Simulizi: Tafadhali baba usitufanye misukule

Huyo baba mtu wacha afe tu, Masalu hakuna kurudi nyuma tafuta tiba upone hao ndugu zako ndugu majina tu wasio na utu watajicheki wenyewe. Alafu mganga nae hasomeki yaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuwa mie ndo Masalu ningemwomba mganga anipatie hiyo dawa chap, kama baba atadanja na adanje chap! Ala!
 
Sehemu ya 16

Kufikia pale nilijikuta nikichanganyikiwa na kushindwa niegemee upande gani, lakini niliamini maisha yangu ni muhimu kuliko kitu chochote chini ya jua. Vile vile sikuwa tayari kumuhurumia mtu aliyepanga kuniangamiza kwa ajili ya tamaa zake za mali.

Uamuzi nilioamua ni kujitengeneza mimi na lolote litakalo tokea kila mmoja ataubeba msalaba wake.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu mganga alinishtua.
“Vipi umeamua nini maana naona umekaa kimya?”

“Mzee wangu mambo ni mazito kila ninalofikiria naliona zito.”
“Kwa hiyo tuache kama ilivyo?”
“Mzee wangu huna ufumbuzi mwingine usio na madhara?”

“Sikiliza kijana wewe unajua matatizo ya familia yenu kuliko mimi, hebu nisaidie nifanye nini?”

“Wewe si ndiye mtaalamu ninayekutegemea.”
“Hutaki kunisikiliza, kwani mimi napenda kuona matatizo, lakini mambo yenyewe yamekaa vibaya.”

“Kwa hiyo?”
“Nimekueleza yote una uamuzi wako mwenyewe wala siwezi kukuingilia lakini ukweli ndiyo huo.”
“Basi fanya unavyoweza.”

“Vipi?”
“Utakaloliona linafaa.”
“Kijana acha kujitoa akili, mimi sipo hapa kwa ajili ya kuwachagulia wateja jinsi ya kufanya.”

“Mzee wangu kwa vile mpango wao ni mbaya kwangu naomba unisaidie mimi.”
“Kwa hiyo upo tayari kwa lolote litakalo tokea?”
“Nipo tayari.”

Leo nitaanza kukupa dawa ya kurudisha nguvu za kiume, lakini usishtuke kusikia taarifa zitakazo kufikia ambazo zitajenga uadui mkubwa kati yako na nduguza.”
“Siwezi kushtuka kwa viumbe wasio na huruma na mimi wewe nipe hiyo dawa kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe.”

“Haya nisubiri.”
Mganga alinyanyuka na kutoka nje, akiniacha na uamuzi mmoja ambao nilikuwa tayari kwa lolote. Baada ya muda aliniita nje, nilitoka na kuelezwa nisubiri kwenye kigoda. Baada ya muda nilimuona mpenzi wangu akiwa amebeba ndoo kutoka kwenye kisima kilichokuwa pembeni ya nyumba ya mganga.

Alipofika, mganga alimueleza ayapeleke nyuma ya nyumba na kuyaweka kwenye beseni. Alifanya vile, aliporudi mganga alizunguka nyuma na baada ya muda aliniita.

Nilimfuata na kukuta kuna beseni lililokuwa na maji yaliyochanganywa na dawa ya unga na majani mabichi kama ya mnyonyo.
“Oga haya maji, kisha haya majani kutajisugua sehemu zako zisizofanya kazi, sawa?”

“Sawa.”
“Haya, ukimaliza kuoga vitu vyote viache huku huku”
“Hakuna tatizo mzee.”

Mganga aliondoka na kuniacha nikivua nguo na kuanza kujimwagia maji kwa mikono huku nikijisugua kwa majani yale mabichi sehemu zangu za siri zilizokwisha nguvu.

Baada ya kumaliza kuoga nilirudi kwa mganga, alinielekeza nikae kwenye kigoda kisha alizunguka nyuma ya nyumba sikujua anakwenda kufanya nini, mara alirudi akiwa ameshikilia majani niliyojisugulia na kuingia kwenye kilinge chake. Baada ya muda aliniita.

Niliingia kibandani na kuketi kwenye ngozi ya ng’ombe, baada ya kuketi mganga alinipa maji yaliyokuwa kwenye kikombe cha plasitiki. Nilikunywa maji yale kisha nilimrudishia kikombe, baada ya kukipokea alisema:
“Sasa nafikiri kazi tumemaliza, weka hapo kwenye kikapu kiasi chochote kama sadaka kwa mizimu.”

Nilichomoa pochi na kuweka elfu hamsini, baada ya kuweka mganga alisema:
“Mpaka sasa kwenu kuna hali ya sitafahamu, inaonesha hapa baba yako ameanguka dukani na anarudishwa nyumba. Ukitaka kumuua haraka baba yako ukikutana na mpenzi wako haimkopeshi salamu utasikia.”
“Sasa mganga kama ni hivyo kuna faida gani ya kuja kwako?”

“Nilikuwa nakujulisha tu, litakalo tokea usishangae, kesho asubuhi njoo haraka maana kuna vita nzito itakayo tokea. Itakuwa mara mbili ya leo, ningeweza kukutengenezea zindiko lakini siwezi kufanya kazi mbili kubwa kwa wakati mmoja.”

“Hakuna tatizo.”
“Basi wewe nenda nyumbani, kama unaweza usionane nao watakutafita sana ili kuhakikisha baba yenu anarudi katika hali ya kawaida. Na kurudi kwa afya ya baba yako, huchukui muda unakuwa msukule wa familia wa kuwaingizia pesa.”

“Siwezi kukubali, kama nimepona nitaendelea na mpenzi wangu kwa vile bila yeye nisingeweza kupona.”
“Hiyo ni juu yako kwa vile yote nimekueleza bila kuacha kitu.”

Baada ya maelezo ya mganga nilitoka na kumpitia mpenzi wangu na kuondoka, tulipofika Pasiansi tulitafuta sehemu kupata chakula kutokana na njaa iliyokuwa ikituchonyota.

Wakati wa kula nilijikuta mtu mwenye mawazo mengi kitu kilichomshtua mpenzi wangu na kutaka kujua kulikoni.
“Masalu kuna nini mbona unaoneka una mawazo mengi?”
“Ni kweli, nina mtihani mzito.”

“Upi huo?”
“Kuhusiana na hali yangu, kama nilivyokueleza, kuna mambo mazito yamejitokeza.”

Sikuwa na jinsi nilimueleza kila kitu sikutaka kumficha kwa vile msaada wake ndiyo uliyofichua yote. Baada ya kunisikiliza alishtuka sana.

“He!”
“Ndiyo hivyo nikubalia ili nigeuzwe ndondocha au nikatae baba afariki na familia kukutwa na matatizo mazito.”

“Mmh! Huo mtihani lakini maisha yako ni muhimu kuliko kitu chochote.”
“Nami ndiyo nimefanya hivyo, ila mganga ameniomba leo nisionekane nao ili kesho turudi mapema kwake.”

“Hakuna haja ya kuangaika, tutafute guest yoyote nzuri hapa hapa Pasiansi ili kesho turudi kwa mganga mapema.

“Kweli wazo zuri, basi tufanye hivyo.”
Nilikubaliana na mpenzi wangu baada ya chakula tulitafuta nyumba ya wageni yenye hadhi na kupanga pale.

Siku ile tulishinda na kulala pale, majira ya saa tano za usiku dada alinipigia simu, nilitaka kuacha kuipokea lakini niliamua kuipokea.
 
Ahsante kibonge mwenzangu..huyo nae asingepokea hiyo simu

Sasa masalu unapokea simu ya nini?
 
Sehemu ya 17

Nilikubaliana na mpenzi wangu baada ya chakula tulitafuta nyumba ya wageni yenye hadhi na kupanga pale.
Siku ile tulishinda na kulala pale, majira ya saa tano za usiku dada alinipigia simu, nilitaka kuacha kuipokea lakini niliamua kuipokea.

“Haloo.”
“Haloo Masalu.”
“Shikamoo”
“Marahaba.”
“Unasemaje?”
“Masalu upo wapi?”
“Una shinda gani?”
“Masalu umefanya nini?”
“Kuhusu nini?”

“Unataka kumuua baba?”
“Kumuua kivipi?”
“Masalu baba akifa utamla nyama.”
“Kama mlivyo mla nyama dada Monika.”
“Nini?”

