Simulizi ya binti Mtanzania anavyopiga kazi kumshauri Rais Lungu wa Zambia

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,100
3,613
Chanzo; Gazeti la Mwananchi: Monday May 10,2021.

Dodoma. Ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 29 tu. Theddy Ladislaus, mzaliwa wa Dodoma kwa sasa ndiye mshauri wa mawasiliano ya kimkakati wa Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu tangu mwaka 2016.

Theddy alitambulishwa kwa wabunge katika Bunge la bajeti linaloendelea jijini Dodoma, baada ya yeye kufanya ziara bungeni.

Binti huyu wa Kitanzania kazi yake ya kwanza ya ushauri ilianza kwa Makamu wa Rais wa Philippines, Jejomar Binay mwaka 2014, katika eneo hilo la mawasiliano ya kimkakati.

Baadaye alifanya kazi hiyo ya kushauri viongozi wa juu na Serikali katika nchi za Nigeria, Ghana, America ya Kusini na sasa Zambia. Theddy wakati akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2014 aliteuliwa kuwa mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba kuwakilisha wanafunzi, wakati huo akiwa mbunge mdogo mwenye umri wa miaka 21.

Ni mtaalamu wa kuwashauri viongozi na kampuni, taaluma aliyopata Ulaya na anafafanua kwamba mawasiliano ya kimkakati ni yale yanayofikisha ujumbe uliokusudiwa kwa wakati.

“Kuna ile system (mfumo) nzima kabla hujawasiliana unapima kwanza. Je, huu ni muda wa kuongea au tunyamaze na tuongee kwa mantiki gani, kama ni tangazo la (Rais John) Magufuli amefariki mnalifikisha vipi kwa umma.

“Je, tu-tweet social media (mtandaoni) au anayekaimu asimame na kutoa tangazo hilo. Sasa hizo mantiki ndio mawasiliano ya kimkakati.

“Unaweza usizione kirahisi, lakini pale kosa linapotokea ndio utajua kwamba huu mgogoro umetokea kwa sababu hatukuwasiliana vizuri. Kwa hiyo inasaidia kuona hamna migogoro,” anasema Theddy.


Alichokifanya Zambia

Theddy anasema kwa takriban miaka mitano sasa huko Zambia wameweza kutengeneza daraja la mawasiliano kati ya Serikali na wananchi wa kawaida kwa kuhakikisha kila mara wanajua Serikali inafanya nini na kwa sababu gani inafanya vitu hivyo.

“Tunahakikisha kunakuwepo mawasiliano ya haraka au kila muda, kwa sababu tukiacha ‘gape’ (nafasi) kwamba mtu anakuwa hajui kwa nini Serikali inafanya hivi na kwa wakati gani ‘then’ migogoro inaanza kujitokeza,” anasema.

Anasema mawasiliano ya kimkakati yameweza kuleta utulivu kwa jamii, kwani mara kwa mara wananchi wamekuwa wakijua sababu za Serikali kuchukua uamuzi wa jambo fulani au pia kujua Rais yuko wapi na anafanya kitu gani na kwa nini anafanya anachokifanya.

Theddy akijibu swali kama kabla ya yeye Serikali ya Zambia ilikuwa haiwasiliani na wananchi wake;

“Zilikuwepo lakini hazikuwa za kimkakati. Kwa hiyo migogoro ya hapa na pale ilikuwa inatokea, kuvuja kwa nyaraka za Serikali, saa zingine unaona mtu anajibu jambo ambalo hapaswi kulijibu.

“Au wakati mwingine unaona hawajafanya utafiti kujua kama kweli hiki kitu kinatokea au ni mgogoro tu ambao watu wameuibua kwa ajili ya sababu za kisiasa,” anasema.

Akizungumzia masuala yanayotokea kwenye mitandao ya kijamii, mfano kashfa na matusi yanayotolewa kwa viongozi, Serikali na wanasiasa, anasema Zambia hayo yapo, lakini wana namna ya kuyashughulikia.

“Hilo lipo na mara nyingi unajua, tunaangalia hizo kashfa. Je, tunazijibu vipi, tunahakikisha kwamba tuna presence (uwepo) hapo, page (ukurasa) ya Rais na nyingine ambazo zinaendana hivyo zina-communicate (wasiliana) ili watu waelewe, lakini pia ili ku- clear (kuondoa) hizo kero au misconceptions (imani potofu).”

