo lakini?”Aliuliza Edna baada ya kupata ahueni sasa baada ya kuona jiji.

“Nia yao wale watekaji ilikuwa ni kutuchanganya na kabla ya kutupeleka kule msituni walikuwa wakituzungusha zungusha ili tukose uelekeo , ila kwangu mimi hilo haliwezekani hata kidogo , nililikalili kila sehemu tuliopita na isitoshe ramani yote ya dunia ipo kichwani , hivyo baada ya kusikia sauti za kutiririka kwa maji ya mto niliweza kufahamu uelekeo”

“Kwanini nahisi kadiri unavyoeleza ndio najikuta sielewi”Aliongea Edna na kumfanya Roma atabasamu.

“Njia rahisi ya kuelewa , wewe nichukulie kama mnyama tu”

“Acha kuongea upuuzi”Aliongea Edna kwa kufoka na kumfanya Roma atulie.

“Wengine wanaweza kukuona kama mnyama , lakini mimi siwezi kukuona hivyo , hivyo usitamke tena neno myama mbele yangu”

“Bebi kumbe na wewe ni mjinga”

“Wewe ndio mjinga”

“Ndio mimi ni mjinga na wewe ni mjinga , hivyo sisi ni wajinga wote”Aliongea Roma.SEHEMU YA 178Upande mwingine ndani ya nyumba namba Kumi na tatu ndani ya mtaa wa makazi ya viongozi mbalimbali ndani ya Paris , ilionekana familia iliokuwa na watu watatu waliokuwa kwenye meza wakipata chakula cha usiku, akiwemo mtoto mdogo aliekuwa na nywele za kujikunja kunja , mwenye umri kimakadirio ya miaka kumi , huku wakimulikwa na mwanga wa taa hafifu , huku mlio wa Uma Pamoja na kugongana kwa vijiko na sahani ukisambaa ndani ya eneo lote.

“Dad, can we go to Disneyland on Sunday? Many of my classmates have already been there”

“Baba tunweza Kwenda Disneyland siku ya jumapili ? Wanafunzi wenzangu wengi ninaosoma nao washawahi Kwenda”Aliongea yule mtoto huku akimwangalia baba yake

“Harry usiwe mjinga , Baba yako yuko bize na kazi”Aliongea mwanamama aliekuwa amevalia sweta Langi ya majivu

“Harry baba yako niko bize na kazi , ila ndani ya mwezi huu nitahakikisha nakupeleka DisneyLand sawa?”

“Lakini baba huwezi kuwa huru na kazi siku zote”Aliongea huku akiangalia chini kwa huzuni , lakini muda huo huo simu ya mwanaume ilianza kuita na yule mwanaume aliipokea na kuanza kuongea kwa kifaransa

“Fodessa hapa, nini tatizo?”

“Chifu tumeweza kupata ripoti kutoka kwa polisi na wameeleza kwamba matajiri ambao tulikuwa tukiwatafuta kutokana na kutekwa wamepatkana ndani ya msitu wa Rommilly Seine, na utararibu wa kuwaokoa ulifanikiwa kwa asilimia mia moja , lakini kwa maelezo ya polisi ni kwamba kuna mtu ambaye hajafahamika mpaka sasa ndio katoa taarifa kwa polisi juu ye eneo husika”

“Wameweza kugundua wahusika ni wakina nani waliofanya utekaji?”

“Kama ilivyokuwa matarajio yetu Chifu , Inasemekana ni Jeshi linalomilikiwa na Appolo ,Golden Sun Totem”Ilisikika sauti na kumfanya Fodessa kumgeukia mke wake kwa muda.

“lakini Chifu , tulijaribu pia kutafuta taarifa Zaidi kupitia Tatoo za watekaji na tumeweza kupata taaarifa zingine”

“Taarifa gani?”

“Tumeweza kugundua majambazi sio wanajeshi wa kundi Golden Sun Totem , bali ni kundi la kigaidi linalofahamika kwa jina la Inferno”

“Inferno!!? , hilo kundi si lishakufaga zamani?”

“Hata sisi tulifikiria hivyo Chifu , lakini kwa taarifa tulizoweza kukusanya , zinaonesha viongozi wa juu walioangamizwa na serikali ya Canada walikuwa ni feki”

“Noted , Wahakikishieni ulinzi mzuri hao mateka ili wasilete shida usiku huu na kufanya mambo kuwa magumu mpaka uchunguzi wetu ukamilike , nakuja sasa hivi, Ila vipi Depney analifahamu hili?”

“Ndio alietuambia tukupigie simu kufatilia kila kitu”

“Okey nakuja”

““Dear, what’s wrong?”Aliuliza kwa Kingereza mke wa Fodesa ana kumfanya bwana huyu ambaye ashaanza kupiga hatua kuelekea upande mwingine wa vyumba asimame na kumwangalia.

“Don’t worry, it’s nothing much. I will be back real soon. Continue with the meal, I have to go now.”Aliongea na kisha akapotelea na kumfanya mke wake amwangalie Harry kwa huzuni , alijua kazi ya mume wake ilikuwa ngumu kiasi cha kumpelekea kuwa bize muda wote , lakini alishindwa kuelewa kwanini kila siku anakurupushwa na kurudi kazini kiasi cha kupelekea mtoto wake kukosa muda wa kukaa nae karibu.

******

Mpaka Roma anakwenda kusimamisha gari ndani ya hoteli ya Sofitel Edna alikuwa ashalala muda mrefu, na Roma ndio aliemumsha.

“Wife tushafika”Aliongea Roma na kumfanya Edna aangalie nje na kushuhudia walikuwa ndani ya uzio wa hoteli hii ya kisasa ya nyota tano, Sofitel Hotel..

Gari yao ilikuwa imechafuka kwa vumbi kwelikweli huku ikiwa pia ni michubuko iliosababishwa na kugongwa na Risasi na kufanya wafanyakazi wa hoteli hii kushangaa.

Goodman ndio aliekuwa wa kwanza kuingia ndani kabisa ya hoteli eneo la mapkezi , huku Edna na yeye akifuatia huku akimuacha Roma Nje ambaye alikuwa akipaki gari Pamoja na kutoa mkoba wa Edna.

Lakini sasa baada ya Roma kuusogelea mlango wa kuingilia ndani , mara gari tatu za polisi zilizokuwa kwenye spidi ya hali ya juu zilisimama ndani ya hoteli hii na wakashuka Polisi wenye miili iliojengeka kimazoezi , wote wakiwa wanaume na kumfanya Roma asimame kwanza na aangalie gari hizo.

Na muda ule ule na Gooman aliekuwa eneo la mapokezi alitoka nje kuangalia ni hali gani inaendelea baada ya kusikia Ving`ora vya gari za polisi,

Moja ya Polisi Mzungu mwenye mwili mkubwa kidogo kuliko wenzake , baada ya kumuona Roma , alimsogelea huku akiweka tabasamu usoni

“Are you Mr Roma Froma Tanzania?”Aliuliza yule mzungu baada ya kumfikia. Lakini Roma alijikuta akimgeukia Goodman na kumwangalia kwa sekunde , aliamini huenda ndio kawaambia polisi kwa simu.

“Mr Roma, I didn’t make a report to the police. I really know nothing at all”Aliongea Goodman kwa kujitetea akimaanisha kwamba hakupiga simu polisi na hana anachokijua.

“I am. Is there anything I can help you with?”(Ndio mimi kuna ambo lolote naweza kuwasaidia) Aliuliza Roma.

“I’m Bolton from the anti-terrorism group in the Paris police department. We have reason to believe that Mr Roma is heavily involved in the kidnap and murder cases which had taken place near Romilly-sur-Seine around two hours ago”

“Naitwa Bolton kutoka kikosi cha polisi zidi ya ugaidi , tunazo sababu za kuamini kuwa Mr Roma umehusika na utekaji Pamoja na mauaji yaliofanyika ndani yam situ wa Romilly-sur-Seine masaa mawili yaliopita”Aliongea yule polisi na kisha akampa ishara polisi wenzake na kumpatia karatasi.

“Hiki n kibali Mr Roma , na unapaswa kuongozana na sisi mpaka kituoni kwa ajili ya kutusaidia katika uchunguzi”Roma alijikuta akiangalia polisi hawa wanne ambao walionekana kuwa tayari kwa lolote , kwani kwa namna walivyokuwa wakimwangalia ni kama walikuwa washathibitisha kama yeye ndio jambazi.

“Officer Bolton, would you just excuse me for a minute? I have some private matters to take care of. You’re causing a huge commotion here which will terrify everyone.”

“Afande Bolton naomba uniruhusu kwa dakika kadhaa , nina jambo binafisi la kushughulikia ili tusisababishe mtafaruku kupekea kumtisha kila mtu hapa”Aliongea Roma.

“Tutafanya kile tunachopaswa kufanya Mr Roma , tukio lililotokea kule msituni sio la kawaida na tunajihadhari zidi yako, kama utataka kuita mwanasheria tutaomba ukalifanyie hilo baada ya kufika kituoni”Aliongea Afande Boltoni na kuwapa ishara wenzake, na pale pale polisi waawili walimsogelea Roma na kumshika kulia na kushoto kwenye mikono , baada ya Roma kukabidhi mkoba wa Edna kwa Goodman.

“Subiriini… Nini kinaendelea?”Aliuliza Edna alietoka harakaharaka baaada ya kushuhudia Roma akiwa amesimama na polisi na alihisi kulikuwa na jambo ambalo alikuwa sawa.

“Edna hatuwezi kuwazuia , wanachokibali tayari cha kumkamata Roma , nahisi wamemshuku kutokana na tukio la kule msituni , tunachotakiwa ni kutaftuta mwanasheria na kumtuma”aliongea Goodman akimzuia Edna kwa kumshika.

Roma alimwangalia Edna na kisha akamkonyeza na siku zote Edna alikuwa akielewa Roma akimkonyeza ilimaanisha asiwe na wasiwasi , lakini licha ya hivyo bado alikuwa ni mwenye wasiwasi na tukio hilo , lakini kwa wakati huo alishindwa kufanya lolote na Polisi walimwingiza Roma kwenye gari na kisha likaondolewa.

“Goodman nitafute mwanasheria namba moja ndani ya jiji hili la Paris , nataka kabla ya asubuhi Roma awe ashatoka Polisi”Aliongea Edna huku akiangalia Gari zinazotokomea kwenye mataa ya jiji hili.

“Edna wala usijali ninajua mwanaesheria namba moja ndani ya Paris na kazi ataifanya vizuri na nina uhakika kabla ya asubuhi atakuwa hapa, Kwasasa unapaswa kupumzika na mimi nitashughulika na kila kitu”Aliongea Goodman na Edna ilibidi atii , kwani hakuwa mwenyeweji ndani ya Paris hivyo alimtegemea Goodman, lakini hata alivyofika kwenye chumba alijihisi moyo wake kuwa mzito kweli huku kichwa chake kikimuwaza Roma tu. Alijiambia kama ingekuwa ni Tanzania angepiga simu tu na Roma angeachiwa , lakini sasa hivi alikuwa ndani ya Paris taifa ambalo hana koneksheni.,wala nguvu yoyote.

Upande wa Roma alikuwa akiwapigisha Stori mapolisi kwa kifaraqnsa huku akiwaambia ameona moja ya msichana mrembo pembeni ya barabara na amempenda kweli na kufanya polisi hawa washndwe hata kumjibu na kumwangalia tu, Roma hakuonyesha wasiwasi.

Ndani ya Robo saa Roma aliweza kufikishwa ndani ya Ghorofa ambalo ndio makao makuu ya jeshi la polisi, walimfunga pingu na kisha wakamtoa na kumuongoza moja kwa moja ndani , licha ya kuwa usiku , lakini taa za vyumba vya jengo hili la polisi zilikuwa zikiwaka , ikimaanisha kuwa wapo watu wanaendelea na majukumu.

Baada ya Lift kujifunga , Bolton hakubonyeza vitufe ambavyo vilikuwa vikiashiria Floor , bali alibonyeza upande mwingiene ambao ulikuwa na ‘Keypand’ ya namba na Boltoni alibonyeza namba kama vile anaingiza Pasword ambazo Roma aliweza kuzikariri mara moja na kuishia kutabasamu na Lift haikuelekea juu Zaidi ya Kwenda chini Ardhini.

“Officer Bolton, I didn’t know this station had an underground base”Alishangaa Roma baada ya kugundua hili jengo lina eneo la Ardhini lililojengewa , lakini Bolton hakumjibu Zaidi ya kumwangalia kwa sekunde

“Mr Roma, you’re impressively calm indeed, but you’re speaking a bit too much.”

“Mr Roma huna wasiwasi kabisa na inafurahisha , lakini unaongea sana”Aliongea Bolron lakini muda huo Lift ilifunguka na kumfanya Roma ashangae namna eneo hilo lilivyojengewa , huku likipendezeswa na Mwanga wa LED , kiasi cha kufanya eneo hili kuonekana kama vile unaangalia Muvi za kisayansi.

Roma aliweza kupiga macho kila kona haraka haraka , aliweza kuhesabu Camera zote zilizofungwa , huku akiangalia Skrini zilizowekwa ukutani huku zikionesha Data zinazopanda na kushuka , lakini pia aliweza kushuhudia mpangilio wa vyumba ulivyojengwa na kufanya eneo hili kuliona kama vile ofisi za CIA au FBI.

Kwa jinsi muonekano wa hapa ndani uliashiria ukubwa wa taifa la Ufaransa .

Roma alitembezwa kwenye Korido mpaka pale Boltoni alipokuja kusimama kwenye mlango wa chumba ambao pembeni yake ulikuwa na sehemu ya kuweka kiganja cha mkono kwa ajili ya kufungua na alifanya hivyo na ndani ya dakika tu mlango ukafunguka na akamwambia Roma aingie.

Kilikuwa ni chumba kikubwa kilichotengenezwa kwa kupakwa rangi ya Samawati kwanzia sakafuni mpaka juu , huku mbele karibu na mlango kukiwa na kioo kikubwa , lakini pia chumba kilikuwa na Kamera kila kona , na katikati kikiwana meza na viti vinne , Na Roma aliweza kutambua kuwa hapa ni ‘Interrogation Room.

Roma alisogezwa na Bolton mpaka kwenye meza , huku Roma akimwangalia mwanaume mwenye nywele nyeupe alieketi kwenye kiti, akiwa bize na kuangalia karatasi zilizokuwa kwenye meza.