“Umenisikia vizuri.”
“Wee fanya mzaha, lakini ole wako baba afe.”

“Na wewe ole wako siku ukisogeza pua yako kwangu mwanga mkubwa we, kwanza nilikuwa nakuchekea sasa hivi sikupendi nakuchukia ni adui yangu namba moja na taarifa zako nazipeleka polisi.”

“Polisi! Utawaambia nini?”
“Kwamba wewe na wenzako ni wauaji.”
“Tumemuua nani?”

“Dada Monika na mtoto wako na ushahidi wa sehemu ulipoziweka hizo maiti ninao na lazima mtanyongwa mwaka huu.”

“Masalu usifike huko hali ya baba ni mbaya sana hebu rudi nyumbani tujue tufanye nini.” Ilibidfi arudishe sauti chini.

“Nirudi mnimalize.”
“Tukumalize?” Alijifanya kushtuka.
“Eeh, baada ya kuniua nguvu za kiume sasa mnataka kunigeuza msukule.”

“Ha! Masalu nani kakudanyanya hivyo?”
“Dada hakuna siri duniani, yaani pamoja na kunipa kidonda hamkuridhika pamoja na utajiri na maisha mazuri kupitia mwili wangu. Mkaamua kuniua nguvu za kiume ili nisiwe na thamani yoyote dunia. Haitoshi mmeniandalia pigo zito la kunimaliza kabisa la kunigeuza msukule ili tu muwe na maisha mazuri.

“Ninyi ni viumbe gani mnaojali fedha kuliko utu wa mtu, mmemtoa kafala dada Monika kwa tamaa zenu, hamkuridhika umemtoa mtoto wako ili uwe na pesa nyingi vile vile hamkuridhika mmenigeukia mimi. Kwa vile hakuna mtu mwingine wa kumpa kidonda hiki mmeamua mnigeuze ndondocha wa familia.”
“Masalu umejuaje?”

“Si kujuaje, kwa nini umeamua kunifanya hivyo?”

“Si kweli.”
“Sawa si kweli, basi baba anakufa.”
“Umeamua kumuua?”
“Mimi na ninyi nani kaamua kumuua mwenzake?”

“Masalu kumbuka baba yetu ni huyu huyu akifa hatutampata mwingine.”
“Kwani kuna mbadala wa dada Monika, baba ni huyo huyo, dada Monika mwingine yupo wapi?”

“Masalu makosa yamekwisha fanyika rudisha moyo uokoe maisha ya baba.”
“Kwanza mnaniambia hivyo mimi nimemfanya nini baba.”

“Inaonekana umekwenda kwa mganga kurudisha nguvu zako za kiume.”
“Mlitaka niwe hivi hivi milele kwa raha zenu, mbona ninyi mna watoto na wanaume?”
“Kwani Masalu upo wapi?”

“Tokea lini mlinitafuta?”
“Basi zungumza na mama,” baada ya muda nilimsikia mama akiniita.
“Masalu.”

“Naam mama, shikamoo.”
“Marahaba mwanangu upo wapi hali ya baba yako ni mbaya sana.”

“Anaumwa nini?”
“Ameanguka kwenye mishughuliko yake, kama ni kweli umefanya wewe njoo umsaidie baba yako, hali inatisha hajitambui anakoroma tu.”

“Mama sihusiani na lolote kuhusiana na matatizo ya baba, naomba mumpeleke hospitali.”

“Ugonjwa huu si wa hospitali.”
“Kwa hiyo mimi ndiye niliyemroga?”
“Hapana Masalu, ila inawezekana ulichokifanya ndicho kilicho muathiri baba yako.”

“Kipi hicho?”
“Unakijua Masalu, hebu rudi haraka nyumbani.”

“Mama ni nani kwako?”
“Mtoto.”
“Nina haki gani kama mmoja wa watoto wako?”

“Haki zote kama walizonazo wenzako.”
“Sasa kama kila mtu ana haki hiyo kwa nini unataka kushiriki katika kunigeuza ndondocha wa familia?”

“Masalu! Wakugeuze kivipi?”
“Mama, unajua vizuri sana si suala la siri, mpango wenu wa kunimaliza nimeugundua lakini nawahakikishia kila atakayenigua nitampoteza.”

“Upo tayari baba yako afe?”
“Mimi situnzi uhai wake bali Mungu aliyetuumba wote, kama wakati wake umefika basi atakufa, kama alivyokufa mtoto wa dada na dada Monika.”

“Kwa nini umekosa huruma?”
“Kwa vile ninyi mnanionea huruma eeeh.”
“Kama ulivyosikia hali ya baba yako ni mbaya kifo chake kitakuhusu.”

“Sishangai hata wewe mama niliyekuwa nakutegemea ni mmoja wapo. Asante sana nashukuru, Mungu yupo atanilinda.”
“Masalu...Masa..,” nilikata simu na kuizima kabisa.

Baada ya mazungumzo nilijikuta nikilia peke yangu jinsi familia yangu ilivyokuwa ikijijali yenyewe na kuwa tayari kupoteza uhai wa mtu ili tu ipate mali.
“Masalu nyamaza mpenzi wangu.”
“Inaniuma.”

“Kweli inauma, lakini kwa nini umekubali kuzungumza nao? Ungezima simu yote haya yasingetokea.”
“Ilikuwa lazima nizungumze nao ili wajue kuwa naelewa kila kitu, pia hata kujua kama kweli hali ya baba ikoje.”

“Kwa hiyo utakwenda kumuona baba yako?”
“Nikitoka kwa mganga nitakwenda.”
“Pole sana inasikitisha, familia yako ina dhambi kubwa.”
“Wee waache sijui kwa Mungu watasema nini?”

“Ulisema wewe ndiye chonzo cha utajili kilichoachwa na marehemu dada yako Monika, ukipona inakuwaje?”
“Sijui, watajua wenyewe, mimi nitaangalia afya yangu.”

“Mmh! Pole sana mpenzi wangu, kupona lazima uwe na roho ngumu ili umeze mfupa.”
“Nimekwisha umeza lolote na liwe, siwapendi mashetani wale.”

Kwa vile muda ulikuwa umekwenda tulipanda kitandani kulala, usiku nilijikuta nikipatwa na hamu ya mapenzi. Lakini nilikumbuka kauli ya mganga kuwa nikikutana kimwili na wenzangu ndiyo kifo cha baba hawezi kuomba hata maji.

Pamoja na hasira kutokana na roho mbaya ya familia yangu juu ya mambo waliyotaka kunifanyia. Nilijikuta nikiingiwa na imani ya kutofanya tendo lile kuokoa maisha ya baba. Tulilala mpaka asubuhi bila kufanya tendo la ndoa, asubuhi tuliamkia kwa mganga.

Hatukuchelewa kufika kwa vile hapakuwa mbali kutoka tulipokuwa tumepanga, ulikuwa mwendo wa dakika ishrini. Ilionesha tulikuwa sisi ndiyo wa kwanza wateja toka nje kufika pale kwa siku ile, tuliowakuta pale ni wale waliokuwa wakitibiwa na kulala pale pale.

Mganga alitukaribisha kama kawaida niliingia ndani peke yangu na mpenzi wangu alibakia nje. Nilipofika hakunisemesha lolote aliendelea na kutoa chupa za dawa kwenye kikapu na kuziweka juu ya ngozi kisha alichukua kalatasi la kaki na kuanza kumiminia unga wa dawa kidogo kidogo kutoka katika kila chupa.

Zilikuwa chupa zaidi ya tano, baada ya kuukusanya unga wa dawa katika kalatasi moja, alichukua chupa iliyokuwa na mafuta kama sikosei ya ng’ombe yalikuwa meupe na mazito. Aliyamiminia yale mafuta na kuyachanganya na mchanganyiko wa dawa kisha alitoka nje.

Baada ya muda alirudi na kunionesha kwa ishara nimfuate, nilimfuata mpaka kwenye kichuguu kimoja ambacho alinielekeza. Kabla ya kupanda juu ya kichuguu alinielekeza kwa ishara nivue shati. Nami nilifanya kama alivyonielekeza.

Baada ya kupanda juu ya kichunguu kifua wazi, alipanda na yeye na kuanza kunichanja kila kona ya mwili huku akinipaka ile dawa aliyochanganya na mafuta mazito. Alipomaliza tulitelemka na kurudi hadi ndani ya kilinge, ndipo aliponisemesha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom