Simulizi ya Kijasusi: Mlango wa 77 "DOOR 77"

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,330
51,836
Simulizi; MLANGO WA 77 "DOOR 77"

Mtunzi; Robert Heriel

Taikon Publishers

0693322300

EPISODE 01
.

Mvumo wa sauti za chura uliendelea kuvuma kama kwaya ya Akapella huku masalia ya matone ya mvua yakiendelea kudondoka kidogokidogo mithili ya nyuzi nyembamba za pamba, yajulikanayo kama Manyunyu ya mvua. Hiyo ni baada ya mvua kubwa kupiga kwa zaidi ya masaa matatu bila kukoma hali iliyosababisha maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam kufurika, huku miundombinu ya mifereji ikizidiwa na kushindwa kuhimili wingi wa mafuriko hayo; hali iliyopelekea uharibifu mkubwa wa barabara na baadhi ya nyumba kwenye mitaa iliyo mabondeni kujaa kama sio kusombwa kabisa na maji. Kama sio Vimulimuli na radi zilizokuwa zikipiga kumulika na kuangaza basi maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam yangelikuwa gizani kutokana na umeme kukatika. Lakini vimulimuli hivyo licha ya kuangaza na kutoa nuru bado havikuhesabika kama msaada zaidi ya kuzidi kuleta hofu ya kutisha kwa waliokuwa macho muda huo. Ilikuwa kama nuru ya kuzimu. Hata hivyo ni kawaida kabisa kwa nchi yetu umeme kukatika mara tuu mvua kubwa ya namna hii kunyesha, hiyo ilikuwa saa kumi alfajiri yakiwa yamesalia masaa machache kupambazuke.

Wakati kwa wengine hasa Wakulima, Mvua kwao ikiwa ni neema kubwa kutokana na shughuli zao za kilimo, hali ilikuwa tofauti kwa Julieta binti mdogo wa miaka kumi na minne aliyekuwa akihangika chini ya Daraja la Kimara akiwa na wenzake ambao daraja hilo ndilo lilikuwa makazi yao kwa ajili ya kulala. Tangu saa saba usiku mvua ilipoanza hawakuweza kupata nafasi ya kulala tena zaidi kuhangaika kujificha upande huu na upande huu kukimbia matone ya mvua, kila walipohama Matone ya mvua nayo yaliwafuata, labda yalikuwa yanataka kuhakikisha wanalowana, na hilo lilitimia baada ya mvua kuzidi kuchanganya. Julieta na wenzake walikuwa wamelowana chapachapa wakitetemeka kwa baridi kama makinda ya ndege. Mama na Baba zao hawa watoto wako wapi, kwa nini wawaache watoto wadogo namna hii wanahangaika na kuteseka kwa kiwango hiki. Mbona kuku wanakumbatia vifaranga vyao mbawani, na ndege huwatunza makinda yao viotani,

Kwao Maboksi ndio yalikuwa Godoro la kulalia, wakifunikwa na giza kila kulipokuchwa, sasa ilikuwa ni msimu wa Masika, msimu wa mvua na kama wahenga walivyosema, hakuna masika isiyo na Mbu. Ndivyo ilivyokuwa Julieta na watoto wenzake waling’atwa na mbu mpaka walishakwisha kuzoea licha ya kuwa mbu walikuwa ni wadudu hatari sana kwa kusababishia malaria lakini hawakuwa na namna ya kuwaepuka.

“ Njooni huku! Afadhali mvua imeisha, asubuhi imekaribia, hamumsikii jimbi huyo anawika” Julieta akasema, akiwa amemkumbatia binti mdogo mwenye umri upatao miaka saba hivi. Wote walikuwa wakitetemeka, walikuwa ni watoto sita, lakini hawakuwa peke yao, upande wa pili alikuwepo mwanaume mmoja kama kichaa kutokana na kuwa na nywele ndefu na ndevu nyingi zilizokuwa varuvaru ambaye naye alikuwa amelowa chapachapa kwa mvua, naye alikuwa mlalanje katika daraja hilo ambalo ni kituo cha kimara ambapo Pembeni yake kulikuwa na kituo cha polisi kilichoambatana na Hospitali ya Kimara.

Julieta ndiye alikuwa mkubwa kuliko wenzake, hivyo yeye ndiye aliyekuwa kama kiongozi wa watoto hawa. Kama ilivyo kwa viongozi wengine, naye Julieta alihakikisha upendo na umoja kwa kila mtoto unazingatiwa, ile ndio ilikuwa familia yake, alijihesabu kama Mama katika familia hiyo. Licha ya hawakuwa ndugu lakini maisha yao yaliyofanana yaliwafanya kuwa kama mapacha wa kuzaliwa. Wakakumbatiana wote sita wakipashana joto, kitambo kidogo yule adui baridi waliyekuwa wanamsikia aliwakimbia, kweli kwenye umoja na mshikamano adui hana nguvu, hilo lilitokea.

Wakati wengine usingizi ukianza kuwanyemelea, Julieta yeye hali yake ya afya ilianza kubadilika, tumbo na kiuno vikaanza kumuuma hali iliyomfanya asijisikie vizuri. Kwa uzoefu wake licha ya kuwa ni binti mdogo lakini akaelewa kuwa hali ile ilisababishwa na desturi ya mwanamke kuingia katika hedhi. Akajua muda mchache ujao damu zingeanza kumtoka, hivyo ilimpasa atafute namna ya kujistiri mbele ya wadogo zake. Wapi atapata kitambaa au taulo ya kuvaa kuzuia damu hizo, hilo ndilo alilokuwa akitafakari, kama ni nguo hakuwa nazo zaidi ya zile alizokuwa amezivaa ambazo nazo ndizo hizo zimelowana na sasa zinakaukia mwilini mwake. Hali kama hiyo ikitokea alizoea kuokota matambara yale aliyoyaona yanauafadhali ndiyo huyavaa kama taulo au pedi. Sasa ni usiku na Mvua ilikuwa imenyesha tena sio mvua ndogo bali mvua kubwa haswa, wapi apate kitambaa kikavu cha kuweza kuzuia damu ambazo tayari zilikuwa njiani kutoka. Kama ingekuwa ni mchana basi angeweza kuenda hata kwa mafundi nguo na kuomba matambara yasiyo na kazi, lakini hilo haliwezekani kutokana na bado ilikuwa ni alfajiri, yapata saa kumi na moja.

Julieta akatoka kinyemela, akawaacha watoto wenzake, akaanza kuranda randa eneo lile kuona kama atapata kitambaa cha kuweza kujistiri nacho, alikuwa akiruka madimbwi pamoja na mifereji ya maji yaliyokuwa yanatiririka yaliyosababishwa mvua, macho yake yalikuwa makini kuangaza huku na huku lakini bado hakuweza kuona kitambaa chochote, akatokea nyuma ya hospitali kisha akasonga mpaka mitaa ya nyuma kabisa, wakati huu damu zilikuwa zishaanza kuvuja, hii haikuwa nzuri sana kwake, alikuwa akijisikia aibu hivyo kila alipoona taa ya gari alikuwa akijificha pembeni ya barabarani kuogopwa kuonwa katika hali ile. Hamad! Akatokea kwenye Lodge moja ambayo ilikuwa haijazungushiwa uzio, akaona Pipa la taka lenye mfuniko kwenye ile Lodge. Akasonga huku akiangalia huku na huku, eneo lote lilikuwa kimya huku mwanga wa alfajiri ukikabiliana kuvukuza giza. Akafungua ule mfuniko wa lile pipa, akachakura chakura zile takataka ndani ya lile pipa, akaona tambara, lilikuwa ni taulo la kuogea, akalichukua kisha akaondoka akiwa analikung’uta na kulikagua. Kutokana lilikuwa ndani ya pipa halikuweza kulowana, hivyo akaona linamfaa. Akatafuta uchochoro alafu akalichana chana lile taulo na kulitengeneza kwa namna iliyomfaa kulivaa kama pedi. Baada ya kujifuta futa damu zilizokwisha kutoka, akajifunga lile taulo kama pedi, kisha akavaa sketi yake. Hapo akajiona yupo sawa, akaondoka kurudi kwa wenzake.

Akiwa anakatiza vichochoro akiwa anarudi darajani akasikia sauti za vijana zikiongea zilizokuwa zinakuja kutokea mbele, kabla hajafikiri chakufanya macho yake yakaona vijana wawili waliokuwa wanakuja, vijana wakashtuka, hawakutegemea kama wangekutana na binti mdogo kwenye uchochoro kama ule muda ule. Julieta alikuwa akitembea huku macho yake akiwa kayainamisha chini akiwa pembeni kabisa ya njia, akawa anasonga huku akiinua macho yake mara kwa mara kuwa tazama wale vijana, akawaona wakiwa wanakuja upande wake, akahama upande mwingine wa njia, na wale vijana nao wakafanya vivyohivyo, akahama tena upande wa pembeni kabisa wa mwanzo aliokuwa, wale vijana nao wakahama kumfuata kumziba asipite, hapo walikuwa wameshakaribiana kama hatua tano tuu! Julieta akasimama, akawa anatazamana nao.

