SIMULIZI: Wakati mwingine kuna vitu vinafikirisha sana katika kuishi kwetu

Lkkl

Member
Dec 25, 2020
24
11
Katika kuishi kuna wakati binadamu anaona vitu mpaka anashangaa. Sasa leo nmeamua kushare tukio ambalo kimsingi lilinitia huzuni sana na stasahau.

Kwa ufupi lilikuwa hivi; kulikuwa na dada mmoja jina lake X alikuwa ni mke wa jamaa jina lake Y wote wenyeji wa Mbeya. Mke akapangwa kikazi mkoa wa Mara maana alikuwa graduate mume akabaki zake Mbeya maana alikuwa form four failure.

Wakati anaenda kuripoti kazini alikuwa na mtoto mdogo, maana alikuwa na watoto wa wili hivo aliacha mmoja nyumbani Mbeya. Sasa kwa kuwa alikuwa na mtoto basi alikwenda kuripoti na mfanya kazi au msaidizi ambae kimsingi alikuwa ndugu wa mume.

Basi wakaenda kuripoti kumbe mume kampa yule msaidizi kazi kuripoti kila anachofanya X na kutuma taarifa. Basi msaidizi karipoti naona mkeo x ana mazoea siku hizi na jamaa Z. Sasa hapo vibwanga vikaanza kila saa jamaa anapiga simu vitisho mara ntakuacha, mara mimi ntakufa, mara nimekuotea umekufa omba sana, mara akaanza kupigia marafiki za X ujue mimi nitamuua, au nimfanye kichaa au nimwachishe kazi X mumkataze nasikia anatoka na Z,. Sikku zilivosogea akamwambia ukija ntakupeleka kwenye korongo nikuchinje, siku nyingine akamwambia mwaka huu lazma nikuue.

TUKIO SASA: Mume anapiga simu njoo nyumbani nina safari kidogo sina wa kumuachia mtoto,mke siku hiyo anakataa, mara anahisi homa kali anaamua kuondoka ghafla trh 3/6. Njiani gari linapinduka anakufa X na mtoto wake tu. Baada ya kifo bwana Y anasema kwa rafiki kifo kile nilikijua kilipangwa tarehe 27/5 kwa kuwa siku hiyo mtu huyu alizini na Z.

MASWALI: Je kwa maneno haya ya kabla na baada ya tukio tunaweza fikiri kuwa ameua. Hivi serikali haiwezi kuwa na mahakama za kuskilikiza visa kama hivi. Je kisheria ukimwambia adui yako kuwa leo utakufa mbele za watu na akafa katika mazingira kama ajali tena pengine ya ajali kupinduka utaonekana mtabiri?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom