Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupo mamitoNilijua haina wafatiliaji
Tupo bhanaHii story nahisi kuishia apa naona haina wafatiliaji
@shunieSEHEMU YA 27
Wakati mwingine nilimchukua na kwenda naye huko ilipokuwa nyumba hiyo, mafundi walikuwa wakiendelea kuijenga kwa nguvu kubwa, kila siku ilikuwa ni lazima wafike hapo na kuendelea na mambo yao.
Nilipanga kuhamia ndani ya nyumba hiyo siku ambayo nitafunga ndoa na Scaila. Nilimueleza hilo kabisa lakini sikutaka kumwambia ni siku gani nilitamani sana kumuoa.
Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni Jumapili ya mwezi wa tatu, nilipokea simu kutoka kwa Hiza na Ally ambao waliniambia walikuwa wakija nyumbani kumuona shemeji yao maana kila siku niliwaambia waje kumuona ila walikuwa na mambo mengi.
Nilimwambia Scaila, nikamwambia ni lazima ahakikishe anavaa vizuri, anapendeza ili marafiki hao watakapokuja basi wachanganyikiwe na kuona nimekuwa mwanaume ninayejua kuchagua mwanamke mzuri.
Hawa wawili huwa wananijua, sikuwa mtu mwepesi kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, ninapenda sana kukaa singo kwa kipindi kirefu nikifanya mambo yangu binafsi ila ninapoamua kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, huwa ninamchagua mwanamke mzuri mno.
Walinizoea hivyo tangu tulipokuwa chuo mpaka kipindi hicho.
Katika kipindi chote huko nyuma waliniambia siku ambayo ningeoa, basi ningemuoa mwanamke mbaya kuliko wote katika dunia hii kwa sababu tu nilipenda kutembea na wanawake wazuri.
“Huyo mkeo, najua atakuwaje! Nishapata picha yale,” aliniambia Hiza huku akicheka, kipindi hicho tulikuwa chuo.
“Mke wangu atakuwa mkali sana, zaidi ya mkeo, zaidi ya mke wa Ally, yaani atakuwa pini, pini kweli,” nilimwambia.
“Hahaha! Mzee baba utachagua koroma!” alisema Ally.
“Mtaona tu.”
Maneno hayo niliyakumbuka vilivyo, niliwatambia sana na sasa ulikuwa muda wa kuwaonyeshea nilikuwa makini kwa kile nilichowaambia miaka ya nyuma, niliamini kila mmoja angemkubali huyu Scaila kwani hakuwa na uzuri wa kawaida.
Ilipofika majira ya saa tisa alasiri, wakanipigia simu na kuniambiwa walikuwa njiani wakija. Nikawakaribisha na kumwambia Scaila ajiandae.
“Wanakuja!” nilimwambia.
“Haina shida. Nawasubiri!” alisema Scaila, hapohapo akamwambia Grace aandae chakula kabisa kwani muda si mrefu wageni wangeingia.
Mmmh natabiri kuumbuka kwa Scaila pindi Ally na Hiza wakimuona.... ngoja tuone.SEHEMU YA 27

SanteeeeehhhSEHEMU YA 29
Nilifurahi sana! Scaila akaelekea jikoni kuendelea na kazi lakini kitu cha ajabu kila nilipokuwa nikimwangalia Hiza, hakuonekana kuwa sawa japokuwa alikuwa akionyesha tabasamu na hata kucheka kila wakati.
Hilo lilinipa mawazo lukuki, sikujua kilichokuwa kikiendelea zaidi, inawezekana kulikuwa na jambo lililokuwa likimtatiza lakini hakutaka kuliweka wazi.
“Mzee baba niaje? Mbona umebadilika?” nilimuuliza.
“Mzee baba huyu demu mkali! Mpaka natamani angekuwa demu wangu!” alisema Hiza na wote kuanza kucheka.
Chakula kiliandaliwa na kuletwa mezani, tukaanza kula huku muda mwingi tukiendelea kuwa na furaha kupita kawaida.
Tulikula kwa dakika arobaini na tano na tulipomaliza, wageni wakaaga, nikaamua kuwasindikiza kwa gari.
“Mmemuonaje kwanza?” niliuliza kwa mbwembwe, nilitaka nianze kusifiwa, nilijisikia raha sana.
“Una mchumba mzuri sana,” alisema Ally.
“Najua kuchagua! Ila niliwaambia tangu chuo, mke wangu atakuwa mkali si mchezo,” niliwaambia
“Sasa cha msingi, kama utaingia ndani ya ndoa, vumilia kwa kila kitu,” alisema Hiza.
“Kivipi?”
“Utakuwa na mke mzuri, sasa kila mwanaume macho yatakuwa juu-juu. Ila nataka uwe na uhakika kama moyo wako unakwambia yule ni mke wako wa ndoa,” alisema Hiza.
“Moyo unaniambia hivyohivyo!”
“Una uhakika?”
“Jamani! Mpaka mikakati ya ndoa nimeanza kwa chini! Hilo wala usijali! Yaani nina uhakika!” nilimjibu.
“Basi inshallah!” alisema Hiza.
“Halafu kingine!” alisema Ally.
“Kipi?”
“Kwenye uhusiano inabidi mvumiliane sana! Sio unakuja kusikia alikuwa na jamaa fulani mzee baba ukapaniki! Haiko hivyo, ni lazima ujue mmepanga kuishi pamoja, hivyo ziba masikio.
Kwenye mapungufu, mvumiliane, hakuna mtu aliyekamilika,” alisema Ally.
“Hilo halina shida pia.”
“Na kingine!” alisema Hiza.
“Kipi?”
“Utakapogundua mabaya yake, usimwambie, fanyia upelelezi wa kina, yaani usikurupuke,” alisema Hiza.
“Mh! Nitaweza kweli?”
“Kwa nini ushindwe? Utaweza tu.”
“Basi sawa.”
|
|
Tukutane Jumatatu.