Wale vijana nao wakawa wanamtazama Julieta kama wakaguzi wasanifu, udenda uliwatoka, ashiki ya ngono zikakamata hisia zao. Walimuona Julieta kama Malaika mdogo aliyewatokea katika kichochoro kile. Uzuri wa Julieta ulikuwa dhahiri, licha ya kuwa alikuwa mtoto chokoraa lakini hiyo haikuzuia uzuri wake kuchomoza kama jua. Julieta alikuwa binti mdogo mwenye urefu uliokadiriwa kumvutia mwanaume yeyote, macho yake makali yenye ulegevu kwa mbali yalizidisha majaribu kwa vijana wale, kama hiyo haitoshi, kilichowamaliza kabisa ni chuchu zake saa sita zilizokuwa zinabembea katika kifua chake kidogo ziliamsha maruani ya wale vijana. Kiblauzi alichokuwa amevaa bado kilikuwa hakijakauka hivyo kilikuwa kimeshikamana na mwili hali iliyopelekea eneo la kifuani kusimama dede jambo ambalo lilizidisha tamaa mbaya ya ngono kwa wale vijana. Ni kweli alikuwa binti wa miaka kumi na minne lakini mvuto wake ulilingana na wasichana wenye miaka ishirini hivi.

Wale vijana wakamsogolea, Julieta akawa anarudi nyuma polepole huku macho yake yakiwa katika nyuso za wale vijana, alikuwa akihamisha macho yake kwa kijana huyu, kisha huyu kila alipokuwa akipiga hatua kurudi kinyumenyume. Wale vijana nao walikuwa wakitembea huku wakimtazama na kumfanyia madoido na mizaha huku wakitabasamu pengine wakimshawishi asikimbie. Lakini Julieta alikuwa mzoefu wa hila za watu wa namna ile, uzoefu wake kama mtoto wa mitaani ulimuambia kuwa vijana wale hawakuwa wema. Akawa anarudi nyuma! Nyuma! Mpaka alipokanyaga dimbwi la maji hapo akasimama alafu akaangalia chini kwenye lile dimbwi la maji aliloziingiza mguu wake. Kisha akainua uso wake kuwatazama wale vijana, akawaona wakicheka kama waliofurahia jambo lile. Julieta akakasirika.

“ Msinisogelee! Nawaonya msinisogelee” Julieta akasema akiwa ameokota kopo lililokuwa karibu na lile dimbwi. Lakini wale vijana wakawa wanamcheka, akainama kisha akawarushia yale maji machafu ya kwenye kile kidimbwi, wakawa wanakwepa huku na huku, naye akawa anawamwagia lakini hilo halikufua dafu kwani vijana wale walichukulia kama mchezo tuu. Kila alivyokuwa akiwarushia maji ndivyo walivyokuwa wakimsogelea. Juliata kuona hivyo akatoka nduki akiwakimbia, wale vijana nao wakamfungia mkia kumkimbiza, hapo tayari ilikuwa inakaribia saa kumi na mbili Asubuhi anga likiwa na nuru huku kwa upande wa mashariki mawingu yenye rangi ya moto yakiwa yanametameta; kwamba muda mchache jua lingechomoza.

Julieta akakimbia huku akipiga kelele lakini wale vijana hawakujali, kila alikokatiza katika mitaa ile hakuna aliyejitokeza kutoa msaada licha ya kuwa tayari kulikuwa kumekucha. Julieta akakimbia mpaka alipotokea eneo ambalo hapakuwa na nyumba nyingi na barabara imesonga ikiwa inamatope, wale vijana nao wakamfungia mkia, kosa moja alilolifanya Julieta ni kuchagua kukimbia upande huu badala ya angekimbilia upande wa barabarani, hivyo kadiri alivyokuwa akikimbia ndivyo alivyokuwa anaingia ndanindani kusiko na makazi mengi ya watu, na wengi nyumba zao zilikuwa ndani ya Uzio. Hata hivyo alikuwa amejitahidi sana kukimbia kwa dakika mbili mbele ya vijana wawili wakiume halikuwa jambo dogo lakini mbio zake bila msaada zingekuwa kazi bure tuu. Wakamkamata wakiwa kwenye eneo lililokuwa na vichaka, kilikuwa kiwanja ambacho bado hakijajengwa, Julieta akawa anapiga makelele huku akiwarushia mateke na makofi lakini wakamdhibiti. Wakampiga Kibao kikali cha usoni, kisha wakamziba mdomo, kisha kwa nguvu wakachana ile blauzi, chuchu zote zikabaki nje, wakaivuta ile sketi kwenda chini, Dooh! Lilikuwa tukio la kikatili sana kwa binti mdogo kama yeye. Julieta alitamani ingekuwa ni hadithi au filamu tena akatamani angekuwa yupo ndotoni anaota lakini lilikuwa tukio la kweli la ubakaji.

Tayari walikuwa wameshamvua kila kitu, bila kujali hali yake ya kutokwa na damu hilo kwao halikuwa kizuizi, siku zote binadamu mwenye tamaa kali ni kama shetani mnywa damu. Ndivyo walivyokuwa wale vijana, Julieta alikuwa akilia akijaribu kufurukuta lakini juhudi zake zikagonga mwamba, hakuwa na ujanja zaidi ya kuwaachia wafanye vile walivyotaka. Lakini msaada huja kama mauti, huja kwa ghafla wakati mwingine bila ya kutazamia. Tena msaada wakati mwingine ukiuomba hauupati, na ukiupata haudumu. Huja pasipo kuuomba na kama ukiuomba sana utakukimbia.

Ghafla Julieta akiwa kafumba macho yake akashangaa wale vijana wakimuachia mikono yake, na kukimbia, kisha kikafuatia kimya upepo wa asubuhi ukipuliza mwili wake usiokuwa na nguo. Julieta akawa anafikiri nini kimetokea, akafumbua macho yake hakuona mtu, wala wale vijana waliokuwa wanataka kumbaka hakuwaona, akakaa kisha akawa anaangaza macho yake huku na kugeuka huku lakini hakuona mtu isipokuwa vichaka na uzio wa nyumba zilizokuwa kwa mbali kidogo. Punde akasikia sauti ya hatua za mtu ajaye, upande wa mkono wa kushoto kulikokuwa na vichaka vingi, macho yake yakiwa na shauku ya kumuona mtu huyo, ghafla alishtuka kumuona mwanaume mmoja mrefu wa wastani, Julieta kwa upesi akachukua sketi yake na kuficha maziwa yake na sehemu ya uchi wake. Huku akiona haya.

“ Usiogope! Kuwa na amani! Wamekimbia!” Mwanaume yule akasema. Julieta akiwa na haya akawa anatazama chini huku akimuangalia yule mwanaume kwa kujiiba.

Yule mwanaume akawa anamkagua Julieta, kisha akapeleka macho yake kwenye ile blauzi iliyochanwa, alafu akaona lile tambara la taulo ambalo Julieta alilifanya kuwa Pedi, kaona damu, akashtuka! Alifikiri wale vijana walikuwa wameshambaka na kumharibu. Julieta aliona uso wa yule mwanaume ukiwa umebadilika akiwa ametazama pembeni, jambo ambalo likamfanya Julieta naye aangalie kule alipoangalia Yule mwanaume, akaona lile taulo. Kisha wakatazamana.

“ Twende hospitalini” Yule mwanaume akasema, Lakini Julieta akawa anakataa kwa kunyanyua mabega juu.

“ Twende! Kitendo walichokufanyia ni hatari kwa afya yako” Yule mwanaume akasema, kisha akawa anakagua uso wa Julieta kusoma akili yake.

“ Usiogope mdogo wangu, kuwa na amani. Tayari umeshabakwa, lazima tuwahi hospitalini kwa ajili ya afya yako, madaktari watatusaidia Sawa mdogo wangu”

“ Ilikuwa bado, nashukuru” Julieta akajibu.

“ Unamaana gani?”

“ Hawakufanikiwa kunifanya lolote!”

“ Eeh! Embu twende Hospitali wewe, utakuwa umechanganyikiwa” Yule mwanaume akasema.

“ Wala sijachanganyikiwa, ninaakili zangu timamu. Naomba uniache niondoke” Julieta akasema, akiwa bado ameficha maziwa na uchi wake kwa ile sketi.

“ Umebakwa mdogo wangu, siku hizi kuna magonjwa mengi, twende hospitalini tujue tunapambana vipi na hili alafu hawa waliofanya hivi tutawatafuta tuu”

“ Nimekuambia sijabakwa! Wapi hujaelewa Kaka” Julieta akafoka, Hapo Yule mwanaume akawa anamtazama Julieta huku akimshangaa, kisha akayapeleka macho yake kwenye ile taulo yenye damudamu kama mtu aulizaye; damu ile imetokana na nini. Julieta naye akaitazama ile taulo yenye damudamu akaelewa kuwa Yule mwanaume zile damu ndizo zimemfanya aone kabakwa.