Reporting to Deputy Chief Director, the suspect Roma Ramoni has been brought for questioning”

“Nikiripori kwa Chifu kiongozi , Mtuhumiwa Roma Ramoni amefikishwa kwa ajili ya kuhojiwa”

“Thanks, Bolton.”Alijibu huku akimpa ishara Roma ya kuketi.SEHEMU YA 179

Roma aliefungwa Pingu alisogea na kisha akavuta kiti na kisha akaketi na kumfanya Makamu Chifu Kiongozi kumwangalia kwa namna ya kumchunguza mwili wake , ni kama alikuwa akimhusisha muonekano wake na tukio na aliweza kuona misuli ya Roma na kuona mtu aliekuwa mbele yake sio wa kawaida na anao muonekano wote wa Kigaidi.

“Sidhani kama Mr Roma ushawahi kutusikia hapo kabla ,sisi ni Kitengo cha usalama wa taifa DGSE lakini pia tunafahamika kama Ofisi namba saba , Naitwa Afande Fodesa , mimi ni Naibu Chifu Kiongozi ndani ya Idara hii, na Boltoni aliekuleta hapa ni msaidizi wangu katika kitengo cha ‘Special Forces’ cha kupambana na ugaidi”Aliongea Fodesa na kumfanya Roma atingishe kichwa kuashiria kuelewa, ndio alikuwa akifahamu vyema sana kuhusu Ofisi Namba saba na historia Nzima ya kuanzishwa kwake na Charles De Gaullie Shujaa aliepigana ndani ya Vita vya pili vya Dunia.

DGSE haikuwa kubwa sana kama vile CIA ,KGB, MOSSAD au Kikosi cha Dhoruba nyekundu kinachomilikuwa na Zeros Organisation.

“Sikufahamu , lakini kuhusu hii idara yenu nishawahi kuisikia”Aliongea Roma.

“Very Nice kama ushawahi kuisikia”Aliongea Fodesa na kisha alitoa picha iliokuwa kwenye mfuko wa shati na kisha alimsogezea Roma kwenye Meza.

“Mr Roma niambie kama ushawahi kuona hio picha , au unaitambua?”Aliuliza Fodessa”

******

Upande mwingine ndani ya hoteli ya Sofitel, baada ya Goodman kuhakikisha Edna kashaingia kwenye chumba chake na yeye alipiga hatua na kufungua mlango wa chumba alichochukua na kisha akavua koti na kulitupia kwenye Sofa na kisha akalegeza tai na baada ya hapo alijibwaga kwenye sofa na kufumba macho kwa dakika kadhaa huku akivuta pumzi nyingi kwa dakika kadhaa na kisha akayafumbua na kuangalia bahasha ya Khaki iliokuwa juu ya meza na kuichukua na kisha kuifungua.

“Marriage Certificate Copy’ Edna Adebayo and Roma Ramoni’ Ndio maneno yalionekana juu ya karatasi ambayo Goodman aliitoa kwenye hio bahasha na kuishikilia mkononi , huku akimalizia na kukung`uta bahasha na picha mbalimbali zilitoka na kujifunua juu ya meza na hapo ndipo zilipo onekana picha za Roma na Edna , picha ambazo zilipigwa kipindii Edna na Roma walipoenda kujiandikisha ndoa yao.

“Edna unajifanya mjanja sio , unajifanya nisingejua kuwa Roma ni mumeo na mmefunga ndoa kwa Zaidi ya miezi miwili sasa , Unafikiri nitamuogopa kisa anajua kuua …. Eti unitafutie Mwanasheria ..Haha.. na hakika lazima nimtafute , na nitahakikisha huyu mbeba mizigo wako kwanzia siku ya kesho humuoni tena nitahakikisha anafungwa miaka mingi Gerezani“Aliongea Goodman kinafiki huku akiweka karatasi kwenye meza na kisha akachukua simu yake na kutafuta namba na baada ya kuipata aliweka simu sikioni.

“Mr Goodman , ni muda wa mapumziko huu”Ilisikika sauti upande wa pili

“Lawyer Charmo, my friend has been brought to the police station around ten minutes ago. I need you to help me do something for him”Aliongea Goodman akimaanisha kwamba ana rafiki yake alieshikiliwa polisi na anahitaji afanye jambo.

“Aah .. Nilijua unanipigia kwa ajili ya mambo yetu yale , kumbe ni juu ya kazi , basi hii ni taarifa nzuri , niambie jina lake nitaelekea kituo cha polisi”

“Anaitwa Roma Ramoni ni Mtanzania , Kesi ya mauaji”

“Goodman , haijalishi ana kesi ya aina gani , kwasababu ni rafiki yako mpaka asubuhi atakuwa ashatoka, Mimi ndio mwanasheria namba mojda ndani ya Paris hii yote, Charmo kama Charmo no more Charmo”

“Mr Charmo nadhani umenielewa vibaya, sijasema nataka atoke”

“Sasa kama hutaki atoke unataka nikafanye kazi gani sasa?”

“Nataka unisaidie kuhakikisha anaozea jela , nafikiri sio kazi kubwa sana kwako Charmo na isitoshe mtu mwenyewe ni wa kawaida sana kutoka nchi masikini kama Tanzania , aliekamatwa ndani ya jiji la Paris kwa mauji na isitoshe ashakamatwa na polisi tayari ni wewe tu kuingizia mbinu zako za kisheria”

“Aaah ,, Goodman wewe ni moja ya wateja wazuti sana, hilo ni swala Dogo”

“Hakikisha huachi alama yoyote na kumbukma sihusiki na hili swala”

“Usijali Mr Goodman, kazi yako hesabu ishaisha”Aliongea na kisha Goodman akakata simu.

Upande mwingine ndani ya chumba cha mahojiano , Roma alionekana kushikilia picha ambayo ilikuwa ikionyesha nembo,Sun Gold Totem ya wale majambazi waliokuwa wamewateka na Roma aliweza kugundua picha hio ilikuwa imepigwa kutoka kwenye sare za moja ya wale magaidi aliowaua.

“Nadhani mpaka sasa mshafahamu kuwa mimi ndio nilipiga simu?”Aliuliza Roma , kwani mpaka hapo alikuwa hana cha kuficha , licha ya kwamba alitumia mawasiliano ya satilaiti , lakini jambo ambalo alitegemea ni kwamba watu ambao walikuwa wanahusika na kesi hio walikuwa ni polisi wa kawaida tu ndio maana alikuwa na uhakika kwamba wasingeweza kumpata , lakini sasa kilikuwa ni kitengo cha usalama wa taifa, kitengo kilichokuwa kikitumia teknolojia kubwa , hivyo aliamini mpaka hapo wangekuwa na taarifa zake.

“Kama ni hivyo basi naamini Mr Roma wewe sio mhusika?’

“Ndio mimi sio mhusuika , ila mimi ndio niliwaua magaidi wote ndio nikapiga simu”Aliongea Roma na kumfanya Fodesa kukosa utulivu , kwake kitendo kilichofanyika kilikuwa ni cha kushangaza kwani wanajeshi wa kundi la Inferno walikuwa ni wengi mno na pia alikuwa akijua uwezo wao wanapoingia katika mapambano , lakini vifo vyao kwa namna ambavyo waliweza kufa , ilishangaza kama swala hilo linaweza kufanywa na mtu mmoja pekee.

“Mr Roma kama kweli wewe ndio uliowaua , ukizingatia na giza , nadhani naweza kusema kwamba wewe ni mtu hatari sana”

“Maneno yako yanaweza kuwa sahihi , lakini tukiongelea kwa mtazamo wa kisheria mimi sina kosa maana nimeua wakati wa kujilinda hivyo naamini Afande Fodesa huwezi kuniweka kwenye kundi la wahalifu na unapaswa kuniachia niondoke”

“Mr Roma kila Raia anayohaki ya kujilinda likitokea tatizo kama hilo , lakini hata hivyo kutokana na huu wezo wako tunakuwa na mashaka na tunaamini kabisa huenda ukawa pia ni moja ya magaidi na isitose pia tuliweza kufatilia taarifa zako na zilituletea shida sana kuliko wanajeshi hawa wa kundi la Inferno”

“Kwa hioo Afande unapanga kufanya nini zidi yangu , maana mpaka sasa hakuna ushaihidi wowote na nadhani unaelewa kuwa sheria haziruhusu kumzuia mtu kituoni kwa muda mrefu kama hakuna ushahidi wa kutosha”Aliongea Roma lakini wakati ule ule Boltoni aliekuwa amesimama pembeni simu yake ya upepo ilianza kuita na aiinyanyua na kusikiliza kwa dakika na kisha akamgeukia Fodesa.

“Chifu ni Mwanashria Charmo kutoka Gordon Law Firm”Aliongea Bolton na kumfanya Fodesa kutingisha kichwa , lakini muda huo huo mlango ulifunguliwa na kumfanya aangalie mlangoni na Depney alionekana akiingia,huku akionyesha wasiwasi kwenye uso wake na alionekana alikuja hapo kwa haraka sana , lakini muda huo huo alivyoona Roma kafungwa na Pingu alizidi kuonesha wasiwasi.

“Director ….” Lakini kabla hata hajamaliza kuongea alikuwa ashafikiwa na kushikwa tai na kunyanyuliwa juu kwa nguvu na Depney na kumfanya Boltoni kushangazwa na tukio hilo.