Akizungumzia jinsi wanavyofanya mawasiliano ya kimkakati kati ya Rais Lungu na wananchi, anasema yeye anafanya kazi chini ya msemaji wa Rais na kwamba huwa wanafuatilia mitandao ya kijamii, kusikiliza redio ili kuangalia watu wanaizungumza vipi Serikali na kama kuna hoja zenye mantiki wazijibu zipi.

Akieleza kama Rais au chama tawala cha Zambia hakina utaratibu wa kujibu kero za wananchi anasema;

“Wanazo, mara nyingi hautatuona sisi kwa sababu tunafanya kama washauri, lakini utashangaa waziri ameenda kujibu au hii haifai Rais kujibu kwa sababu ni suala dogo atajibu mbunge, atajibu mwingine.

“Kwa hiyo strategically (kimkakati) inatakiwa kujua hii ni issue (jambo) ndogo Rais hatakiwi kujibu anatakiwa kujibu mtu wa kawaida.”

Akieleza kama mawasiliano ya kimkakati yamesaidia kupunguza matusi na kashfa za mtandaoni dhidi ya viongozi na Serikali huko Zambia, Theddy anasema:

“Ninasema sana, yaani kuanzia ule uongo, unajua kuna uongo ni very cheap (upuuzi) kusema kwamba mheshimiwa Rais sijui kaanguka, sijui amepotea, sijui unajua mambo kama hayo.

“Kwa hiyo imesaidia sana. Kipindi cha mwaka 2015 na 2016 kulikuwa kuna kero nyingi kwenye migogoro, confusion (mkanganyiko), miscommunication (mawasiliano mabaya) na misleading information (upotoshaji). Anasema kutokana na kazi wanayofanya, upotoshaji na kashfa zimebaki kwa kiwango cha chini na kwamba, zilizopo ni zile ambazo ni kero kweli.

Theddy anasema dawa ya kupambana na upotoshaji wa mitandaoni ni kulitolea jambo ufafanuzi kabla halijafikishwa kwenye mitandao ili kumkosesha umuhimu mpotoshaji.

Kuhusu sheria ya makosa ya mtandao, alisema Zambia imesainiwa hivi karibuni, lakini kubwa linalofanyika ni kutoa elimu kwa wananchi kwamba kutoa matusi na kashfa hakuishii kwa viongozi au Serikali, bali ni kuichafua nchi.

Hata hivyo, anasema haikatazwi mtu kukosoa kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya. “Kila mtu ana haki, lakini unavyozidisha na kusema uongo unaharibu picha nzima ya nchi.”


Kukutana na Rais Lungu

Akieleza kama katika utendaji wake wa kazi amewahi kukutana ana kwa ana na Rais Lungu, anasema anapokutana naye huwa haongelei kuwa na mshauri binti mdogo wa Kitanzania, bali huwa anathamini kazi wanayofanya.

“Hata sio mimi, sana anaongelea kazi ana-appreciate (thamini) sana kazi na pale ambapo tutakuwa tumepunguza kasi atasema ili muongeze bidii zaidi,” anasema Theddy.

simulizi-pc.jpg
 

Ngoja nisubir comments za mabaharia waseme huyu alifikaje top level kiasi hicho ..Ni ngumu mm naona huyu lady ana kitu cha ziada
 
Aje Chamwino au Magogoni. Na yeye ni mjanja amekuja kujibrand ili mama amuone.
 
Kuna maana gani mtu kuwa Rais halafu anatumia akili ya mtu mwingine, si wampe huyo binti urais badala ya nchi kuwa na middle man!
 
Hakuna cha maana nilichokiona hapo.Zambia haina lolote la maana la kuzungumzika Africa
 
Haya mdogo wangu Theddy, Huyo Lungu unaye mfanyia kazi ameshapigwa chini! Chonde chonde, rudi uje umsaidie mama yako huku Bongo.

Yale mawasiliano ya mkakati na Salim Kikeke siku ile, kiukweli yalivuruga kabisa hali ya hewa nchini. Maana hana watu sahihi katika hicho kitengo.
 
Daah, nimependa anavyojieleza yaani nimeelewa vyema.

Mawasiliano ya Kimkakati, Sijui na sisi tuna hii idara apa Bongo ama?
 
Back
Top Bottom