“ Hazijatokana na ubakaji Kaka” Julieta akasema huku akiwa anaaibu sasa akaanza kulia huku,

“ Nashukuru sana kaka kwa msaada wako, ilibaki kidogo tuu wanibake, sina chakukulipa, Mungu mwenyewe ndiye atakulipa” Julieta akasema. Yule mwanaume hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali licha ya kuwa bado alikuwa na wasiwasi na kutokuelewa kile kilichotokea.

“ Unaitwa nani?”

“ Julieta!” Julieta akajibu.

“ Julieta?”

“ Abee!”

“ Pole sana mdogo wangu, nisikuulize maswali mengi najua umechoka, vaa nguo tuondoke” Yule mwanaume akasema, huku akigeuka upande wa pili ili kumpisha Julieta avae nguo zake. Kitambo kidogo Julieta alikuwa keshavaa Sketi yake na ile blauzi yake iliyokuwa imepauka, sketi na mwili wake hasa kwenye kisogo kulikuwa na matope kutokana na kukurukakara za tukio lililopita. Yule mwanaume akageuka, akamkuta Julieta akiwa kava nguo lakini eneo la kifuani likiwa wazi kutokana na blauzi aliyokuwa amevaa ilikuwa imechanwa vibaya. Yule mwanaume akamtazama Julieta kwa nusu dakika, kisha akasema;

“ Usijali! Kila kitu kitakuwa sawa Julieta”

Wakatoka kule vichakani na kutokea barabarani tayari kulikuwa kumepambazuka, magari na mtu mmoja mmoja waliokuwa wanapita kwenda kwenye shughuli zao walikuwa wameanza kuwa wengi. Julieta akaona gari aina ya Toyota Rumion ya rangi ya kijivunyeusi ikiwa imepaki pembeni ya barabara. Yule mwanaume akaenda mpaka kwenye lile gari kisha akafungua mlango, alafu akageuka nyuma kumtazama Julieta ambaye bado alikuwa anawasiwasi.

“ Usiogope, ingia ndani ya gari tuondoke”

“ Twende wapi?”

“ Nakupeleka nyumbani kwenu”

“ Kwetu!” Julieta akaitikia kwa kushangaa,

“ Kumbe! Au unataka nikupeleke wapi? Yule mwanaume akasema,

“ Samahani kaka yangu, naomba uniache hapahapa, labda unisaidie tuu pesa kidogo ya kula leo” Julieta akasema,

“ Sawa, nitakupa pesa ya kula, kwani wazazi wako wanaishi wapi?” Yule mwanaume akasema, Julieta akaanza kulia, yule mwanaume tangu awali alihisi Julieta ni mtoto wa mtaani, licha ya kuwa alikuwa ni binti mzuri lakini hali ya uchokoraa ilikuwa imemvaa pia..

“ Usilie, ingia ndani ya gari, sawa mdogo wangu” Yule mwanaume akasema, huku akiwa ameshamsogelea Julieta karibu na kumpiga piga begani akimbembeleza, wapitanjia walikuwa wakiwashangaa, Julieta akaingia ndani ya gari, kisha wakaondoka.

****************************************

Kutoa ni moyo wala si utajiri, mtu ampapo mhitaji kitu pasipo kuombwa hujijengea heshima kubwa nafsini mwake, tena heshima hiyo ni bora zaidi ya kitu hicho kama angebaki nacho. Ukarimu ni vazi la roho kama vile nguo zinavyousitiri mwili ndivyo ukarimu unavyoisitiri roho ya mtu. Kufadhili wageni, kuwahurumia masikini ndivyo mafundisho yasemavyo. Lakini sio kila mtu anamoyo wa kutoa, ukarimu ni karama adhimu ambayo wachache sana huwa nayo. Peter Gozbeth Mirambo alikuwa miongoni mwa wanaume wachache waliojaaliwa karama hiyo.

Baada ya kumnunulia Julieta Nguo na mahitaji yake madogo madogo, wakaelekea mpaka Makongo, yalipo makazi yake, ndiye Peter Mirambo ambaye alikuwa akipenda kuitwa PM.

Julieta alikuwa akishangaa jumba kubwa la Mwanaume aliyekuwa amemuokoa kutoka kwenye tukio la kikatili, bado alikuwa ndani ya gari, lilikuwa jumba kubwa la kisasa, ambalo kwa nje kulikuwa na vigae na bustani zenye maua pamoja na ukoka, gari likasimama eneo maalumu la maegesho. Kisha Yule mwanaume ndiye Peter Mirambo akashuka, akazunguka upande wa pili na kuufungua mlango wa gari huku akimpa ishara Julieta kuwa akaribie kwani wameshafika. Julieta akashuka.

Julieta akiwa ndani ya mavazi mapya nadhifu waliyoyanunua Mlimani City alikuwa kapendeza sana, wala usingedhani kuwa ndiye yule Julieta wa Darajani Kimara ambaye alikuwa Chokoraa. Alikuwa ndani ya kigauni cha rangi ya Zari, chini akiwa amevaa viatu aina ya mosimo vilivyomkaa vyema, akashuka akiwa kabeba mfuko ambao ndani yake kulikuwa na nguo zingine walizonunua, Pedi, sabuni ya kuogea, mafuta ya ngozi pamona na kandambili. Julieta alikuwa anajikaza kutabasamu lakini uso wake ulikuwa unashindwa kuficha maumivu aliyokuwa akiyapata, Peter Mirambo aligundua kuwa Julieta hayuko sawa, tayari alishajua kuwa Julieta yupo kwenye hedhi, akampa dawa ya kutuliza maumivu walipokwisha kuingia ndani.

Peter Mirambo alikuwa akiishi na Housemaid ambaye alikuwa akimsaidia kazi za nyumbani, hivyo kuja kwa Julieta kunaifanya familia hiyo kuwa na watu watatu. Baada ya kutambulishana, Peter mirambo aliingia chumbani kwake, kisha akaenda kujimwagia maji kutokana na usiku wote kuutumia na mchumba wake aishiye Kimara. Akiwa bafuni alikumbuka jinsi usiku wote alivyoutumia na Leila, maji yakiwa yanammwagia usoni kwenye bomba la mvua aliiona taswira ya Leila ikiwa akili mwake, hali alikuwa akiifurahia sana, na mara kadhaa alikuwa akiimba huku akijipaka sabuni kwenye mwili wake. Basi ndivyo yalivyo mambo ya ujana. Huwezi tenganisha ujana na mapenzi. Akamaliza kuoga, alipofika chumbani kwake akakuta simu yake ikiwa missed Call tatu. Kisha kulikuwa na ujumbe uliosomeka “ G108” kwa haraka Peter Mirambo akabonya bonya simu kisha akaiweka sikioni,

“ Ndio Mkuu! Sawa! Ok.. Nakuja sasa hivi Mkuu, Sawa” Peter alikuwa akiongea na mtu kwenye simu, kisha simu ikakatika, akawa anajiandaa upesiupesi kama mtu aliyechelewa, ndani ya dakika moja alikuwa keshamaliza kuvaa, akaliendea kabati la siri lililokuwa kwenye kile chumba, akalifungua macho yake yakapokelewa na silaha za moto zilizokuwa zimepachikwa kwa ufundi katika kabati lile, akachukua bastola, kisha akafunga kabati lile. Akaiweka ile bastola kibindoni na kulishusha shati lake alilokuwa amelivaa. Alafu akatoka.

“ Jamani! Mimi natoka eeh! Nafikiri kila kitu kiko sawa, sitachelewa kurudi, lakini kama nitachelewa basi pesa ya mboga za jioni iko pale mezani, sawa mama zangu” Peter Mirambo akasema akiwa anatabasamu, alikuwa akipenda sana mizaha,

“ Sawasawa Boss!” Housemaid akajibu,

“ Nilikuambia usipende kutumia jina hilo, niite Kaka, sawa”

“ Samahani, kila saa nasahau! Sawa kaka”

“ Namna Hiyo” Peter Mirambo akasema,

“ Hahahaha” Housemaid pamoja na Julieta wakaangua kicheko. Peter naye akawa anacheka huku akiondoka pale kuukabili mlango wa sebuleni wa kutokea, lakini kabla hajaufikia akasimama na kuwageukia,

“ aaam! Kuweni makini, msitoketoke hovyo nje, lakini pia muwe na siku njema, okey!”

“ Hahahah! Sawa kaka tumekuelewa” Wakajibu. Kisha akawaacha.

“ Kaka anavituko kweli, yaani ni mcheshi kweli” Housemaid akasema, huku akiweka chai mezani.

“ Anaonekana!” Julieta akajibu, wakanywa chai kila mtu akiwa na mawazo yake. Julieta hakuwa mtu wa maneno mengi, hali hiyo ilipelekea kusiwe na mazungumzo ya mara kwa mara.

Julieta alipomaliza kula alienda chumbani kwake, huko mawazo mengi yalimjia, aliwakumbuka wadogo zake aliowaacha kule Daraja la kimara, alijikuta shauku ya kutaka kurudi ikimvaa kwa nguvu.

“ Lazima watakuwa na wasiwasi na mimi, hawajui niko wapi, pengine wanawasiwasi kuwa kuna baya huenda limenipata, wale ni kama ndugu zangu, nimeisha nao kwa muda sasa, nimeshawazoea. Sijui hata kama wamekula, hakuna wa kuwalinda zaidi yangu, hakuna wa kuwatafutia chakula zaidi yangu, kubwa zaidi hakuna wa kuwapa upendo zaidi yangu. Mimi ni kama mama yao, hata kama sina kitu” Julieta alikuwa akiwaza huku akijigeuza geuza kitandani. Mawazo hayo yalimkosesha amani, pengine kwa mtu mwingine ile ingekuwa bahati kubwa ya kumfanya asahau aliokuwa anasota nao, lakini kwa Julieta haikuwa hivyo. Alikuwa na moyo wa ajabu. Julieta akaamka kutoka kitandani, akasonga mpaka kwenye Dressing table iliyokuwa mule chumbani, akasimama mbele ya kioo kikubwa akawa anajitazama. Akajitazama huku akijikagua mwili wake vile kile kigauni kilivyompendeza, akatabasamu.. Kisha akasema; Nisamehe Kaka peter, umekuwa mwema kwangu, lakini sina budi kurudi katika familia yangu. Mimi ni Mama mwenye watoto watano wanaonitegemea” Hapo akawa anatabasamu zaidi huku machozi yakiteleza katika mashavu yake machanga.

Akachukua ule mfuko wenye vitu walivyonunua Mlimani City, kisha akaviweka juu ya kitanda, alafu akatoka nje ya chumba kwenda kuangalia kama Housemaid kaka mkao upi kusudi atoroke, kwa bahati Housemaid naye alikuwa chumbani kwake, akarudi upesi mpaka chumbani, akachukua ule mfuko na kutoka harakaharaka kabla Housemaid hajatoka chumbani, huyo akatoa nje na kufungua geti la kutokea, akatoroka.

************************************

“ Wameiteka Meli yetu iliyokuwa imebeba silaha, tangu nchi hii imepata uhuru haijawahi kutokea Meli zilizobeba silaha zinazotoka nchi za nje kutekwa kuja hapa nchini kutekwa. Silaha zinasafirishwa kwa siri kubwa, wala sio jambo la vyombo vya habari au suala la umma kufahamu, hata ndani ya jeshi sio kila mtu anayepaswa kujua tuna silaha kwa kiwango gani, achilia mbali lini na wapi tumeagiza silaha hizo, lakini chakushangaza Meli yetu imetekwa na watu wasiojulikana, hii inatisha, lazima kuna msaliti anayetuzunguka. Sasa jambo hili kwanza liwe siri, sitaki kulisikia popote hasa katika vyombo vya habari, pili nahitaji kikosi maalum chakwenda kuokoa meli hiyo, tatu, huyo msaliti tufanye juu chini aweze kupatikana” Mkuu wa majeshi Haidari Mwera akasema,

“ Inashangaza kwa kweli! Kwani Mkuu huko silaha zilipoagizwa hazikutoa Escort kuhakikisha silaha zinafika mpaka hapa salama?” Moja ya wanakikao akauliza,

“ swali hilo halina maana ndugu yangu, kwa sasa tunatakiwa tufikiri namna ya kuikomboa Meli hiyo, na kuhakikisha silaha zote zinarudi mikononi mwetu salama, hatuna muda wa kuwaza mambo ya Escort ya mahali tuliponunua hizo silaha” CDF Haidari akasema,

“ Hii ndio raMani ya mahali Meli yetu ilipo kwa sasa, ipo katika kisiwa hiki hapa ambapo mpaka saa kumi na moja alfajiri ya leo kulingana na data za IMSI au STINGRAYS tuliyoipachika katika moja ya sehemu ya siri kwenye meli ile. Mnaweza kuitazama, na itabidi tuondoke kuwafuata mapema kabla hawajagunudua kuwa kuna vifaa tulivyoviweka melini vinavyotupa location ya wapi walipo. Wote mnafahamu kuwa teknolojia imekua, na wao sio wajinga kiasi cha kushindwa kutambua jambo dogo kama hili. Naamini watakuwa wanahangaika kuvi-detect hivyo vifaa ili kuharibu mawasiliano.” CDF akasema huku akikionyesha kisiwa hicho Kupitia Projector iliyokuwa ikionyesha ramani ya bahari ya hindi na kisiwa ambapo meli hiyo inadaiwa ipo.

“ Peter Mirambo”

: Ndio Mkuu” Peter Mirambo akasimama na kutoa saluti kwa ukakamavu kisha akakaa.

“ Wewe ndio utasimamia Operesheni hii, naamini hakuna ambalo litaenda vinginevyo. Nataka ndani ya masaa arobaini na nane, meli hiyo iwe hapa. Bahati nzuri wewe ni Komando na jasusi mwenye mafunzo yanayotufanya tukuamini, kuanzia sasa misheni hii ipo chini yako, mpaka umefika hapa nadhani Boss wako ameshakueleza kila kitu, idara zetu za Ulinzi na usalama ni kawaida kushirikiana katika masuala nyeti kama haya kwa maslahi ya taifa” Akameza mate kisha akaendelea,

“ Nasisitiza jambo hili liwe siri” CDF akamaliza, kilikuwa kikao cha siri cha watu wanne wawili wakiwa viongozi wa juu wa jeshi la wananchi, Peter Mirambo na Waziri wa Ulinzi.

“ Tutakupatia Kikosi cha watu kumi kwa ajili ya kazi hiyo, Sawa Peter!” Yule kiongozi mwingine wa jeshi akasema, Peter akaitikia “Sawa Mkuu”

“ Tayari kikosi hiko kimeshajiandaa, anayesubiriwa ni wewe, kipo ufukweni mwa bahari kwa ajili misheni kuanza, nafikiri umejiandaa”

“ Ndio Mkuu, Mwanajeshi muda wote yupo tayari kulinda nchi yake” Peter Mirambo akasema, huku akiandika Identification number iliyokuwepo kwenye ramani katika screeni ya projector iliyopo ukutani. Alikuwa akiinukuu katika Diary yake ya kijasusi, ambayo ilikuwa ndogo yenye urefu wa inchi tatu na upana inchi mbili. Kikao kikafugwa, Peter Mirambo akaagana na wakubwa wake wa kazi, akatoka.

IMSI ni kirefu cha International Mobile Subscriber Identity(IMSI Catcher) au kwa jina jingine huitwa Stingray ni kifaa cha kiteknolojia ambacho hutumika katika shughuli za kiserikali hasa za ulinzi na ujasusi, kifaa hiki huwekwa sehemu maalum kama kwenye simu, gari au Drone au kwenye jengo au sehemu yoyote inayolengwa ili kunasa na kupata taarifa kama sauti au maandishi, pamoja na kuonyesha Location na umbali ambao kifaa hiko kipo. Hivyo Meli iliyokuwa imetekwa ilikuwa imewekwa kifaa hiki, ambacho kimewasaidia kutambua mahali meli hiyo ilipo. Hata hivyo Kila teknolojia inaudhibiti wake, kwa kujua hilo ndio maana inampasa Peter Mirambo na kikosi chake wafanye haraka kabla Watekaji wa Meli hawajagundua jambo hilo.

Peter Mirambo akawasili Ufukweni akiwa ndani ya mavazi ya kijeshi yenye rangi ya Bluu, na kofia ngumu, akiwa amejidhatiti kwa silaha za kivita, yeye ndiye aliyekuwa anasubiriwa. Mara baada ya kuingia katika Boat ya kijeshi safari ikaanza, zilikuwa Boat mbili za kijeshi, Boat moja ilikuwa na wanajeshi sita, na ile aliyoipanda G108 Peter Mirambo ilikuwa na watu watano, na kufanya jumla ya kikosi hatari cha watu kumi na moja. G108 ni Secret Agent Code name ya Peter Mirambo, ambayo hutumika katika shughuli zake za kijasusi.

Wakati Boat hizo zikichanja mawimbi ya bahari, Peter Mirambo akatoa Laptop yake kutoka katika begi lake la kijeshi, kisha akaiwasha, alafu baada ya kuiwasha akaingia katika program ya siri aliyokuwa anaijua yeye mwenyewe, kitambo kidogo akiwa anasubiri jambo Fulani kutoka kwenye Laptop yake, akatoa ile Diary yake ya kijasusi, kisha akaingiza zile Identification number alizozichukua kwenye ile ramani, baada ya kuziweka na kuziruhusu zijichakate, punde kioo cha Laptop kikawa kinaonysha ramani ya bahari ya hindi na baadhi ya visiwa vidogo vidogo vilivyokuwamo. Kulikuwa na kialama chekundu kilichokuwa kinamwekuamwekua katika moja ya kisiwa kwenye ile ramani. Hiyo ilimaanisha kuwa Bado Meli ilikuwepo katika kilekile kisiwa.

“ Watakuwa wanafanya nini hapa, au wanashusha silaha kwenye kisiwa hiki, au huenda wanazihamisha silaha katika meli au boat zao” Peter Mirambo akawa anawaza huku upepo wa bahari na matone matone ya maji ya mawimbi ya bahari yakiwa yanawapiga mara kwa mara kadiri boat ilivyokuwa inakata mawimbi.

Rada iliyokuwa kwenye Laptop iliwaelekeza upande ambao wanapaswa kuufuata, Majini na angani sio sawa na ardhini. Ardhini unaweza kukumbuka kwa urahisi eneo Fulani au upande Fulani kutokana na uwepo wa vitu kama Milima, majengo, misitu, kona au mteremko na vitu hivyo ukavifanya kama alama ya kukuonyesha uelekeo aidha ni mashariki au magharibi kwa kadiri jua lichweapo au lizamapo. Lakini uwapo Baharini au Angani ni ngumu kuelewa na kujua uelekeo. Hii ndio inafanya umuhimu kifaa kiitwacho Radar ambacho kitasaidia kujua uelekeo, upande upi ni mashariki, na wapi ni magharibi. Ugunduzi wa Marine Compass( Dira ya baharini) ni moja ya teknolojia iliyosaidia sana katika usafarishaji kwa njia ya maji.

Kwa mbali kidogo kama Maili tatu hivi wakaona kitu mfano wa kichuguu. Peter akiwa kachuchumaa nyuma yake akiwa kasimamiwa na wenzake wawili walikuwa wakiangalia kwenye Laptop ambapo walipata ujumbe kuwa zimesalia dakika kumi hivi kufika katika kisiwa hicho, hiyo ni baada ya lisaa limoja na nusu ya safari yao. Peter akasimama, kisha akachukua M22 Binocular ambayo ni Darubini maalumu ya kijeshi, akaipachika kwenye uso wake na kuangaza mbele, akitazama huku na huku upande wa kile kitu mfano wa kichuguu walichokiona. Natazama akaona kisiwa kidogo chenye vichaka na mitimiti, lakini hakuona Meli, jambo hilo likamfanya akose utulivu, akarudia tena kuangalia Kupitia Darubini mara hii akiwa makini zaidi, kwa pembeni kabisa ya kile kisiwa akashtuka kuona Mwanaume mmoja aliyevalia mavazi ya kijeshi yenye rangi ya nyasi kavu akiwa naye ameshikilia Darubini, ni kama wakawa wanatazamana.

” Tj001 Be aware, the enemy has seen us. Over!” Peter Mirambo akasema akiwa ameinamisha mdomo wake kwenye kifua mahali ilipo Radiocall ya kijeshi. Kila mmoja akajiweka tayari kwa ajili ya kazi.

“ Tutakizunguka kisiwa, Ninyi mtaenda upande wa kushoto wa kisiwa sisi tutaenda kwa upande wa kulia. Tupo sawa” Peter Mirambo akapaza sauti, na hapohapo sauti ya kikosi kama mtu mmoja ikaitikia “Tupo sawa Mkuu”. Kisha Boat hizo mbili zikachanguka na kutawanyika moja kushoto nyingine kulia, wakati huo Milio ya risasi na mabomu kutoka kwenye kile kisiwa yakiwa yanarushwa kuwafuata. Mapambano yalikuwa makali lakini Peter Mirambo na wenzake wakazidi kusonga mbele huku nao wakishambulia. Wale watekaji walikuwa wamejipanga haswa, silaha zao zilikuwa kali na zamoto, pia watumiaji wake nao walionekana wamebobea katika vita.

Makombo ya RPG – 7 yalikuwa yakizikosa kosa Boat za Peter Mirambo na wenzake, hali iliyokuwa inapelekea milipuko ya maji baharini baada ya kutua. Sasa zilikuwa zimebakia mita moja wafike katika kisiwa kile, lakini katika hali ya hatari na kusikitisha moja ya boat yao ikalipuliwa, na kuteketea papohapo. Peter Mirambo akiwa katika mapambano makali aliomuona kwa mbali mshambuliaji akiachia Kombora lililokuwa limesetiwa kupiga Boat yao, kabla hajafungua mdomo kuwajulisha wenzake tayari kombora lile lilikuwa limeshapaa hewani na muda uliobaki usingemtosha kunyanyua mdomo kusema lolote. Akamshika mmoja ya wanajeshi wenzake na kuruka naye Baharini huku miguuni wakilambwa lambwa na moto wa mlipuko wa Kombora.

Itaendelea kesho saa nane mchana.

Vitabu vilivyo tayari
1. Mlio wa Risasi Harusini
2. Wakala wa Siri
3. Kaburi la Mwanamuziki

Unalipia oda unapata kitabu chako.
Kila kitabu bei Tsh 15,000/=

0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
Zipo nyingi tuu Mkuu.

Ila nyingi ni zazamani.

Kama Balozi wa lamu, hapo utamkuta mtu aitwaye Umsulopagus
Za kwako nyingi hujamaliza.Ni vizuri uwe unatoa utangulizi then utuambie kitabu kimetoka na kinapatikana wapi.ili tukuunge mkono si vizuri kutiririka halafu unaingia mitini.
 
Leo
 
Duh....nikama singanojr anatunga bure...Uzi Wake unastori ndefuuuu
 
MLANGO WA 77 "DOOR77" Sehemu 02
Mtunzi; Robert Heriel
Whatsapp 0693322300

Sehemu 02

Ilipoishia

Makombo ya RPG – 7 yalikuwa yakizikosa kosa Boat za Peter Mirambo na wenzake, hali iliyokuwa inapelekea milipuko ya maji baharini baada ya kutua. Sasa zilikuwa zimebakia mita miamoja wafike katika kisiwa kile, lakini katika hali ya hatari yakusikitisha moja ya boat yao ikalipuliwa, na kuteketea papohapo. Peter Mirambo akiwa katika mapambano makali aliomuona kwa mbali mshambuliaji akiachia Kombora lililokuwa limesetiwa kupiga Boat yao, kabla hajafungua mdomo kuwajulisha wenzake tayari kombora lile lilikuwa limeshapaa hewani na muda uliobaki usingemtosha kunyanyua mdomo kusema lolote. Akamshika mmoja ya wanajeshi wenzake na kuruka naye Baharini huku miguuni wakilambwa lambwa na moto wa mlipuko wa Kombora.
ENDELEA
Akiwa majini kwa upesi akaogelea akikata mawimbi kukimbia mlipuko wa lile kombora uliokuwa umechanganyika na maji ya bahari. Haikumchukua muda mrefu alikuwa ameshafika ufukweni, huku nyuma yake akifuatiwa na mwanajeshi mwenzake aliyekuwa amemuokoa. Hakuwa na muda wa kusubiri akasonga kufuata vichaka vya kile kisiwa kisha akajificha, kwenye moja ya kichaka, hapo akawa anapumua upesiupesi huku akijifuta maji yaliyokuwa usoni mwake, nguzo zake zikiwa zimelowana, akamgeukia mwanajeshi mwenzake aliyekuwa anamalizia kutoka baharini, akimharakisha afanye upesi kwa kutumia ishara ya mkono.

Akachukua Darubini iliyokuwa inaning’inia kwenye kifua chake ikiwa na kamba iliyopita kwenye shingo yake, kisha akaiweka machoni na kuanza kuangaza huku na huku kufuata vilipo vichaka na kilima kidogo cha kile kisiwa, hakuona mtu yeyote, akatoa bastola mafichoni kisha akasonga mbele kufuata vichaka huku nyuma yake akifuatwa na mwenzake. Akapandisha kwenye kile kilima kilichokuwa kina vichaka vilivyostawi pamoja na minazi michache, alipokaribia kilele cha kile kilima akalala karibu na ngema kisha akatoa darubini ndio ile M22 Binacular na kuiweka machoni na kuchungulia upande wa pili, akashtuka kuona Meli kubwa yenye Maandishi yaliyosomeka ‘MANDARIN PACIFIC” Chini yake kukiwa na picha ya Kasa, akaona Boat kubwa zipatazo kama tano hivi, Boat tatu zikiwa zinaondoka, mbili zikiwa zimesimama lakini kulikuwa na watu waliokuwa na hekaheka za kuhamisha maboksi kutoka kwenye meli kubwa kwenda kwenye zile Boat. Moja kwa moja Peter Mirambo akajua kuwa zilizokuwa zinahamishwa ni zile silaha zilizokuwa zimetekwa. Alihisi mapigo yake yakianza kwenda mbio, akahamisha macho yake yaliyosaidiwa na darubini upande mwingine hapa akashtushwa kuona kundi la watu waliotekwa wakiwa wamefungwa mikono yao kwa nyuma, walikuwa wametekwa na wale maharamia waliokuwa wamevalia nguo za kijeshi zinazofanana na rangi ya nyasi kavu, na makofia makubwa yenye rangi ya nyasi kavu waliyokuwa wanyeyavaa kichwani wengine wakiwa wameyaning;iniza mgongoni huku usoni na shingoni wakiwa na mitandio myeusi, mkononi wakiwa na bunduki zenye mnyororo wenye risasi nyingi. Hii ilimaanisha walikuwa wamejidhatiti kikamilifu.

Peter Mirambo akaanza kuwakagua wale mateka mmoja baada ya mwingine Kupitia darubini yake, Wakati akiwa anaendelea kuwakagua yule mwenzake naye alikuwa ameshafika akiwa kalala karibu na Peter,

“ Wapo wengi itabidi kuomba msaada, pekee yetu hatutaweza, wanasilaha nyingi zaidi yetu”

“ Sikiliza Beka, wingi wao sio kitu, na wala kuwa na silaha nyingi kwenye vita sio kushinda vita. Kushinda vita kunahitaji Ujuzi ambao tayari tunao, mbinu na timing ambayo itatufanya tutumie nguvu na muda kidogo. Vita ni mahesabu” Peter Mirambo akasema, huku akiwa anamtazama Beka.

“ Ulichosema sijakataa Mkuu, lakini tazama mimi nina bunduki hii, nawe unahiyo bastola tuu, labda na kisu au silaha zingine ndogondogo lakini wenzetu nadhani unawaona” Beka akajibu,

“ Beka silaha ya kwanza kwenye vita ni akili, ukiweza kuitumia akili yako vilivyo hakuna vita itakayokushinda, Hata uwe na Silaha gani kama huna akili huwezi shinda katika vita. Naamini wametuzidi kwa silaha unazoziona lakini hawajatuzidi akili. Jeshini tulifundishwa kutumia Akili kupambana na adui yeyote katika mazingirta yoyote……”

“ Pm! Pm! Angalia kule” Beka akamkatisha Peter Mirambo, kisha Peter akaangalia upande walipokuwa wale mateka waliokuwa kwenye Meli. Akaona Wale maharamia wakiwapiga wale mateka, kisha walishtuka baada ya kuona moja ya mateka akipigwa risasi ya kichwa na kudondoka chini. Ilikuwa kama muda wa kuwaua wale mateka hasa waliokuwa wanaleta ubishani.

“ Hatuwezi ruhusu wawaue watu wetu” Peter Mirambo akasema huku akiwa anawaangalia Kupitia kwenye Darubini.

“ Sikiliza Beka, wewe ni bingwa wa kulenga shabaha, wakati mimi nawafuata wewe utabaki hapahapa kuni-cover, nikifika kwenye ule mnazi pale aliposimama yule Bwege, nikishamvamia basi utaanza kushambulia, nafikiri tumeelewana” Peter akasema huku akiinuka akiwa kashika bastola yake na kuanza kusonga kinyemela huku akijificha kwenye miti na vichaka akiteremka kule chini ufukweni walipokuwa wale Maharamia. Ndani ya dakika mbili alikuwa amemkaribia yule mtu ambaye alikuwa kwenye mnazi akiwa anazunguka zunguka akilinda usalama wa eneo lile bila kujua kuwa nyuma yake yupo kiumbe hatari anayeitaka roho yake. Kama chatu kwa upesi Peter akamrukia yule haramia kisha wakadondoka chini na kabla Haramia akili yake haijafanya kazi, tayari Peter mirambo alikuwa ameshakishika kichwa cha yule haramia na kuivunja shingo yake. Lilikuwa tukio la ambalo halikumaliza sekunde kumi, kimya kimya kwa weledi wa hali ya juu kabisa. Hayo yote Beka alikuwa akiyashuhudia akiwa amebaki kule juu kwenye kilima.

Peter akachukua ile bunduki aina ya AK47 kisha akasonga akiwa mwingi wa tahadhari akijificha kwenye vichaka. Sasa alikuwa amewakaribia wale maharamia na mateka pasipo ya kuonwa, akamsikia haramia mmoja akimkemea moja ya mateka na kumshinikiza atoe siri za jeshi la nchi, yule haramia akamuwekea bastola mateka ili ampige risasi lakini kabla hajafanya hivyo Peter mirambo akampiga risasi ya kichwa, yule haramia akadondoka chini, hali hiyo ilizua taharuki sio tuu kwa maharamia bali mpaka kwa Mateka, walikuwa wakiangaza macho yao huku na huko kutazama ilipotokea hiyo risasi, huku wale maharamia wakijaribu kujihami lakini walikuwa wamechelewa, kila walipojitahidi kufurukuta walijikuta wakidondoka kwa kupigwa risasi, kazi nzuri iliyofanywa na Beka pamoja na Peter iliwafanya wachanganyikiwe.

Mapambano hayo yakiendelea, mateka nao hawakuzubaa, kila mmoja alikuwa anahangika kwa namna yake kujiokoa, nao walikuwa na mafunzo ya kijeshi hivyo haikuwa ngumu kwao kujisaidia. Peter alikuwa ameshajitokeza akiwa anahama akijificha kwenye mti mmoja wa mnazi kuufuata mti mwingine akiwasogelea wale maharamia huku akiwa covered kwa nyuma na Beka ambaye alikuwa juu kabisa kwenye Kilima, maharamia wengine waliokuwa kwenye Meli na Boat wakajitokeza kukabiliana na Peter hali iliyoongeza mapambano kuwa makali zaidi, huku milio ya risasi na milipuko ya mabomu ikitawala katika kisiwa hicho. Mateka baada ya kujiokoa nao waliongeza nguvu kuwasaidia Peter na Beka hali iliyozidi kuwafanya maharamia wazidiwe, sasa walianza kurudi nyuma wakikimbilia majini kuzifuata Boat mbili zilizokuwa zimesalia pale, hiyo ilimaanisha kuwa wameshindwa, Peter akiwa na wenzake wakazidisha mashambulizi wakijaribu kuwazuia wale maharamia wasiwatoroke lakini hilo halikuwezekana. Maharamia baadhi waliamua kukimbia na zile boat mbili wakiwaacha wenzao wengine wakiwa hawajapanda, Jambo hilo halikuwafurahisha maharamia walioachwa na Boat, ilikuwa kama wamesalitiwa, walijikuta wakijisalimisha kwa kunyoosha mikono juu. Peter na wenzake wakawakamata wale maharamia waliojisalimisha, wakawafunga pingu kisha wakawapakiza kwenye ile Meli ya Mandarin Pacific yenye picha ya Kasa. Safari ya kurudi Dar es salaam ikaanza. Walikuwa maharamia wanne waliokamatwa wakiwa uhai huku maharamia waliouawa wakiwa zaidi ya kumi.

***************************

“ Nimetumia gharama kubwa kujenga nyumba zile, unafikiri pesa niliyoitumia pale itarudije kama sitofanya jambo la kueleweka, eeh! Kwamba hizi kodi za milioni mbili kwa mwezi ndio zitarudisha gharama zangu zote za ujenzi. Come on! Embu tuzungumze kama watu wenye akili Kaka! Fikiria nyumba zile tatu za Mikocheni nimetumia karibu Bilion moja na nusu kuzijenga alafu nitegemee kweli zitarudi kwa namna hii. Hiyo itakuwa biashara kichaa” Akaiweka sigara mdomoni kisha akavuta pafu ndefu akiwa kafumba macho yake, alafu akaitoa mdomoni na kukung’uta majivu kwenye kisosi maalum cha kuwekea majivu ya sigara, alafu akapuliza moshi Kupitia mdomo wake aliokuwa ameuunda kwa kuukunja kama anapiga mlunzi, alafu akaachia moshi mwingine kwenye pua yake kubwa iliyokuwa imetanuka, ikiwa imeshikilia miwani nyeusi kichwani akiwa na kipara, mdomoni akiwa amezungukwa na ndevu kiasi zilizochongwa vizuri, huku kidevu kukiwa na mzuzu wa namna yake. Mbele yake kulikuwa na meza ndogo aina ya coffee table ya kioo ikiwa na vinywaji ambavyo ni hakika vilikuwa vya gharama, nyuma yake walisimama warembo wawili wazuri sana waliokuwa na kazi moja tuu ya kuuchombeza mwili wake huku wakinengua kwa manjonjo ya kikahaba. Jina lake ni Tobias Marengo, tajiri mwenye jeuri ya pesa. Tobias akaendelea kuzungumza na mwanaume mmoja aliyekuwa ameketi upande wa pili wa coffee table wakiwa wanatazamana.

“ Unafahamu sisi pesa zetu sio kama zenu ninyi wanasiasa, ninyi wenzetu mnaafadhali kwa sababu kazi yenu kubwa ni kujichotea tuu vile mtakavyo, lakini vipi siye hatuna visima vya kuchota pesa kama ninyi. Pesa zenu hazina matumizi, mnawekewa mafuta bure, mnakaa nyumba za bure, mnajipimia mapesa kwa kujipa kazi za hapa na pale….”

“Hahaha! Tobias acha maneno yako! Kutuona sisi tunapata urahisi kupata pesa ni kutuonea, hata hivyo sijasikia ukisema mbona ninyi hatuwalipishi kodi, mnafanya biashara bure kabisa, hilo haulioni, tena zingine biashara hatari na haramu kwa nchi zetu” Yule Mwanaume akasema akiwa kamkatisha Tobias.