“Wewe mwanaharamu , unanitafutia nini matatizo , nani kakuambia ukamate kamate watu pasipo ruhusa yangu?”Aliongea kwa hasira

“Director ulinipa majukumu ya kufanyia kazi kesi hii ya utekaji na tulifanikiwa kugundua Roma ndio aliehusika na kupiga simu polisi na nilivyomhoji kakiri kwamba ndio alioua watekaji , Director ume..”

“Kwahio kukupa jukumu hili ndio unataka kunisababishia matatizo , kwanini kila unachofanya kinafanya mimi nafokewa na wakubwa na kutishiwa kuondolewa kwenye nafasi yangu , nahisi unanifanyia makusudi”Aliongea na kisha akamsukuma.

“Mr Roma naitwa Depney , nitangulize kuomba radhi , kwa kitendo cha kukamatwa na huyo mpumbavu , tafadhari sana usimjali”Aliongea Depney baada ya kumsogelea Roma.

“Usijali sana Afande Depney , Fodesa yupo kwenye majukumu yake ya kazi na alichokifanya sio kosa”Aliongea Roma huku akisimama.

“Asante sana Mr Roma kwa kuelewa , nitakufungulia sasa pingu”

“Haina haja naweza kuzifungua mwenyewe”Aliongea Roma na pale pale akavuta zile pingu na zika katika katikati na kudondoka chini na kumfanya Depney kutoa macho. Na sio yeye tu hata kwa Fodesa na Bolton walishangaa.

“Mr Roma naomba unifuate nikusindikize mpaka nje”Aliongea Depney lakini Fodesa akawazuia.

“Director licha ya kwamba unacheo kikubwa , lakini haimaanishi unaweza kumtoa mhalifu ndani ya hiki kituo..”

“Fodesa usinianze..”Aliongea kwa kumkata jicho na kisha alitangulia mbele na wakatoka kabisa moja kwa moja na kuingia kwenye Lift , Roma alijikuta akutabasamu baada ya kujiona yupo huru , kwanza hakuwa na wasiwasi , kwani hata kama angeamua kutoka kwa Force angeweza hivyo kwani ingekuwa ni kitendo tu cha kubomoa kituo, lakini hata hivyo alishangaa ni mtu gani ambaye ameagiza kutolewa kwake kiasi cha kumfanya Depney kuwa na wasiwasi mkubwa.

Dakika chache mbele walikuwa nje kabisa ya jengo na Depney alimuongoza Roma mpaka kwenye gari aina ya Roll Royce iliokuwa imesimama huku wanaume wawili waliokua, wamevalia suti wakiwa wamekaa kulia na kushoto kwenye gari, Baada ya Roma kuifikia tu , kioo kilishushwa na hapo hapo akamuona mzungu mmoja aliemfahamu na kumfanya atabasamu.

“Ndio maana Depney alikuwa na wasiwasi , kumbe ni Edward kutoka Rothchild family”Aliwaza Roma huku akiangaliana na yule mwanaume aliekuwa ameachia tabasamu kama lote.

Ndio alikuwa ni Edward binamu yake na Profesa Clark aliekuwa akitokea kwenye familia yenye nguvu ndani ya bara la ulaya na duniani kote ? Rothchild family.

“Hades hatujaonana muda mrefu tokea urudi Tanzania , hebu ingia kwenye gari”Aliongea Edward na Roma alifungua mlango na kuzama kwenye Gari, lakini ni kama vile alikuwa akisubiriwa , kwani ile anaingia tu na kukaa mwanamke mrembo alimvaa mdomoni akitaka kumkisi.

“Catherine!”Alishangaa Roma kwani hakutarajia kumuona Malkia wa Wales kuja mpaka hapo.SEHEMU YA 180

Ni muda wa saa moja kamili za jioni gari tatu aina ya Range Rover Sport rangi nyeusi zilionekana ndani ya Bagamoyo Road zikipita eneo la Mbuyuni zikiwa kwenye mwendo zikielekea Tegeta , mbele kulikuwa na gari ambayo ilikuwa na wanausalama na katikati ilikuwa ni gari aliopanda mheshimiwa mwenyewe Senga, na siku hii hakuwa amevalia suti kama ilivyozoeleka akitoka ikulu, bali hapa alikuwa amevalia koti rangi nyeusi, suruali ya Jeans rangi ya Bluu Pamoja na Raba za Nike, huku machoni akiwa amevalia miwani ya jua , kwa jinsi alivyoonekana ni kama alikuwa kijana, watu wengine ambao walikuwa kwenye gari yake ni Kabwe, ambaye ni Komandoo lakini pia msaidizi wa karibu wa Mheshimiwa , Pamoja na Bodigadi na wote walikuwa kwenye mavazi ya kawaida , lakini pia hata gari zao zilikuwa zimebadilishwa namba na kuwekwa za kawaida na hio ilikuwa ikifanyika mara nyingi sana kila Mheshimiwa anapotoka pasipo kutaka kuonekana au kutambulika.

Gari zilitembea huku ukimya ukitawala kwenye gari , mheshimiwa alikuwa akiangalia upande wa nje huku akionekana kuwa kwenye mawazo mengi , alikuwa akiwaza ni jambo gani ambalo baba yake alikuwa akitaka kumwambia mpaka kumtaka aende nyumbani , licha ya kwamba baba yake alipompigia simu , alimwambia aende kumsalimia lakini siku zote akisikia kaulu ya aina hio ni kwasababu kuna maagizo muhimu sana ambayo baba yake anataka kumueleza.

Dakika chache mbele kutokana na mwendo waliokuwa wakitumia , waliweza kufika Tegeta na sasa walikuwa wakiingia Tegeta Kibaoni.

Upande mwingie ndani ya eneo la Bunju A ilionekana gari alina ya Semi-Trailler ikipiga mwendo kuelekea Dar , kwa mwendo wa kawaida kabisa huku ikionekana kuwa na mzigo mzito kweli, Gari hii yenye kichwa cha Rangi nyeupe iliendelea kusonga taratibu.

Upande wa Dereva alionekana Noriko Gumila akiwa ameshikilia Usukani huku akiwa na sura isiokuwa hata na Chembe ya huruma , Pembeni yake alionekana Dereva ambaye hakuwa akijitambua na ilionekana Noriko Okawa alikuwa amemzimisha na kisha akachukua udereva yeye , na kwa jinsi alivyokuwa akiendesha dhamiria yake ilionekana kuwa wazi kabisa na alionekana kufahamu kuwa ndani ya madakika machache gari ya mheshmiwa itamfikia.

Gari ya Noriko Okawa iliokuwa ishapita Bunju A, ilionekana kwenye mwendo na gari tatu za msafara wa mheshimiwa Raisi Senga , pia zilionekana zikiwa kwenye mwendo zikiwahi Bagamoyo kata ya Kerege, yalipo makazi ya Afande Kweka.

Sasa Ile Noriko anakaribia ndani ya eneo la Boko Magengeni , akiwa makini na usukani wake kuangalia mbele alijikuta akipatwa na wasiwasi baada ya kuhisi ukinzani wa Nguvu za ziada ndani ya eneo la Karibu na kumfanya akose utulivu, lakini bado hakutaka kuogopa , misheni aliopewa na Mheshimiwa Kamau , alitakiwa kuitimiza kwa namna yoyote ile.

Dereva aliekuwa akiendesha gari aina ya V8 iliokuwa mbele kabisa katika msafara huu wa Gari tatu za Mheshimiwa Senga , aliweza kuiona Semi Trailler ya kampuni ya Swift Transit , iliouwa mbele yake ikija kwa spidi , lakini kwakua ilikuwa kwenye nafasi yake , hakupatwa kabisa na wasiwasi na yeye aliendelea kutembea kwa spidi ile ile.

“Kwiiiiiii…..,,,Ckreech”

“Sh**t”Aliropoka Gumilla huku akiangalia kwenye Kioo Msafara wa Gari za Mheshimiwa Senga zikitokomea kwenye macho yake na kujikuta akipiga piga usukani kwa hasira

Hakuelewa ni nini kilitokea , lakini Gari ilizima na Breki kujifunga zenyewe kiasi cha kumpelekea kutotimiza azima yake ya kuligonga Gari la Mheshimiwa Senga na mpaka muda huo aliamini kuna nguvu ambayo haikuwa ya kawaida iliokuwa mita kadhaa kutoka alipokuwepo yeye , siku zote Mchawi humtambua Mchawi mwenzake kutokana na Nguvu zao za kilozi na hii ndivyo ilivyokuwa kwa Gumila aliweza kuhisi mtu mwenye uwezo kama wake.

Baada ya kama dakika tatu kupita Gari ilirudi katika hali yake ya kawaida na kumfanya Gumilla atoe tusi m mpaka muda huo alikuwa tayari kwa ajili ya kupambana , kwani aliamini mtu aliemzuia kutotimiza azma yake , alikuwa ni Adui yake namba moja , na hivyo anatakiwa kupambana nae kwa kumfelisha.

Gumillah alimgeukia dereva na sijui alimfanyia nini na palepale Dereva akaashituka huku akiangaza angaza kulia na kushoto kama mtu aliekuwa amechanganyikiwa , lakini ajabu hakuona mtu kwenye siti ya Udereva na gari ilikuwa ikiendelea kusonga mbele na palepale akili yake ikarudi na kurukia usukani na kuiongoza gari.

Mita mia moja kutoka Bunju B , kwenye Daraja ambalo lilikuwa likitenganisha mkoa wa Dar Es salaam na Mkoa wa Pwani, alionekana Gumillaha akiibuka kama jini na kukanyaga mchanga mwingi uliokuwa chini ya Daraja huku akizungusha kichwa chake kulia na kushoto.

“Jitokezee”Aliongea kwa hasira kwa lugha ya kijapani huku bado akiendelea kuzungusha kichwa chake kulia na kushoto, ukweli ni kwamba alikuwa akihisi uwepo wa mtu ndani ya hili eneo , lakini jambo ambalo linamshangaza ni kwamba licha ya kwamba adui yake alikuwa naye ndani ya eneo hilo , lakini alishindwa kumuona na kujiuliza Adui yake anatumia njia gani kujificha.

“Gumillah Rudi ulikotoka , mimi sio saizi yako”Ilisikika sauti ya kike ikigonga kwa namna ya Mwangi kwenye masikio ya Gumillah , Sauti ambayo alikuwa akiisikia yeye tu , kutokana na ‘Frequency’ zinazotumika kuwa nje ya uwezo wa Binadamu kusikia.

“Siondoki mpaka nihakikishe kifo chako , kwa kunifelisha Misheni yangu”Aliongea Gumillah kwa Kijapani.

“Hahaha..Hahaha…Unafikiri unaweza kupambana na mimi?”

“Acha kujificha wewe Malaya , unaniogopa ndio maana hujitokezi”

“Kama unavyotaka nitajitokeza”Ilisikika sauti kwenye masikio yake huku akijipanga kupigana , lakini alivyoangalia mbele alijikuta macho yakimtoka.

“Zenzhei!!!!”Aliita kwa sauti baada ya kumuona mtu anaemtambua , akiwa mita kadhaa kutoka aliposimama , licha ya eneo hili kuwa na giza , lakini kwa kutumia uwezo wao aliweza kumuona mwanamke mrembo aliekuwa mbele yake.

Ndio alikuwa ni Zenzhei mlinzi wa Afande Kweka , lakini hapa akiwa na utofauti kidogo kama alivyoonekana siku kadhaa akiwa na Mzee Kweka , alikuwa akionekana kuwa mtu mzima , lakini hapa alionekana kijana kabisa tena mwanamke mrembo , na haikueleweka imewezekana vipi.

“Noriko!!!”Aliiita Zenzhei kwa sauti tamu huku akificha siraha yake kimazingara na hivyo hivyo kwa upande wa Gumillah alificha Upanga wake Kimazingara huku ile sura Ngumu aliokuwa nayo Gumillah ikipotea na sasa aliweza kuonekana kuwa mwenye sura ya kawaida ya Kijapani na palepale walisogeleana na kukumbatiana… Lilikuw ani tukio la Ajabu kufanyika na ilionekana walikuwa wakifahamiana.

“Zhenzei nilikutafuta Zaidi ya miaka sabini sasa”Aliongea Noriko Gumillah kwa Lugha ya Kijapani na kumfanya Zenzhei kutoa machozi na kumwangalia Gummillah na wakakumbatiana tena.

Upande mwingine ndani ya jumba la Kifahari alilokuwa akiishi Afande Kweka , alionekana Raisi Senga akiwa ameketi ndani ya chumba cha kujisomea cha Baba yake , huku pia Mzee Kweka akiwa ameketi kwa mtindo wa kuangaliana na Mwanae Senga.

“Senga !, Blandina na Denisi wote wapo hai”

“ Baba unasema nini!!!?”

“Namaanisha hivi mtoto wako Denisi yupo hai , vile vile Blandina mama yake Denisi yupo hai”Aliongea Raisi kweka pasipo kuwa na wasiwasi kabisa na hii ni baada ya lisaa moja kupita tokea Senga aingine hapo ndani.

“Hapana …Hapana , Baba hilo haliwezekani baba, Umekosea, Denisi na Blandina walishakufa na nishawasahau kwenye Maisha yangu, Baba utakuwa unazeeka vibaya , unapaswa kupumzika sasa na mimi nitachukua majukumu yote ya kifamilia”Aliongea Senga pasipo kubadili mwonekano wake, ,haikueleweka alikuwa na hisia gani muda huo.

Mzee Kweka alichukua bahasha iliokuwa kwenye Kijistui upande wake wa kushoto na kisha akamsogezea Mheshimiwa Senga.

“Huo ndio uthibitisho, sijazeeka kama unavyodhania”Aliongea na Mheshimiwa Senga alichukua Bahasha hio ya Khaki huku mikono ikimtetemeka na alitoa karatasi Pamoja na picha na kuweka Mezani na akaanza na Karatasi tatu zilizokuwa zimepigwa pini kwa Pamoja.

“TOP SECRET ” ndio neno lililokuwa juu ya karatasi ya kwanza , wasomi wanaita ‘Cover Page’.

Na Mheshimiwa Senga alifungua kurasa namba Moja na kuanza kusoma maandishi yaliokuwa kwenye karatasi hio na alijikuta kila alivyokuwa akiendelea kusoma , mikono ilianza kutetemeka.

END OF SEASON 6

0687151346 NICHECK WATSAPP
 

Similar Discussions

21 Reactions
Reply
Top Bottom