“ Hahah! Kwa hiyo kuchota pesa za wananchi sio biashara haramu! Hahahah! Usinichekeshe Mheshimiwa. Unanionea wivu sio? Mimi kufanya biashara hii lengo kuu ni kurudisha pesa niliyowekeza na wala sina mpango wa kuifanya milele biashara hii” Tobias akasema huku akimuagiza mrembo mmoja amuwekee kinywaji kwenye bilauri.

“ Hilo ndilo tatizo lako Tobias, tangu lini mimi nikuonee wivu, sisi ni marafiki wa muda mrefu, sidhani ni jambo zuri kunitolea maneno ya kashfa kama haya. Nilichokuwa nakupa ni taarifa kuwa kuna watu wanaojifanya ni wazalendo ambao hawataki biashara kama hizi, hivyo unapaswa aidha uziache au uongeze umakini zaidi. Mimi kama rafiki yako nimekosea kukupa taarifa hii?”

“ Sijasema umekosea bhana! Ulichofanya Kunitaarifu ni sahihi, lakini watu hao wajifanyao wazalendo wananini cha kututishia, sisi tunapesa na pesa ndio kila kitu, kama tunanunua serikali sembuse hao mijusi watutishe. Tayari mfumo mzima tumeununua, hakuna anayekohoa mbele yetu. Mizizi yetu ni mirefu sana iliyojichimbia ndani zaidi, na matawi yetu ni yale makubwa yaliyobeba matunda mengi, nani atathubutu kuingiza mkono wake kwenye mdomo wa mamba” akameza fumba la mate kisha akaendelea,

“ Huna haja ya kuhofia rafiki angu labda uniambie kama kuna jingine” Tobias alikuwa anaongea kwa kujiamini sana, maneno yake na alivyo yalimtosha kumshawishi mtu yeyote awe na matumaini naye. Yule mwanaume akasema akiwa amemaliza kinywaji chake kilichokuwa kwenye bilauri;

“ Jingine lipo” alafu akataka kujiongezea kinywaji kwenye bilauri lakini Tobias akamzuia, huku akiwaamrisha wale wanawake warembo wafanye kazi yao, baada ya wale warembo kummiminia kinywaji kwenye Bilauri, Tobias akasema;

“ Lipi hilo?”

Yule mwanaume akabugia kinywaji mfululizo mpaka kilipofika robo ya bilauri chini kabisa ndipo akaishusha na kuiweka bilauri mezani, alafu akasema;

“ Kuna vijana wajinga sana!” akaongea huku akitingisha kichwa chake, alafu akaendelea,

“ Nilikuwa na dili Fulani hivi kubwa sana, lilikuwa dili nono yaani ningelipiga hili ningekuwa nimefika mbali sana, tayari nilikuwa nimeshachukua advance yake. Lakini kuna vijana wajinga mno wameniangusha, mbaya zaidi wamekamatwa wapo sero, Daaah!” Yule mwanaume akashsusha pumzi nzito kama Bata dume.

“ Sasa hofu yako ni nini?” Tobias akauliza akiwa anawasha sigara nyingine mdomoni,

“ Tobias! Swali gani unaniuliza? Vipi wale vijana wakitoa muongozo huoni nikijulikana itakuwa ndio mwisho wangu?”

“ Hahahahahahah!” Tobias akacheka kwa nguvu na kumfanya yule mwanaume amtazame kwa mshangao.

“ Mheshimiwaaa! Hahah! Kumbe mwoga sana eeh! Hahahah” Tobias akacheka tena.

“ Unajua Tobias dharau zako zitakuja siku moja kukuponza, hii ishu ndio iliyoniteta hapa, kiukweli tangu jana tukio lilipotokea sijalala ndio maana nimeamkia kwako” Yule mwanaume akasema,

“ Kwa hiyo ndio ukaona uingie kwa gia ya kunitishia na hao wazalendo uchwara wako, ahahahah! Mheshimiwa mbinu zako zinachekesha sana”

“ Toby, tuachane na hayo, unanisaidiaje mwenzako maana nikileta mchezo naweza kutwa na jambo baya” Yule mwanaume akamkatisha Tobias.

“ Hilo jambo dogo sana, embu subiri nikajiandae tutoke hapa alafu tutaona namna ya kusaidiana” Tobias akasema, akanyanyuka, wale warembo wawili wakamvalisha koti laini mfano wa taulo kwani muda wote alikuwa kavaa kikaptura cha kushindia akiwa kifua wazi, akaondoka na wale warembo akimuacha pale yule mwanaume. Hazikupita dakika kumi Tobias akarejea akiwa mwenyewe pasi na wale warembo, kisha wakatembea mpaka eneo la upande wa pili yalipomaegesho ya magari, hapo dereva alipowaona akawahi haraka kufungua mlango kisha Tobias akaingia ndani ya gari, na yule mwanaume akiwa naye kafunguliwa mlango na dereva wake, naye akaingia ndani ya gari. Wakatoka.

Wakiwa njia maeneo ya Daraja la Salenda maeneo ya Upanga, Tobias alishtushwa kitu alichokuwa amekiona nje ya gari wakati wapo kwenye Foleni, lilikuwa kundi la watoto Ombaomba waliokuwa wakifuata gari moja moja wakiomba msaada wa fedha au chakula. Kilichomfanya Tobias ashangae ni Binti wa miaka ipatayo kumi na nne kugonga kwenye dirisha la gari lake, alikuwa binti mrembo, maji ya kunde mwenye urefu wa wastani huku kifuani zikining’inia chuchu ndogo zenye kutamanisha, macho ya binti yule yalikuwa mazuri lakini yenye ukali ulioshindwa kujificha. Tobias akiwa kwenye Foleni alijikuta akifungua kioo cha dirisha na kusalimiana na binti yule chokoraa.

“ Shikamoo! Naomba pesa ya kula” Yule binti akasema akiwa dirishani,

“ unaitwa nani?” Tobias akamuuliza pasipo kuitikia shikamoo ya binti yule,

“ Naitwa Imaculata, naomba pesa ya chakula Uncle” Imaculata akasema akiwa kama mtu mwenye haraka baada ya kuona magari yameruhusiwa kuondoka. Tobias akatoa noti ya shilingi elfu kumi akampa huku akisema;

“ Chukua binti yangu, nitapita tena kesho”

Gari likatia moto likamuacha yule binti, Tobias alijikuta akigeuka nyuma na kumchungulia yule binti Kupitia upande wa nyuma wa gari yake, akamuona Imaculata akiwakimbilia wenzake kwa furaha huku akiwaonyesha ile noti ya elfu kumi. Tobias akajikuta akitabsamu uso wake ukiwa nyuma ya miwani nyeusi.

“ Binti huyu atanifaa sana katika kazi zangu hizi, kuliko aranderande na kuchomwa na jua huku barabarani ni bora nikamchukua, nitakuwa nimemsaidia sana” Tobias akawaza, muda huo gari ilikuwa ikikatiza kufuata njia iendayo Kinondoni makaburini.

**************************************

Peter Mirambo alishangazwa na taarifa ya kutoroka kwa Julieta, hazikuwa taarifa nzuri hata kidogo, pamoja na kuwa alikuwa amechoka baada ya kutoka kwenye mapambano na maharamia lakini aliamini akirudi nyumbani na kumkuta Julieta kungempa nguvu mpya, lakini kitendo cha kumkosa Julieta nyumbani ndio kilimchosha zaidi kuliko hata alivyokuwa akipigana na maharamia.

“ Unasema hakuaga” Peter Mirambo alimuuliza mara mbilimbili Housemaid wake akitegemea angepata majibu yenye matumaini.

“ Huyu atakuwa karudi kwa wenzake tuu” Peter akawaza, Usiku ulikuwa umeshaingia tofauti na siku zingine leo hakutaka kutoka wala kula chochote, akalala bila ya kula. Habari za kutoroka kwa Julieta zilitia ganzi tumbo lake.

Kulipopambazuka aliamkia Sero maalumu ya watu wenye makosa makubwa kama ugaidi, sero hiyo ndipo walipohifadhiwa wale maharamia watano waliokamatwa, Peter Mirambo akaenda moja kwa moja kwenye hilo gereza la siri ambalo sio maarufu na lisilojulikana na raia wa kawaida. Akaingia kwenye chumba Fulani maalumu cha mahojiano, chumba kile kilikuwa na nuru hafifu kutokana kutokuwepo na dirisha hata moja, nuru hiyo ilitokana na taa iliyokuwa kwenye meza ndefu ya mita mbili hivi na upana wa mita moja, ambapo upande mmoja wa meza kulikuwa na kiti kilichoangaliana na kiti kingine kilichokuwa upande mwingine wa meza, kisha akaamuru walinzi wamlete haramia mmoja kwa ajili ya mahojiano. Kitambo kidogo akaingizwa haramia mmoja mrefu kiasi mwenye mwili mwembamba mwenye sura ya kisomali, akiwa amedhibitiwa kwa pingu mikononi na miguuni. Wakamkalisha kwenye kiti maalum wale walinzi wakawaacha Peter Mirambo na yule Haramia.

Peter Mirambo akawa anatazamana na yule kijana haramia, akawa anamfanyia usahili kwa wa macho pasipo kusema lolote. Kisha Peter akaingiza mkono mfukoni na kutoa sigara na kiberiti cha gesi na kumrushia kwenye meza yule kijana haramia, Yule kijana akatazama ile sigara kisha akayarejesha macho yake kwa Peter. Hapohapo Peter akasimama akazunguka ile meza mpaka upande aliokuwa ameketi yule kijana haramia, alafu akamsogelea mpaka kwa nyuma ilipo mikono yake, akatoa funguo za pingu na kumfungua mikono yake. Kisha akarudi kuketi sehemu yake.

Kwa kitambo kidogo pakawa kimya huku wakitazamana, kisha yule kijana akaichukua ile sigara kwenye meza pamoja na kiberiti akaiwasha, kisha akavuta pafu mbili tatu alafu akawa anaisikilizia jinsi ilivyokuwa ikiingia kwenye mapafu, alafu akakohoa kwa nguvu kama mtu anayepaliwa. Lakini Peter hakushtuka, akawa anamtazama tuu.

“ Unataka kujua nini kutoka kwangu?’ Yule kijana akazungumza akiwa na utulivu wa kipekee.

“ Nataka kujua mambo mengi sana kutoka kwako” Peter akajibu,

“ Hahaha! Mbona mimi sina mambo mengi, huenda mimi sio mtu sahihi wa kunihoji” Yule kijana akacheka huku akizungumza moshi ukitokea mdomoni.

“ Kitendo cha wewe kuwepo hapa muda huu, umeshakidhi vigezo vya kuhojiwa na kuwa unamambo mengi” Peter Mirambo akasema akiwa ametabasamu. Kisha akaendelea,

“ Niite Peter Mirambo, mpelelezi mahiri, Vipi nawe jina lako”

“ Tarikh”

“ Napenda watu kama wewe, hamtaki kusumbuana wala kupoteza muda, Tarikh!” Peter Mirambo akaita,

“ Naam Mpelelezi”

“ Nataka uniambie nani aliyewatuma kuiteka Meli ya Mandarin Pacific?”

“ Hata mimi sijui” Tarikh akajibu.

“ Hujui kivipi? Au wewe ndiye kiongozi wa maharamia?” Peter Akasema,

“ hahhahaha! Usinichekeshe bhana” Tarikh akacheka, alikuwa akiongea Kiswahili chenye lafudhi ya Mombasa. Peter naye akacheka kisha akanyamaza ghafla na kumkazia macho Tarikh,

“ Kama sio wewe kiongozi wa Maharamia niambie nani kiongozi wenu? Kama utasema kweli nitajua namna ya kukusaidia, hivyo ni uamuzi wako kukubali msaada wangu au kukaidi upate matatizo”

“ Kiukweli mimi sijui kiongozi mkuu”

“ Tuachane na kiongozi wenu mkuu, Wewe unapokea Oda kutoka kwa nani?” Peter Mirambo akauliza akiwa anamtazama Tarikh kwa jicho la udadisi. Hapo Tarikh akaacha kuvuta sigara kwa kitambo kama mtu anayetafakari, muda wote Peter alikuwa akihakikisha anasoma mwenendo wa macho ya Tarikh na mijongeo ya mwili. Saikolojia ya mwanadamu inaeleza kuwa mwili wa binadamu unazungumza hata bila ya mdomo. Ikiwa Maiti inazungumza sembuse mwili wa mtu aliyehai. Hicho ndicho kilimfanya Peter Mirambo azidishe umakini katika kaungalia macho ya Tarikh, namna anavyovuta pumzi pale anapomuuliza swali, kuvuta na kutoa pumzi pia ni sehemu muhimu ya kupata taarifa kutoka kwa mtu.

“ Unapokea Oda kwa nani” Peter Mirambo akarudia swali,

“ Sijui” Tarikh akajibu, Peter akatoa mfukoni kalamu na diary ndogo ya kijasusi, kisha akaandika andika jambo Fulani, jambo ambalo lilimfanya Tarikh awe anaangalia kile alichokuwa anaandika Peter.

“ Okay! Yale maboksi mliyoyaiba mmeyapeleka wapi?” Peter akasema,

“ Zile silaha?” Tarikh akajikuta ameropoka,

“ Hazikuwa silaha” Peter akajibu,

“ Hazikuwa silaha! Haiwezekani zile zilikuwa ni silaha tuliambiwa hivyo”

“ Mlidanganywa, zile hazikuwa silaha” Peter Mirambo akasisitiza

“ wewe unataka kunichezea kama mtoto. Hahahah!” Tarikh akasema

“ Mimi au hao waliowatuma ndio wamewasaliti na kuwachezea michezo ya kitoto, sasa mtakufa pekee yenu” Peter Mirambo akasema, akatoa simu kisha akabonyeza bonyeza, alipomaliza akairudisha simu mfukoni. Alafu akamtamzama Tarikh.

“ Kijana umeuzwa kwa bei rahisi sana, subiri utajionea, nataka uone jinsi ulivyomjinga” Wakati Peter anaongea mlango ukafunguliwa, akaingia mwanamke aliyevaa nguo za kijeshi akiwa kabeba sinia ambalo juu yake kulikuwa na chupa ya chai pamoja na vikombe na mkate. Bila kusalimia akatenga vile vikombe, akamimina chai, kisha akafungua ule mkate, alafu akaondoka bila ya kusema lolote.

“ Karibu kifungua kinywa Ndugu Tarikh” Peter ndiye aliyekuwa wakwanza kuchukua kipande cha mkate na kuanza kula. Tarikh naye akafanya hivyo, wakiwa wanakula, Peter akatoa ile simu janja yake, akabonyeza bonyeza kisha akamsogezea Tarikh aangalie, Tarikh alishtuka kuona ndani ya ile Meli ya Mandarin Pacific kukiwa na Maboksi yakipakiwa ndani ya yale maboksi kulikuwa na vifaa vya kieletroniki na wala hakuona silaha yoyote. Tarikh akajikuta akipaliwa na chai kwa kile alichokuwa amekiona.

Peter Mirambo akachukua simu, kisha akamtazama Tarikh aliyekuwa amebaki ametumbua macho kama Fundi saa aliyepoteza nut.

“ Haiwezekani! Huo ni uongo” Tarikh akasema,

“ Kwenye michezo hatari hakuna kisischowezekana Bwana mdogo, umeshasalitiwa hapo uchague kufa pekeako au utoboe jahazi mzame wote” Peter Mirambo akasema,

“ Siwezi kufa pekeangu mimi, huu ni ushenzi:”

“ Muda wangu wa kukuhoji umeisha, sitakupa nafasi nyingine zaidi ya sasa, je unataka kuniambia au hautaki, Usiponiambia wewe yupo mwenzako kati ya wale wanne waliobakia watasema ukweli, na atakayesema ukweli ndiye tutampunguzia adhabu, kazi kwako” Peter akamaliza kuongea akanyanyuka kisha akamfuata na kumfunga pingu. Muda wote Tarikh alikuwa akitafakari, wakati anataka kutoka, Tarikh akasema;

“ Subiri Kaka” Peter akamtazama, wakawa wanatazamana. Kisha Peter akarudi kwenye ile meza akiwa kasimama,

“ Unauhakika!”

“ Uhakika wa jambo gani?”

“ Kwamba tumeuzwa?”

“ Kama huniamini ngoja niondoke, muda umeisha, nilidhani unajambo la maana kumbe unataka kuniuliza upuuzi”

“ Mimi nitasema ukweli wote kama utaniahidi jambo moja”

“ Jambo gani?”

“ Kama utaniahidi kuniachia huru”

“ Sawa, niambie ukweli” Peter akasema akiwa anaomba kimoyomoyo Tarikh afunguke,

“ Imaculata! But Noo! Hapana siwezi Kaka, wataniua mimi” Tarikh akawa anaongea kama kichaa,

“ Imaculata?” Peter Mirambo akajikuta anang’aka. Lakini kabla Tarikh hajaongea chochote Mlango unafunguliwa wanaingia wanaume wawili waliovalia suti zilizowakaa vyema, Peter Mirambo anasalimiana nao, kisha mwanaume mmoja anamwambia Peter Mirambo amfuate ofisini. Wakati Peter bado akiwa hajaelewa vizuri nini kinaendelea akashangaa moja ya watu wale waliokuja akitoa bastola na kumpiga yule kijana risasi ya kichwa, Tarikh anadondoka chini wakati Peter akiwa anajaribu kumzuia yule mwanaume asimpige Risasi lakini alikuwa amechelewa.

Peter akawa anajaribu kumnyanyua Tarikh kuona kama atakuwa hai lakini alikuwa keshapoteza maisha.

iTAENDELEA
KESHO MCHANA.

Vitabu vilivyotayari
1. Mlio wa risasi harusini Tsh 15,000/= Hardcopy. Softcopy 8000
2. Wakala wa siri Tsh 15,000

namba za miamala
0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom